Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona?

Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona?

Leo silahi naona jf kula suborfurm imekuwa ni burudani. ayaani hata ukionda kwnye okes hucheki ukija kwenye isiasa ndio unacheka mpaka........
 
cabinet-baada-ya-muungano.jpg

Mwandishi Maggid Mjengwa ameamua kujiweka wazi kuwa ni mtetezi wa Oscar Kambona, katika mfululizo wa maandiko yake Mjengwa anaonekana kujenga utetezi wake kwa uthubutu wa Kambona kutofautiana na Nyerere kwa maana nyingine alikuwa jasiri wa nyakati zile na mtu aliyesimamia alichokiamini.

Binafsi sina ugomvi na mawazo ya Mjengwa na niweke wazi kuwa Maggid Mjengwa ni kaka yangu katika maswala ya uandishi na nimewahi hata kuzungumza naye uso kwa uso ila katika utetezi wake naona kuna mapungufu kadhaa ambayo naamini anajaribu kuyakwepa kuyazungumzia au la bado anayafikiria.

Kwanza kabisa ukirejea maandiko ya mwandishi Mzee Mwanakijiji yeye katufunulia juu ya kile tusichokijua kuwa hata Oscar Kambona aliwahi kukiri kwa kinywa chake kuwa kweli Nyerere ni baba wa taifa , hapa kuna utata kidogo unaoibua maswali kuwa je oscar Kambona alikuwa anapingana na Nyerere au walitofautiana kwenye maswala fulani tu?

Pili ambalo naamini ni la muhimu je kila anayesimamia anachokiamini ni shujaa? iwapo Mjengwa anaamini hivi basi anajipinga mwenyewe kwa maana amewahi kupinga vikali misimamo ya Osama bin Laden tena akihitimisha kwa kumwita muuaji na gaidi asilani hakumwita shujaa ingawaje Osama alikuwa anatetea kile alichokiamini.

Hivyo ipo haja ya Mjengwa kurudi tena kwenye kumbukumbu zake ajibu maswali haya ya msingi ambayo yatauweka utetezi wake katika mizani inayopimika vinginevyo sikubaliani na utetezi wake naona kama umejengwa kwa misingi ya kitaaluma(uandishi) kuliko mantiki(logic).

Nova Kambota
+255717 709618
novakambota@gmail.com
www.novakambota.com
 
nashindwa kumuelewa Maggid anakusudia kitu gani katika huo utetezi wake, ngojea tumsubiri Maggid aje ajibu hoja!
 
Oscar Kambona; Upande wa pili wa shilingi III
Na Maggid Mjengwa,
UKWELI una hulka moja njema, kuwa hata ukiuficha chini ya uvungu wa kitanda kwa miaka 50, iko siku utatoka wenyewe nje bila kusubiri kuvalishwa viatu. Daima, kweli udhihiri.

Tunaadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika. Kukumbuka na kuyazungumza mema na mabaya tuliyoyapitia kutatusaidia kutafuta namna bora ya kwenda mbele kama taifa. Mwaka 2061, miaka 50 ijayo, nchi yetu itaadhimisha jubilei ya miaka 100 ya uhuru wetu. Wengi wetu tutakuwa tumetangulia mbele ya haki. Lakini, historia itabaki kutuhukumu.

Kuvunja ukimya na kuzungumzia mema na mabaya yaliyopita itatusaidia kujenga misingi imara ya taifa letu hata kwa miaka 50 ijayo.
Tuna wajibu wa kizalendo wa kutoa ushahidi wetu kwa kusimulia tuliyoyapitia ili waliopo na wajao waweze kuyachukua mema na kutorudia makosa yaliyofanyika nyuma.

Kuna tulioshuhudia Tanzania iliyokuwa na ustawi na dalili za kuendelea kustawi. Tumeshuhudia pia n i kwa jinsi gani wingu hilo la matumaini lilivyokuwa likipotea kwa kasi ya kutisha na kupisha jua kali lililoleta ukame wa kisiasa na kiuchumi katika nchi yetu.

Na msingi wa haya yote ni ubaguzi wa kisiasa na kutoruhusu mazingira ya uwepo wa fikra mbadala. Kuwachukia wenye ’ akili’ na walio tayari kuzitumia akili zao kwa manufaa ya nchi yao. Hivyo basi, watu hao hutengwa na mfumo wa uongozi wa kisiasa uliopo.
Na huo ndio msingi wa uwepo w a hoja ya ubaguzi wa kisiasa. Na dhambi hii ya ubaguzi wa kisiasa ndilo gamba gumu la kitaifa tunalopaswa kulivua. Maana, ndio hali yenye kusababisha maradhi yetu mengi kama taifa ikiwamo ufisadi uliotamalaki.

“ Zidumu fikra sahihi za Mwenyekiti wa CCM!”

Najua msomaji umeingiwa na kigugumizi katika kutafuta jibu la salamu hiyo. Hivyo basi, si ngeni kwako, lakini inakutatiza. Enzi hizo, Mtanzania yeyote yule, ndani ya Tanzania, hakutakiwa kujibu chochote kingine kwa salamu hiyo isipokuwa “ Zidumu!”. Vinginevyo, akae kimya. Salamu hiyo ilikuwa ni kwa Mwenyekiti Mao Tse Tung wa China ya Kikomunisti, nasi tukaiiga. Ukawa mwanzo wa hulka ya kumfanya kiongozi wetu mkuu kuwa ‘ Mungu mtu’. Julius Nyerere aliikubali salamu hiyo. Tafsiri yake; wenye kuitoa salamu hiyo waliacha kufikiri. Kazi hiyo walimwachia Mwalimu. Na Mwalimu Nyerere alipata uwanja mpana wa kutoa fikra zake bila kupata maswali mengi.

Na mfumo ukawepo uliomwacha Mwalimu afikiri peke yake. Waliofikiri tofauti na Nyerere na hasa fikra za kumkosoa na kumshutumu, basi, kuna ambao walikuwa na kazi ya kuwafuatilia watu hao. Ikazaliwa hofu miongoni mwa wananchi, kikafuata kimya kikuu. Hakuna nchi ya kisasa inayojengwa na wananchi wenye hofu.

