Ukweli ni upi katika kuvunjwa kwa EAMWS na kuundwa BAKWATA?

Ukweli ni upi katika kuvunjwa kwa EAMWS na kuundwa BAKWATA?

Waislamu wenyewe si wapenzi wa elimu duniya.wengi hii si kipaumbele sana.
Nenda zanzibar kaangalie.lakini maeneo mengi aliyotawala mwarabu elimu ilizorota sana.mwarabu alifungua madrasa na misikiti.

Mzungu shule,hospital na makanisa.uislamu ni Dini ya Malalamiko dunia nzima tumeshawazoea nyie.shauri yenu mnakuwa na gubu kama mwanamke mgumba.

Katika gazeti la Hoja (Ijumaa, Novemba 15 – 21, 2019), kuna makala ‘’Mufti Zubeir alivyoikarabati BAKWATA,'' iliyoandikwa na Hemed Kimwanga.

Makala hii ingepita kama makala nyingine yeyote ile endapo makala isingekuwa na mambo ambayo si kweli kuhusu kuundwa kwa BAKWATA.

Imekuwa kawaida sana hasa katika miaka ya hivi karibuni kwa kusemwa na kuandikwa mengi ambayo si ya kweli kuhusu asili ya BAKWATA.

Kimwanga anasema na hapa najitahidi kunukuu kwa uchache yale aliyoandika.

Kimwanga anamuhusisha Julius Nyerere kwa kuvunjwa EAMWS na kuundwa kwa BAKWATA.

Kimwanga anasema, ‘’...uongozi wa Mufti umekidhi matumaini yaliyokuwa moyoni mwa Mwalimu Julius Nyerere kwa kushauri mpaka kuiva kwa ndoto zake za kuiona Tanzania ikiwa na Baraza lake la Kiislam ambalo litakuwa huru katika mashirikiano na vyombo vingine vya mlengo huo ndani na nje ya nchi.’’

Kimwanga anaandika anasema East African Muslim Welfare Society ilikuwa, ‘’chini ya uongozi na utawala wa Prince Aga Khan wa Uingereza...’’

Kimwanga anaendelea, ‘’...kuna mantiki ndogo sana ambayo ilifanya serikali ya Mwalimu Nyerere kuivunja EAMWS.

Alitaka Waislam wa Tanzania wajiongoze wenyewe.
Siyo kupokea maagizo kutoka London kwa Prince Aga Khan kupitia Nairobi...’’

Historia ya BAKWATA hivi sasa inafanana na historia ya TANU kwani historia ya BAKWATA kama ilivyo historia ya TANU imekuwa ikijaza hofu kwa baadhi ya watu kiasi ya kupelekea kusemwa uongo mwingi kwa kuogopa ukweli.

Haikunichukua muda wakati naisoma makala hii kutambua kuwa Kimwanga anaandika kitu ambacho yeye kwa kweli kabisa hakijui.

Sheikh Mohamed Ayub alikuwa heshi kuwausia wanafunzi wake kwa kuwaaambia kuwa popote linapokuwa jambo kuhusu Uislam wafike ili ikiwa patakuwa na jambo ambalo haliko sawa watanlieleza kwa ukweli wake.

Sheikh Mohamed Ayub akiwaambia wanafunzi wake kuwa, "Semeni, msiposema, hayo wasemayo yasio kweli, yataonekana ni kweli."

Ingekuwa kweli Mwalimu Nyerere anataka Waislam wasipokee amri kutoka London basi angelianza na kanisa lake mwenyewe, Kanisa Katoliki na kuishughulikia Vatican iliyokuwa na uwakilishi Tanzania nzima kama ifuatavyo:

White Fathers (Tabora), Karema, Kigoma, Mbeya, Mwanza na Bukoba; Holy Ghost Fathers (Morogoro na Kilimanjaro), Benedictine Fathers (Peramiho na Ndanda) Capuchin Fathers (Dar es Salaam) Consolata Fathers (Iringa na Meru), Passionist Fathers (Dodoma) Pallotine Fathers (Mbulu), Maryknoll Fathers (Musoma), na Rosmillian Fathers (Iringa).

Kimwanga kaandika mengi ambayo sijaona kama iko haja ya kuyasemea hapa na ningependa kueleza kuwa historia ya BAKWATA inafahamika na sababu za kupigwa marufuku EAMWS pia zinafahamika.

EAMWS imevunjwa wakati tayari ilikuwa na mipango ya kuwainua Waislam katika elimu na walikuwa wanajenga Chuo Kikuu Cha Waislam mradi ambao ulikuwa unakwenda sambamba na ujenzi wa shule Tanzania nzima.

Hapo yalipo Makao Makuu ya BAKWATA pamoja na shule hiyo ya Kinondoni imejengwa na EAMWS.

