Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona?


Comredi Maswali:

Naona unarudi yale niliyosema. Nilisema sina source na watanzania wengi pia hapa hawana source. Vilevile tupo wengi tuliozaliwa muda mrefu baada ya haya matukio kutokea.

Source na data unazoleta zinakubalika, ingawaje hatuna njia ya kuhakiki. Lakini kisichokubalika mtazamo au tafsiri ya source na data zenyewe kwa wakati wa sasa.

Kwa kipindi cha sasa ambacho tunaona viongozi wengi walivyoboronga hatuwezi kukubaliana na tafsiri zao kwa Kambona alikuwa mtu wa kupenda ujiko au mwenye tabia mbaya.

Mtu anaposema Kambona alichemka mwaka 1960 kwa kutoa matamshi ya kudai uhuru wakati Nyerere yuko UK, nitamwona kuwa ana matatizo fulani. Kwa mtazamo wa sasa Kambona was ahead of his time kwa kutumia haki yake ya kuzungumza. Ni watanzania wangapi waliweza kusema tunataka uhuru wetu mbele ya mkoloni miaka hiyo?

Je hao waliokaa kimya wakimsubiri Nyerere wamelisaidia vipi taifa? Nachoona wamejenga taifa lenye nidhamu ya woga tu. Hivi Kambona angekuwepo kwenye baraza la JK si angemwambia kuwa JK unachemsha BIG TIME bila kuona aibu?

Kwa kukupa mfano kuna watanganyika waliosema kuwa uhuru wa mwaka 1961 ulikuwa unatolewa mapema. Ukichukua mtazamo wa miaka ya 1960 unaweza kusema hawa jamaa walikuwa wasaliti. Lakini kwa sasa hivi inaonyesha kabisa uhuru tulipata mapema.


Kitu kingine cha maana cha kuangalia kuhusu Kambona ni fani aliyosomea. Ingawaje alipata matatizo ya kumaliza shule, Kambona alisomea sheria. Kati ya marais 43 wamarekani 25 walisomea sheria. Viongozi wa nchi nyingi za ulaya ni wanasheria.

Waliosomea sheria wanaangalia maisha kutoka view points mbalimbali na wako huru kuzungumza mawazo yao na inawezekana kama maisha ya Kambona yalikuwa magumu kwa kufanya kazi na watu ambao wana mtazamo mmoja kama Nyerere na Kawawa.

Kuhusu source unazoleta endelea kuzimwaga na ninasaidia sana na ikiwezekana zilete kama zilivyo bila kufanya harmonization.
 
Maalim Bin Maryam:
Ni kweli kwamba haitakiwi kuangalia data za zamani kwa mtazamo wa sasa. Hapo tupo boti moja.

Labda nifafanue zaidi kuhusu 1960. 1960 Nyerere alitumwa na TANU kwenda ku-negotiate na wakoloni kuhusu uhuru. Uamuzi ulishafanywa kwamba uhuru tutapewa; swali lilikuwa tarehe ngapi, serikali itakuwa vipi, pesa zitatoka wapi n.k. Wakati mwenzake anajadili hizo details, yeye akaweka demands nyingine nyumbani bila kujadili na viongozi wa chama. Hilo likafanya mazungumzo yawe magumu kidogo. Huo ni mfano mmoja nilitoa kuonyesha kwamba Kambona alikua anakosea stepu saa nyingine.

Kama nilivyosema hapo awali. Kuna mengi Kambona alifanya yanafurahisha, ikiwa ni pamoja na uongozi wake wa ALC. Kuna wanao-criticize uongozi huo lakini mimi naona alifanya mengi mazuri.

Kuhusu upinzani wa Kambona kwenye sera za Ujamaa, mimi naona hili itabidiwa liangaliwe tena kwa makini. Kuna uwezekano alikuwa opportunist kwenye hilo baada ya mambo yake kuharibika. Nasema hivyo kwasababu alikuwa karibu sana na Nkrumah. Kuna barua nimesoma alimwandikia Nkrumah anasema anataka socialism. Inaonekana alikuwa anapendelea eastern bloc. Huku ana-attack Nyerere's Ujamaa, kule anaongelea anataka socialism. Sasa sera za socialism nazo zingetupeleka mbali kweli kama Kambona angekuwa Raisi?
 

Mimi nimesoma shule katika nchi ya wazungu ya kibaguzi. Nakumbuka wakati mwingine grade zangu katika masomo mengine nilibaguliwa.

