Ukweli ni kwamba bodaboda ana fursa na anamzidi kipato Mwalimu

Ukweli ni kwamba bodaboda ana fursa na anamzidi kipato Mwalimu

Kitu km hujui/huna experience nacho,nivema ukae kimyaaaaa itaficha ujinga ulonao.tulia usome comment tu ndugu...zitakusaidia kufungua ulimwengu usioujua
Labda kama ww peke yako ndio dereva wa bodaboda tuna vijana tumewapa hizo bodaboda kwenye maeneo tofauti nchi hii.

Hizo stori zenu za kupata 60K kila siku kawadanganye wajinga wenzio.
Sikatai baadhi ya siku kupata hiyo 60K lakini sio daily.
Vijana wa siku hizi mnajiingopea hadi nafsi zenu ili iweje?
Na endapo kuna kijana ana uwezo wa kuingiza 60K kila siku na anahitaji bodaboda mpya aje inbox mm atanipa 15K tu kwa siku kwa mwaka mmoja baada ya hapo bodaboda ni yake.
 
Mimi naona boss kununua boda boda kumpa kijana naiona kama biashara kichaaa labda boda boda uwe mwenyewe alafu uwe na akili kichwani hapo kidogo hela utaiona.kwa maaana unanunua boda 2,700,000 cash then unampa kijana analeta 15,000 per day miezi 10 ni kama 4,500,000 ukija kutoa faida unapata 1,800,000 kwa miezi kumi ,wastani wa 180,000 kwa mwezi.......ki mahesabu ni kama hela yako unaila kidogo kidogo tu labda uwe na side hustle.au uwe ni muajiriwa hiyo hela ya boda boda iwe kwa ajili ya kujichanga na kununua nyingine ili ziwe biashara endelevu.
 
Mshakaa na boda boda mkawauliza? Mtafute bodaboda muulize kama hiyo 50elfu anapata kwa siku.

Zamani bodaboda walipiga pesa si siku hizi, mtaani vijana wanalalama.
Yaani awe ameshakula, ameweka mafuta, apeleke hesabu kwa bosi kisha abakiwe na 50 elfu 😂

Siku hizi akitoa hesabu, mafuta, na kula yake kuipata 15 tu kazi.
Nina kama mdogo wangu ambae hapo awali alishaendesha pikipiki zangu kabla ya kuachana na hii biashara kichaa.
Sijui mapato ya walimu ila nawajua bodaboda kiasi chake.
Hauwezi kupata hata wa kwenye Miji Mikjbwa wakijitahidi kuanzia asubuh Hadi usiku ndio 30,000 ila huku mwingine huwa wanapata 10,000-15,000 in most cases..

Bajaji tuu anayepeleka hesabu haweai laza 30,000 Ni nadra sana kwa sasa.
 
Kama boda boda pikipiki ni yake anamzidi . Sababu wastani hapo ni kama 16,000/ kwa siku. Mi Namjua dereva mmoja wa boda ya mkaa analipa kila siiku 15, kwa boss wake nae anapata ya kula na kuishi. Hata wanao uza maji tu wana hela ndefu kwa siku. Mwalimu anajazia tuiton na vi semina vinginevyo ananufaika na bima ya afya na pesheni akistaafu lakini kula nyama tu kwenye bucha inabidi achungulie mfukoni sababu kg1 ni 9000/= bila viungo shida sana ajira jamani. labda awe na mshahara wa laki 8 mbele hukoo
Kwa Tanzania hapa salary ya kuanzia 600k unaishi vizuri na change ya 150-200k una sevu..

Hii Pesa boda sii rahisi kuipata tusidanganyane..
 
Kuna bodaboda wana vichwa vyao vya asubuhi na jioni yani go and return. Unakuta anapoamka tu saa kumi na moja ana vichwa vyake kumi vya kila siku kuwapeleka na kuwarudisha kutoka kazini. Tufanye kila kichwa ni buku nne yani kwenda buku mbili kurudi buku mbili hapo sijapiga hesabu wa buku tano nawale wakudaka njiani na kijiweni
Labda Dar
 
Bodaboda kupata 50000 kwa siku inawezekana sana lakini kinachowaponza hawana nidhamu ya pesa kabisa. Bodaboda wengi ni vijana hawawazi kusave sababu anajua kesho atatafuta na atapata tena hivyo pesa yao inaishia kwenye pombe, kamari/madubwi ( hapa asilimia 80 ya hela inaishia), bangi na kuhonga wanawake.

Bodaboda hawana uchungu na hela kabisa yeye kumpeleka mwanamke bure asidai hata 100 ni kawaida badi hajalipia guest na kumlisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ndio point watu wengi hatuna nidhan ya pesa kama inaingia kidogo kidogo kwa siku tunashindwa ku manage ndipo wanapokwama wengi hapa wanao hustle nje ya ajira sio boda tu..

Mtu deile anaingiza efu 30 net kwa kuwa deile ipo anapiga bia, anagongea wake za watu by the of the month saving haifiki laki tano...

Na mademu wanalijua hili ndio mana wanashobokea boda boda pesa ipo...

Ukikuta boda anajielewa anakua na maendeleo sana anakua anacheza ligi moja na wanaolamba net 1.5 milion kwa mwezi

Sent from my Pixel 3a using JamiiForums mobile app
kwa hiyo boda akisev hiyo pesa anaweza nunua pkpk 3 walau kwa mwaka? hahaahahaa,,,bodaboda siku hizi ni nyingi mno 15k inapatikana kwa shida na kama ingekuwa kweli wanapata 50k per day nafikiri kusingekuwa na tatizo la ajira tz na Africa kwa ujumla
 
Back
Top Bottom