Waislam hawakuwa na ujinga kuivunja EAMWS wakati inajenga Chuo Kikuu na shule kuwainua Waislam ambao ukoloni uliwanyima elimu na kutoa uwanja mpana kwa makanisa kuhodhi elimu ambayo waliitoa kwa ubaguzi kwa waumini wao kwa kipindi cha zaidi ya miaka 100.

Kimwanga asome historia ya kweli ya Tanganyika atafahamu kwa nini EAMWS ilivunjwa na sababu haikuwa kupokea amri kutoka kwa Prince Aga Khan wa Uingereza (sic).

Aga Khan hakuwa London bali akiishi Paris na mgogoro wa EAMWS ulipokuwa umepamba moto alijiuzulu nafasi yake ya Patron kutoka Paris.
 
Mzee/ Bwana saidi unahangaika sana na siku hizi watu wamesha ku ignore. You cant change the past. You can change the present and future. Ukiwa mlalamishi sana mwishowe watu wanakuchoka.
 
Mzee wangu said pigania haqq katika kusema ukwel ata hayo unayoyasema yatasabibisha kukatisha uhai wako
 
Waislamu wenyewe si wapenzi wa elimu duniya.wengi hii si kipaumbele sana.
Nenda zanzibar kaangalie.lakini maeneo mengi aliyotawala mwarabu elimu ilizorota sana.mwarabu alifungua madrasa na misikiti.

Mzungu shule,hospital na makanisa.uislamu ni Dini ya Malalamiko dunia nzima tumeshawazoea nyie.shauri yenu mnakuwa na gubu kama mwanamke mgumba.

Ujinga sio kitu kizuri. Pole sana mkuu
 
Walisubiri nini kujenga awali?
Magu2016,
Hawakusubiri baada ya uhuru mwaka wa 1961 ndipo ikaitishwa Muslim Congress ya Kwanza mwaka wa 1962 na shule za msingi na sekondari zikaanza kujengwa.

Au unakusudia ujenzi wa shule na Chuo Kikuu ungefanyika wakati wa kupigania uhuru?
 
Laki...
Chuki na uchochezi katika kusema kweli?

Unataka vizazi vijavyo viamini kuwa Waislam walikuwa watu wapumbavu kiasi waliivunja EAMWS wakati wanajenga shule na Chuo Kikuu?

Tuna wajibu wa kueleza ukweli na kupinga proaganda za watu kama Kimwanga.
Unajua kuwa hadi leo historia ya Auschwitz bado inasomeshwa?
Kwani Bakwata ya leo haiwezi kujenga Vyuo Vikuu na Shule nchi nzima?
 
Mzee/ Bwana saidi unahangaika sana na siku hizi watu wamesha ku ignore. You cant change the past. You can change the present and future. Ukiwa mlalamishi sana mwishowe watu wanakuchoka.
Komeo...
Sidhani kama mimi ni mlalamishi kwa kuwa hapa nilipo sibughudhi mtu wala simtukani mtu.
Ninachofanya ni kusoemsha historia ya uhuru wa Tanganyika ambayo ilikuwa imepotea.

Wala hii haijawa na nia ya kubadilisha ''past'' chembelecho.

Nimeweza kupitia maandishi yangu ''papers'' na vitabu nilivyoandika, kuibadili historia ya Tanganyika hasa kipindi cha ''nationalist politics.''

Nimekuandikieni hapa historia za wazalendo na matukio ya kupambana na ukoloni ambayo hamkuwa mnayajua.

Wala hakuna anaenichoka.
Kila watu wakijua nimefika barzani wanajazana kunisikiliza.

Wanakuja kunisikiliza kwa kuwa wanaelimika na wakati huo huo wanaburudika.
Hivi sasa nashindwa kumudu kujibu ''msgs'' ninazopokea na mialiko ya kuzungumza.

Hii si dalili ya mtu aliyechusha.
Naona kama vile unaghadhibishwa na kalamu yangu hayakupendezi haya ninayoandika.
 
Waislamu wenyewe si wapenzi wa elimu duniya.wengi hii si kipaumbele sana.
Nenda zanzibar kaangalie.lakini maeneo mengi aliyotawala mwarabu elimu ilizorota sana.mwarabu alifungua madrasa na misikiti.

Mzungu shule,hospital na makanisa.uislamu ni Dini ya Malalamiko dunia nzima tumeshawazoea nyie.shauri yenu mnakuwa na gubu kama mwanamke mgumba.
Komeo...
Kuhusu Zanzibar inaelekea huijui historia ya visiwa hivyo na matokeo yake ndiyo haya unayosema kidogo umenifanya nicheke.

Kuhusu madras.
Elimu imeingizwa Pwani ya Afrika ya Mashariki na kuja kwa Uislam.

