Ukweli ni upi katika kuvunjwa kwa EAMWS na kuundwa BAKWATA?

Ukweli ni upi katika kuvunjwa kwa EAMWS na kuundwa BAKWATA?

Bado kuna idadi kubwa tu ya wale ambao hadi leo hawatambui Baraza.
Abunuwasi,
Nilimuuliza mmoja wa viongozi wa BAKWATA kama ipo haja ya kusheherekea miaka 50 ya BAKWATA nikamwambia kuwa kwa kufanya hivyo watakuwa wanasheherekea dhulma.

Nimefuatilia katika TV sherehe yote hadi kutoa vyeti kwa waasisi wa BAKWATA ingawa viongozi wakubwa waliohusika na mgogoro ule sikusikia hata majina yao kutajwa.

Nilijua kwa nini hawawezi kuwataja.

Mmoja katika hao walioadhnimishwa alimfanyia uadui mkubwa Sheikh Hassan bin Ameir kupelekea Sheikh Hassan kukamatwa usiku wa manane kurejeshwa Zanzibar na kupigwa marufuku asitie mguu wake Bara.

Lakini liko moja katika sherehe ile lilinifurahisha na kunitia furaha upeo wa furaha.
BAKWATA hawakuwa na ujasiri wa kutaja jina la Sheikh Hassan bin Ameir.

Haiwezekani ikatajwa historia ya Waislam Tanzania na ukanda huu wa Pwani ya Afrika ya Mashariki, Malawi, Congo, Rwanda na Burundi asitajwe Sheikh Hassan bin Ameir.

Achilia mbali mchango wake katika kupigania uhuru wa Tanganyika na historia yake katika TANU.

Leo hata katika majumba yetu tukiwarehemu waliotangulia jina la kwanza kutajwa ni la Sheikh Hassan bin Ameir.

Sheikh Hassan katuachia historia kubwa ya kutukuka.

'Nilipokea ujumbe huu kutoka Burundi baada ya msomaji mmoja kunisoma nikimtaja Sheikh Hassan bin Ameir:

"Si kwamba Waswahili wa Burundi zama za ukoloni walijibagua na kujitenga mbali na elimu.

La hasha!
Waswahili walikuwa na elimu ya kutosha zama hizo ukiwalinganisha na makabila mengine.

Walikuwa wanatumia herufi za Kiarabu (alphabet arabe) kwa kuandika Kiswahili na walikuwa wanajuwa kupiga hesabu (calcul).

Walikuwa na shule zao ambazo ni madrasa.
Walikuwa wakiandika tungo mbalimbali ikiwemo mashairi.

Walitengwa kwenye elimu kwa maksudi na ukoloni.

Hasa ukoloni wa Wabeleji ambao uliwanyima wazi Waswahili elimu mpya ya Kimagharibi na kuwapa Kanisa Katoliki umiliki pekee (monopole) wa kuitoa elimu katika nchi.

Waswahili walilalamika zama hizo wala hawakulala.

Waliunda chini ya uongozi wa marehemu Sheikh Amrani Juma taasisi iitwayo ASMARU (Association Scolaire Musulmane du Ruanda-Urundi) yaani Taasisi ya Kielimu ya Waislam wa Ruanda-Urundi).

Na walipeleka malalamiko yao mbele ya Serikali na kuwambia nyiye ni wabaguzi, tunaomba na sisi tupewe ruzuku (subventions) ili tujenge shule zetu na tuwalipe walimu wetu waweze kuwafundisha watoto zetu bila kubadiliwa dini yao ya Uislam na Kanisa ambalo ndio njia lilitumia kubadili imani za watoto baada kuona limeshindwa kuwabadili watu wazima.

Ruzuku hiyo iliombwa kwa sababu pesa hizo ni michango ya raia wanaipa Serikali kwa kulipa kodi mbalimbali, na Waswahili walikuwa ni walipa kodi wakubwa.

