Wakuu,
Hii thread inakataa kona nyingi. Nafikiri itakuwa jambo la busara kama tukifungua thread nyingine ya 1964 Army Mutiny. Je Kambona alihusika vipi na maasi hayo? Sina uhakika kwa kweli. Lakini nikiangalia data nilizoweza kupata, siwezi ku-speculate kwamba Kambona alikuwa na mipango yake mwenyewe. Ndio kuna maswali bado sijapata majibu yake. Lakini kwa sasa naacha hivyo mpaka pale nitapopata ushahidi zaidi.
Kurudi kwa Kambona, kuna article nimeandika lakini siwezi kuweka hapa mpaka ikichapishwa. Kuna mengi ningependa kusema lakini kwa sasa nitasema machache tuu.
Kulikuwa na power struggle kati ya Nyerere, Kambona, na Kawawa. Nyerere na Kawawa walikuwa pamoja. Hiyo struggle ilianza pale Kambona alivyorudi kutoka London. Alirudi baada ya kufeli mtihani wake wa mwisho kule. Katika mvutano wa power, Kambona akawa na kikundi chake kilichojulikani kama vijana "radicals." Hawa walikuwa wanataka mabadiliko makubwa ya haraka. Kuna baadhi ya mawazo yao yalikuwa mbali, lakini mengine walikuwa wanalazimisha haraka. Hilo lilimtia Kambona katika matatizo na wazee wa TANU. Nyerere hakuwa pekee kupingana na Kambona. Aliyekuwa anafanya mipango mingi ya kumtoa Kambona alikuwa ni Kawawa. Yeye alikuwa anaongea na wazee ambao wakawa tayari kumtoa Kambona. Na Kambona kwa upende wake, alifanya makosa mengi ambayo yaliwapa sababu adui zake kumtoa.
Kambona alikuwa on top wakati alipokuwa Chairman wa ALC, na alipofanya mipango ya kusaidia mapinduzi ya Zanzibar na muungano. Alimtumia rafiki yake Harue Tambwe, Commissioner wa Tanga, kuongea na Hanga baada ya mapinduzi. Hanga alikuwa roommate wa Kambona London wakati anasoma. Na pia alikuwa on top wakati wa maasi ya jeshi. Aliweza kuongea na wanajeshi akawapooza mpaka pale Nyerere alipopata nafasi ya kuwaita waingereza kuzima hayo maasi. Pamoja na kwamba yeye alisaidia kusuluhisha hilo tatizo kama Minister of Defense, naona intelligence system yote ili-fail; yeye, Lusinde, C. Mzena na wengine walikuwa gizani, lakini pia kuna baadhi ya ripoti ambazo zingewapa clues wali-ignore. Zaidi ya hapo sijaona ushahidi wowote. Siwezi kutoa speculations.
Januari 22, Nyerere alitembelea sehemu zilizoshambuliwa na wanajeshi. Alikuwa na mke wake na Lusinde. Tukumbuke hiyo ilikuwa baada ya maasi kuanza. Wakati huo Nyerere alikuwa analala State House. Kwa siku mbili, kuanzia January 20 mpaka 22, Nyerere hakuwa mafichoni. Kama kulikuwa na mpango wa kumuua nafikiri wangemuua. Ila ni kweli kwamba situation ilikuwa inazidi ku-deteriorate. Hata kabla Nyerere hajaomba msaada wa jeshi la waingereza, according to the National Military Command Center, Joint Chief of Staff report, balozi wa uingereza alishaomba jeshi lao liwe karibu kuokoa maisha ya raia wao na wamarekani.
Kusema kweli hawa wanajeshi wa TNG wasingefika mbali. Waingereza na Wamarekani walishaanza kuleta majeshi yao kuzima maasi. Waingereza waliita vikosi vyao viliyokuwa Kenya on January 20 vije karibu na Dar: 4940 regular soldiers, 3230 Gurkas and Colonials, na walikuwa na 5 Beverly type aircraft, 6 Twin Pioneers. Kwa wamarekani, USS Manley ilkuwa 1000 miles northeast of Dar es Salaam. State Department ikaomba ipelekwe Dar on Jan 20 ikutane na British HMS Rhyl ambayo tayari ilikuwa maeneo ya Dar. Top Secret American document "CINSTRIKE/USCINCMEAFSA OPLAN" inasema ifuatavyo: "purpose-to provide for either US assistance to UN sponsored action in Tanganyika or U.S. unilateral action in conjunction with friendly forces in Tanganyika, to restore order and maintain or re-establish the legitimate government. Mission: conduct operations to neutralize or destroy dissident forces, to prevent entry or seizure by Communist or other forces, to restore order and to assist in maintain or re-establishing the legitimate government of Tanganyika." Kama waingereza wasingekuja, wamarekani wangekuja. Na tukumbuke jeshi la Tanganyika likuwa dogo sana wakati huo. Sio zaidi ya 1000 kama sijakosea. Kwa wale wanao-speculate kwamba Kambona alikuwa na mipango mingine, inawezekana alikuwa anafahamu kwamba west ililikuwa tayari kutumia nguvu kurudisha serikali.
