Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona?

Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona?

Historia inaonyesha aligombana na Nyerere, navyanzo mbalimbali vya habari hadi sasa vinashindwa kueleza ukweli juu ya hasa kile kilichosababisha kuzuka kwa tofauti kati ya Mwalimu Nyerere na Kambona.

Kila mtu amekuwa akijaribu kueleza ugomvi wa wawili hawa kadiri ajuavyo.

Kuna madai kwamba viongozi hawa wawili ambao kwa sasa wote ni marehemu, walianza kutofautiana baada ya maasi ya wanajeshi.

Inadaiwa kuwa Nyerere alitaka kuanzisha mfumo wa chama kimoja nchini ili kuimarisha usalama na Kambona alipinga hoja hiyo kwa maelezo kwamba mfumo huo ungezorotesha uhuru na maendeleo ya demokrasia. Hoja hiyo ikafikishwa bungeni kwa maamuzi na kwa bahati mbaya kwa Kambona akashindwa lakini akagoma kusaini muswada huo.

Katika safari ya China ya Mwalimu ya mwaka 1965, alipendezwa na mfumo wa kikomonisti wa Mao, na akataka kuanzisha mfumo kama huo kwa jina la ‘Ujamaa’ hapa nchini.

Dhana ya msingi ya mfumo wa Ujamaa ilikuwa ni kuwahamishia watu katika vijiji vya ujamaa na kutaifisha viwanda na vitegauchumi vilivyokuwa vikimilikiwa na watu binafsi ili kuwa chini ya wananchi, hatua iliyopingwa vikali na Kambona kwa maelezo kwamba ungeongeza umaskini na udhibiti wa serikali kwa watu.

Inadaiwa kuwa kulikuwa na msuguano mkali, kiasi kwamba ilimlazimu Kambona alijiuzulu nyadhifa zake ndani ya serikali na chama na hatimaye yeye na familia yake wakakimbilia Nairobi, Kenya na kisha Uingereza ambako walipatiwa hifadhi ya kisiasa.

Mara baada ya kukimbia nchi, mali za Kambona zilichukuliwa na serikali, huku ndugu zake wawili, wakiwekwa kizuizini bila ya kufikishwa mahakamani na kufungwa kwa zaidi ya miaka kumi.

Inaaminika kuwa wazo la Kambona lilikubaliwa na baadhi ya viongozi wa chama na serikali.

Hii inatokana na kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake, Bibi Titi Mohammed, Michael Kamaliza ambaye alikuwa mwanaharakati wa chama cha wafanyakazi, mwanachama wa TANU na waziri, pamoja na Gray Mattaka, Eliya Chipaka na Prisca Chiombola kwa tuhuma za uhaini.

Viongozi hao walihukumiwa pamoja na Kambona licha ya kuwa alikimbilia London lakini walikata rufaa katika Mahakama Kuu ya Afrika Mashariki na wakaachiwa huru.

Hata pamoja na kuachiwa huru,walikamatwa na serikali na kufungwa tena.

Tuhuma kubwa ya Kambona ni kwamba aliiba pesa nyingi za umma, na kukamatwa nazo alipopekuliwa katika uwanja wa Embakasi, mjini Nairobi jambo ambalo alilipinga kwa miaka mingi na kuliweka wazi katika taarifa yake kwa waandishi wa habari Septemba 6, 1967 huko London. Kambona alikwenda mbali zaidi akaitaka serikali ya Tanzania kuiomba Kenya kutoa ukweli juu ya jambo hilo, jambo ambalo halikufanyika hadi kifo chake.

Inaaminika kuwa maisha ya Kambona jijini London yalikuwa ya shida na dhiki. Mwaka 1982, baadhi ya ndugu wa Kambona waliachiwa toka kizuizini baada ya juhudi za Waziri Mkuu wa New Zealand, Robert Muldoon.

Mwaka 1990, Kambona akiwa na matumaini makubwa ya mabadiliko ya kisiasa katika Tanzania, aliunda chama kiitwacho Tanzania Democratic Alliance, akiwa bado uhamishoni.

Mwaka 1992, wakati mfumo wa vyama vingi ulipoanzishwa Tanzania, Kambona aliomba kurudi nchini.

