Statarea,
Inawezekana ni kwa ajili ya labda umri wako, kiwango cha elimu, malezi na mambo mengine mengi tu "exposure," nk. nk.
Nakueleza haya nikiamini mimi nimekupita kwa umri mimi ni mzee kwa hiyo utaniheshimu kwa uzee wangu.
Naamini umefanya kwa kuwa hujui na kama hujui unastahili kusamehewa.
Kwetu sisi Waislam Mtume Muhammad SAW hafanyiwi utani.
Usimtaje Mtume SAW kwa utani.
Hiyo ni kufru kubwa sana ambayo hakuna Muislam yeyote duniani anaweza kustahamili.
Naamini umeelewa na hutorudia tena jambo hili.
Nikejeli mimi unavyopenda lakini weka heshima kwa Mtume Wetu SAW.
Statarea,
Hi si ''historia yangu,'' wala si ''historia ya ajabu ajabu.''
''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism,'' Minerva Press London 1998 sasa ni kitabu kinachotambulika kama ''corrective history,'' na ni kitabu muhimu katika ''political history'' ya Tanganyika.
Kitabu kimesahihisha historia rasmi iliyokuwa inatakiwa itambulike.
Publishers hapa nyumbani waliuogopa mswada wangu kwa kuwa ulikuwa unapingana moja kwa moja na historia iliyokuwapo lakini ndiyo watu waliokuwa wanaijua na kuiamini.
Baada ya kutoka kitabu changu wasomi wakataka kujua kama kweli kulikuwa na ''Muslim Struggle,'' Tanganyika iliyopambana na ukoloni wa Waingereza.
Naam kitabu kimeeleza hilo.
Kitabu kimeleta elimu mpya kwa ushahidi usiokuwa na shaka kuwa historia ya Tanganyika ilikuwa imepindishwa kwa kukusudia kutokana na hofu ya Uislam baada ya uhuru kwani kabla ya uhuru Uislam katika kupambana na ukoloni haukuwa tishio.
Hii ndiyo historia mabingwa wa African History duniani, Northwestern University, walinialika nikaizungumze chuoni kwao.
Naam nilizungumza katika Ukumbi wa Eduardo Mondlane, Evanston, Chicago.
Hii sasa si ''historia yangu'' wala si historia ya ''ajabu ajabu.''
Hii ni historia kama ilivyotakiwa iwe,
Nathubutu kusema kuwa histroria ya ajabu ajabu ni hiyo iliyoandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni (1981) iliyomkwepa Abdul Sykes, Ally Sykes, Kleist Sykes, Hamza Mwapachu, Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Suleiman Takadir, Sheikh Yusuf Badi, Sheikh Rashid Sembe, Zubeir Mtemvu, Yusuf Olotu, Ali Migeyo, Iddi Faizi Mafungo, Paul Bomani, Bilal Rehani Waikela, Omari Suleiman, Rashid Ali Meli, Schneider Abdillah Plantan, Dr. Michael Lugazia, Dr. Luciano Tsere, Dr. Joseph Mutahangarwa, Saadani Abdu Kandoro, Dr. Vedasto Kyaruzi, Bi, Tatu bint Mzee, Bi. Chiku bint Said Kisusa, Bi. Titi Mohamed, Oscar Kambona, Bi. Halima Selengia, Bi. Amina Kinabo, Bi. Fatma bint Matola, Bi. Zarula bint Abdulrahman na haya ni majina machache katika orodha ya wapigania uhuru wengi ambayo mimi nimeyarejesha katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.