Ukweli ni upi katika kuvunjwa kwa EAMWS na kuundwa BAKWATA?

Ukweli ni upi katika kuvunjwa kwa EAMWS na kuundwa BAKWATA?

Na jaribu kupitia hapa "general history of Africa " volume II by UNESCO. Hasa katika hii sehem ya Africa Nationalism na independence. Hiyo michango ya watu kutoka taasis mbalimbali labda inatambulika kama Minor reasons za ukuaji wa Nationalism na vichocheo tu vya uhuru wa nchi hzo ikiwemo Tanganyika na Zanzibar. Sio kama ndio sababu pekee na kuu kias hicho ukisemacho wewe Mzee wangu... sababu za kuanzishwa kwa TAA na baadae TANU hakutazamwi tu kwa mchango wa wazee waliokuwepo ndani ya mipango hyo Bali nguvu/sababu za nje huzingatiwa sana.

Sasa kama wakija watu wa historia ya kanisa hapa Tanzania kipind cha uhuru nao watadai et nao ni wamuhimu kuliko waislamu...watasema sjui Independence Churchs, role za christian education,...tukiweka msukumo huo ambao Mzee wangu unataka tutaanza kusimuliana minor history nakuacha HISTORIA yenyewe. Je nikwer kwamba kwa asilimia kubwa uhuru wa nchi zetu ulitokana na juhudi zetu nasio mabadiliko ya kiuchumi na Siasa za dunia. nadhani hii ndio historia mengine hayo yamekuja kaingia ndani ya sababu hii kuu

king joniva

Hakuna tatizo ndugu yangu mimi nimeandika historia ya wazee wangu unaiamini sawa la unaona haina umuhimu pia si ubaya.

Muhimu kwangu ni kuwa historia ya wazee wangu iliyokuwa imefutwa nimeirejesha na sasa inafahamika.

Unataka kubakia na historia ile iliyoandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni huo ni uamuzi wako sina uwezo wa kukuzuia.

Amini kile akili yako inakuelekeza.
 
Utaongea weee lakini watz hawana mpango na wewe wana ku ignore sana mkuu pole!!

Sema wewe, siyo Watanzania. Mimi simui-gnore.
Mzee Said anatufundisha mambo mengi sana. Binafsi nimeanza kuamini wanaoumia na anayoyasema mzee wetu ni Wakristo waliojimwambafai huko nyuma na sasa mzee anawaweka uchi.

I think we need a new revolution.
 
@king joniva,

Hakuna tatizo ndugu yangu mimi nimeandika historia ya wazee wangu unaiamini sawa la unaona haina umuhimu pia si ubaya.
Muhimu kwangu ni kuwa historia ya wazee wangu iliyokuwa imefutwa nimeirejesha na sasa inafahamika.
Unataka kubakia na historia ile iliyoandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni huo ni umuzi wako sina uwezo wa kukuzuia.
Amini kile akili yako inakuelekeza.

Sio kwamba siamini ndani ya historia hizi za wazee wetu, nikifanya hivyo means sintakuja kuamin hata historia kizazi changu pia. Tatizo unatusimulia historia Ambayo imekuwa "historia jumuishi" tangu ilipoanza kuzungumzia juu ya Taifa letu, katika hila sinashaka kukosolewa hakukwepeki maana kila mtu atamleta Mzee / wazee wake kuwa ndio wajenzi wakuu wa nguzo za nchi yetu kuliko Nyerere, Tewa Said Tewa, Kambona, Saadan Kandoro, familia ya Sykse n.k...hivyo kulinda mpasuko wa historia yetu ni afadhar tubaki kutumia Fact za historia zinazo kubarika, hzo nyingine zitakuwa ni sehem tu ya historia yetu.

Kuna post yako Moja nimeisoma kuwa historia yetu imepindishwa thus why najaribu ku-argue. Sorry kama nakosea M.S
 
Sio kwamba siamini ndani ya historia hizi za wazee wetu, nikifanya hivyo means sintakuja kuamin hata historia kizazi changu pia. Tatizo unatusimulia historia Ambayo imekuwa "historia jumuishi" tangu ilipoanza kuzungumzia juu ya Taifa letu, katika hila sinashaka kukosolewa hakukwepeki maana kila mtu atamleta Mzee / wazee wake kuwa ndio wajenzi wakuu wa nguzo za nchi yetu kuliko Nyerere, tewa said tewa, Kambona, saadan kandoro, familia ya Sykse n.k...hivyo kulinda mpasuko wa historia yetu ni afadhar tubaki kutumia Fact za historia zinazo kubarika, hzo nyingine zitakuwa ni sehem tu ya historia yetu.
Kuna post yako Moja nimeisoma kuwa historia yetu imepindishwa thus why najaribu ku-argue
Sorry kama nakosea M.S

King...
Mimi nimeandika historia baada ya kufanya utafiti ulionichukua muda mrefu sana na hapa achilia mbali kuwa nimelelewa ndani ya historia hii na kusikia mengi yakihadithiwa katika mazugumzo ya kila siku..

