Ukweli ni kwamba bodaboda ana fursa na anamzidi kipato Mwalimu

Uko sawa, walimu waache kazi wakapige bodaboda ambayo kwa siku wataingiza elfi 50 hadi 60!!!!

Umetisha mpwayungu. Mwalimu aliyekuchapa ataipata, na siku ukipata mwanya utamtoa Uhai!
 
Kuna bodaboda wana vichwa vyao vya asubuhi na jioni yani go and return. Unakuta anapoamka tu saa kumi na moja ana vichwa vyake kumi vya kila siku kuwapeleka na kuwarudisha kutoka kazini.

Tufanye kila kichwa ni buku nne yani kwenda buku mbili kurudi buku mbili hapo sijapiga hesabu wa buku tano nawale wakudaka njiani na kijiweni
 
Uko sawa, walimu waache kazi wakapige bodaboda ambayo kwa siku wataingiza elfi 50 hadi 60!!!!

Umetisha mpwayungu. Mwalimu aliyekuchapa ataipata, na siku ukipata mwanya utamtoa Uhai!
Umeharibu hapo mwisho. Ujinga wa walimu haunifanyi niwachukie Bali nawadharau
 
Kuna wengine wanamiliki bodaboda zao sio ya boss
 
Inawezekana kwa siku chache kupata hiyo pesa lakini sio daily net income yake iwe 60K.
Kumbuka bodaboda haitumii maji.
Ingekuwa rahisi bodaboda kupata kipato cha 60K kwa siku graduates wasingejazana huku mtaani na kuwa ombaomba na malaya kwa kasi ya 5G.
 
Umeongea point. Chakula cha walimu ni ugali maharage tu tangu nikiwa mtoto. Mchele mpaka atoke town kuchukua mshahara anashuka kwenye bus na mkate mreeefuu
 
Hawana mtaji wa kununua pikipiki. Saizi boxer au tvs Mpya inakimbilia million 3
 
Achana na hawa bodaboda wa vibarazani Kuna bodaboda wa bolt na uber hawa jamaa wanapata hela sana kwa siku kukunja elfu 40 ni kawaida
 
Haya tuanzie hapa
A. Mwalimu ana uwezo wa kuajiri bodaboda zaidi ya 10.
B. Mwalimu ana uwezo wa kupata fursa nyingi zaidi kupitia elimu yake.
C......
Sio kweli. Pikipiki moja tu ni mitihani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…