Wana TANU wa aina ya Oscar Kambona na Bibi Titi Mohammed wakawa na wakati mgumu. Hawa ndio wale waliokuwa na ujasiri wa kusema wanachofikiri na hata kumshutumu hadharani Mwana TANU mwenzao, Julius Nyerere.

Na TANU ilikuwa na wapiganaji wengine wengi ambao hawasikiki. Mathalan, si Watanzania wengi wa kizazi cha sasa wanaojua juu ya Bibi Titi Mohammed zaidi ya kuwa kuna barabara moja kubwa katikati ya Jiji inayoitwa kwa jina hilo.

Hakika, huwezi kuandika historia ya TANU ikakamilika bila kutaja mchango wa Bibi Titi Mohammed. Hivyo basi, huwezi kuandika historia ya mapambano ya kudai uhuru wa Tanganyika ikakamilika bila kutaja mchango wa mwanamama huyu shujaa, Bibi Titi Mohammed.

Katika miaka ya mwanzo ya uhuru wa Tanganyika, wakati wasomi wetu wengi wakiwamo waadhiri wa Chuo Kikuu , kwa kukosa ujasiri na kujiamini, walijigeuza ‘ nyumbu’ . Bibi Titi Mohammed aliyefundishwa kusoma na kuandika na Oscar Kambona aliweza kusimama na kumkosoa Julius Nyerere hadharani.

Na Bibi Titi huyu hakumwonea aibu hata mwalimu wake, Oscar Kambona aliyemfundisha kusoma na kuandika. Mama huyu anayejiamini alipata kumshutumu Kambona kwa kuamua kuondoka nchini badala ya kubaki na kumkabili Nyerere akiwa ndani ya Tanzania.

Kuna mengi ya kuandika juu ya Bibi Titi Mohammed ambaye baadae alifungwa kwa mashtaka ya uhaini. Alipotoka gerezani alitengwa kisiasa. Hakuonekana hadharani kwa miaka mingi. Ni kwenye wakati wa uongozi wa Rais Ali Hassan Mwinyi ndipo Bibi Titi Mohammed alirudishwa kundini. Na ndio kisa cha kuzawadiwa hata jina la mtaa kwa kutambua mchango wake kwa taifa hili.

Wakati umebadilika. Julius Nyerere aliweza kusoma alama za nyakati. Nilichokiona miaka kumi ya mwisho ya uhai wa Nyerere ni pale Mwalimu alipoamua kumtafuta Julius ndani ya Mwalimu. Maandiko na hotuba za Nyerere za miaka kumi ya mwisho wa uhai wake zinamwonyesha Nyerere aliyekuwa na mazungunzo na nafsi yake kwa maslahi ya taifa.

Nyerere aliyejitazama na kujitathmini upya. Aliziona nguvu zake, aliyaona mapungufu yake pia. Hakuona udhaifu, bali ujasiri, kutamka hadharani, kuwa kuna makosa yamefanyika katika uongozi wake. Na akavunja mwiko pia, akaanza kukishutumu hadharani chama chake CCM. Chama alichoshiriki kukiasisi.

Kitu ambacho Nyerere hakuweka bayana ni ukweli kuwa, makosa makubwa yaliyofanyika katika ujenzi wa msingi wa taifa hili, na chini ya uongozi wake, ndio yaliyochangia kwa kiasi kikubwa kutufikisha hapa tulipo. Na tumeona, katika kujitafakari kwa Nyerere, kuwa Kimtazamo, Nyerere wa miaka kumi ya mwisho alikuwa karibu sana na rafiki yake wa zamani Oscar Kambona ingawa wawili hawa hawakukutana tena ana kwa ana hadi pale Mungu alipowatanguliza mbele za haki.

Nyerere alifanya ziaza China mwaka 1965. Kilichofuatia ni kuasisi mfumo wa Chama kimoja. Likaja Azimio la Arusha. Kwa namna moja au nyingine, ziara ya Nyerere China itabaki kuwa chanzo kilichoharakisha kuvunjika kwa misingi ya ustawi wa taifa changa la Tanganyika. Tukubali, kuwa Julius Nyerere, katika dhamira yake njema ya kuijenga Tanganyika, alichukua maamuzi ya haraka sana ikiwamo kuua mfumo wa vyama vingi na kuanzisha Azimio La Arusha na utekelezaji wake ikiwamo utaratibu wa Ujamaa Vijijini bila kuwa na maandalizi ya kutosha. Ni maamuzi yaliyotugharimu kama taifa.

Tunajua, kuwa , wananchi wengi walilazimishwa kwa nguvu kuayaacha makazi yao ikiwamo mashamba yao na kwenda kujiunga na vijiji vya Ujamaa. Hali hii ilipelekea kuporomoka kwa uzalishaji wa mazao . Kuna wananchi waliongiwa chuki na Serikali yao, hivyo basi, kutokua na moyo mmoja katika kutekeleza yale ambayo waliaambiwa wayafanye..

Ni mazingira kama hayo ambayo Oscar Kambona na wengine katika TANU waliyaona kabla kuwa yangetokea. Hivyo basi, kuwa na mitazamo tofauti na Julius Nyerere. Na ilikuwaje basi mara ile Mkutano wa TANU kule Arusha ulipopitisha Azimio La Arusha Januari 1967?

Inasemwa, kuwa kulikuwa na majadiliano makali. Na dhahiri Julius Nyerere na Oscar Kambona walitofautiana hadharani juu ya namna ya utekelezaji wa Azimio la Arusha. Ilipofika wakati wa kupiga kura, Kambona alipiga kura ya kupinga Azimio La Arusha.

Na ajabu ya jambo hili. Katika Serikali iliyoundwa baada ya Azimio, Nyerere alimpaOscar Kambona aongoze Wizara ya Mipango ambayo pia ingekuwa na jukumu la kutekeleza mpango wa Ujamaa Vijijini. Haukupita muda Kambona alijivua nyadhifa zake za chama na Serikali. Hakuwa tayari kutumikia Serikali na Chama katika mazingira yale.

