Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Katika gazeti la Hoja (Ijumaa, Novemba 15 – 21, 2019), kuna makala ‘’Mufti Zubeir alivyoikarabati BAKWATA,'' iliyoandikwa na Hemed Kimwanga.
Makala hii ingepita kama makala nyingine yeyote ile endapo makala isingekuwa na mambo ambayo si kweli kuhusu kuundwa kwa BAKWATA.
Imekuwa kawaida sana hasa katika miaka ya hivi karibuni kwa kusemwa na kuandikwa mengi ambayo si ya kweli kuhusu asili ya BAKWATA.
Kimwanga anasema na hapa najitahidi kunukuu kwa uchache yale aliyoandika.
Kimwanga anamuhusisha Julius Nyerere kwa kuvunjwa EAMWS na kuundwa kwa BAKWATA.
Kimwanga anasema, ‘’...uongozi wa Mufti umekidhi matumaini yaliyokuwa moyoni mwa Mwalimu Julius Nyerere kwa kushauri mpaka kuiva kwa ndoto zake za kuiona Tanzania ikiwa na Baraza lake la Kiislam ambalo litakuwa huru katika mashirikiano na vyombo vingine vya mlengo huo ndani na nje ya nchi.’’
Kimwanga anaandika anasema East African Muslim Welfare Society ilikuwa, ‘’chini ya uongozi na utawala wa Prince Aga Khan wa Uingereza...’’
Kimwanga anaendelea, ‘’...kuna mantiki ndogo sana ambayo ilifanya serikali ya Mwalimu Nyerere kuivunja EAMWS.
Alitaka Waislam wa Tanzania wajiongoze wenyewe.
Siyo kupokea maagizo kutoka London kwa Prince Aga Khan kupitia Nairobi...’’
Historia ya BAKWATA hivi sasa inafanana na historia ya TANU kwani historia ya BAKWATA kama ilivyo historia ya TANU imekuwa ikijaza hofu kwa baadhi ya watu kiasi ya kupelekea kusemwa uongo mwingi kwa kuogopa ukweli.
Haikunichukua muda wakati naisoma makala hii kutambua kuwa Kimwanga anaandika kitu ambacho yeye kwa kweli kabisa hakijui.
Sheikh Mohamed Ayub alikuwa heshi kuwausia wanafunzi wake kwa kuwaaambia kuwa popote linapokuwa jambo kuhusu Uislam wafike ili ikiwa patakuwa na jambo ambalo haliko sawa watanlieleza kwa ukweli wake.
Sheikh Mohamed Ayub akiwaambia wanafunzi wake kuwa, "Semeni, msiposema, hayo wasemayo yasio kweli, yataonekana ni kweli."
Ingekuwa kweli Mwalimu Nyerere anataka Waislam wasipokee amri kutoka London basi angelianza na kanisa lake mwenyewe, Kanisa Katoliki na kuishughulikia Vatican iliyokuwa na uwakilishi Tanzania nzima kama ifuatavyo:
White Fathers (Tabora), Karema, Kigoma, Mbeya, Mwanza na Bukoba; Holy Ghost Fathers (Morogoro na Kilimanjaro), Benedictine Fathers (Peramiho na Ndanda) Capuchin Fathers (Dar es Salaam) Consolata Fathers (Iringa na Meru), Passionist Fathers (Dodoma) Pallotine Fathers (Mbulu), Maryknoll Fathers (Musoma), na Rosmillian Fathers (Iringa).
Kimwanga kaandika mengi ambayo sijaona kama iko haja ya kuyasemea hapa na ningependa kueleza kuwa historia ya BAKWATA inafahamika na sababu za kupigwa marufuku EAMWS pia zinafahamika.
EAMWS imevunjwa wakati tayari ilikuwa na mipango ya kuwainua Waislam katika elimu na walikuwa wanajenga Chuo Kikuu Cha Waislam mradi ambao ulikuwa unakwenda sambamba na ujenzi wa shule Tanzania nzima.
Hapo yalipo Makao Makuu ya BAKWATA pamoja na shule hiyo ya Kinondoni imejengwa na EAMWS.
Waislam hawakuwa na ujinga kuivunja EAMWS wakati inajenga Chuo Kikuu na shule kuwainua Waislam ambao ukoloni uliwanyima elimu na kutoa uwanja mpana kwa makanisa kuhodhi elimu ambayo waliitoa kwa ubaguzi kwa waumini wao kwa kipindi cha zaidi ya miaka 100.
Kimwanga asome historia ya kweli ya Tanganyika atafahamu kwa nini EAMWS ilivunjwa na sababu haikuwa kupokea amri kutoka kwa Prince Aga Khan wa Uingereza (sic).
Aga Khan hakuwa London bali akiishi Paris na mgogoro wa EAMWS ulipokuwa umepamba moto alijiuzulu nafasi yake ya Patron kutoka Paris.