Nilipoanza utafiti kwanza nimesoma nyaraka zote zilizokuwa mikononi mwa Sykes family ambazo zinakwenda nyuma hadi miaka ya 1920s.

Ukimtoa John Iliffe hakuna mtafiti ambae amepata kuzisoma nyaraza hizi hadi hii leo.

Nimemsoma Herman von Wissman akiwa kijijini Kwa Likunyi, Imhambane Mozambique alipokwenda kutafuta askari mamluki aliokujanao hadi Pangani kuanza vita na Bushiri bin Salim Al Harith kisha na Mtwa Mkwawa.

Katika askari hawa Sykes Mbuwane akiwa mmoja katika hilo jeshi.

Anaeeleza historia hii ni Chief Mohosh ambae ndiye alikuwa kiongozi wa jeshi hili baadae baada ya vita vile akawa mkuu wa Germany Constabulary Tanganyika lakini sasa akiwa anafahamika kama Affande Plantan.

Historia hii Affande Plantan ndiyo aliyomweleza Kleist Sykes mtoto wake wa kulea baada ya kifo cha baba yake Sykes Mbuwane Mto Ruaha wakati wakirejea Bagamoyo baada ya vita na Mkwawa.

Historia hii Kleist Sykes akaiandika katika mswada wa kitabu kabla hajafa nwaka wa 1949 na ilichapwa kama ''seminar paper,'' (1968) na mjukuu wake Aisha ''Daisy'' Sykes na utaipata Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, East Africana na pia ni sura katika kitabu alichohariri John Ikiffe, ''Modern Tanzanians,'' (1973).

Haya nimeyaeleza hapa mara nyingi.

Nimefika hadi Pangani na kuangalia bandari walikoshukia askari hao na kupiga picha sehemu nyingi za mji kusukuma fikra zangu.

Nimemsoma Kleist Sykes anavyoeleza kukutana kwake na Dr. Kwegyr Aggrey 1924 mtu aliyemshajiisha kuunda African Association.

Nimezungumza na baba yangu aliyekua katika mtaa wa Kipata na Abdul Sykes anihadithie yote anayokumbuka kuona katika 1950s wakati Abdul anaanza harakati za kuunda TANU nk.nk.

Baba yangu ndiye aliyenieleza kuwa yeye kamjulia Nyerere nyumbani kwa Abdul Sykes mwaka wa 1952 na akijua kuwa Abdul alikuwa na mpango wa kuunda chama cha siasa na hili kaelezwa na Abdul mwenyewe siku alipomtambulisha kwa Nyerere.

Sasa kusema ati atakuja mtu kusema kuwa na yeye wazee wake waliunda chama cha siasa sawa hakuna wa kumkataza lakini chama hicho hakitakuwa TANU kwani muasisi wa TANU anafahamika kwa ushahidi.

Ndiyo hapo nilipokuwa nalichangamsha darasa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam na kuwashangaza hadi walimu wangu kwa yale niliyokuwa nayajua na hii ndiyo sababu kitabu cha maisha ya Abdul Sykes kimeweza kubadili historia nzima ya Mwalimu Nyerere na historia ya uhuru wa Tanganyika.

Bahati mbaya sana historia hii hamuipendi inawachoma moyo mnapenda tubaki na historia inayomtaja Nyerere peke yake kuwa ndiye muasisi wa TANU na harakati za kudai uhuru 1954.

Katika picha hiyo hapo chini yuko Kleist Sykes na Ramadhani Mashado Plantan wa pili kushoto katika hao waliokaa chini na hapo ndipo ilipokuja kuzaliwa TANU na Mashado Plantan akiwa mmoja wa wazalendo waliohudhuria mkutano wa kwanza wa TANU August 1954.