Kuna watu hapa wanasema Kambona alichemsha shule. Lakini tukumbuke kuwa Kambona alikwenda kusomea sheria na kwa kipindi kile mwaafrika alikuwa hatakiwi kuwa mwanasheria na ma-profesa wengi wa sheria walikuwa ni watu wa upper-class. Hivyo, kuna uwezekano mkubwa pia experience yake ya shule ilimfanya aingie kwenye u-radical fulani.

Nyerere alisoma social science na walimu wengi wa social-science wamelenga sana upande wa kushoto. Hivyo experience yake ilikuwa nyingine.

Najua umepitia Not-Yet-Uhuru. Kwa matokeo ya shule tu na GPA, Odinga alikuwa mkali kuliko wanafunzi wengi kule Makerere. Lakini mtazamo wake wa kuwa mwafrika asilia na kubatizwa kwa jina la kiafrika kuliwastua wazungu. Pamoja na mafanikio yake hakupewa nafasi ya kusoma zaidi na wale waliokuwa chini yake na kukubali uzungu walipewa nafasi za kuendelea zaidi.

Mwalimu kwa namna fulani aliukubali uzungu. Sijaona kitabu chochote kinachoonyesha alikuwa na u-radical wa kiafrika akiwa Tabora au Makerere. Na kwa mtaji huu alipata nafasi za kusoma. Na hata TAA ilipobadilika kuwa TANU kitu cha kwanza ni kukubali wanachama wasio na asili ya kiafrika kitu kilichowahudhi baadhi ya ma-radical. Na hii pattern inaendela mpaka sasa, ukiwa mwanafunzi radical you go nowhere.

Katika kusoma na kufanya kazi na wazungu, waafrika wamekuwa na experience tofauti na hizi experience zimewafanya baadhi kuwa ma-radical na wengine kuwabeba wazungu. Hivyo basi, experience za maisha ni lazima vilevile zitumike katika kutoa hoja.

Kuhusu Kambona kufuata U-socialist, tusitoe hukumu kwa yeye kuwa na fikra tu kwani Léopold Senghor alikuwa m-socialist aliyeamini vyama vingi na uhuru wa vyombo vya habari. Na kulikuwepo uwezekano mkubwa kwa Kambona kuwa m-socialist na kujali haki za watu kuliko kuwa mjamaa mwenye kuongoza nchi kwa muundo wa baba paroko.
 

jee si kweli hoja ya kutaka uhuru wa tanganyika ucheleweshwe kama ikibidi kuwangoja kenya na uganda haikumletea mwalimu matatizo kwenye tanu? hoja hii haikuwa ya tanu. na mwalimu kwa kujua hili ilibidi aisambaze sekretariati/kamati kuu ya tanu ili kuwavunja nguvu wale waliotaka mkabili na hili. sasa kama huu ndio ukweli kambona alikosea nini kuweka madai hayo? jee nyaraka zinasema nini kuhusu hili?
 

Ni kweli Nyerere alisukuma ishu ya East African Community, na alisema yuko tayari kusubiri mpaka Kenya na Uganda wawe tayari. Alivyoulizwa na moja ya magazeti, nafakiri ilikuwa London Times, akasema hiyo ni personal opinion yake mwanzoni. Alikuwa hajaongea na viongozi wengine kuhusu hilo. Hapo hamna utatanishi. Ila, itabidi nirudi kuangalia tarehe gani alitoa wito huo na lini alienda London ku-negotiate na Sandys. Hizo negotiations za uhuru zilikuwa very delicate.

Nina data za kuonyesha Kambona ali-support East African Community. Tena yeye alikuwa mmoja wa viongozi waliokuwa mstari wa mbele akisafiri Kenya/Uganda mara kwa mara kujadili hilo. Baadaye akamwandikia Nkrumah (1968/9) kwamba EAC ilikuwa ni plan ya imperialist powers.
 


Kuhusu Kambona kufeli mtihani wake wa mwisho London, naona unatoa speculations. Tunaweza kutoa speculations mpaka kesho. Lakini kuna uwezekano kuwa wazungu hawakutaka amalize kama ulivyosema. Na nina data inayoweza ku-support hilo. Kulikuwa na German doctor alimtibu Kambona 1964 TZ. Huyu daktari alikuwa na training ya psychiatry akawapa wakubwa ripoti. Alisema experience ya Kambona London na wazungu ilikuwa mbaya ikampa "complex" kubwa. You might be onto something here.