Hata na hivyo Serikali ya kikoloni ilikataa kuwapa chochote Waswahili, lakini la kushangaza ikakubali kuwapa Waprotestanti ambao pia walilalamika.

Waprotestanti walipewa ruzuku ya 50,000 F (Franka elfu khamsini) ambazo zilikuwa nyingi sana kwa zama hizo.

Hatimaye Waswahili wakapiganisha huku na kule na kupata msaada toka kwa ndugu zao Watanganyika na kujenga shule moja ya watoto wao ambayo ni Jumuiya (Jina la Jumuiyatul Islamiyya fii Tanganyika).

Hiyo shule ipo hadi leo Barabara ya Nane na ya Tisa Buyenzi.

Alikuja kutoka Tanganyika Mufti Hassan bin Amir kuzindua shule hiyo. #WazeeWetuHawakuwaWazembe Mungu awarehemu.''
 
Dah nimefika kwenye hiyo shule mwaka jana nilipokua buja

Rommy,
Tunaweza kupata picha yake?
Hajapata kutokea sheikh kama Mufti Sheikh Hassan bin Ameir.

Nimeandika historia ya maisha yake lakini sichoki kumsoma na kujisoma mwenyewe:

''Nyerere was a familiar face at the 'darsa' of Sheikh Hassan bin Ameir in down town Dar es Salaam.

It is said whenever Nyerere went to see Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Hassan would always as a rule, dismiss his students and would sit down with Nyerere and his entourage for hours on end discussing on the future of Tanganyika.

Under Sheikh Hassan bin Ameir’s wings no Muslim dared to challenge Nyerere. [11] Sheikh Hassan bin Amir's ‘madras’ in Dar es Salaam therefore played a multiplicity of roles.

It was a centre of religious knowledge as well as centre for mass mobilisation and agitation against the colonial government.

It was difficult to distinguish between visitors who came to visit Sheikh Hassan bin Ameir.

they come to the Mufti to seek ‘fatwa’ for a ‘mushkel’ or had they come to exchange notes on the political climate in the country.

Nyerere realised very early in his political career the power and respect commandeered by Mufti Sheikh Hassan bin Ameir and he never took any important decision without consulting him.''

1574094757840.png

Marehemu Sheikh Ali bin Abbas mwanafunzi mtoto wa Sheikh Hassan bin Ameir wakati alipokuwa anasomesha Dar es Salaam katika miaka ya 1950. Hapa yuko nyumbani kwake na mtafiti wa Kimarekani James Brennan kutoka Chuo Kikuu Cha Champagne, Chicago aliyefika kumhoji. Sheikh Ali bin Abbas alimsaidia sana mwandishi Mohamed Said katika kumjulisha maisha ya siasa ya Sheikh Hassan bin Ameir.​
 
Bwana Mohamed,
Hivi unadhani ni kitu gani hasa kilichofanya serikali ya awamu ya kwanza kuvunja EAMWS?
Abunuwasi,
Hofu ilitokana na kule kutambua nguvu na umoja walioonyesha Waislam wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika chini ya TANU.

Masheikh wote walikuwa kitu kimoja ndani ya TANU wakiongozwa na Sheikh Hassan bin Ameir aliyekuwa Mufti wa Tanganyika.

Juhudi za kuwapa elimu vijana wa Kiislam zikazidisha hofu hii na ilipofika sasa EAMWS imeshaweka jiwe la msingi pale Chang'ombe kujenga Chuo Kikuu hapa ikawa lazima EAMWS ipigwe marufuku BAKWATA iundwe ili miradi yote ya elimu ipotelee mbali kwa kuhakikisha kuwa BAKWATA itaendeshwa na watu ambao hawana uwezo wala uzoefu wa kuendesha taasis kubwa na muhimu kama hiyo kama waliokuwanayo Sheikh Hassan bin Ameir, Tewa Said Tewa na Aziz Khaki huyu alikuwa Ismailia.

