zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 20,537
- 31,729
Shida husomi biblia kijana nchi ya ahadi ipo misri hadi iraq ila mmeng'ang'ania tu palestina ya watuMisri ni nchi inayojulikana mipaka yake iko toka enzi za abraham na ilijulikana hivyo wataendaje kuishi huko
Wwe umesema wapalestina ni waarab waliohamia tu ila unasahau wapalestin ni uzao wa Abraham pia kiufupi waisrael na wapalestina wote ni watoto wa baba mmoja hata utafiti wa DNA wa American journal of human genetics umethibitisha hilo sasa kwanni muwatenge hao kutoka urithi wa baba yao?? Nani alisema baraka ni za Yakobo peke ake hadi ajimilikishe ardhi??Hivi unajua jina la palestina limetokana na nini au unabisha tu
Hiki ulicholeta hapa ni maandiko ya kumpwleka mtu mbinguniKijana unapingana na biblia yako
Wagalatia 3
28 Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu.
29 Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.
Ila bado mnaamini waisraeli wana ahadi zao wakati biblia imeshahitimisha hapa kuwa wote ni sawa na uzao wa Abraham ni wakristo wote sasa kwanni muamini ile nchi ni ya wayahudi pekeee?? Kwanni mnaipinga biblia yenu wenyewe!!??
Sasa huo ni ujinga wa hao waarabu cha Mungu hakipingwi na ukikipinga hutashinda ndicho kilichotokea wakajikuta wanachukuliwa na maeneo yao mengineSasa kwanini hamsemi haya kwa uwazi mnajificha kwenye mwavuli kuwa ni nchi ya ahadi.... Mpka wa nchi ya ahadi upo kwenye hesabu ila leo hii kuna maeneo hayapo ndani ya ramani ile ila wayahudi wanayakalia je ni haki hiyo??
Utumwa ulikuja baada ya kuja mfalme mwingine ambae hakutambua Yusuf aliifanyia nini misri huku akiogopa kutokana na wingi wao huenda wakaja kuwatawala ndio wakaanza kuwatumikisha kama watumwa na kusahau yote waliyotendewa na YusufWalifanywa watumwa irrespective walifikaje misri ndio najengea hoja kwamba ni kwanini unahalalisha laana ya Nuhu kwa canaan kwamba ndio ilisababisha canaan ije kutawaliwa na israel ila wana wa israel utumwani mbona hamsemi ni laana??huoni kuna undumilakuwili..... Je ina maana waafrika kwenda utumwani ulaya ni laana pia???
Kwa akili yako ni wayahudi feki ila ni kizazi cha kabila la Yuda waliozamia maeneo mbalimbali baada ya uharibifu wa mji wote wa yersalemu walioufanya warumi kutokana na waisrael kuwa waasi dhidi ya dola la Roma wakati huoNi nabii gani kawarudisha hawa wayahudi wazungu israel maana miaka yote ni manabii ndio huwarudisha wayahudi kwao ssa naomba unitajie ni nabii gani kawarudisha hawa wayahudi feki israel??
Akili zako ndio zimeishia hapa?Shida husomi biblia kijana nchi ya ahadi ipo misri hadi iraq ila mmeng'ang'ania tu palestina ya watu
Mwanzo 15
18 Siku ile BWANA akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati,
Kwanni hamuendi misri au iraq mnagombania nchi na wapalestina?? Why wakati nchi ya ahadi hipo hadi huko if at all NCHI YA AHADI ndio hoja yenu??
Nimesema waarabu wa kiislamu walivamia eneo ambalo sio LaoWwe umesema wapalestina ni waarab waliohamia tu ila unasahau wapalestin ni uzao wa Abraham pia kiufupi waisrael na wapalestina wote ni watoto wa baba mmoja hata utafiti wa DNA wa American journal of human genetics umethibitisha hilo sasa kwanni muwatenge hao kutoka urithi wa baba yao?? Nani alisema baraka ni za Yakobo peke ake hadi ajimilikishe ardhi??
Unasema "Hatutafuti history ya nyuma" sasa hio ardhi Abraham kapewa Leo? au na wewe unatumia reference za KIHISTORIA?Hatutafuti history ya nyuma tunachoangalia ni pale Ibrahim alipopewa ardhi Hiyo kuwa urithi wake huko mwanzo inawezekana kabisa ilikua yao lakini MUNGU wa Ibrahim alimpa Ibrahim tena kwa agano dhabiti lisilo wezwa kuvunjwa, Hivyo ndugu zenu wapelestina wanajisumbua tu.