AFRICAN ASSOCIATION OFFICE 1933.jpg
 
King...
Mimi nimeandika historia baada ya kufanya utafiti ulionichukua muda mrefu sana na hapa achilia mbali kuwa nimelelewa ndani ya historia hii na kusikia mengi yakihadithiwa katika mazugumzo ya kila siku..

Nilipoanza utafiti kwanza nimesoma nyaraka zote zilizokuwa mikononi mwa Sykes family ambazo zinakwenda nyuma hadi miaka ya 1920s.

Ukimtoa John Iliffe hakuna mtafiti ambae amepata kuzisoma nyaraza hizi hadi hii leo.

Nimemsoma Herman von Wissman akiwa kijijini Kwa Likunyi, Imhambane Mozambique alipokwenda kutafuta askari mamluki aliokujanao hadi Pangani kuanza vita na Bushiri bin Salim Al Harith kisha na Mtwa Mkwawa.

Katika askari hawa Sykes Mbuwane akiwa mmoja katika hilo jeshi.

Anaeeleza historia hii ni Chief Mohosh ambae ndiye alikuwa kiongozi wa jeshi hili baadae baada ya vita vile akawa mkuu wa Germany Constabulary Tanganyika lakini sasa akiwa anafahamika kama Affande Plantan.

Historia hii Affande Plantan ndiyo aliyomweleza Kleist Sykes mtoto wake wa kulea baada ya kif cha baba yake Sykes Mbuwane Mto Ruaha wakati wakirejea Bagamoyo baada ya vita na Mkwawa.

Historia hii Kleist Sykes akaiandika katika mswada wa kitabu kabla hajafa nwaka wa 1949 na ilichapwa kama ''seminar paper,'' (1968) na mjukuu wake Aisha ''Daisy'' Sykes na utaipata Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, East Africana na pia ni sura katika kitabu alichohariri John Ikiffe, ''Modern Tanzanians,'' (1973).

Haya nimeyaeleza hapa mara nyingi.

Nimefika hadi Pangani na kuangalia bandari walikoshukia askari hao na kupiga picha sehemu nyingi za mji kusukuma fikra zangu.

Nimemsoma Kleist Sykes anavyoeleza kukutana kwake na Dr. Kwegyr Aggrey 1924 mtu aliyemshajiisha kuunda African Association.

Nimezungumza na baba yangu aliyekua katika mtaa wa Kipata na Abdul Sykes anihadithie yote anayokumbuka kuona katika 1950s wakati Abdul anaanza harakati za kuunda TANU nk.nk.

Baba yangu ndiye aliyenieleza kuwa yeye kamjulia Nyerere nyumbani kwa Abdul Sykes mwaka wa 1952 na akijua kuwa Abdul alikuwa na mpango wa kuunda chama cha siasa na hili kaelezwa na Abdul mwenyewe siku alipomtambulisha kwa Nyerere.

Sasa kusema ati atakuja mtu kusema kuwa na yeye wazee wake waliunda chama cha siasa sawa hakuna wa kumkataza lakini chama hicho hakitakuwa TANU kwani muasisi wa TANU anafahamika kwa ushahidi..

Ndiyo hapo nilipokuwa nalichangamsha darasa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam na kuwashangaza hadi walimu wangu kwa yale niliyokuwa nayajua na hii ndiyo sababu kitabu cha maisha ya Abdul Sykes kimeweza kubadili historia nzima ya Mwalimu Nyerere na historia ya uhuru wa Tanganyika.

Bahati mbaya sana historia hii hamuipendi inawachoma moyo mnapenda tubaki na historia inayomtaja Nyerere peke yake kuwa ndiye muasisi wa TANU na harakati za kudai uhuru 1954.

Katika picha hiyo hapo chini yuko Kleist Sykes na Ramadhani Mashado Plantan wa pili kushoto katika hao waliokaa chini na hapo ndipo ilipokuja kuzaliwa TANU na Mashado Plantan akiwa mmoja wa wazalendo waliohudhuria mkutano wa kwanza wa TANU August 1954.
Kama umefanya research na ukaguzi rasmi wa kihistoria juu ya taarifa na vyanzo hivyo, Mimi naikubali hiyo historia, na nina uhakika Tanzania tuna historia kubwa isiyo fahamika, NI VYEMA IKAWA WAZI kwa umma wa Watanzania. Asante mkuu kwa kunielewesha!!!!!!
 