Na baadae uvumi ukasambaa, kuwa kulikuwa na jaribio la kumpindua Julius Nyerere. Kukawa na kamata kamata. Katika mazingira hayo, Oscar Kambona alifungasha virago vyake. Yeye, mke na watoto wakaikimbia nchi waliyozaliwa kwa kupitia mpaka wa Namanga.

Huku nyuma, kamata kamata iliendelea, hakukuwa na habari kamili, bali uvumi ulioshamiri. Na sheria ya kuweka watu kizuini ilitumika barabara. Lakini, haikuwa uvumi, taarifa za kukamatwa baadhi ya ndugu wa Kambona. Hawa ni pamoja na Ottini na Mattiya Kambona. Walisekwa gerezani bila kufunguliwa mashtaka. Oscar Kambona aliyekimbilia London akawa sasa ’ adui’ wa nje. Nini zaidi kilitokea? Fuatilia sehemu ya mwisho ya makala haya juma lijalo.
( Makala haya yamechapwa katika Raia Mwema, leo Jumatano)
MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo
 
Kwa ufahamu wangu wa Historia ya Tanzania Osca Kambona ni mmoja wa watu walioteseka kwa sababu ya kuwa na mtazamo tofauti na mwalimu. Hakika mjadala huu ni afya ya Watanzania kwa sababu historia ya waliopingana na mwalimu "imechakachuliwa" bila kujali ukweli na mchango wao katika nchi hii. Kwakumbukumbu yangu nakumbuka nyumba za Kambona RIP moja kule masaki karibu na police Mess na nyingine msasani kwa mwalimu zilikua zinakaliwa na Kawawa na Obote na sina hakika kama walikua wanalipia pango kokote.Kwangu huu ulikua unyanganyi. Ingawa sina uhakika lakini hazikua zimetaifishwa kwasababu hazikua na thamani kubwa kama maelekezo ya utaifishaji yalivyokua. Kambona RIP hakutajwa kokote tena labda kwenye nyimbo za mchakamchaka shuleni ambazo zilikua zinamkashifu. Mkuu Maggid na wengine hapa JF tusaidieni kuweka historia sawa kuhusiana na Mzalendo huyu aliyezulumiwa (kwa mtazamo wangu) kwa kuwa na mawazo tofauti na fikra zisizo sahihi za mwenyekiti.
 
oscar kambona; upande wa pili wa shilingi iii
na maggid mjengwa,
ukweli una hulka moja njema, kuwa hata ukiuficha chini ya uvungu wa kitanda kwa miaka 50, iko siku utatoka wenyewe nje bila kusubiri kuvalishwa viatu. Daima, kweli udhihiri.

Tunaadhimisha miaka 50 ya uhuru wa tanganyika. Kukumbuka na kuyazungumza mema na mabaya tuliyoyapitia kutatusaidia kutafuta namna bora ya kwenda mbele kama taifa. Mwaka 2061, miaka 50 ijayo, nchi yetu itaadhimisha jubilei ya miaka 100 ya uhuru wetu. Wengi wetu tutakuwa tumetangulia mbele ya haki. Lakini, historia itabaki kutuhukumu.

Kuvunja ukimya na kuzungumzia mema na mabaya yaliyopita itatusaidia kujenga misingi imara ya taifa letu hata kwa miaka 50 ijayo.
Tuna wajibu wa kizalendo wa kutoa ushahidi wetu kwa kusimulia tuliyoyapitia ili waliopo na wajao waweze kuyachukua mema na kutorudia makosa yaliyofanyika nyuma.

Kuna tulioshuhudia tanzania iliyokuwa na ustawi na dalili za kuendelea kustawi. Tumeshuhudia pia n i kwa jinsi gani wingu hilo la matumaini lilivyokuwa likipotea kwa kasi ya kutisha na kupisha jua kali lililoleta ukame wa kisiasa na kiuchumi katika nchi yetu.

na msingi wa haya yote ni ubaguzi wa kisiasa na kutoruhusu mazingira ya uwepo wa fikra mbadala. Kuwachukia wenye ' akili' na walio tayari kuzitumia akili zao kwa manufaa ya nchi yao. Hivyo basi, watu hao hutengwa na mfumo wa uongozi wa kisiasa uliopo.
Na huo ndio msingi wa uwepo w a hoja ya ubaguzi wa kisiasa. Na dhambi hii ya ubaguzi wa kisiasa ndilo gamba gumu la kitaifa tunalopaswa kulivua. Maana, ndio hali yenye kusababisha maradhi yetu mengi kama taifa ikiwamo ufisadi uliotamalaki.
- huu ndio unafiki uliotujaa watanzania, hadi wanatunyanyapaa wapinzani huku makazini, na ndicho kinaendelea pale bungeni....ndiyooooo siyoooooooo

" zidumu fikra sahihi za mwenyekiti wa ccm!"

najua msomaji umeingiwa na kigugumizi katika kutafuta jibu la salamu hiyo. Hivyo basi, si ngeni kwako, lakini inakutatiza. Enzi hizo, mtanzania yeyote yule, ndani ya tanzania, hakutakiwa kujibu chochote kingine kwa salamu hiyo isipokuwa " zidumu!". Vinginevyo, akae kimya. Salamu hiyo ilikuwa ni kwa mwenyekiti mao tse tung wa china ya kikomunisti, nasi tukaiiga. Ukawa mwanzo wa hulka ya kumfanya kiongozi wetu mkuu kuwa ' mungu mtu'. Julius nyerere aliikubali salamu hiyo. Tafsiri yake; wenye kuitoa salamu hiyo waliacha kufikiri. Kazi hiyo walimwachia mwalimu. Na mwalimu nyerere alipata uwanja mpana wa kutoa fikra zake bila kupata maswali mengi.

Na mfumo ukawepo uliomwacha mwalimu afikiri peke yake. Waliofikiri tofauti na nyerere na hasa fikra za kumkosoa na kumshutumu, basi, kuna ambao walikuwa na kazi ya kuwafuatilia watu hao. Ikazaliwa hofu miongoni mwa wananchi, kikafuata kimya kikuu. Hakuna nchi ya kisasa inayojengwa na wananchi wenye hofu.