Haaahaaaa kwahiyo urithi wa ahadi za Abraham ni ya kwenda mbinguni na sio ahadi zote?? Unaweza tupa mstari unaosema ahadi hazihusianishi hadi ardhi?? Kwanni unailisha maneno bibliaHiki ulicholeta hapa ni maandiko ya kumpwleka mtu mbinguni
Mimi nazungumzia ardhi ya wana wa Israel mkuu Acha kupindisha mada
Na hii ndio shida ya wafia dini hivi hujui kuna wapalestina wakristo na wayahudi pia?? Na je unafaham kuna raia wa israel ambao ni waislam kabisa ingawa sio waarabu??? Je ina maana hao waislam wakiisrael nao ni wajinga na wale wapalestina wakristo/wayahudi ndio sio wajinga???Sasa huo ni ujinga wa hao waarabu cha Mungu hakipingwi na ukikipinga hutashinda ndicho kilichotokea wakajikuta wanachukuliwa na maeneo yao mengine
Ni ujinga wao tu hawa waarabu wa kiislamu
Sasa nitajie nchi yeyote sahivi ambayo wakazi wa hapo walikuwepo miaka 2000 nyuma ntajie hata sehem moja...... Tanzania wote tulitoka pande zingine za afrika vivo hivyo hata ulaya sasa kwanni kwa palestina kuhamia ardhi nyingine kama tu ulimwengu mzima ulivyofanya iwe nongwa??Nimesema waarabu wa kiislamu walivamia eneo ambalo sio Lao
Ndio zimeishia hapo naomba uniambie kwanni wayahudi wanakaa kwenye 10% ya nchi ya ahadi ilihali mipaka ya kibiblia ya nchi ya ahadi ni kubwa zaidi?? Kwanni wasiende misri au syria ambayo kibiblia ndimo nchi ya ahadi kwanni walazimishe kugombanka ardhi na wapalestina?? Kwanni hawafuati mipaka ya kibiblia wanajiamulia wenyewe alafu wakristo mnashabikia tu bila kuhoji??Akili zako ndio zimeishia hapa?
Kabila ya yuda ndio ashkenazi??? Umesoma wapi hayo unayosema..... Wayahudi walishachangamana na hao waliorudi 90% ni ashkenazi jews na asili yao ni ukooo wa japhet sio shem hivyo hawana damu yeyote na wayahudi halisi..... Biblia iko wazi wayahudi halisi bado wako utumwani na watarudi nchi yao kipindi cha mpinga kristo na messiah Yesu akirudi ssa hao ashkenasizi toka lini wametoka ukoo wa shem ambao ndio Abraham alitokea humo? Hao walishachangamana na wazungu so sio wayahudi tena ni kitu kingine kabisaKwa akili yako ni wayahudi feki ila ni kizazi cha kabila la Yuda waliozamia maeneo mbalimbali baada ya uharibifu wa mji wote wa yersalemu walioufanya warumi kutokana na waisrael kuwa waasi dhidi ya dola la Roma wakati huo
Ha ha ha umenichekesha sana huo mstari wa mwisho eti "HABARI NYINGI JUU YAO ZINAPATIKANA KATIKA BIBLIA" ungeongezea nahii sentensi ya 'UKITAKA VICHEKESHO KAMA HIVI SOMA THREAD YANGU"Wafilisti walikuwa kabila la watu wa Ulaya ambao walivuka Bahari ya Kati na kisha kushindwa kuvamia Misri waliteka pwani ya Kanaani (1175 KK hivi) wakifaidika na silaha za chuma walizozitumia dhidi ya watu waliokuwa na zile za shaba tu, wakiwa wenyeji au Waisraeli.
Ingawa hawakuwa wengi, waliathiri sana nchi yao mpya, kiasi cha kuiachia jina la Palestina.
Habari nyingi juu yao zinapatikana katika Biblia.
Mkuu bora umekuja ... Nikiri tu kabla sijasoma thread yako ile kuhusu waisrael feki na mmi nilikuwa muumini wa propaganda kama hizi ila ulinifumbua macho na vile vitabu ulivyorecommend tusome vimenibadilisha kabisa mtazamo wangu kuhusu suala hili popote ulipo ubarikiweHa ha ha umenichekesha sana huo mstari wa mwisho eti "HABARI NYINGI JUU YAO ZINAPATIKANA KATIKA BIBLIA" ungeongezea nahii sentensi ya 'UKITAKA VICHEKESHO KAMA HIVI SOMA THREAD YANGU"
Hakuna biblia iliyoandika hayo uliyoyaandika ndiomaana umeshindwa hata kuweka kifungu kimoja umejiandikia tu mtu wa watu,umejiskia tu kuandika ili bando lako liishe kihalali
thanks a lot nimefarijika sana kusikia hivyo ila kuna wakristo wengi sana bado ni mashabiki wa israel wengi wao hawana uelewa tu hata mimi nilikuwa hivyo zamani sishangai sana jitahidi hata na wewe kwa nafasi yako kuelimisha na wengineMkuu bora umekuja ... Nikiri tu kabla sijasoma thread yako ile kuhusu waisrael feki na mmi nilikuwa muumini wa propaganda kama hizi ila ulinifumbua macho na vile vitabu ulivyorecommend tusome vimenibadilisha kabisa mtazamo wangu kuhusu suala hili popote ulipo ubarikiwe
Inaonyesha unamjibu kiulokole sana wakti mada umeileta jukwaani na hapa unatakiwa umjibu kwa majibu yanayoeleweka sasa ukisema ilikuwa ya MUNGU kila mtu anaelewa kila kitu ni cha MUNGU ila je ni ya Israelites au wapalestinaIlikuwa ya Mungu na waliyoishi huko walikuwa waperisi na wakanaan ndio walikuwa wenyeji wa ardhi hiyo
Huyo atakuwa mungu wa mama Yako Sio mungu wangu! Mungu wangu hawezi kubariki uwizi wa ardhi ya watuHata mimi nabariki kwasababu ni haki yao na ni urithi wao na ni ardhi yao na wanacho kitaka ni mipaka yao halali waliyopewa na MUNGU wao ambae ni MUNGU wako pia, na hawataacha wapelestina watakapo achia aridhi yao waliyopewa urithi, na ukae ukiamini kwamba anguko la palestina limekalibia.