Mimi sijatoa hukumu kuhusu Kambona na demokrasia. Nimeuliza swali. Lakini ukisema pengine angefuata muundo wa Senghor, ambaye ali-retire France na kufia France, basi ukubali kwamba kuna uwezekano Kambano angeweza kuwa dikteta. Vyote vinawezekana.
 


Ni speculation tu lakini sio conclusion. Lakini kwa macho yangu nimeshuhudia vijana wa kiafrika wakibadilika na kuwa na u-radical kutokana na exprience ya maisha yao Ulaya. Kambona ata kama alishindwa shule kutokana na uwezo wake, lakini mazingira aliyosomea yatamfanya aamini kuwa kulikuwa na njama.
Haya mambo nimeyaona kwa baadhi ya vijana wa kiafrika wanaosoma Ulaya na Marekani.

Taarifa zilizokuwepo mitaani ni kuwa Kambona hakutaka Ujamaa. Na vile vile sijaona kazi yoyote ya kitaaluma aliyoandika kuhusu mambo ya siasa, kama unayo naomba utupe rejea. Viongozi wengi wa kiafrika ambao hawakuwa na kazi zao za kishule zilizohusu siasa za ujamaa, waliingia moja kwa moja kwenye Marxsim na Leninism. Matokeo ya Marxsim na Leninism kwa nchi za kiafrika yalikuwa ni vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyochukua miaka mingi kwisha. Kama una uhakika kwamba alikuwa anataka socialism basi matokeo yasingekuwa mazuri.
 

Maswali:

Nadhani jambo la Africa mashariki lilikuwa mezani na aliongea na viongozi wengine. Sina kumbukumbu ya sehemu niliyosoma hizo lakini Nyerere alisema Mzee Karume hakuwa na matatizo na alisema Nyerere wewe utakuwa rais.

Na katika sehemu nyingine niliyosoma, Nyerere na Obote walikwenda kumuona Jomo Kenyatta kuhusu shirikisho, Mzee Jomo akakataa.
 
Sera ya Socialism ni nzuri sana kwa rais kwa sababu anatukuzwa, kuheshimiwa na kuogopwa kama Munguni, ni nzuri sana kwa sababu in a way unakuwa kama umejihakikishia kit cha milele, kwa hiyo mtu yoyote mwenye prospects za kuwa Rais au hata akiwa rais atakubali socialism. Lakini kwa wananchi ni system mbya sana mabyo imejaa uuaji, ukatili na umaskini. Marshal ES anaweza kueleza vizuri, sisi wengine ujamaa wa Nyerere tumefeel umaskini wake lakini fear walifeel wengine!
 

Umeni quote vibaya...soma tena nilivyoandika Jasusi.Sikutaja Watanzania wote bali wengi wao.
Wengi wetu tumerithi hali ya woga uliopandikizwa na utawala wa chama kimoja chini ya Mwalimu na hilo ndilo tatizo la kukubali kuongozwa na Chama hicho hicho miaka nenda rudi hata kama kwa wakati huu tuna mfumo wa vyama vingi.Hatuwezi kuchagua Chadema kwa mfano kwa sababu tumekuwa brain washed na legacy ya Mwalimu.

Ni kwa vipi nchi hii kubwa isiweze kuwa na wabunge japo 40% kutoka Chadema au CUF? Hebu jiuilize ! Ni kwa sababu tuaamini sana sera za CCM au tuna mapungufu kwenye kufikiri na kuchanganua mambo?

Wakati majirani walidai katiba mpya na wakaunda jopo ambalo lilitayarisha report iitwayo BOMAS..na kisha wakafanya baadaye referendum ya kikatiba mwaka 2005 sisi tumefanya nini kama Watanzania?
Kama wewe ni Mtanzania hasa unaweza kunieleza sisi tuna bahati mbaya au tuna kasoro zipi zinazotufanya tukubali kuwa katika hali tuliyo nayo sasa hivi?

Je ni asilimia ngapi ya wananchi wangapi unaweza kuwasimamisha barabarani ukawauliza nini maana ya katiba ya nchi wakakujibu kwa usahihi?

Tuna mapungufu na mapungufu hayo ni matokeo ya utawala wa Mwalimu katika miaka 25 ya awamu ya kwanza.Mawazo ya ukiritimba,elimu ya siasa ya wakati huo na woga mkubwa uliowekwa ndani ya mioyo ya Watanzania na utawala huo bado vitaendelea kuchangia katika kutufanya watu tusiokuwa na uwezo wa kuamua nini cha kufanya.
 
