Ukweli ni upi katika kuvunjwa kwa EAMWS na kuundwa BAKWATA?

Ukweli ni upi katika kuvunjwa kwa EAMWS na kuundwa BAKWATA?

Nyaru...
Waislam waliathirika zaidi kwa kuwa mfumo wa utawala uliokuwapo uliwatenga katika elimu.

Serikali ilitoa "grant in aid," kwa makanisa kwa ajili ya elimu na shule hizi zikawabagua Waislam.

Ili kusoma ilibidi mwanafunzi abatizwe.
Hili lilikuwa sharti gumu sana.

Kwa ujumla ikawa kama vile elimu imekabidhiwa kwa kanisa.

Shule chache zilizojengwa na Waislam zilikataliwa kupewa msaada huu.

Ndiyo maana ikawa Waislam wako mbele katika kupigania uhuru kuuondoa ukoloni.

Sent using Jamii Forums mobile app

Ikumbukwe kabla ya hapo walitangulia Waarabu kwanza! Walihasi watu hasa!


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ikumbukwe kabla ya hapo walitangulia Waarabu kwanza! Walihasi watu hasa!


Sent from my iPhone using JamiiForums
Dongo...
Waarabu walitangulia na ndiyo walioleta elimu pwani yote ya Afrika ya Mashariki kupitia madrasa.

Waislam wakawa ndiyo watu wa kwanza kupata zile R3 yaani Reading, Writing and Arithmetic zikitumika herufi za Kiarabu.

Mmeshionari Johann Krapf alipofika Vuga kwa Chifu Kimweri mwaka wa 1848 alimkuta anajua kusoma na kuandika yeye na wanae.

Wamishionari hawakupendezewa na haya maendeleo waliyoyakuta na wakishirikiana na wakoloni matumizi ya hati za Kiarabu zikapigwa marufuku ikawa umma wa Waislam pwani yote ya Afrika ya Mashariki ghafla wakageuzwa kuwa watu wasiojua kusoma wala kuandika.

Historia ya elimu haikuanza na kuja kwa Ukristo huku kwetu ingawa historia ambayo wanayoifundisha ni kuwa Kanisa ndilo lililoleta elimu.

Naamini sasa umeelewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ikumbukwe kabla ya hapo walitangulia Waarabu kwanza! Walihasi watu hasa!


Sent from my iPhone using JamiiForums

Na wewe ulitokana na kizazi cha waliohasiwa pamoja na Watanzania wasiopungua million 50 hivi sasa?

Kwa idadi hiyo na uwepo wako leo hii, ni wazi kuwa waliofanya hiyo kazi ya kuwahasi babu zako hawakufanya kazi nzuri au siyo?
 
Back
Top Bottom