Ukweli ni upi katika kuvunjwa kwa EAMWS na kuundwa BAKWATA?

Nani aliyedhulumiwa?
 
Interesting. Wamedhulumiwa nini? Maana dhuluma ni kitu kiovu kabisa
Ndahani,
Bahati mbaya sana kuwa kitabu cha Prof. Hamza Mustafa Njozi, ''Mwembechai Killings...'' (2002) kilipigwa marufuku na serikali.

Kitabu kile Njozi alikiandika baada ya Rais Mkapa kusomewa risala na Waislam Ukumbi wa Diamond mara tu alipouchukua urais wa nchi.

Risala ile iliyosomwa na Ramadhani Madabida ilieleza dhulma wanazofanyiwa Waislam kwa miaka mingi.

Rais Mkapa katika kujibu ile risala akasema Waislam walete ushahidi wa kisayansi.
Ndipo Njozi akaandika kitabu kile.

Yaliyomo ndani ya kitabu kile hakika ni mazito na uzito wake ni kuwa ikiwa yale yataanikwa hadharani yatabadili historia ya nchi yetu yote.

Sijui waliohusika na njama hizo maana wametajwa kwa majina Waislam watawatazamaje na wao wenyewe kwa walio hai watajisikiaje katika jamii.

Kwa viongozi ambao wameshatangulia mbele ya haki nini itakuwa ''legacy,'' yao katika nchi hii?

Ukweli ni kuwa majina mazuri na sifa tulizowapa kama wazalendo itabidi zote zifutike.
Sikushangaa kitabu kilipopigwa marufuku.

Ndahani,
Toka ulipouliza hilo swali nani kadhulumiwa mimi nilikaa kimya sikutaka kukujibu kwa sababu nauogopa ukweli huu.

Lakini ukarejea tena baada ya kujibiwa.
Ndipo nikaona nami nitie neno ili ujue huenda unauliza kwa dhati hujui kitu unataka kujua.
 
Kwanza kabisa, hakuna jambo lililochini ya jua likawa zito mpaka likashindikana kupatikana majawabu yake. Historia nzima ya mwanadamu inashuhudia hivyo.
Kama kuna dhuluma nzito ambayo haiwezekani, basi jibu lake halipo ndani ya safari yetu.
Nauliza tena, dhuluma zipi walizofanyiwa waislamu Tanzania na uthibitisho wake? Mkapa hakukosea. Lazima tuyaseme mambo kisayansi maana vinginevyo tutaanza kuwa wazushi
 
Ndahani,
Nimekueleza kuwa ushahidi wa kisayansi ulitolewa kwa Rais Mkapa kama alivyoshauri.
Prof. Njozi akaandika kitabu.

Serikali baada ya kukisoma kitabu uamuzi uliotolewa ni kukipiga kitabu marufuku.
Kuwa na kitabu, "Mwembechai Killings..." ni kosa la jinai.

Labda kitabu kingeruhusiwa kiingie nchini kisomwe leo wewe usingeuliza kuhusu dhulma ungekuwa ushajua hilo tatizo na labda hatua za kuondoa hii dhulma zingekuwa zinaendelea ili ipatikane haki na usawa kwa wote.

Wanaomjua Prof. Njozi watakuambia kuwa ni msomi makini na ni katika waandishi walio kwenye kundi la pekee ndani na nje ya mipaka yetu.

Muhali mkubwa kwake yeye kuwa ''mzushi.''

Sifa hii haiwezi hata kwa mbali kumuenea.
 
Sio kama ajui madhira na ukatili unaowakuta waislam wa wasidhani tumesahau mauaji ya halaiki 2001 zanzbar dhidi ya Waislam bado kumbukumbu tunazo kichwani, madada zetu walivyobakwa na kuzalilishwa ikapelekea wengine kuomba ifadhi ya ukimbizi nchi jirani.historia itaandikwa upya in sha Allah
 
Kwenye public forums kama hizi, ili hoja iwe hoja tuache mawakili au maprofesa wasomi. Hata Lipumba ni Professor msomi.
Mwageni facts. Tuache kusema bila kuweka hizo information. Ni muhimu sana. Vinginevyo inakuwa kama ni porojo
 
Risala ile iliyosomwa na Ramadhani Madabida ilieleza dhulma wanazofanyiwa Waislam kwa miaka mingi.

Hiyo dhuluma wanafanyiwa na nani kwa lengo gani?
Na iweje wewe tu ndiyo unalalamika kila siku mbona Mimi naishi na waislam sijawahi kusikia wakilalamika kama wewe.
 
Kwenye public forums kama hizi, ili hoja iwe hoja tuache mawakili au maprofesa wasomi. Hata Lipumba ni Professor msomi.
Mwageni facts. Tuache kusema bila kuweka hizo information. Ni muhimu sana. Vinginevyo inakuwa kama ni porojo
Ndahani,
Narudia tena kukueleza kuwa ushahidi unaoutaka upo kwenye kitabu cha "Mwembechai Killings..."

Itakuwa vizuri kama utakisoma kitabu hicho usome ushahidi ndiyo uweze kusema kama serikali ilipiga marufuku chembelecho, "porojo" za Prof. Njozi au ilitishika na ukweli wake.
 
Hiyo dhuluma wanafanyiwa na nani kwa lengo gani?
Na iweje wewe tu ndiyo unalalamika kila siku mbona Mimi naishi na waislam sijawahi kusikia wakilalamika kama wewe.
Baddest,
Si kuwa husikii wanayosema ndiyo iwe hakuna tatizo.
Peleleza utajua.
 

Mzee Mohammed,
Kuna ubaya gani kutupa hiyo elimu? Hiko kitabu si hakipo sokoni?
 
Kk waislam wenyewe tumeyataka. Kulkuwa hakuna haja yule wanaomuita baba wa taifa kumuweka mbele

Sent using Jamii Forums mobile app
 
na iko siku ukweli utasimama in Shaa Allah
 
Volume 2 UNESCO history of Africa hakuna habari za Uhuru wa Africa ... we umeona wapi hizo habari
 
Volume 2 UNESCO history of Africa hakuna habari za Uhuru wa Africa ... we umeona wapi hizo habari
Claytonx,
Nami namuuliza King swali jingine.

Hivi yeye anatia wasiwasi historia niliyoandika ya watu niwajuao vyema kuamini vyanzo vingine?

Kipi kinachomfanya yeye asiniamini mimi?
 
Claytonx,
Nami namuuliza King swali jingine.

Hivi yeye anatia wasiwasi historia niliyoandika ya watu niwajuao vyema kuamini vyanzo vingine?

Kipi kinachomfanya yeye asiniamini mimi?
Hakuamini kwasababu haijui historia vizuri... mi sioni sababu ya kuendelea kuficha ukweli ... ukweli uwekwe wazi na watu wachague kuuamini au kutokuuamini lakini sio kuuficha
 
Siyo kweli Mkuu Watanganyika wote waliathirika, mpaka leo matokeo yake yako wazi,
Nyaru...
Waislam waliathirika zaidi kwa kuwa mfumo wa utawala uliokuwapo uliwatenga katika elimu.

Serikali ilitoa "grant in aid," kwa makanisa kwa ajili ya elimu na shule hizi zikawabagua Waislam.

Ili kusoma ilibidi mwanafunzi abatizwe.
Hili lilikuwa sharti gumu sana.

Kwa ujumla ikawa kama vile elimu imekabidhiwa kwa kanisa.

Shule chache zilizojengwa na Waislam zilikataliwa kupewa msaada huu.

Ndiyo maana ikawa Waislam wako mbele katika kupigania uhuru kuuondoa ukoloni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…