Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #101
Abunuwasi,Bado kuna idadi kubwa tu ya wale ambao hadi leo hawatambui Baraza.
Nilimuuliza mmoja wa viongozi wa BAKWATA kama ipo haja ya kusheherekea miaka 50 ya BAKWATA nikamwambia kuwa kwa kufanya hivyo watakuwa wanasheherekea dhulma.
Nimefuatilia katika TV sherehe yote hadi kutoa vyeti kwa waasisi wa BAKWATA ingawa viongozi wakubwa waliohusika na mgogoro ule sikusikia hata majina yao kutajwa.
Nilijua kwa nini hawawezi kuwataja.
Mmoja katika hao walioadhnimishwa alimfanyia uadui mkubwa Sheikh Hassan bin Ameir kupelekea Sheikh Hassan kukamatwa usiku wa manane kurejeshwa Zanzibar na kupigwa marufuku asitie mguu wake Bara.
Lakini liko moja katika sherehe ile lilinifurahisha na kunitia furaha upeo wa furaha.
BAKWATA hawakuwa na ujasiri wa kutaja jina la Sheikh Hassan bin Ameir.
Haiwezekani ikatajwa historia ya Waislam Tanzania na ukanda huu wa Pwani ya Afrika ya Mashariki, Malawi, Congo, Rwanda na Burundi asitajwe Sheikh Hassan bin Ameir.
Achilia mbali mchango wake katika kupigania uhuru wa Tanganyika na historia yake katika TANU.
Leo hata katika majumba yetu tukiwarehemu waliotangulia jina la kwanza kutajwa ni la Sheikh Hassan bin Ameir.
Sheikh Hassan katuachia historia kubwa ya kutukuka.
'Nilipokea ujumbe huu kutoka Burundi baada ya msomaji mmoja kunisoma nikimtaja Sheikh Hassan bin Ameir:
"Si kwamba Waswahili wa Burundi zama za ukoloni walijibagua na kujitenga mbali na elimu.
La hasha!
Waswahili walikuwa na elimu ya kutosha zama hizo ukiwalinganisha na makabila mengine.
Walikuwa wanatumia herufi za Kiarabu (alphabet arabe) kwa kuandika Kiswahili na walikuwa wanajuwa kupiga hesabu (calcul).
Walikuwa na shule zao ambazo ni madrasa.
Walikuwa wakiandika tungo mbalimbali ikiwemo mashairi.
Walitengwa kwenye elimu kwa maksudi na ukoloni.
Hasa ukoloni wa Wabeleji ambao uliwanyima wazi Waswahili elimu mpya ya Kimagharibi na kuwapa Kanisa Katoliki umiliki pekee (monopole) wa kuitoa elimu katika nchi.
Waswahili walilalamika zama hizo wala hawakulala.
Waliunda chini ya uongozi wa marehemu Sheikh Amrani Juma taasisi iitwayo ASMARU (Association Scolaire Musulmane du Ruanda-Urundi) yaani Taasisi ya Kielimu ya Waislam wa Ruanda-Urundi).
Na walipeleka malalamiko yao mbele ya Serikali na kuwambia nyiye ni wabaguzi, tunaomba na sisi tupewe ruzuku (subventions) ili tujenge shule zetu na tuwalipe walimu wetu waweze kuwafundisha watoto zetu bila kubadiliwa dini yao ya Uislam na Kanisa ambalo ndio njia lilitumia kubadili imani za watoto baada kuona limeshindwa kuwabadili watu wazima.
Ruzuku hiyo iliombwa kwa sababu pesa hizo ni michango ya raia wanaipa Serikali kwa kulipa kodi mbalimbali, na Waswahili walikuwa ni walipa kodi wakubwa.
Hata na hivyo Serikali ya kikoloni ilikataa kuwapa chochote Waswahili, lakini la kushangaza ikakubali kuwapa Waprotestanti ambao pia walilalamika.
Waprotestanti walipewa ruzuku ya 50,000 F (Franka elfu khamsini) ambazo zilikuwa nyingi sana kwa zama hizo.
Hatimaye Waswahili wakapiganisha huku na kule na kupata msaada toka kwa ndugu zao Watanganyika na kujenga shule moja ya watoto wao ambayo ni Jumuiya (Jina la Jumuiyatul Islamiyya fii Tanganyika).
Hiyo shule ipo hadi leo Barabara ya Nane na ya Tisa Buyenzi.
Alikuja kutoka Tanganyika Mufti Hassan bin Amir kuzindua shule hiyo. #WazeeWetuHawakuwaWazembe Mungu awarehemu.''