Baada ya kufikia apex ya power na popularity January-April 1964, Kambona akaanza kuporomoka pole pole. Hii inaweza kuwa na sababu tofauti. Pengine alioona yupo juu sana na akawa anafanya maamuzi makubwa ya serikali bila kujadili na wakubwa wengine; pili kuna uwezekano wakubwa wenzake walimwonea wivu baada ya maasi na wakawa wanamtafutia sababu ya kutoa.
Kwa upande wangu naona turning point ilikuwa jinsi alivyo-handle "Western Plot" Novemba 1964. TANU National Executive Council ilikutana Desemba 16-18, 1964 kukawa na motion ya kum-discipline Kambona kwa jinsi alivyo handle "Western Plot." Sina uhakika nani aliweka hiyo motion, lakini nafikiri ni Peter Siyovelwa (1970s alikuwa minister responsible for Usalama). Motion ya kum-censure Kambona ikapita. Baada ya hayo yote, aliachiwa aendelee na kazi yake. Lakini mambo yalikuwa hayajaisha. Machi 5-8, 1965 TANU Annual Conference, wazee wa TANU wakaja juu. Wali-recommend Nyerere amtoe Kambona kwa jinsi alivyo deal na "Western Plot." Behind the scene engineer alikuwa Kawawa.
Stormy Cabinet meeting ikafanyika March 9-10, 1965. Usiku wa March 10, mkutano wenye mvutano ukaendelea; kikundi kimoja kilikuwa na Nyerere, Kawawa na wengine na upande mwingine Kambona, Lusinde, Babu, Kamaliza, Maswanya na wengine. Mwishoni upande wa Nyerere ukashinda. Uamuzi ukawekwa Kambona atolewe na aingizwe Sijaona. Baada ya yote hayo, Nyerere hakumtoa Kambona. Babu aliweza kumshawishi Karume amwambie Nyerere huu sio wakati wakubadilisha serikali na kama atafanya hivyo atahatarisha muungano.
Kambona alikuwa na maadui wengi TANU. Wazee wa TANU walitaka atolewa tangu 1964 na Nyerere alikataa mpaka 1966 walipoanza kushtuka na kukutaa Kambona alikuwa na 50,000Sterling pounds akaunti yake pale Tanzania. Serikali ika-freeze hiyo akaunti wakati Kambona yuko Holland akipata matibabu na wao wakifanya uchunguzi. Sikubali kwamba Kambona hakuwa na pesa. Hata kama aliishi kimaskini Uingereza. Sources zinasema alikuwa na cash nyingi sana Nairobi baada ya kutoroka 1966. Nimeona barua aliyoandika Kambona anamtumia Kwame Nkrumah pesa Guinea 1968. Na 1969, Kambona alimwonyesha P.K. Leballo $70,000 cash ambazo alikuwa anatakaa kutumia kwa mipango yake ya kupindua nchi. Mzena alitoa ushahidi huo alipoenda mahakama wakati wa kesi ya 1970.
Kwa ujumla wengi waliokuwa katika kikundi cha "radicals" hawakufika mbali. Wote walikwisha. K. Geugeu, Eli Enangisye, Michael Kamaliza, Chipaka brothers, Gray Mataka, Bibi Titi Mohamed, Hanga, Babu, Tambwe, Major Herman, Colonel Chacha, wote walikuja ku-losti. Mpaka Director of CID, Akena, alitiwa ndani kwa kum-tip Kambona kuhusu arrest warrant. I.M. B. Munanka nae alikuwa suspect kwa sababu ya uhusiano wake na Kambona. UCLA trained Dr. Wilbert A. Klerruu alipewa posti nzuri 1966, ingawa alikuwa upande wa Kambona. Aliuliwa baadaye katika hali ya utatanishi 1973. Inasemekana mkulima aliyemuua Dr. Klerruu alikuwa mmoja wa watu wakwanza kunyongwa na serikali.
Kuna mengi ya kuendelea, lakini ngoja niishie hapo. Kambona aliharibu sana pale alipotaka kujaribu kupindua nchi pamoja na kuwa na mawazo mengine mazuri. Kwa hilo alichemsha sana. NO EXCUSE FOR THAT!