Kusudio ya haya yote ilikuwa ni lazima Waislam wabanwe kwenye elimu wawe watu wa chini siku zote na ndiyo unaona Waislam waliwahi kufanya maandamano wakidai kuwa Baraza la Mitihani chini ya Dr. Joyce Ndalichako linahujumu shule za Kiislam.

Haya yanatokea nusu karne baada ya Tanganyika kuwa huru.

Mwaka wa 1987 kulikuwa na mtafaruku mkubwa pale Prof. Malima alipandika barua kwa Rais Mwinyi kumweleza aliyoyakuta yanafanyika ndani ya Wizara ya Elimu wakati yeye alipochaguliwa kuwa waziri wa kwanza Muislam katika wizara hiyo.

Prof. Malima aliondolewa katika wizara hiyo.
Tahadhari hizi kwa serikali si ngeni Waislam wametahadharisha sana kuhusu suala hili.
 
Ipo siku haki itapatikana biidhinllah
Hii nchi hii ina mfumo kristo wallah dhulma dhidi ya Waislam wa tanganyika haitaliacha kanisa salama na wallah tunaumia kwa haya yanayotokea , Allah amjalie sheikh wetu ilunga Pepo ya juu in sha Allah ameacha athari kubwa sn kwa kizazi cha leo maneno yake bado yanaishi japo watu wasema vijana punguzeni jazba wallah hatutapunguza mpk hizza yetu itakaporudi bi idhniLlaah
 
Abunuwasi,
Hofu ilitokana na kule kutambua nguvu na umoja walioonyesha Waislam wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika chini ya TANU.

Masheikh wote walikuwa kitu kimoja ndani ya TANU wakiongozwa na Sheikh Hassan bin Ameir aliyekuwa Mufti wa Tanganyika.

Juhudi za kuwapa elimu vijana wa Kiislam zikazidisha hofu hii na ilipofika sasa EAMWS imeshaweka jiwe la msingi pale Chang'ombe kujenga Chuo Kikuu hapa ikawa lazima EAMWS ipigwe marufuku BAKWATA iundwe ili miradi yote ya elimu ipotelee mbali kwa kuhakikisha kuwa BAKWATA itaendeshwa na watu ambao hawana uwezo wala uzoefu wa kuendesha taasis kubwa na muhimu kama hiyo kama waliokuwanayo Sheikh Hassan bin Ameir, Tewa Said Tewa na Aziz Khaki huyu alikuwa Ismailia.

Kusudio ya haya yote ilikuwa ni lazima Waislam wabanwe kwenye elimu wawe watu wa chini siku zote na ndiyo unaona Waislam waliwahi kufanya maandamano wakidai kuwa Baraza la Mitihani chini ya Dr. Joyce Ndalichako linahujumu shule za Kiislam.

Haya yanatokea nusu karne baada ya Tanganyika kuwa huru.

Mwaka wa 1987 kulikuwa na mtafaruku mkubwa pale Prof. Malima alipandika barua kwa Rais Mwinyi kumweleza aliyoyakuta yanafanyika ndani ya Wizara ya Elimu wakati yeye alipochaguliwa kuwa waziri wa kwanza Muislam katika wizara hiyo.

Prof. Malima aliondolewa katika wizara hiyo.
Tahadhari hizi kwa serikali si ngeni Waislam wametahadharisha sana kuhusu suala hili.

Hapa unamaanisha kuwa mkwamo wa maendeleo ya waislam ulianzia kwa kuvunjwa kwa EAMWS ambao walitaka kuanzisha chuo kikuu. Hivi kuwa na Elimu ni mpaka uwe umesoma mpaka chuo kikuu?

Na sote tunafahamu kuwa wakati wa ukoloni waislam walikuwa wachache sana mashuleni, je nani angeenda huko chuo kikuu kwa miaka hiyo ya 60's bila kupitia shule za awali? Au mtu angeingia tu chuoni as long as he was a moslem regardless of qualifications?

