Akilihuru
JF-Expert Member
- May 20, 2022
- 1,512
- 2,980
Kwema ndugu, leo nikiwa maeneo fulan nilikutana na ubishi. Ubishi huo ulitokana na baadhi ya vijana wanaoishi katika kata ya Wazo, Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es salaam.
Vijana hawa walikuwa wanabishana kuhusu maeneo fulani yanayopatikana katika kata hiyo ya Wazo ambapo wapo waliodai kwamba katika kata zote za Wazo Salasala ndio mtaa unaoongoza kwa kuwa na watu wenye hadhi au waliowahi kuwa na hadi serikalini, pia wakadai kwamba Salasala ndio inayoongoza kuwa na majumba makubwa, mazuri na ya kisasa, pia inaongoza kwa hali ya hewa nzuri na maeneo bomba ya kutulia na kupanga mikakati ya kimaisha, pia eti Salasala imechangamka hata kibiashara ukilinganisha na maeneo mengine nk.
Ghafla wakadakia wengine ambao walidai kwamba Mivumoni ndio kwenye hizo sifa zilizotajwa hapo juu,
huku mungine akisema kuwa Madale ndio moto wa kuotea mbali,
mara wengine waseme Kisanga, mara wengine eti Kilima hewa, wengine Kilima hewa juu, wengine wazo kwenyewe.
Sasa wakuu kwa wale wenyeji na wazoefu wa maeneo hayo naomba mnipe majibu ili nikirudi tena kule nikikutana na ubishi wa aina hiyo nimalize ubishi kwa kutumia fact nitazopata humu.
Kati ya maeneo hayo tajwa ni wapi pa kishua na palipochangamka zaidi kibiashara na kimaendeleo.
Karibuni tuchangie kistaarabu wakuu.