Mjadala mzuri sana.
Matusi tu ndio hatuyataki kwakuwa tunajifunza mengi sana ambayo hatukuyajua.
Ndugu zanguni,
Mimi ugomvi wangu mkubwa na marehemu
Ally Sykes ni kuwa yeye
alikataa kabisa kuchukua juhudi yoyote kuona kuwa hizi nyaraka muhimu
anazikabdihi Nyaraka za Taifa kwa ajili ya kizazi kijacho.
Yeye siku zote akiamini kabisa kuwa zitachomwa moto na akapata kunieleza
ugomvi uliozuka baada ya uhuru kati yake yeye na baadhi ya viongozi katika
TANU waliotaka akabidhi nyaraza zile TANU na yeye akakataa kwa hoja kuwa
hizo ni mali yao.
Hiki kilikuwa kisa cha pekee kabisa lakini moyo wangu ulikuwa mzito sana
kukieleza katika kitabu cha marehemu kaka yake.
Hata hivyo niliandika makala kuhusu nyaraka, ''zilizopotea,'' katika historia ya
uhuru wa Tanganyika na makala hii ilichapwa katika Africa Events (London).
Ikiwa nitapata makala hii katika maktaba yangu In Sha Allah nitaiweka hapa
jamvini la sikuiona nitaweka yale niliyoandika katika kitabu cha
Abdul Sykes
kuhusu, ''upotevu,'' huu wa nyaraka.