Soma hoja yangu between lines... ili uone kuwa the allegation that "moslems became enemies of Nyerere just because EAMWS planned to have a university" is a bit unrealistic.
 
Nanren,
Naamini umesoma mengi kuhusu historia ya EAMWS ambayo hukuwa unayajua na hii imeongeza uelewa wako katika historia ya Tanganyika.

Mimi siko hapa kufanya ubishi mimi niko hapa kueleza yale ambayo si hadhir kwa wengi.

Nia yangu ni watu waelimike.

Unaweza kuamini upendavyo mimi sina tatizo na hayo.

Naamini umeona tofauti kubwa kati ya yale aliyoeleza Kimwanga na haya unayosikia kutoka kwangu kuhusu historia ya EAMWS.
 
Mzee naomba nikuulize tena kidogo. Kwa historia uliyopata kutoka kwa wazee wako, lawama zako unaelekeza kwa nani haswa!? Serikali, kanisa, BAKWATA, au nyie wenyewe!?
 
Mzee naomba nikuulize tena kidogo. Kwa historia uliyopata kutoka kwa wazee wako, lawama zako unaelekeza kwa nani haswa!? Serikali, kanisa, BAKWATA, au nyie wenyewe!?
Cpt,
Sikuandika kwa nia ya kulaumu.
Nimeandika ili historia ya kweli ifahamike.
 
Nanren,
Naamini umesoma mengi kuhusu historia ya EAMWS ambayo hukuwa unayajua na hii imeongeza uelewa wako katika historia ya Tanganyika.

Mimi siko hapa kufanya ubishi mimi niko hapa kueleza yale ambayo si hadhir kwa wengi.

Nia yangu ni watu waelimike.

Unaweza kuamini upendavyo mimi sina tatizo na hayo.

Naamini umeona tofauti kubwa kati ya yale aliyoeleza Kimwanga na haya unayosikia kutoka kwangu kuhusu historia ya EAMWS.

Poa, kiongozi.
Naona unaendelea na majibu yako ya kijanja janja.
 
Katika gazeti la Hoja (Ijumaa, Novemba 15 – 21, 2019), kuna makala ‘’Mufti Zubeir alivyoikarabati BAKWATA,'' iliyoandikwa na Hemed Kimwanga.

Makala hii ingepita kama makala nyingine yeyote ile endapo makala isingekuwa na mambo ambayo si kweli kuhusu kuundwa kwa BAKWATA.

Imekuwa kawaida sana hasa katika miaka ya hivi karibuni kwa kusemwa na kuandikwa mengi ambayo si ya kweli kuhusu asili ya BAKWATA.

Kimwanga anasema na hapa najitahidi kunukuu kwa uchache yale aliyoandika.

Kimwanga anamuhusisha Julius Nyerere kwa kuvunjwa EAMWS na kuundwa kwa BAKWATA.

Kimwanga anasema, ‘’...uongozi wa Mufti umekidhi matumaini yaliyokuwa moyoni mwa Mwalimu Julius Nyerere kwa kushauri mpaka kuiva kwa ndoto zake za kuiona Tanzania ikiwa na Baraza lake la Kiislam ambalo litakuwa huru katika mashirikiano na vyombo vingine vya mlengo huo ndani na nje ya nchi.’’

Kimwanga anaandika anasema East African Muslim Welfare Society ilikuwa, ‘’chini ya uongozi na utawala wa Prince Aga Khan wa Uingereza...’’

Kimwanga anaendelea, ‘’...kuna mantiki ndogo sana ambayo ilifanya serikali ya Mwalimu Nyerere kuivunja EAMWS.

Alitaka Waislam wa Tanzania wajiongoze wenyewe.
Siyo kupokea maagizo kutoka London kwa Prince Aga Khan kupitia Nairobi...’’

