Bin Maryam
JF-Expert Member
- Oct 22, 2007
- 685
- 13
Bin Maryam,
Kuna system ya kuchambua data kutafuta ukweli. Kwa mfano, fani ya Political Science ina methodology yake ya kuchambua data; hilo ni kweli kuhusu fani zote nyingi. Unaposema wakati wa kusoma makaratasi umepitwa, sijui unataka nini sasa? Data zipo, na kuna njia ya kuchambua hizo data kutafuta ukweli. Unaposema haitakiwa kusoma data sasa hivi na kuwa na mtazamo wa zamani, mimi ningependa kukutaarifu kwamba unaposoma data za zamani ni lazima uziangalie kwa mtazamo wa kipindi unachoongelea. Naona sasa tunacheza sarakasi na maneno tuu. Hamna cha msingi kinachosemwa.
Alnadaby,
Kusema watu wanajipendekeza kutokana na umaskini sio kweli. Tanzania ni nchi maskini. Lakini ukumbuke sisi hatuko pekee. Nchi gani Afrika iliendelea sana kipindi cha 1960s na 70s? Wengine wanasema maskini wakati wanamapesa ya mafuta. Whatever you say about Nyerere's handling of the mutiny, he came on top when its all said and done.
YournameisMINE,
Bila kuangalia Nchi zote za Africa zili-fair vipi kwenye hicho kipindi na kuchambua umaskini wa bara zima, hatutaweza kuendelea kamwe. Tanzania haikuwa pekee. Jiulize kwanini? Kuna matatizo ambayo nchi zote za Afrika zimepitia na zinaendelea kupitia leo. Wale waliokuwa wanadai u-capitalist mbona hawajaendelea? Sera za Nyerere pekee sio sababu hatujaendelea. Neither socialist nor capitalist leaning African states have developed when compared to the rest of the world. Put it in a larger context and lets begin to analyze "why" and "how"
Comredi Maswali:
Naona unarudi yale niliyosema. Nilisema sina source na watanzania wengi pia hapa hawana source. Vilevile tupo wengi tuliozaliwa muda mrefu baada ya haya matukio kutokea.
Source na data unazoleta zinakubalika, ingawaje hatuna njia ya kuhakiki. Lakini kisichokubalika mtazamo au tafsiri ya source na data zenyewe kwa wakati wa sasa.
Kwa kipindi cha sasa ambacho tunaona viongozi wengi walivyoboronga hatuwezi kukubaliana na tafsiri zao kwa Kambona alikuwa mtu wa kupenda ujiko au mwenye tabia mbaya.
Mtu anaposema Kambona alichemka mwaka 1960 kwa kutoa matamshi ya kudai uhuru wakati Nyerere yuko UK, nitamwona kuwa ana matatizo fulani. Kwa mtazamo wa sasa Kambona was ahead of his time kwa kutumia haki yake ya kuzungumza. Ni watanzania wangapi waliweza kusema tunataka uhuru wetu mbele ya mkoloni miaka hiyo?
Je hao waliokaa kimya wakimsubiri Nyerere wamelisaidia vipi taifa? Nachoona wamejenga taifa lenye nidhamu ya woga tu. Hivi Kambona angekuwepo kwenye baraza la JK si angemwambia kuwa JK unachemsha BIG TIME bila kuona aibu?
Kwa kukupa mfano kuna watanganyika waliosema kuwa uhuru wa mwaka 1961 ulikuwa unatolewa mapema. Ukichukua mtazamo wa miaka ya 1960 unaweza kusema hawa jamaa walikuwa wasaliti. Lakini kwa sasa hivi inaonyesha kabisa uhuru tulipata mapema.
Kitu kingine cha maana cha kuangalia kuhusu Kambona ni fani aliyosomea. Ingawaje alipata matatizo ya kumaliza shule, Kambona alisomea sheria. Kati ya marais 43 wamarekani 25 walisomea sheria. Viongozi wa nchi nyingi za ulaya ni wanasheria.
Waliosomea sheria wanaangalia maisha kutoka view points mbalimbali na wako huru kuzungumza mawazo yao na inawezekana kama maisha ya Kambona yalikuwa magumu kwa kufanya kazi na watu ambao wana mtazamo mmoja kama Nyerere na Kawawa.
Kuhusu source unazoleta endelea kuzimwaga na ninasaidia sana na ikiwezekana zilete kama zilivyo bila kufanya harmonization.