Nimeandika paper mbili kuhusu somo hil kwa hiyo nayajua haya kukushinda:
  1. The Question of Muslim Stagnation in Education in Tanzania - A Muslim Riddle (Paper presented at the Conference of the Global World of the Swahili Intercultural Dialogue on the Indian Ocean Zanzibar, February 20 - 23, 2003).
  2. Islamic Education and Intellectualism in Eastern Africa ‘Themes from the Pulpit in Tanganyika (Tanzania Mainland) 1800 – 2000’ (Paper presented at International Symposium on Islamic Civilisation in Eastern Africa Kampala, Uganda organised by the Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA), Istanbul and the Islamic University in Uganda, Mbale December 15th – 17th 2003).
Nakushauri soma kitabu cha Ali Muhsin Barwani, ''Conflict and Harmony in Zanzibar,'' kitabu hiki kitakusaidia kuijua historia ya Zanzibar hasa katika elimu.

1573931481367.png

Kushoto ni Sheikh Ali Muhsin Barwani na Mwandishi Muscat 1999
Huna unalojua katika somo hili.

Johann Ludwig Krapf kafika kwa Chief Kimweri mwaka wa 1848 kamkuta anajua kusoma na kuandika yeye na watoto wake wote wakitumia irabu za Kiarabu.

Waislam ndiyo watu wa kwanza pwani ya Afrika ya Mashariki kujua zile R 3, yaani Reading, Writing and Arithmetic.

Elimu haikuja na wamishionari kama mnavyofundishwa.

Nia yangu ni kukufahamisha kuwa haya mambo nayajua usidhani kama niko hapa kubabaisha.
 
Hata Mimi babu yangu Alichangia kuleta uhuru hata kabla ya hao akina Sykse...tena ndie alipelekea kuwepo na hamasa ya kupigania haki za watu weusi...je na Mimi nijitape kuwa najua historia ya uhuru wetu kuliko wewe
 
Johann Ludwig Krapf kafika kwa Chief Kimweri mwaka wa 1848 kamkuta anajua kusoma na kuandika yeye na watoto wake wote wakitumia irabu za Kiarabu.

Waislam ndiyo watu wa kwanza pwani ya Afrika ya Mashariki kujua zile R 3, yaani Reading, Writing and Arithmetic.
Hivi nikijua kusoma kwasababu ya elimu ya waingereza nakuwa mkristo??!!....hiv kuongea kiarabu ni kuwa Muislamu
 
Mzee/ Bwana saidi unahangaika sana na siku hizi watu wamesha ku ignore. You cant change the past. You can change the present and future. Ukiwa mlalamishi sana mwishowe watu wanakuchoka.
Yes, the real strong history will never be changed by weak narrations!!!!
 
Yes, the real strong history will never be changed by weak narrations!!!!
King...
Kipi kipimo chako kuwa hii historia ni ya maana au hii ni puruzai chembelecho ''weak narrations?''

Kwa miaka mingi historia hii haikujulikana.

Nini kilitokea baada ya vyuo vikuu Ulaya na Marekani kujua kuwa kipo kitabu kipya kilichoongeza elimu katika historia ya Tanzania?

Kitu cha kwanza kilikuwa ni ''book review'' zilizofanywa na mabingwa wa African History - John Iliffe, James Brennan na Jonathon Glassman na kuchapwa katika Cambridge Journal of African History (1998/99).

Naamini unaijua Cambridge University.

Mwandishi kutiwa katika mradi wa historia kwa shule za msingi na Oxford University Press, Nairobi na wakachapa kitabu changu kimoja, ''The Torch on Kilimanjaro,'' (2007)

Kuchapwa kitabu changu kingine kuhusu Uchaguzi wa Kura Tatu 1958, ''Uamuzi wa Busara,'' Abantu, (2008).

Mialiko University of Iowa, Iowa City, USA, Northwestern University, Chicago, Illinois, USA na Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin (2011).

Contributing author Dictionary of African Biography (DAB), Oxford University Press 2011, New York.

Huu ulikuwa mradi wa Harvard na Oxford University Press, New York.
Naami na hawa unawafahamu.

Yako mengi lakini haya nadhani yanakutosha.
Can you by any stretch of imagination consider the above as weak?
 