Historia ya BAKWATA hivi sasa inafanana na historia ya TANU kwani historia ya BAKWATA kama ilivyo historia ya TANU imekuwa ikijaza hofu kwa baadhi ya watu kiasi ya kupelekea kusemwa uongo mwingi kwa kuogopa ukweli.

Haikunichukua muda wakati naisoma makala hii kutambua kuwa Kimwanga anaandika kitu ambacho yeye kwa kweli kabisa hakijui.

Sheikh Mohamed Ayub alikuwa heshi kuwausia wanafunzi wake kwa kuwaaambia kuwa popote linapokuwa jambo kuhusu Uislam wafike ili ikiwa patakuwa na jambo ambalo haliko sawa watanlieleza kwa ukweli wake.

Sheikh Mohamed Ayub akiwaambia wanafunzi wake kuwa, "Semeni, msiposema, hayo wasemayo yasio kweli, yataonekana ni kweli."

Ingekuwa kweli Mwalimu Nyerere anataka Waislam wasipokee amri kutoka London basi angelianza na kanisa lake mwenyewe, Kanisa Katoliki na kuishughulikia Vatican iliyokuwa na uwakilishi Tanzania nzima kama ifuatavyo:

White Fathers (Tabora), Karema, Kigoma, Mbeya, Mwanza na Bukoba; Holy Ghost Fathers (Morogoro na Kilimanjaro), Benedictine Fathers (Peramiho na Ndanda) Capuchin Fathers (Dar es Salaam) Consolata Fathers (Iringa na Meru), Passionist Fathers (Dodoma) Pallotine Fathers (Mbulu), Maryknoll Fathers (Musoma), na Rosmillian Fathers (Iringa).

Kimwanga kaandika mengi ambayo sijaona kama iko haja ya kuyasemea hapa na ningependa kueleza kuwa historia ya BAKWATA inafahamika na sababu za kupigwa marufuku EAMWS pia zinafahamika.

EAMWS imevunjwa wakati tayari ilikuwa na mipango ya kuwainua Waislam katika elimu na walikuwa wanajenga Chuo Kikuu Cha Waislam mradi ambao ulikuwa unakwenda sambamba na ujenzi wa shule Tanzania nzima.

Hapo yalipo Makao Makuu ya BAKWATA pamoja na shule hiyo ya Kinondoni imejengwa na EAMWS.

Waislam hawakuwa na ujinga kuivunja EAMWS wakati inajenga Chuo Kikuu na shule kuwainua Waislam ambao ukoloni uliwanyima elimu na kutoa uwanja mpana kwa makanisa kuhodhi elimu ambayo waliitoa kwa ubaguzi kwa waumini wao kwa kipindi cha zaidi ya miaka 100.

Kimwanga asome historia ya kweli ya Tanganyika atafahamu kwa nini EAMWS ilivunjwa na sababu haikuwa kupokea amri kutoka kwa Prince Aga Khan wa Uingereza (sic).

Aga Khan hakuwa London bali akiishi Paris na mgogoro wa EAMWS ulipokuwa umepamba moto alijiuzulu nafasi yake ya Patron kutoka Paris.
mimi ni Mkatoliki. naunga mkono hoja yako kwa 110% shehe wangu.
 
🤲🤲🤲
Nanren,
Niliweka post hii kujibu makala ya Kimwanga iliyochapwa katika gazeti la Hoja (Ijumaa, Novemba 15 – 21, 2019), kuna makala ‘’Mufti Zubeir alivyoikarabati BAKWATA,'' iliyoandikwa na Hemed Kimwanga. ambayo ilieleza historia ya BAKWATA ambayo haikuwa kweli.

Imekuwa jambo la kawaida katika miaka ya hivi karibuni kwa BAKWATA kujieleza kuwa waliundwa na Waislam wenyewe kwa kuwa hawakutaka kuwa katika jumuia ya Kiislam ambayo ina Wahindi ndani yao kwani wao walitaka Uislam wa watu weusi peke yao.