Alnadaby,
Hii mara ya pili umeelezea vizuri zaidi. Ungeyasema hayo mwanzoni wala nisingekuwa na comment. Ila bado ninajiuliza, hivi tatizo na kasumba ya Mwalimu au tatizo ni ukosefu wa uongozi wenye vision nchini? Kama tatizo ni kasumba ya Mwalimu, ambayo imekolea hata kwenye vichwa vya wajukuu zetu basi tumekwisha. Lakini ikiwa tatizo ni uongozi usiokuwa na vision basi bado kuna matumaini. Mwalimu alifanya kwa kadri ya uwezo wake katika mazingara ya wakati wake. Mwalimu alikuwa mtu wa kwanza kukasirishwa na vitendo vya viongozi walioiga "mabaya" yake. Alilisema hilo kuhusu Mkapa. Na sababu mojawapo ya kuachia ngazi ni kutoa nafasi kwa wengine wajaribu mambo "mbadala" kwa ajili ya Tanzania yetu. Hiyo ndiyo changamoto ya kizazi chetu na vizazi vijavyo. Ningependa kusikia mtu anasema hapa Mwalimu alikosea hivi na mimi nitajaribu kurekebisha hivi. Lawama peke yake hazitufikishi popote. Tanzania must move forward.
 


Comredi (Kamarada) Jasusi:

Ngoja nikupe analogy. Nikiwa boarding nilikuwa na rafiki wa kijaluo. Huyu jamaa alikuwa anakuja shule kimasikini sana na akatoa historia ifuatayo. Baba yake alikuwa na mbuzi wengi, wakati kaka yake aliyemtangulia anaoa alitumia mbuzi kulipa mahari. Kwa bahati mbaya baba akashikwa na ugonjwa na akaacha wosia kwamba mbuzi waliobakia ni wa mtoto wake aliyebakia (rafiki yangu) na watumike kwa mahari.

Wakati rafiki yangu anamaliza darasa la saba, baba alikuwa amefariki zamani na yeye akataka kutumia urithi wake kwenda shule. Akimwambia kaka yake auze mbuzi kulipia shule kaka akawa anakataa na kusema mbuzi hawa ni wa mahari. Basi jamaa ikabidi awe anarudirudia shule mpaka akafaulu kusoma shule ya serikali.

Akamuuliza kaka yake, sasa nakwenda shule ya serikali unaweza kuuza mbuzi angalau wawili nipate mahitaji ya shule. Kaka akasema mbuzi hawa wanasubiri ndoa na hakuna atakayetoka. Jamaa akaja shule akasoma kwa taabu na akapata nafasi ya ualimu. Wakati huohuo mbuzi wakawa wanazaa lakini kaka akawa anampa mdogo wake hesabu hilehile alioacha baba.

Tukirudi kwenye hoja. Muundo mzima wa serikali na Chama tawala aliounda Nyerere ni kama mbuzi wa urithi na walio madarakani sasa ni kama kaka zetu wanaojifanya kuulinda urithi kwa manufaa yetu.

Nyerere alikuwa na nafasi kubwa ya ku-influence mabadiliko ya katiba lakini alihamua kuacha. Kama alikuwa na uwezo wa kutoa lawama kwa Mwinyi au Malecela, alikuwa na uwezo mkubwa wa kuona kuwa muundo wake wa utawala ulikuwa haifuhi.
 
Ni wazi kwamba Kambona anahitajika kuwemo kwenye hisoria ya nchi yetu kama mmojawapo wa wanaharakati wa demokrasia!Ni wazi historia ya Kambona ilichafuliwa kwa makusudi na watanzania kufichwa ukweli kutokana na utawala wa kiimla wa kijamaa..Tunakopitia na kuelekea hivi sasa ni huko ambako Kambona alitaka tupitie miaka hiyo ya 1960's mara baada ya uhuru.Alikuwa na nia nzuri na taifa lake!Alikuwa mkweli na mwenye utu..pia muungwana!Ni wazi kuwa kama angekuwa na nia mbaya ya kumpindua Nyerere angeweza kufanya hivyo kwani alikuwa na nafasi hiyo!Lakini uchu wa madaraka na wasiwasi wa kutokaa madarakani kwa muda mrefu kulimfanya mwalimu kuwa na wasiwasi na kumsema kuwa Kambona sio mtu mzuri kwani anasikilizwa kuliko yeye..hivyo akaamua kujilimbikizia madaraka na kuanzisha utawala wa kidikteta hivyo kupeleka wasiwasi wa hali ya juu kwa Bw Kambona ambaye aliamua kukimbilia nje ya nchi kwa usalama wa maisha yake!
 