Kama umefanya research naukaguzi rasmi wa kihistoria juu ya taarifa na vyanzo hivyo, Mimi naikubar hiyo historia, Na nina uhakika Tanzania tuna historia kubwa isiyo fahamika.....NIVYEMA IKAWA WAZI kwa Umma wa watanzania. Asante mkuu kwa kunielewesha!!!!!!
King...
Historia ya Kleist Sykes na wanae ipo katika Dictionary of African Biography mradi wa Harvard na Oxford University Press New York.

Hizi ni vol. VI za tawasifu fupi za watu mashuhuri Afrika.

Nilishirikishwa kama mmoja wa waandishi 500 kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni.
 
Sasa mkuu kuna shida Gani kuziweka taarifa hizo kuwa rasmi katika Historia ya nchi, ni nin kinachokwamisha jambo hili....? Maana ni muhimu kwa mustakabari wa vizazi vyetu na vijavyo......
 
Najaribu kufikiria, huyu Kleist Sykes alipata wapi ujasiri wa kuanzisha chama cha kupinga ukoloni, wakati alikuwa anaishi kwa fadhila za wakoloni, na watoto wake Abdul na Ally aliwatoa kwa wazungu wakawasaidie vita huko Burma. inawezekana hiki chama cha AA kilianzishwa na wazungu ili kupunguza nguvu za wapinga ukoloni wa ukweli akina Bushiri, Mkwawa , n k
 
Huwa nasoma sana maandiko yako Mzee Mohamed Said. Mara nyingi huwa marefu na ambayo huwa hayaleti muungano wa kitaifa. Mtu akimaliza kusoma hujengewa chuki tu, na ndio maana kwenye maandiko yako huwa na majibizano yasiyojenga.

Shida yako kuu ni hiyo mistari hapa chini ambayo hujirudiarudia kwenye uandishi wako kila unapokosolewa. Huwa wajificha chini ya mwamvuli wa kuwa na uhusiano wa kidugu au kuwahi kuishi na kusimuliwa na hao wapigania Uhuru wako na pia kujidai umefanya utafiti ambao kwa mtazamo wako utafiti wako ndio pekee huwa sahihi. Kwa hiyo kusikia historia zitolewazo na vinywa vya wengine kwako huwa ni uongo, na unataka tuamini usemacho wewe tu.

Wote tuna historia toka viunoni mwa wazazi wetu; mojawapo ya historia anayopewa kila mtu ni wazazi kutwambia walipokuwa shule walikuwa wazuri sana kimasomo. Kumbe wazazi hujifagilia tu.

Kuna reference za vitabu vichache ambazo wewe hudai zinatoka upande wa pili ambazo huzitumia pale zinapoungana na mtazamo wako wa Waislamu kuonewa na tawala za kikoloni na baada ya Uhuru.

Historia yako yoyote unapoitoa huegemea upande mmoja ambao ulishauchagua tangu utotoni. Huwezi ukawa mwanahistoria uliyechagua upande. Labda tukuite mtetezi.

Lakini sawa, labda kwa siku ya leo tukubali kwamba Waislam walionewa wakati na baada ya ukoloni. Sasa utalalamika hadi lini? Hata muuza sumu ya panya, huzima kipaza sauti baada ya kukamilisha mauzo ya siku na usiku kuingia. Shauri Waislam wafanye nini toka hapa walipo? Toa mashauri ambayo yataleta amani na si kutujengea chuki kila siku kwa kufuata historia zako ambazo hutaki zikosolewe. Hivi Muislam wa sasa itamjenga historia au maamuzi ya kutoka hapa alipo sasa?

Barbarosa,
.....ni historia ambayo inawahusu wazee wangu nami nimeishi ndani ys historia hii.

Nawajua wazee wangu na historia ya uhuru wa Tanganyika.....

Wengine nimebahatika kuwaona kwa macho yangu na kuzungumzanao....

....Na hawa ndiyo walionisomesha mimi historia hii na nikaandika kitabu kilichobadili historia yote ya uhuru wa Tanganyika.
 
najaribu kufikiria, huyu Kleist Sykes alipata wapi ujasiri wa kuanzisha chama cha kupinga ukoloni, wakati alikuwa anaishi kwa fadhila za wakoloni, na watoto wake Abdul na Ally aliwatoa kwa wazungu wakawasaidie vita huko Burma. inawezekana hiki chama cha AA kilianzishwa na wazungu ili kupunguza nguvu za wapinga ukoloni wa ukweli akina Bushiri, Mkwawa , n k

Laki...
Ungesoma kitabu cha Abdul Sykes ungekuwa umejifunza mengi na usingeuliza maswali kama haya. Kuanzisha associations ikiruhusiwa na Waingereza kwani kulikuwa na European, Asian na Arab Association na Waafrika waliwakilishwa na Mzungu jina lake Father Gibbons kutoka Pugu Mission.