Maajabu ya BAKWATA yanaanza hapa.

Hii kuwa na Wahindi katika Uislam wa Tanganyika BAKWATA wanadai ndiyo sababu kubwa ya kuundwa BAKWATA.

Watu wawili hapa Tanzania ndiyo waliofanya utafiti kuhusu BAKWATA na kuchapa kazi zao.
Dr. Mayanja Kiwanuka (1973) na Mohamed Said (Islam and Politics in Tanzania (1989):

Amazon product ASIN B0006CNXGA
Nimekuwekea rejea hizo mbili usome uone tofauti kati ya utafiti wangu na wa Dr. Kiwanuka katika somo moja hilo hilo.

Nilipokuwa namsoma Kimwanga nilicheka tu maana sikuwa na lingine la kufanya ila kucheka.

Mjadala ulipoanza hapa Majlis kuna wachangiaji waliingia kwa ghadhabu na kejeli wengine kufikia kunitukana.

Nasoma kisha nacheka.
Sikuwa na lingine lakufanya.

Katika akili ya binadamu kuna akili ya ndani, ndani ya akili ya kwanza.

Hii akili ya pili na ndani ni mfano wa mahkama ya rufaa pale panapokuwa na uamuzi wa kwanza hii akili ya pili hufanya kama kuishtua akili ya kwanza kuiambia irejee tena katika uamuzi wake huenda pana kitu.

Ninapokejeliwa na kutukanwa na nikimaliza kucheka hunyanyua upya kalamu yangu na hapa sasa sizungumzi tena na akili yako ya kwanza sasa nailenga akili yako ya pili kwa kuja na ushahidi unaotakiwa na huu huwa zaidi ya ule wa kwanza.

Kwa kawaida nifanyapo hivi napata majibu mazuri ya aina mbili.

Kejeli na matusi hupungua na ikiwa wale watukanao na kukejeli wataamua kubakia kwenye mnakasha wanarudi na adabu na heshima kamili au wataukimbia mjadala.

Nanren,
Baada ya kumsoma Kimwanga na Mohamed Said imekudhihirikia nani asemae kweli.
 
Bado BAKWATA inanguvu kupita hizo taasisi nyingine , misikiti karibu yote nchi nzima imejengwa na BAKWATA. nadhani hata wewe Mohamed Said unaswali misikiti iliyojengwa na BAKWATA
 
Bado BAKWATA inanguvu kupita hizo taasisi nyingine , misikiti karibu yote nchi nzima imejengwa na BAKWATA. nadhani hata wewe Mohamed Said unaswali misikiti iliyojengwa na BAKWATA
Laki...
Katika kitu ambacho BAKWATA hakina ni nguvu.
Kama isingekuwa serikali BAKWATA ingekuwa ishakufa miaka mingi.

Mwaka wa 1993 BAKWATA kwa sheria ilikuwa ifutwe kwa kushindwa kuitisha mkutano wa uchaguzi kwa kuwa haikuwa na fedha.

ِAugstine Mrema wakati huo Waziri wa Mambo ya Ndani na Makamu Waziri Mkuu akaitisha mkutano Ukumbi wa Diamond kuchangisha fedha kusaidia BAKWATA iitishe mkutano kuepuka kufungiwa..

Waislam hawakuhudhuria mkutano ule lakini Kanisa lilipeleka ujumbe mzito na lilichangia fedha kuinusuru BAKWATA.

BAKWATA haina msikiti popote pale misikiti uionayo yote imejengwa na Waislam wenyewe.
Hii ndiyo nguvu kubwa ya BAKWATA.

Taasisi za Kiislam zipo na zinakubalika na Waislam kwa kuwa wao ndiyo walioziunda na zinafanya kazi nzuri nchi nzima.
 
Back
Top Bottom