zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 20,537
- 31,729
Kazi kwelikweli nani aliyekwambia wafilisti ndio wapalestina?? Wafilisti wametokea ukoo wa caphtor mwana wa mizraim sasa wapi na wapi na wapalestina?? Hivi hii story mnaitoaga wapi kuwa wapalestina ni wafilisti??? Kwanni mnapotosha hata makanisani nasikiaga sana hadi nashangaa mnatoa wapi hizo taarifa....Wafilisti walikuwa kabila la watu wa Ulaya ambao walivuka Bahari ya Kati na kisha kushindwa kuvamia Misri waliteka pwani ya Kanaani (1175 KK hivi) wakifaidika na silaha za chuma walizozitumia dhidi ya watu waliokuwa na zile za shaba tu, wakiwa wenyeji au Waisraeli.
Ingawa hawakuwa wengi, waliathiri sana nchi yao mpya, kiasi cha kuiachia jina la Palestina.
Habari nyingi juu yao zinapatikana katika Biblia.
Alafu kingine nchi ya ahadi kibiblia inafika hadi Euphrates na inaanzia mto nile mbona sijawahi sikia wakienda kuishi misri au iraq ambapo ndipo mto frati upo?? Why palepale mashariki ya kati?? Kana kwamba ardhi wanayodai kupewa ndio palepale tu kwanini hili kiasi wawatese wapalestina wasio na hatia
Mwisho kusema wapalestina warudi walipotoka ni kauli ya ajabu sababu hta wayahudi walihamia tu pale na walikuta wazawa......hivyo basi hakuna sababu yeyote ya kuwatesa wapalestina kama waliishi wa wagibeoni vizuri ingawa waliwakalia kimabavu basi waishi hivyo hivyo na palestina yaani nchi moja yenye haki sawa wakumbuke hata wao walipokuwa utumwani walipokelewa na nchi nyingi tu kwanni leo hii wawaone wapalestina kama hawana haki eti sababu walipewa hiyo nchi..... Mbona wao walipewa hifadhi nchi nyingi tu sembuse leo hii waone wengine ndio hawafai kuishi hapo!! Sio undumilakuwili huu
Mimi ni mkristo ila kiukweli hawa wayahudi wenye nywele nyeupe na macho ya blue!! Wanakosea sana