Hapakuwa na suala la ujasiri.

Ukitaka kuujua ujasiri wa Kleist itakubidi usome War Diaries zake katika WW I Kleist na nduguye Schneider Plantan wakipigana chini ya Paul von Lettow Vorbeck katikajeshi la Wajerumani dhidi ya Waingereza.

Abdul Sykes aliingizwa katika KAR kupigana Burma kwa mujibu wa sheria na Ally yeye alitoroka nyumbani kujiunga na jeshi na akapokelewa ingawa alikuwa hajafikia umri.

Sijui hizi lugha za "fadhila,"unakusudia kitu gani.
 
Huwa nasoma sana maandiko yako Mzee Mohamed Said. Mara nyingi huwa marefu na ambayo huwa hayaleti muungano wa kitaifa. Mtu akimaliza kusoma hujengewa chuki tu, na ndio maana kwenye maandiko yako huwa na majibizano yasiyojenga.

Shida yako kuu ni hiyo mistari hapa chini ambayo hujirudiarudia kwenye uandishi wako kila unapokosolewa. Huwa wajificha chini ya mwamvuli wa kuwa na uhusiano wa kidugu au kuwahi kuishi na kusimuliwa na hao wapigania Uhuru wako na pia kujidai umefanya utafiti ambao kwa mtazamo wako utafiti wako ndio pekee huwa sahihi. Kwa hiyo kusikia historia zitolewazo na vinywa vya wengine kwako huwa ni uongo, na unataka tuamini usemacho wewe tu.

Wote tuna historia toka viunoni mwa wazazi wetu; mojawapo ya historia anayopewa kila mtu ni wazazi kutwambia walipokuwa shule walikuwa wazuri sana kimasomo. Kumbe wazazi hujifagilia tu.

Kuna reference za vitabu vichache ambazo wewe hudai zinatoka upande wa pili ambazo huzitumia pale zinapoungana na mtazamo wako wa Waislamu kuonewa na tawala za kikoloni na baada ya Uhuru.

Historia yako yoyote unapoitoa huegemea upande mmoja ambao ulishauchagua tangu utotoni. Huwezi ukawa mwanahistoria uliyechagua upande. Labda tukuite mtetezi.

Lakini sawa, labda kwa siku ya leo tukubali kwamba Waislam walionewa wakati na baada ya ukoloni. Sasa utalalamika hadi lini? Hata muuza sumu ya panya, huzima kipaza sauti baada ya kukamilisha mauzo ya siku na usiku kuingia. Shauri Waislam wafanye nini toka hapa walipo? Toa mashauri ambayo yataleta amani na si kutujengea chuki kila siku kwa kufuata historia zako ambazo hutaki zikosolewe. Hivi Muislam wa sasa itamjenga historia au maamuzi ya kutoka hapa alipo sasa?
Ozzanne,
Kwako wewe kuandika historia ya kweli ni kuvunja udugu ila kupotosha historia ni kuunga udugu na kuleta umoja wa kitaifa.

Wala wewe huna haja ya kuniamini ninapoeleza kuwa babu yangu Salum Abdallah ni muasisi wa TANU Tabora na ni muasisi wa Tanganyika Railways African Union (TRAU) akiwa rais 1955 na aliongoza migomo mikubwa mitatu ya wafanyakazi wa reli, 1947, 1949 na 1960.

Ukipenda amini kuwa wala watu hawa hawakupata kuwepo Tanganyika.

Wala sina sababu ya kujidai.

Hawa ni wazee wangu na wala sikuwachagua.

Nimezaliwa wakati wao kwa uchaguzi wa Mungu.

Wala hawa wazee hawakupanga kuwa Nyerere atatoka kwao atakuja Dar es Salaam atamtafuta Abdul Sykes na wataungana na wazalendo wengine kupigania uhuru wa Tanganyika.

Historia hii ndiyo historia ya wazee wangu ambayo ilipotea nami nikaiandika ili isipotee na iwepo hadi siku ya kiama.

