Pundit
JF-Expert Member
- Feb 4, 2007
- 3,733
- 141
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wakuu,
Nimerudi kuangalia vitu viwili vitatu inaonekana ni kweli Kambona alikuwa anataka umaarufu wa haraka. Kutoa mfano, nina ripoti moja inahusu ishu moja ya "alleged" forged documents kuhusu Marekani kutaka kupindua nchi kwa ushirikiano na wareno mwishoni wa 1964. Serikali ilipata document moja iliyokuwa inaonyesha mipango ya siri ya kupindua nchi. Kambona aliharakisha kukimbia kutoa habari OAU na vyombo vya habari kwamba Wamarekani wanapanga kupindua nchi kwa kutumia mercenaries. Wamarekani wakaleta mtaalamu wao achunguze hiyo paper, balozi wa marekani akaande moja kwa moja kwa mwalimu kumwonyesha ushahidi kwamba ni feki.
Balozi anaripoti Nyerere alishika kichwa na mikono miwili. Akamwambia balozi, and I quote: "I don't know what Kambona is doing"? Wamarekani walitaka Nyerere aseme publicly kwamba ilikuwa ni uongo. Yeye akakataa kwasababu ishu ilishafika mbali sana. It was a major diplomatic dissaster and very embarassing to Mwalimu.
Hii haikuwa mara ya kwanza au ya pili Kambona kukurupuka na kuharibu mambo. Kuna mifano mingine. Nyingine ilitokea 1960 wakati Nyerere amesafiri. Kambona aliwaambia wakoloni tunataka uhuru sasa hivi na alikuwa anaoongea kama mmoja wa viongozi wa chama. Huo ulikuwa wakati Nyerere ana-negotiate na U.K. kuhusu uhuru. Ikaja kuleta matatizo mengi. Kwa ujumla ni kwamba Kambona alikuwa anakosea stepu wakati mwingine. Na nakubaliana nanyi kwamba inaonekana alikuwa anataka umaarufu.
Hii ripoti ninayo. Kinachonisikitisha ni kwamba Bongo hizi ripoti wanaficha, lakini ulaya na kwengine zinapatikana. Mengi wasiyotaka kuongelea yapo kwenye ripoti za nje. Siwalaumu sana, lakina kuna mengi mazuri nchi yetu ilifanya lakini ni vigumu sana kupata access ya data na kuandika hizo historia. Matokeo yake ni kwamba tunaachwa kwenye giza.
Mkuu marehemu Chiume, alisoma bongo na kuwa waziri wa Malawi, Nyirenda na Kambona, walikuwa ni wa-Malawi, lakini ninaaamini kuwa wanavyo vijiji bongo
Mbona Lusinde na Cigweyemisi wanadaiwa vilevile kuwa ni Wamalawi.
Babu/Baba yao alikuja Mvumi kama Mmisionari. !
[/B][/I]
Ukienda nyuma kidogo utasema Wangoni ni Wazulu, Nyerere ni Mtutsi etc etc
Kwa mtaji huu wabantu wote Wa-Nigeria /Cameroon, si wametokea nyanda za Jos huko?
Wakina Cigwiyemisi walizaliwa na kukulia Dodoma, baba yao alikuwa anakaa karibu sana na Chief Mazengo.It doesn't get any more authentic than that.
Bin Maryam,
Nimejaribu sana kusoma kuhusu mapinduzi ya Zanzibar na maasi ya 1964. Sijaona jipya lililosemwa hapa.
Hebu tuambie: kulikuwa na sababu gani ya kupindua serikali 1964? Ulikuwa unataka tutawaliwe na Sultani nini?
Ni kweli Marekani ilifanya mambo mengi ya kijasusi Afrika kipindi kifupi 1960-66, ikiwa ni pamoja na kumtoa Nkrumah. Kuhusu Western Plot ya 1964, nimeona documents nyingi, na nime-conclude kwamba haikuwa na ukweli. Kwanza, Top Secret document niliyo quote hapo juu ya wamarekani inaonyesha walikuwa tayari kutumia jeshi lao kurudisha serikali mapema 1964. Katika vita baridi, Nyerere aliweza kuwamuda east/west vizuri. Pili, viongozi wa serikali, including Nyerere, walikuja kusema documents zilikuwa feki. Lukumbuzya, alimpa balozi wa marekani barua ya serikali kumaliza hiyo ishu ya plot Novemba 1964. Wakasema wanaomba mambo yaishe. Wamarekani wakataka Nyerere aseme publicly, yeye akakataa. Tatizo likaamka tena Desemba 9 UN wakati Permanent Representative wa TZ aliposema plot ilikuwa kweli. Mchana wa Desemba 9, ikabidi Nyerere aongelee tena hiyo ishu kwenye speech yake ya independence rally. Akasema serikali imetuma barua US na these exchanges will be the end of this thing.
Kama una data, sio speculations, sema tujifunze.
1960 Kambona alichemsha. Nyerere alikuwa ana-negotiate details za uhuru, na yeye akaweka demands bila kujadili na viongozi wa TANU. Statement yake ika-complicate negotiations za uhuru.
[/B][/I]
Ukienda nyuma kidogo utasema Wangoni ni Wazulu, Nyerere ni Mtutsi etc etc
Kwa mtaji huu wabantu wote Wa-Nigeria /Cameroon, si wametokea nyanda za Jos huko?
Wakina Cigwiyemisi walizaliwa na kukulia Dodoma, baba yao alikuwa anakaa karibu sana na Chief Mazengo.It doesn't get any more authentic than that.
Alnadaby,
Watanzania si watu wenye fikra duni kama unavyotaka tuamini. Na hii ya kumpakazia Mzee wa watu Mchonga kuwa ndiye alitufanya tuwe na fikra duni, miaka 22 tangu aachie ngazi na miaka nane tangu afariki ni kuashiria kwamba hata wajukuu zetu watakuwa watu wa fikra duni. Na kwa mantiki hiyo Watanzania wataendelea kuwa watu wa fikra duni. I am not buying that.