Wana tanu wa aina ya oscar kambona na bibi titi mohammed wakawa na wakati mgumu. Hawa ndio wale waliokuwa na ujasiri wa kusema wanachofikiri na hata kumshutumu hadharani mwana tanu mwenzao, julius nyerere.

Na tanu ilikuwa na wapiganaji wengine wengi ambao hawasikiki. Mathalan, si watanzania wengi wa kizazi cha sasa wanaojua juu ya bibi titi mohammed zaidi ya kuwa kuna barabara moja kubwa katikati ya jiji inayoitwa kwa jina hilo.

Hakika, huwezi kuandika historia ya tanu ikakamilika bila kutaja mchango wa bibi titi mohammed. Hivyo basi, huwezi kuandika historia ya mapambano ya kudai uhuru wa tanganyika ikakamilika bila kutaja mchango wa mwanamama huyu shujaa, bibi titi mohammed.

Katika miaka ya mwanzo ya uhuru wa tanganyika, wakati wasomi wetu wengi wakiwamo waadhiri wa chuo kikuu , kwa kukosa ujasiri na kujiamini, walijigeuza ' nyumbu' . Bibi titi mohammed aliyefundishwa kusoma na kuandika na oscar kambona aliweza kusimama na kumkosoa julius nyerere hadharani. huu ni ugonjwa ulioasisiwa na mwalimu na hadi leo unaendelea. Mwalimu aliweka watu vizuizini ndani na nje ya nchi...na kuwanyima wasipate promortion makazini mwao. Ugonjwa huu upo hadi leo kwenye taasisi za serekali ambapo mtu ukijulikana kuwa sio ccm basi hesabu kuwa promotion ni kalaghabaho!!! Lakini tunamshukuru mola kuwa siku sio nyingi ugonjwa huu unapata dawa!

na bibi titi huyu hakumwonea aibu hata mwalimu wake, oscar kambona aliyemfundisha kusoma na kuandika. mama huyu anayejiamini alipata kumshutumu kambona kwa kuamua kuondoka nchini badala ya kubaki na kumkabili nyerere akiwa ndani ya tanzania. du kweli alikuwa shujaa, however, hakuwa na vingi vya kupoteza kwani alikuwa pipoz zaidi......shida kwa wasomi wengi hutishwa na kunyimwa stahili zao. Kambona hakuwa tayari kuendelea kuwa waste ilhali kila mtu anapiga kelele za zidumu fikra za mwenye kifimbo! Na aliyembishia aliitwa mhaini....nyerere pia alijua kuwa mama titi hakuwa na impact kama ambavyo ingekuwa kwa kambona

kuna mengi ya kuandika juu ya bibi titi mohammed ambaye baadae alifungwa kwa mashtaka ya uhaini. Alipotoka gerezani alitengwa kisiasa. Hakuonekana hadharani kwa miaka mingi. Ni kwenye wakati wa uongozi wa rais ali hassan mwinyi ndipo bibi titi mohammed alirudishwa kundini. Na ndio kisa cha kuzawadiwa hata jina la mtaa kwa kutambua mchango wake kwa taifa hili.

Wakati umebadilika. Julius nyerere aliweza kusoma alama za nyakati. Nilichokiona miaka kumi ya mwisho ya uhai wa nyerere ni pale mwalimu alipoamua kumtafuta julius ndani ya mwalimu. Maandiko na hotuba za nyerere za miaka kumi ya mwisho wa uhai wake zinamwonyesha nyerere aliyekuwa na mazungunzo na nafsi yake kwa maslahi ya taifa.

Nyerere aliyejitazama na kujitathmini upya. Aliziona nguvu zake, aliyaona mapungufu yake pia. Hakuona udhaifu, bali ujasiri, kutamka hadharani, kuwa kuna makosa yamefanyika katika uongozi wake. Na akavunja mwiko pia, akaanza kukishutumu hadharani chama chake ccm. Chama alichoshiriki kukiasisi.

Kitu ambacho nyerere hakuweka bayana ni ukweli kuwa, makosa makubwa yaliyofanyika katika ujenzi wa msingi wa taifa hili, na chini ya uongozi wake, ndio yaliyochangia kwa kiasi kikubwa kutufikisha hapa tulipo. Na tumeona, katika kujitafakari kwa nyerere, kuwa kimtazamo, nyerere wa miaka kumi ya mwisho alikuwa karibu sana na rafiki yake wa zamani oscar kambona ingawa wawili hawa hawakukutana tena ana kwa ana hadi pale mungu alipowatanguliza mbele za haki.

Nyerere alifanya ziaza china mwaka 1965. Kilichofuatia ni kuasisi mfumo wa chama kimoja. Likaja azimio la arusha. Kwa namna moja au nyingine, ziara ya nyerere china itabaki kuwa chanzo kilichoharakisha kuvunjika kwa misingi ya ustawi wa taifa changa la tanganyika. Tukubali, kuwa julius nyerere, katika dhamira yake njema ya kuijenga tanganyika, alichukua maamuzi ya haraka sana ikiwamo kuua mfumo wa vyama vingi na kuanzisha azimio la arusha na utekelezaji wake ikiwamo utaratibu wa ujamaa vijijini bila kuwa na maandalizi ya kutosha. Ni maamuzi yaliyotugharimu kama taifa.

Tunajua, kuwa , wananchi wengi walilazimishwa kwa nguvu kuayaacha makazi yao ikiwamo mashamba yao na kwenda kujiunga na vijiji vya ujamaa. Hali hii ilipelekea kuporomoka kwa uzalishaji wa mazao . Kuna wananchi waliongiwa chuki na serikali yao, hivyo basi, kutokua na moyo mmoja katika kutekeleza yale ambayo waliaambiwa wayafanye..

Ni mazingira kama hayo ambayo oscar kambona na wengine katika tanu waliyaona kabla kuwa yangetokea. Hivyo basi, kuwa na mitazamo tofauti na julius nyerere. Na ilikuwaje basi mara ile mkutano wa tanu kule arusha ulipopitisha azimio la arusha januari 1967?