Bora wasingeandika kabisa kuliko kuandika historia iliyopotoshwa.

Ikiwa unayo historia ya TANU mfano wa hii yangu iandike isomwe kama dunia inavyosoma yangu.

Nimekusoma ahsante sana.
 
Sheikh dhulma imefanywa sana,hakika yana mwisho...Inshaalah

Ozzanne,
Kwako wewe kuandika historia ya kweli ni kuvunja udugu ila kupotosha historia ni kuunga udugu na kuleta umoja wa kitaifa.

Wala wewe huna haja ya kuniamini ninapoeleza kuwa babu yangu ni muasisi wa TANU Tabora na ni muasisi wa Tanganyika Railways African Union (TRAU) akiwa rais 1955 na aliongoza migomo mikubwa mitatu wafanyakazi wa reli, 1947, 1949 na 1960.

Ukipenda amini kuwa wala watu hawa hawakupata kuwepo Tanganyika.

Ikiwa unayo historia ya TANU mfano wa hii yangu iandike isomwe kama dunia inavyosoma yangu.

Nimekusoma ahsante sana.
 
Nini kiliifanya EAMWS kuhamisha makao yake makuu kutoka Mombasa hadi Dar?

Kama ni Nyerere ndiye aliyeua EAMWS na kuanzisha BAKWATA, je ni yeye mwenyewe aliua EAMWS kule KENYA? Aliwaanzishia baraza gani kule?
 
Mzee said naisi kama nimewahi kukuona masjid idrisa kariakoo mwaka 2009 baada ya swala ya ijumaa, nakumbuka siku hiyo ulisimama na kusema leo ninawaletea historia ya tanganyika kabla ya uhuru nakumbuka siku hiyo waislam wengi walitulia sehem zao wakisubiri kusikia kile ulichowaandalia, sina kumbukumbu vzr ulisema kua miongoni wa wapigania uhuru waliokua hai hadi leo (2009) ni wawili tu ambao wazee sn na hali yao si nzr, nakumbuka ulisema uchunguzi wako ulikuchukua miaka mingi sn kukamilika, historia iliishia kwa Waislam wengi sn msikitini pale kulitokwa na machozi sn nami nikiwemo hii ni baada ya kugundua tumedhulumiwa sn na mbaya zaidi kwenye history babu zetu hawawamo, mzee said kama ni ww kweli basi allah akuifadhi mzee wangu. nakumbuka ilikuwa ndo mara ya kwanza report ile inatolewa na kulikua na wapiga picha wengi na video shooting kibao ulivaa kanzu Nyeupe na kofia yako Nyeupe, Allah kareem mzee wangu ipo siku haqq itajienga na batili in sha Allah na tupo vijana allahmdulilah
 
Bibi upo na shule zako? Shule ni kwa ajili ya kupata elimu tu lakini akili tumepewa na Mwenyezi Mungu ambazo zinakufanya ujitambue wewe ni nani na zinakuwezesha kuyamudu mazingira uishiyo. Sasa mimi ukiniambia sijasoma well and good! Lakini ukiniambia sina akili hapo ndiyo itaniuma kwa sababu akili tumeumbwa nazo na Mungu!
Haya unachosoma huelewi, nani kaandika hujasoma? Kanisome tena.
 
Mohamed Said, inawezekana chuki zako zimetokana na familia ya Sykes kufilisiwa mali zao kipindi Nyerere alipoanza kampeni zake za ujamaa kuanzia mwaka 1964,familia ya sykes ilikumbwa na kimbunga kilichowakumba akina kambona, titi mohamed, kaselabantu etc
 
Hiyo mihadhara na research unazoenda kuzifanya huko vyuo vya ulaya, UK, German zinafadhiliwa na nani? ni taasisi au mtu binafsi anaekufadhili?
 
Nyerere kafariki, mmeshindwa nini kujenga Chuo Kikuu mpaka sasa?

Katika gazeti la Hoja (Ijumaa, Novemba 15 – 21, 2019), kuna makala ‘’Mufti Zubeir alivyoikarabati BAKWATA,'' iliyoandikwa na Hemed Kimwanga.

Makala hii ingepita kama makala nyingine yeyote ile endapo makala isingekuwa na mambo ambayo si kweli kuhusu kuundwa kwa BAKWATA.

Imekuwa kawaida sana hasa katika miaka ya hivi karibuni kwa kusemwa na kuandikwa mengi ambayo si ya kweli kuhusu asili ya BAKWATA.

