Interesting. Wamedhulumiwa nini? Maana dhuluma ni kitu kiovu kabisa
Ndahani,
Bahati mbaya sana kuwa kitabu cha Prof. Hamza Mustafa Njozi, ''Mwembechai Killings...'' (2002) kilipigwa marufuku na serikali.
Kitabu kile Njozi alikiandika baada ya Rais Mkapa kusomewa risala na Waislam Ukumbi wa Diamond mara tu alipouchukua urais wa nchi.
Risala ile iliyosomwa na Ramadhani Madabida ilieleza dhulma wanazofanyiwa Waislam kwa miaka mingi.
Rais Mkapa katika kujibu ile risala akasema Waislam walete ushahidi wa kisayansi.
Ndipo Njozi akaandika kitabu kile.
Yaliyomo ndani ya kitabu kile hakika ni mazito na uzito wake ni kuwa ikiwa yale yataanikwa hadharani yatabadili historia ya nchi yetu yote.
Sijui waliohusika na njama hizo maana wametajwa kwa majina Waislam watawatazamaje na wao wenyewe kwa walio hai watajisikiaje katika jamii.
Kwa viongozi ambao wameshatangulia mbele ya haki nini itakuwa ''legacy,'' yao katika nchi hii?
Ukweli ni kuwa majina mazuri na sifa tulizowapa kama wazalendo itabidi zote zifutike.
Sikushangaa kitabu kilipopigwa marufuku.
Ndahani,
Toka ulipouliza hilo swali nani kadhulumiwa mimi nilikaa kimya sikutaka kukujibu kwa sababu nauogopa ukweli huu.
Lakini ukarejea tena baada ya kujibiwa.
Ndipo nikaona nami nitie neno ili ujue huenda unauliza kwa dhati hujui kitu unataka kujua.