Ukweli ni upi kuhusu Kiswahili kuwa lugha ya kufundishia?

Kiswahili kifundishwe Kama somo Ila kisitumike katika Elimu kwa sababu kiswahili akiwezi kukupa maarifa maana vitabu vyote muhimu vipo katika kiingereza.
 
Kasi ya ukuaji wa maendeleo ya dunia hususani katika sayansi na technolojia yanaenda kasi sana kuliko ukuaji wa kiswahili na uchumi wetu. Kwaio kutumia kiswahili katika nyanja zote za elimu itakua ni sawa na kufunga tairi ya bajaji kwenye land cruiser jambo ambalo litaleta matatizo zaidi kuliko msaada. Tujipe muda muda wa kujenga uchumi wetu na kiswahili kipate kukua maradufu huenda ikafaa kutumika huko miaka ya mbele lakini sio sasa.
 
Mbona wanaopanga sera kama wajanja ,mbona wao watoto wao wanasoma shule ya kingereza tangu awali na wengine wanasoma international schools kabisa..

Mbona huu unafiki hautoisha milele ,kama tuliamua kuchukua elimu ya mkoloni why tusichukue na lugha husika kabisa.


Overhaul ya elimu ya Tanzania si kupunguza idadi ya madarasa ni kucopy na mazingira ya mwanafunzi kuelewa maudhui ya masomo katika ulimwengu wa kisasa ...Kama kingereza hata interview za leo na kazi za ofisini kinatumika ,kwa nn tusikifanye lugha ya kufundishia kutoka awali.

Mbona kenya wamefanikiwa !? Hawa watunga sera wao mbona hawaendani na sera wanazotunga ? Watoto wao wanasoma nje kabisa ili kujua lugha vizuri.
 
Kwani zimeanza kutumia lugha zao baada ya kujiweza au toka kabla katika hali kama ya kwetu ?
Korea wameanza kutumia kikorea kwenye maandishi mwaka 1444,

Tanzania tumeanza kujifunza kiswahili cha kuongea (sio kuandika) 1961,
Ukiacha na pwani maeneo mengi ya ndani watu walikuwa hawakijui kiswahili hadi miaka ya 2000 mwanzoni, sasa unataka kulinganisha mataifa hayo mawili?
China walianza way back before wakorea, same to wajapani
 
Kwa nini China, Japan, Korea lugha ya kufundishia sio kingereza wao hawataki hizo fursa za kimataifa unazo ziona wewe peke yako kwa sababu ya kingereza ?
Wao Wana vingi vinavyohitajiwa na wengi, hivyo wale wandohitaji hulamika kujifunza lugha yake.

Ndiyo maana Vuta vya Urusi na Ukraine vimetikisa Uchumi wa dunia. Lakini kama ingelikuwa ni Vuta vya Uganda na Burundi, wala isingekuwa na athari kubwa sana Kimataifa.

Hayo yote uliyoyataja ni Mataifa "makubwa".
 
Kwa hiyo tatizo lako ni kuchelewa kuanza na kuwahi kuanza sio kitu kingine ?
 
Kuandika tu kunakupa shida. Aiseeh! una matatizo mengi kuliko hiki unacho jadili.
 
Sijui wale wazee wa Bakita wanafanya nn ofisini,na mshahara wanakula,imagine Lugha imekosa mvuto endelevu ndio maana asilimia nyingi ya Watanzania wanawasiliana Kwa lugha zisizo rasmi ikiwemo kiswakinge.Ukitaka kujua hili Baraza linafanana na jipu chukulia mfano wa maneno mapya ya kizazi hiki Cha teknlojia,Decoder hawa watu wameamua iitwe kishumbuzi.
Unajiuliza walilipata wapi neno la ajabu ajabu hivyo for such cool invention??Je walichukua kisu Waka jumlisha na mbuzi au ilikuwaje?
 
Ni ccm na mauzauza yao. Wanyonge kama wanavyopenda kuitwa, watasomeshwa kwa Kiswahili, wenye nchi (ccm) wanawasomesha wa kwako kwa lugha za duniani ili watawale milele.

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo tatizo lako ni kuchelewa kuanza na kuwahi kuanza sio kitu kingine ?
Mkuu, ukizungumza kwa fact hakuna advantage yeyote ya kutumia kiswahili katika taifa hili katika ulimwengu ambao kila kukicha unazidi kuwa kijiji,
Kuna vitu sio lazima tuvilazimishe sana, halafu kiswahili sio lugha ya watanzania wengi, ni lugha ya kuja tu kama zilivyo English na zinginezo, lugha zetu ni za kikabila, then tunaanza kujifunza kiswahili ambacho kwenye historia ni mchanganyiko wa lugha ya kiarabu na watu wa pwani ya East Africa, so mtu wa kigoma zote English na Kiswahili ni lugha za kuja
 
Kwa hiyo tatizo lako ni kuchelewa kuanza na kuwahi kuanza sio kitu kingine ?
Mkuu, ukizungumza kwa fact hakuna advantage yeyote ya kutumia kiswahili katika taifa hili katika ulimwengu ambao kila kukicha unazidi kuwa kijiji,
Kuna vitu sio lazima tuvilazimishe sana, halafu kiswahili sio lugha ya watanzania wengi, ni lugha ya kuja tu kama zilivyo English na zinginezo, lugha zetu ni za kikabila, then tunaanza kujifunza kiswahili ambacho kwenye historia ni mchanganyiko wa lugha ya kiarabu na watu wa pwani ya East Africa, so mtu wa kigoma zote English na Kiswahili ni lugha za kuja
 
Sidhani Kama unaelewa ulicho andika
 
πŸ™πŸ™πŸ™
 
Fact ni kwamba mtu afundishwe kwa lugha yenye matumizi ndani ya taifa lake kwa asilimia zaidi ya 90%.

kati ya kingereza na Kiswahili ni lugha ipi ina asilimia hizo za matumizi ndani ya Tanzania ?
 
Hapa kinachofanyika na viongozi wa nchi ni kuendelea kutengeneza matabaka mawili ya watawala na watawaliwa. Hakuna mbunge wala waziri wala rais wala makamu wake wala waziri mkuu wala majaji na watu kama hao waliostaafu wanawapeleka shule za kawaida watoto wao. Wengi ni international schools au English medium schools.
Lakini cha ajabu haohao ndio wanaokomaa wanasema Kiswahili kiendelee kutumika tangu chekechea kwa sababu ndio utamaduni wetu
 
βœ…βœ…βœ…
 
Iko kisw
Iko kiswahili chenyewe unaijua mpk unaenda gombania lugha za watu
 
Fact ni kwamba mtu afundishwe kwa lugha yenye matumizi ndani ya taifa lake kwa asilimia zaidi ya 90%.

kati ya kingereza na Kiswahili ni lugha ipi ina asilimia hizo za matumizi ndani ya Tanzania ?
Maswali matatu muhimu:

Swali la kwanza: ni nani anayepigia debe utumiaji wa Kiswahili kwenye ngazi zote za Elimu?
Jibu: miongoni mwao ni wanasiasa!

Swali la pili: watoto wa wanasiasa wengi wanasoma zipi?
Jibu: shule za English Medium za ndani na nje ya nchi

Swali la tatu: kwa nini wanasiasa wengi wanapenda kuwapeleka watoto wao shule za English Medium?
Jibu: Mkuu "So special" atusaidia jibu🀣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…