Attachments

  • THE TORCH ON KILIMANJARO.jpg
    THE TORCH ON KILIMANJARO.jpg
    5.5 KB · Views: 2
  • NORTHWESTERN UNIVERSITY EVANSTON CHICAGO.JPG
    NORTHWESTERN UNIVERSITY EVANSTON CHICAGO.JPG
    18.4 KB · Views: 2
  • SYKES BOOK ALL EDITIONS.jpg
    SYKES BOOK ALL EDITIONS.jpg
    54.1 KB · Views: 2
  • UAMUZI WA BUSARA.JPG
    UAMUZI WA BUSARA.JPG
    22 KB · Views: 3
Hata Mimi babu yangu Alichangia kuleta uhuru hata kabla ya hao akina Sykse...tena ndie alipelekea kuwepo na hamasa ya kupigania haki za watu weusi...je na Mimi nijitape kuwa najua historia ya uhuru wetu kuliko wewe
King...
Mimi sijitapi ila naeleza historia ya wazee wangu historia ambayo ilikuwa imepotea.
 
all in all waislam bado mpo na mashallah some of you mmebarikiwa chochote kitu inashindikana nini hayo malengo ya eamws mkayabeba nakuyatekeleza under bakwata or without bakwata kuliko kulalamika na kulaumu ambako hakusaidii kitu. sheikh nurdin kishki anafanya na anafanikiwa ila wengineo ni walalamikaji tu huku wakisubiria makontena ya tende toka saudia
 
Young...
Hapa mimi nasomesha historia ya kweli sielewi hii, "kulalamika," wewe umeitoa wapi.
Tufanye mjadala wa adabu na staha.

Hii lugha ya "makontena ya tende," itatuharibia huu mjadala.
Mimi si mtu wa lugha za kejeli.
 
King...
Kipi kipimo chako kuwa hii historia ni ya maana au hii ni puruzai chembelecho ''weak narrations?''

Kwa miaka mingi historia hii haikujulikana.

Nini kilitokea baada ya vyuo vikuu Ulaya na Marekani kujua kuwa kipo kitabu kipya kilichoongeza elimu katika historia ya Tanzania?

Kitu cha kwanza kilikuwa ni ''book review'' zilizofanywa na mabingwa wa African History - John Iliffe, James Brennan na Jonathon Glassman na kuchapwa katika Cambridge Journal of African History (1998/99).

Naamini unaijua Cambridge University.

Mwandishi kutiwa katika maradi wa historia kwa shule za msingi na Oxford University Press, Nairobi na wakachapa kitabu changu kimoja, ''The Torch on Kilimanjaro,'' (2007)

Kuchapwa kitabu changu kingine kuhusu Uchaguzi wa Kura Tatu 1958, ''Uamuzi wa Busara,'' Abantu, (2008).

Mialiko University of Iowa, Iowa City, USA, Northwestern University, Chicago, Illinois, USA na Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin (2011).

Contributing author Dictionary of African Biography (DAB), Oxford University Press 2011, New York.

Huu ulikuwa mradi wa Harvard na Oxford University Press, New York.
Naami na hawa unawafahamu.

Yako mengi lakini haya nadhani yanakutosha.

Najaribu kupitia hapa "general history of Africa " volume II by UNESCO. Hasa katika hii sehemu ya Africa Nationalism na independence. Hiyo michango ya watu kutoka taasisi mbalimbali labda inatambulika kama Minor reasons za ukuaji wa Nationalism na vichocheo tu vya uhuru wa nchi hzo ikiwemo Tanganyika na Zanzibar.

Sio kama ndio sababu pekee na kuu kiasi hicho ukisemacho wewe Mzee wangu... sababu za kuanzishwa kwa TAA na baadae TANU hakutazamwi tu kwa mchango wa wazee waliokuwepo ndani ya mipango hyo Bali nguvu/sababu za nje huzingatiwa sana.

Sasa kama wakija watu wa historia ya kanisa hapa Tanzania kipind cha uhuru nao watadai et nao ni wamuhimu kuliko waislamu...watasema sjui Independence Churchs, role za Christian education,...tukiweka msukumo huo ambao Mzee wangu unataka tutaanza kusimuliana minor history nakuacha HISTORIA yenyewe. Je nikwer kwamba kwa asilimia kubwa uhuru wa nchi zetu ulitokana na juhudi zetu nasio mabadiliko ya kiuchumi na Siasa za dunia. nadhani hii ndio historia mengine hayo yamekuja kaingia ndani ya sababu hii kuu.
 
King...
Mimi sijitapi ila naeleza historia ya wazee wangu historia ambayo ilikuwa imepotea.
Sawa nimekuelewa Mzee MS, na sio kwamba nakupinga, coz ni vyema kutunza historia za wazee wetu. Tatizo ni kule kujaribu kufanya wengine hawajui juu ya historia yetu na kuwa hao tunao watambua kuwa mstari wa mbele katika kujenga historia ya nchi yetu sio kitu mbele ya wazee wako hao. Najaribu tu kufikir kwa kina kabla ya hao wazee or wakati na baada, je kulikuwa hakuna wengine Kabsaa waliotoa mchango zaid yao kwa kiwango hicho unachotuaminisha Mzee wetu MS.
 
Back
Top Bottom