Inasemwa, kuwa kulikuwa na majadiliano makali. Na dhahiri julius nyerere na oscar kambona walitofautiana hadharani juu ya namna ya utekelezaji wa azimio la arusha. Ilipofika wakati wa kupiga kura, kambona alipiga kura ya kupinga azimio la arusha.

Na ajabu ya jambo hili. Katika serikali iliyoundwa baada ya azimio, nyerere alimpaoscar kambona aongoze wizara ya mipango ambayo pia ingekuwa na jukumu la kutekeleza mpango wa ujamaa vijijini. Haukupita muda kambona alijivua nyadhifa zake za chama na serikali. Hakuwa tayari kutumikia serikali na chama katika mazingira yale.

Na baadae uvumi ukasambaa, kuwa kulikuwa na jaribio la kumpindua julius nyerere. Kukawa na kamata kamata. Katika mazingira hayo, oscar kambona alifungasha virago vyake. Yeye, mke na watoto wakaikimbia nchi waliyozaliwa kwa kupitia mpaka wa namanga.

Huku nyuma, kamata kamata iliendelea, hakukuwa na habari kamili, bali uvumi ulioshamiri. Na sheria ya kuweka watu kizuini ilitumika barabara. Lakini, haikuwa uvumi, taarifa za kukamatwa baadhi ya ndugu wa kambona. Hawa ni pamoja na ottini na mattiya kambona. Walisekwa gerezani bila kufunguliwa mashtaka. Oscar kambona aliyekimbilia london akawa sasa ' adui' wa nje. Nini zaidi kilitokea? Fuatilia sehemu ya mwisho ya makala haya juma lijalo.
( makala haya yamechapwa katika raia mwema, leo jumatano)
mjengwa - picha, habari & matangazo

shule nzuri, aksante maggid.... Nadhani kuna haja ya idara ya makumbusho kuanzisha taratibu za kukusanya documentation kama hizi ambazo zitasaidia kujijenga kama taifa! Historia hujirudia!
 
oscar kambona; upande wa pili wa shilingi iii
na maggid mjengwa,
ukweli una hulka moja njema, kuwa hata ukiuficha chini ya uvungu wa kitanda kwa miaka 50, iko siku utatoka wenyewe nje bila kusubiri kuvalishwa viatu. Daima, kweli udhihiri.

Tunaadhimisha miaka 50 ya uhuru wa tanganyika. Kukumbuka na kuyazungumza mema na mabaya tuliyoyapitia kutatusaidia kutafuta namna bora ya kwenda mbele kama taifa. Mwaka 2061, miaka 50 ijayo, nchi yetu itaadhimisha jubilei ya miaka 100 ya uhuru wetu. Wengi wetu tutakuwa tumetangulia mbele ya haki. Lakini, historia itabaki kutuhukumu.

Kuvunja ukimya na kuzungumzia mema na mabaya yaliyopita itatusaidia kujenga misingi imara ya taifa letu hata kwa miaka 50 ijayo.
Tuna wajibu wa kizalendo wa kutoa ushahidi wetu kwa kusimulia tuliyoyapitia ili waliopo na wajao waweze kuyachukua mema na kutorudia makosa yaliyofanyika nyuma.

Kuna tulioshuhudia tanzania iliyokuwa na ustawi na dalili za kuendelea kustawi. Tumeshuhudia pia n i kwa jinsi gani wingu hilo la matumaini lilivyokuwa likipotea kwa kasi ya kutisha na kupisha jua kali lililoleta ukame wa kisiasa na kiuchumi katika nchi yetu.

na msingi wa haya yote ni ubaguzi wa kisiasa na kutoruhusu mazingira ya uwepo wa fikra mbadala. Kuwachukia wenye ’ akili’ na walio tayari kuzitumia akili zao kwa manufaa ya nchi yao. Hivyo basi, watu hao hutengwa na mfumo wa uongozi wa kisiasa uliopo.
Na huo ndio msingi wa uwepo w a hoja ya ubaguzi wa kisiasa. Na dhambi hii ya ubaguzi wa kisiasa ndilo gamba gumu la kitaifa tunalopaswa kulivua. Maana, ndio hali yenye kusababisha maradhi yetu mengi kama taifa ikiwamo ufisadi uliotamalaki.
- huu ndio unafiki uliotujaa watanzania, hadi wanatunyanyapaa wapinzani huku makazini, na ndicho kinaendelea pale bungeni....ndiyooooo siyoooooooo

“ zidumu fikra sahihi za mwenyekiti wa ccm!”

najua msomaji umeingiwa na kigugumizi katika kutafuta jibu la salamu hiyo. Hivyo basi, si ngeni kwako, lakini inakutatiza. Enzi hizo, mtanzania yeyote yule, ndani ya tanzania, hakutakiwa kujibu chochote kingine kwa salamu hiyo isipokuwa “ zidumu!”. Vinginevyo, akae kimya. Salamu hiyo ilikuwa ni kwa mwenyekiti mao tse tung wa china ya kikomunisti, nasi tukaiiga. Ukawa mwanzo wa hulka ya kumfanya kiongozi wetu mkuu kuwa ‘ mungu mtu’. Julius nyerere aliikubali salamu hiyo. Tafsiri yake; wenye kuitoa salamu hiyo waliacha kufikiri. Kazi hiyo walimwachia mwalimu. Na mwalimu nyerere alipata uwanja mpana wa kutoa fikra zake bila kupata maswali mengi.

Na mfumo ukawepo uliomwacha mwalimu afikiri peke yake. Waliofikiri tofauti na nyerere na hasa fikra za kumkosoa na kumshutumu, basi, kuna ambao walikuwa na kazi ya kuwafuatilia watu hao. Ikazaliwa hofu miongoni mwa wananchi, kikafuata kimya kikuu. Hakuna nchi ya kisasa inayojengwa na wananchi wenye hofu.

