Ukweli ni kwamba Lukuvi na Kabudi walifutwa Uwaziri

Suzy Elias

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2021
Posts
1,067
Reaction score
6,200
Kwa nini Samia hakutaka kuwa wazi tu kuwahusu hao jamaa na kuamua kutudanganya eti watapewa kazi maalum ilihali sivyo?!

Ukweli humweka mtu huru na kwalo Samia ingetosha alipowateua wengine na kuwaacha kina Lukuvi na wenzake angekaa kimya na kuendelea na hamsini zake.

Hilo la Lukuvi na Kabudi kufanya kazi maalum ni uongo wa mchana kweupe!

Ukweli ni kwamba Lukuvi na Kabudi walifutwa kazi ya uwaziri na si vinginevyo.
 
Wewe umejuaje kama hawajapewa hiyo kazi maalumu?
 
na wao ni wajinga, yaani SSH aliwa zuga eti atawapa 'kazi nyingine' na wao wakamwamini na kuingia cha kike, nyuma ya pazia dhamira ya ya mama ilikuwa ni kuwang'oa madarakani ma- 'pro magufuli', adi sasa wanaweza wasiamini masikio yao lakini ndiyo imetoka hiyoo
 
U
Unawapenda?
 
Maisha ni kupanda na kushuka⛷️
 
Sasa wao ujinga wao ni upi??

Wangekataa kung'olewa au??
 
Prof Kabudi alitamka kuwa atakuwepo makongamano mengi ya wanazuoni kwa kuwa anamuda wa kutosha.
 
Kazi maalum hazitangazwi hazarani. Wako kazini as of now
 
Asante kwa taarifa
 
Walipata nafasi wakaingiza mapanga🤣🤣
 
Wenye Akili tulisema kuwa Waliondolewa kwakuwa walikuwa ni Team Hayati Magufuli na wangeachwa Serikalini wangeweza kutumika Kumkwamisha Mama yenu kwa Kutumika na Kundi lao lililokuwa nyuma yao hamkutuelewa.
 
Huwenda huyu mama hawangoi pro magufuli bali potential contestants ambao wangepose risk kwake
 
... hawakuzaliwa kuwa mawaziri anyway.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…