nasikia mzee kambona na mzee kawawa walikuwa hawapatani
Kawawa ndiye alikuwa pioneer mkuu wa vurugu zote hizo..nafikiri alimjaza mwalimu maujinga wakati wakiwa wamejificha kule kigamboni mara baada ya jeshi kuasi..nafikiri alimwongezea mwalimu wasi wasi kwa kumwambia mbona Kambona yeye hawaogopi wananjeshi hao na ni kwanini wanamsikiliza!
 
Mushi1,
Tofauti kati ya Kambona na Nyerere zilianza baada ya Azimio la Arusha. Kambona alipinga ile kanuni ya maadili ya uongozi kwa sababu wakati huo yeye na Bibi Titi walikuwa wameanza kujenga majumba Darisalama. Hii ya kusema kuwa Kambona alikuwa mwanademokrasia ni spin tu za kuandika historia upya. Sababu nyingine iliyopelekea kutofautiana na Nyerere ilimhusu Kawawa. Kambona hakumpenda Kawawa kabisa na ni kama Nyerere aliweka msumari wa mwisho katika jeneza pale alipompa Kawawa cheo cha ukatibu mkuu wa TANU, nafasi ambayo alikuwa anaishikilia awali Kambona. Nawashangaa wanaosema kuwa Kambona alikuwa mwanademokrasia kwa kuwa tu alitofautiana na Nyerere.
 
UKWELI NI KWAMBA MALI ZOTE ZILITAIFISHWA NA SASA ZIMEBINAFSISHWA AGAIN!KAMBONA WAS RIGHT!UNGEKUTA TUNA MAENDELEO ZAIDI KWANI TUNGEKUWA NA UFAHAMU MKUBWA ZAIDI WA KUUJENGA UCHUMI WETU!ALIYOKUWA AKIYAPIGANIA KAMBONA BACK IN A DAY NDO TUNAYOYAFANYA HIV SASA..LAKINI TOO LATE!MWALIMU ALIAMUA KUKUMBATIA MFUMO WA KIJAMAA ILI AWEZE KUCONSERVE FULL POWER OVER EVERYBODY..KAMBONA ALIONA HUO NI MWELEKEO WA KIDIKTETA!KAMBONA NI MWANAHARAKATI NA ANASTAHILI KUANDIKWA VYEMA KWENYE SIASA ZA NCHI YETU!
 
hivi hapa tuli-conclude kitu gani vile??!! kwamba Kambona historia impe au isimpe?
 
hivi hapa tuli-conclude kitu gani vile??!! kwamba Kambona historia impe au isimpe?
HISTORIA IMPE NAFASI KWANI ALIITAKIA MEMA NCHI YAKE JAMANI!TUSI MTREAT MTANZANIA MWENZETU KAMA VILE HASTAHILI HESHIMA KWA YALE ALIYOKUWA AKIYAPIGANIA!TUSIFANYE HIVYO KWASABABU TU TULIKUWA BRAINWASHED BILA KUPATA UKWELI KAMILI TULIIMBISHWA NYIMBO ZA KUMTUSI NA KUMKASHFU MTU AMBAYE KUSEMA UKWELI NIMEGUNDUA HAKUWA MBAYA KIASI HICHO!
 
Hii thread iko hapa labda kwa sababu kuna watu wanapenda kulia zaidi na kukosa haja kwa hiyo wakaishushia hadhi yake.
 
Ni muhimu kuandika historia upya kwa mambo mengi tuliyo ambiwa kiimla.Watu tumekalilishwa mambo bila kujua ukweli,hongera JF kwa kutufumbua wengi.Kwa mfano hivi kweli yule jamaa aliongoza mapinduzi pale kisiwani? mbona kuna habari kuwa Mganda mmoja ndiye aliyeongoza na hakuna anayekanusha? Au jina Tanzania ni nani alitunga mbona hatuambiwi? Hivi ni kweli jamaa alijiuzulu Uwaziri mkuu wa kwanza au kulikuwa na mshikeli ndani ya bunge kuhusu Wazawa wenzake? Jamani wenye uwezo waandike historia vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…