Kimwanga anasema na hapa najitahidi kunukuu kwa uchache yale aliyoandika.

Kimwanga anamuhusisha Julius Nyerere kwa kuvunjwa EAMWS na kuundwa kwa BAKWATA.

Kimwanga anasema, ‘’...uongozi wa Mufti umekidhi matumaini yaliyokuwa moyoni mwa Mwalimu Julius Nyerere kwa kushauri mpaka kuiva kwa ndoto zake za kuiona Tanzania ikiwa na Baraza lake la Kiislam ambalo litakuwa huru katika mashirikiano na vyombo vingine vya mlengo huo ndani na nje ya nchi.’’

Kimwanga anaandika anasema East African Muslim Welfare Society ilikuwa, ‘’chini ya uongozi na utawala wa Prince Aga Khan wa Uingereza...’’

Kimwanga anaendelea, ‘’...kuna mantiki ndogo sana ambayo ilifanya serikali ya Mwalimu Nyerere kuivunja EAMWS.

Alitaka Waislam wa Tanzania wajiongoze wenyewe.
Siyo kupokea maagizo kutoka London kwa Prince Aga Khan kupitia Nairobi...’’

Historia ya BAKWATA hivi sasa inafanana na historia ya TANU kwani historia ya BAKWATA kama ilivyo historia ya TANU imekuwa ikijaza hofu kwa baadhi ya watu kiasi ya kupelekea kusemwa uongo mwingi kwa kuogopa ukweli.

Haikunichukua muda wakati naisoma makala hii kutambua kuwa Kimwanga anaandika kitu ambacho yeye kwa kweli kabisa hakijui.

Sheikh Mohamed Ayub alikuwa heshi kuwausia wanafunzi wake kwa kuwaaambia kuwa popote linapokuwa jambo kuhusu Uislam wafike ili ikiwa patakuwa na jambo ambalo haliko sawa watanlieleza kwa ukweli wake.

Sheikh Mohamed Ayub akiwaambia wanafunzi wake kuwa, "Semeni, msiposema, hayo wasemayo yasio kweli, yataonekana ni kweli."

Ingekuwa kweli Mwalimu Nyerere anataka Waislam wasipokee amri kutoka London basi angelianza na kanisa lake mwenyewe, Kanisa Katoliki na kuishughulikia Vatican iliyokuwa na uwakilishi Tanzania nzima kama ifuatavyo:

White Fathers (Tabora), Karema, Kigoma, Mbeya, Mwanza na Bukoba; Holy Ghost Fathers (Morogoro na Kilimanjaro), Benedictine Fathers (Peramiho na Ndanda) Capuchin Fathers (Dar es Salaam) Consolata Fathers (Iringa na Meru), Passionist Fathers (Dodoma) Pallotine Fathers (Mbulu), Maryknoll Fathers (Musoma), na Rosmillian Fathers (Iringa).

Kimwanga kaandika mengi ambayo sijaona kama iko haja ya kuyasemea hapa na ningependa kueleza kuwa historia ya BAKWATA inafahamika na sababu za kupigwa marufuku EAMWS pia zinafahamika.

EAMWS imevunjwa wakati tayari ilikuwa na mipango ya kuwainua Waislam katika elimu na walikuwa wanajenga Chuo Kikuu Cha Waislam mradi ambao ulikuwa unakwenda sambamba na ujenzi wa shule Tanzania nzima.

Hapo yalipo Makao Makuu ya BAKWATA pamoja na shule hiyo ya Kinondoni imejengwa na EAMWS.

Waislam hawakuwa na ujinga kuivunja EAMWS wakati inajenga Chuo Kikuu na shule kuwainua Waislam ambao ukoloni uliwanyima elimu na kutoa uwanja mpana kwa makanisa kuhodhi elimu ambayo waliitoa kwa ubaguzi kwa waumini wao kwa kipindi cha zaidi ya miaka 100.

Kimwanga asome historia ya kweli ya Tanganyika atafahamu kwa nini EAMWS ilivunjwa na sababu haikuwa kupokea amri kutoka kwa Prince Aga Khan wa Uingereza (sic).

Aga Khan hakuwa London bali akiishi Paris na mgogoro wa EAMWS ulipokuwa umepamba moto alijiuzulu nafasi yake ya Patron kutoka Paris.
 
Back
Top Bottom