Wana tanu wa aina ya oscar kambona na bibi titi mohammed wakawa na wakati mgumu. Hawa ndio wale waliokuwa na ujasiri wa kusema wanachofikiri na hata kumshutumu hadharani mwana tanu mwenzao, julius nyerere.

Na tanu ilikuwa na wapiganaji wengine wengi ambao hawasikiki. Mathalan, si watanzania wengi wa kizazi cha sasa wanaojua juu ya bibi titi mohammed zaidi ya kuwa kuna barabara moja kubwa katikati ya jiji inayoitwa kwa jina hilo.

Hakika, huwezi kuandika historia ya tanu ikakamilika bila kutaja mchango wa bibi titi mohammed. Hivyo basi, huwezi kuandika historia ya mapambano ya kudai uhuru wa tanganyika ikakamilika bila kutaja mchango wa mwanamama huyu shujaa, bibi titi mohammed.

Katika miaka ya mwanzo ya uhuru wa tanganyika, wakati wasomi wetu wengi wakiwamo waadhiri wa chuo kikuu , kwa kukosa ujasiri na kujiamini, walijigeuza ‘ nyumbu’ . Bibi titi mohammed aliyefundishwa kusoma na kuandika na oscar kambona aliweza kusimama na kumkosoa julius nyerere hadharani. huu ni ugonjwa ulioasisiwa na mwalimu na hadi leo unaendelea. Mwalimu aliweka watu vizuizini ndani na nje ya nchi...na kuwanyima wasipate promortion makazini mwao. Ugonjwa huu upo hadi leo kwenye taasisi za serekali ambapo mtu ukijulikana kuwa sio ccm basi hesabu kuwa promotion ni kalaghabaho!!! Lakini tunamshukuru mola kuwa siku sio nyingi ugonjwa huu unapata dawa!

na bibi titi huyu hakumwonea aibu hata mwalimu wake, oscar kambona aliyemfundisha kusoma na kuandika. mama huyu anayejiamini alipata kumshutumu kambona kwa kuamua kuondoka nchini badala ya kubaki na kumkabili nyerere akiwa ndani ya tanzania. du kweli alikuwa shujaa, however, hakuwa na vingi vya kupoteza kwani alikuwa pipoz zaidi......shida kwa wasomi wengi hutishwa na kunyimwa stahili zao. Kambona hakuwa tayari kuendelea kuwa waste ilhali kila mtu anapiga kelele za zidumu fikra za mwenye kifimbo! Na aliyembishia aliitwa mhaini....nyerere pia alijua kuwa mama titi hakuwa na impact kama ambavyo ingekuwa kwa kambona

kuna mengi ya kuandika juu ya bibi titi mohammed ambaye baadae alifungwa kwa mashtaka ya uhaini. Alipotoka gerezani alitengwa kisiasa. Hakuonekana hadharani kwa miaka mingi. Ni kwenye wakati wa uongozi wa rais ali hassan mwinyi ndipo bibi titi mohammed alirudishwa kundini. Na ndio kisa cha kuzawadiwa hata jina la mtaa kwa kutambua mchango wake kwa taifa hili.

Wakati umebadilika. Julius nyerere aliweza kusoma alama za nyakati. Nilichokiona miaka kumi ya mwisho ya uhai wa nyerere ni pale mwalimu alipoamua kumtafuta julius ndani ya mwalimu. Maandiko na hotuba za nyerere za miaka kumi ya mwisho wa uhai wake zinamwonyesha nyerere aliyekuwa na mazungunzo na nafsi yake kwa maslahi ya taifa.

Nyerere aliyejitazama na kujitathmini upya. Aliziona nguvu zake, aliyaona mapungufu yake pia. Hakuona udhaifu, bali ujasiri, kutamka hadharani, kuwa kuna makosa yamefanyika katika uongozi wake. Na akavunja mwiko pia, akaanza kukishutumu hadharani chama chake ccm. Chama alichoshiriki kukiasisi.

Kitu ambacho nyerere hakuweka bayana ni ukweli kuwa, makosa makubwa yaliyofanyika katika ujenzi wa msingi wa taifa hili, na chini ya uongozi wake, ndio yaliyochangia kwa kiasi kikubwa kutufikisha hapa tulipo. Na tumeona, katika kujitafakari kwa nyerere, kuwa kimtazamo, nyerere wa miaka kumi ya mwisho alikuwa karibu sana na rafiki yake wa zamani oscar kambona ingawa wawili hawa hawakukutana tena ana kwa ana hadi pale mungu alipowatanguliza mbele za haki.

Nyerere alifanya ziaza china mwaka 1965. Kilichofuatia ni kuasisi mfumo wa chama kimoja. Likaja azimio la arusha. Kwa namna moja au nyingine, ziara ya nyerere china itabaki kuwa chanzo kilichoharakisha kuvunjika kwa misingi ya ustawi wa taifa changa la tanganyika. Tukubali, kuwa julius nyerere, katika dhamira yake njema ya kuijenga tanganyika, alichukua maamuzi ya haraka sana ikiwamo kuua mfumo wa vyama vingi na kuanzisha azimio la arusha na utekelezaji wake ikiwamo utaratibu wa ujamaa vijijini bila kuwa na maandalizi ya kutosha. Ni maamuzi yaliyotugharimu kama taifa.

Tunajua, kuwa , wananchi wengi walilazimishwa kwa nguvu kuayaacha makazi yao ikiwamo mashamba yao na kwenda kujiunga na vijiji vya ujamaa. Hali hii ilipelekea kuporomoka kwa uzalishaji wa mazao . Kuna wananchi waliongiwa chuki na serikali yao, hivyo basi, kutokua na moyo mmoja katika kutekeleza yale ambayo waliaambiwa wayafanye..

Ni mazingira kama hayo ambayo oscar kambona na wengine katika tanu waliyaona kabla kuwa yangetokea. Hivyo basi, kuwa na mitazamo tofauti na julius nyerere. Na ilikuwaje basi mara ile mkutano wa tanu kule arusha ulipopitisha azimio la arusha januari 1967?

Inasemwa, kuwa kulikuwa na majadiliano makali. Na dhahiri julius nyerere na oscar kambona walitofautiana hadharani juu ya namna ya utekelezaji wa azimio la arusha. Ilipofika wakati wa kupiga kura, kambona alipiga kura ya kupinga azimio la arusha.

Na ajabu ya jambo hili. Katika serikali iliyoundwa baada ya azimio, nyerere alimpaoscar kambona aongoze wizara ya mipango ambayo pia ingekuwa na jukumu la kutekeleza mpango wa ujamaa vijijini. Haukupita muda kambona alijivua nyadhifa zake za chama na serikali. Hakuwa tayari kutumikia serikali na chama katika mazingira yale.

Na baadae uvumi ukasambaa, kuwa kulikuwa na jaribio la kumpindua julius nyerere. Kukawa na kamata kamata. Katika mazingira hayo, oscar kambona alifungasha virago vyake. Yeye, mke na watoto wakaikimbia nchi waliyozaliwa kwa kupitia mpaka wa namanga.

Huku nyuma, kamata kamata iliendelea, hakukuwa na habari kamili, bali uvumi ulioshamiri. Na sheria ya kuweka watu kizuini ilitumika barabara. Lakini, haikuwa uvumi, taarifa za kukamatwa baadhi ya ndugu wa kambona. Hawa ni pamoja na ottini na mattiya kambona. Walisekwa gerezani bila kufunguliwa mashtaka. Oscar kambona aliyekimbilia london akawa sasa ’ adui’ wa nje. Nini zaidi kilitokea? Fuatilia sehemu ya mwisho ya makala haya juma lijalo.
( makala haya yamechapwa katika raia mwema, leo jumatano)
mjengwa - picha, habari & matangazo

shule nzuri, aksante maggid.... Nadhani kuna haja ya idara ya makumbusho kuanzisha taratibu za kukusanya documentation kama hizi ambazo zitasaidia kujijenga kama taifa! Historia hujirudia!
 
Kwa ufahamu wangu wa Historia ya Tanzania Osca Kambona ni mmoja wa watu walioteseka kwa sababu ya kuwa na mtazamo tofauti na mwalimu. Hakika mjadala huu ni afya ya Watanzania kwa sababu historia ya waliopingana na mwalimu "imechakachuliwa" bila kujali ukweli na mchango wao katika nchi hii. Kwakumbukumbu yangu nakumbuka nyumba za Kambona RIP moja kule masaki karibu na police Mess na nyingine msasani kwa mwalimu zilikua zinakaliwa na Kawawa na Obote na sina hakika kama walikua wanalipia pango kokote.Kwangu huu ulikua unyanganyi. Ingawa sina uhakika lakini hazikua zimetaifishwa kwasababu hazikua na thamani kubwa kama maelekezo ya utaifishaji yalivyokua. Kambona RIP hakutajwa kokote tena labda kwenye nyimbo za mchakamchaka shuleni ambazo zilikua zinamkashifu. Mkuu Maggid na wengine hapa JF tusaidieni kuweka historia sawa kuhusiana na Mzalendo huyu aliyezulumiwa (kwa mtazamo wangu) kwa kuwa na mawazo tofauti na fikra zisizo sahihi za mwenyekiti.

Ipecacuanha,

Ni kweli, nyumba ya Kambona pale Msasani ikaja kupata mpangaji mpya, aliitwa Milton Obote, rafiki mwingine wa Julius Nyerere.
 
Majjid,

..kwa kumbukumbu zangu, Bibi Titi Mohamed, baada ya kipindi kirefu cha kutoonekana, aliibuka mwaka 1983/84 kwenye mkutano ambao Mwalimu alitangaza vita dhidi ya walanguzi na wahujumu uchumi. nadhani Mwalimu alimuita jukwaani ili wananchi wamuone.

..hii article yako ina mambo mengi ambayo yanapaswa hajaziliwe. matumaini yangu ni kwamba utafanya hivyo, or ppl will take up your work and advance it.

..moja ya mambo ambayo ingependeza kama ungeya-address ni mjadala mzima kati ya Nyerere vs Kambona. hoja za Kambona zilikuwa zipi? Nyerere naye alijenga hoja gani? Je, hali ilikuwaje ktk mkutano wa mchakato wa Azimio la Arusha? Je, kuna wajumbe zaidi ya hao "mafahali wawili" ambao walichangia mjadala huo? mwisho, Tanu ilipitisha vipi hoja ya Azimio la Arusha.

..pia umeeleza kwamba kulikuwa na kamata-kamata, na Kambona alitoroka yeye na familia yake. hapa nadhani ungesaidia kama ungepata tarehe za matukio ya kamata-kamata, na pia ungeeleza wahusika waliokamatwa. Je, waliokamatwa walikaa ndani muda gani/wapi? Je watuhumiwa hao walipata kushtakiwa kwa makosa yoyote?

..binafsi nadhani unaweza kuja na kitu kikubwa zaidi, chenye mchango mzuri wa kihistoria, kama utafanya research ya kutosha.
 
Hizi ndo zilikuwa zikiitwa "zidumu fikra za mwenyekiti! ziduku!"
Upumbavu mkubwa huu wa mchonga aliotuachia na unaendelea kututafuna mpaka leo.
Asante Majjid for this useful information to us.
 
Majjid,

..kwa kumbukumbu zangu, Bibi Titi Mohamed, baada ya kipindi kirefu cha kutoonekana, aliibuka mwaka 1983/84 kwenye mkutano ambao Mwalimu alitangaza vita dhidi ya walanguzi na wahujumu uchumi. nadhani Mwalimu alimuita jukwaani ili wananchi wamuone.

..hii article yako ina mambo mengi ambayo yanapaswa hajaziliwe. matumaini yangu ni kwamba utafanya hivyo, or ppl will take up your work and advance it.

..moja ya mambo ambayo ingependeza kama ungeya-address ni mjadala mzima kati ya Nyerere vs Kambona. hoja za Kambona zilikuwa zipi? Nyerere naye alijenga hoja gani? Je, hali ilikuwaje ktk mkutano wa mchakato wa Azimio la Arusha? Je, kuna wajumbe zaidi ya hao "mafahali wawili" ambao walichangia mjadala huo? mwisho, Tanu ilipitisha vipi hoja ya Azimio la Arusha.

..pia umeeleza kwamba kulikuwa na kamata-kamata, na Kambona alitoroka yeye na familia yake. hapa nadhani ungesaidia kama ungepata tarehe za matukio ya kamata-kamata, na pia ungeeleza wahusika waliokamatwa. Je, waliokamatwa walikaa ndani muda gani/wapi? Je watuhumiwa hao walipata kushtakiwa kwa makosa yoyote?

..binafsi nadhani unaweza kuja na kitu kikubwa zaidi, chenye mchango mzuri wa kihistoria, kama utafanya research ya kutosha.
Joka Kuu,

Ahsante sana. Ni kweli, ninapoandika haya naona kuna mengi zaidi ya kusimulia. Lakini, kazi hiyo ni yetu sote, ni yako pia.
 
Joka Kuu,

Ahsante sana. Ni kweli, ninapoandika haya naona kuna mengi zaidi ya kusimulia. Lakini, kazi hiyo ni yetu sote, ni yako pia.

Tunachotaka ni historical facts kuthibitisha hayo madai yako, siyo simulizi au hadithi tu. Since you brought up these things, the onus of proof is on you. Huwezi kuandika thesis halafu ukategemea Wakosoaji au Wasomaji watakuwa na ushahidi wa kuthibitisha hoja au madai yako.
 
Nyerere alifanya ziaza China mwaka 1965. Kilichofuatia ni kuasisi mfumo wa Chama kimoja. Likaja Azimio la Arusha. Kwa namna moja au nyingine, ziara ya Nyerere China itabaki kuwa chanzo kilichoharakisha kuvunjika kwa misingi ya ustawi wa taifa changa la Tanganyika. Tukubali, kuwa Julius Nyerere, katika dhamira yake njema ya kuijenga Tanganyika, alichukua maamuzi ya haraka sana ikiwamo kuua mfumo wa vyama vingi na kuanzisha Azimio La Arusha na utekelezaji wake ikiwamo utaratibu wa Ujamaa Vijijini bila kuwa na maandalizi ya kutosha. Ni maamuzi yaliyotugharimu kama taifa.
Maggid,
Kama mwandishi, unatakiwa kuwa factual. Uamuzi wa kuanzisha chama kimoja cha siasa ulifanyika 1963, na wala si 1965 kama unavyotaka kutuaminisha.
 
Una mwanzo mzuri..ila kafanye utafiti zaidi ili uweze kua na valid arguments katika insight yako...husitegemee masimulizi ya kihisia...
Kweli kabisa.
Ukishahusisha kuundwa kwa one party state na ziara ya Nyerere China umeshakuwa biased kabisa katika mada kwa sababu vitu hivyo viwili havina uhusiano wowote. Katika uchaguzi wa 1962 TANU ilibeba 98% ya kura zote. Maggid angeanzia hapo. Kwamba kutangazwa kwa one party state kulikuwa fait accompli iliyotokana na hali halisi ya siasa za Tanganyika wakati huo. Baada ya hapo tunaweza kujikita katika pros na cons za uamuzi huo.
 
Hata kama Tanu ingebeba asilimia 100 ya kura zote hii haimaanishi kwamba Wananchi walitaka TANU ivifute vyama vingine vya siasa, Wananchi kuichagua TANU kwa asilimia hizo labda ni kutokana na kuvutiwa na TANU na uongozi wake, sasa umejuaje pengine Wapinzani hapo baadae wangejijenga, wakajiuza kwa wananchi, wakaleta mbadala wa mawazo kwa wananchi huenda baadae wangekubalika.
Hebu jiulize TANU ilipokuja na azimio la arusha, ukosefu wa Vyama Vingine vya kuleta sera mbadala kwa wananchi kulisaidia Azimio kupita kiulaini na kuwa enforced kupitia vijiji vya ujamaa n.k.

Au Chukulia mfano mgombea Uraisi kupitia TANU (mwalimu) katika uchaguzi kusimama na kivuli, bila shaka angekuwepo mgombea mwingine kupitia Upinzani au hata ndani ya chama chenyewe cha TANU na CCM vingesaidia wigo mpana wa demokrasia.

Mfumo wa Chama kimoja ungepitishwa na Wananchi wenyewe lingekuwa jambo jingine, lakini so far serikali ya TANU kujiamulia kuviondoa bila kuwashirikisha wananchi ni dhahiri demokrasia haikufuatwa.
 
Hadithi zako ni kama za tamthilia za Shigongo ni za kufikirika zaidi kuliko ukweli wenyewe japo zinavutia.

Utoto unakusumbua, kuna lipi hapo la kufikirika.Those are the facts ni mambo ambayo kutokana na utoto wako na kutotaka kujua historia ya nchi yako ndivyo vinavyowafanya wasomi wa kileo kutokumfahamu mtu kama Kasela Bantu...na contribution yake katika struggle ya independence???!!
 
Maggid, Ahsante sana kwa mjadala wako mzuri unaotoa historia iliyofichika kwa muda mrefu sasa. Ukipata nafasi jaribu kumtafuta mdogo wake Kambona anayejulikana kama Matia Kambona aliyeko uhamishoni nchini Uingereza. Binafsi nimepata nafasi ya kuongea naye na ana mengi kuhusiana na historia ya Oscar Kambona, kwa sasa yupo nchini kama vile mtalii na anaangalia uwezekano wa kurudi nchini ila bado ana hofu na mfumo wa usalama wa taifa ambao uliwanyanyasa sana kipindi cha Nyerere ila ana matumaini Katiba mpya itapitisha sual la uraia wa nchi mbili ili aweze kurudi rasmi. Ameandika vitabu kama vitatu hivi ambavyo kwa contents zilizopo ndani nahisi huenda vikapata upinzani sana kukubaliwa na wengi ila huo ndio ukweli mchungu ambao inabidi Watanzania tuukubali. Kila la heri Maggid!
 
Back
Top Bottom