Hata hivyo, serikali ya Tanzania ilimkatalia katakata. Kuona hivyo, Kambona aliiomba serikali ya Uingereza kumpa pasi ya kusafiria kurudi Tanzania, lakini pia akakumbana na tishio la kukamatwa na kuwekwa ndani pindi angelitua.

Septemba 5, 1992, bila woga wa kukamatwa, Kambona alitua katika ardhi ya Tanzania na hakushikwa, badala yake alipewa miezi mitatu awe amekamilisha utata wa uraia wake.

Nia yake ya kushiriki kwa nguvu katika harakati za siasa ilitiwa doa na kudorora kwa afya yake akisumbuliwa na shinikizo la damu.

Afya yake ilizidi kuwa mbaya, na hivyo akalazimika kurudishwa tena London Uingereza kwa matibabu.

Hata hivyo, Juni,1997, Kambona alifariki akipishana kwa siku chache tu na mdogo wake Otini Kambona ambaye pia alikuwa nchini humo kwa matibabu ya moyo.

Katika namna ambayo yaweza kuelezwa kuwa ni tendo pekee la kumuenzi mwanasiasa huyo mashuhuri, serikali ilikubali kusafirisha mwili wake na wa Otini na pia shughuli zote za mazishi.

Kambona ameacha mke na watoto wawili, akiwemo Neema Kambona ambaye hivi karibuni alijiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) tawi la London. Mtoto wa kwanza, Mosi Kambona aliuawa miaka si mingi sana iliyopita mjini London katika mazingira ya kutatanisha.

Kambona ameondoka, lakini pamoja na kuwepo kwa dosari hiyo ya kusigana katika siasa, alifanya makubwa mengi. Ni kiongozi pekee ambaye askari wa jeshi walipoasi na kuwalazimu Mwalimu Nyerere na Rashid Kawawa kukimbia, angeweza kutwaa madaraka ya nchi baada ya kufanya mazungumzo yaliyowalainisha wanajeshi hao.

Bila tamaa Kambona, alikwenda Kigamboni kuwachukua Mwalimu Nyerere na Kawawa waliokuwa mafichoni, na kubaki mwaminifu kwa nafasi yake ya uwaziri aliyokuwa nayo.

Kambona kasahaulika pamoja na uaminifu huo na mema yote kiasi kwamba hakuna hata sehemu ya kumbukumbu inayomwelezea kwa mazuri yake. Ameingizwa katika kapu la waliosahaulika.
Kambona alikuwa Mzaliwa wa wapi hapa Nchini?
 
Marehemu Oscar Kambona alizaliwa mwaka 1925 katika kijiji cha Kwambe kilichopo mwambao mwa ziwa Nyasa, karibu na Mbamba-bay, wilaya ya Mbinga, Mkoa wa Ruvuma. Alikuwa mtoto wa marehemu Rev. David Kambona na Bibi Miriam Kambona.

Naomba kuwasilisha...
Duh Kumbe Mzee wa Home Karibu na Liparamba Kabisa
 
Salute kwako Ushimen.
Nadhani umejibu kwa kirefu kuliko hata matarajio ya muuliza swali.

Kwa hayo tu yanatosha kumwonesha kama mtu anayestahili kuenziwa kama shujaa wa historia ya taifa letu kabla na baada ya Uhuru
 
BBC ilianza Matangazo yake kwa lugha ya Kiswahili mwaka 1957. Tarehe 27 Juni 1957 sauti ya Kiswahili ilisikika mara ya kwanza;

msemaji alikuwa Oscar Kambona aliyekuwa wakati ule mwanafunzi wa chuo kikuu huko London na baadaye waziri wa mambo ya nje wa kwanza baada ya uhuru wa Tanzania.

Naombeni kuulize huyu mzee yupo wapi kwa sasa?.
Nazan alfariki 1997 kama sjakosea
 
d
Kambona kasahaulika pamoja na uaminifu huo na mema yote kiasi kwamba hakuna hata sehemu ya kumbukumbu inayomwelezea kwa mazuri yake. Ameingizwa katika kapu la waliosahaulika.
daaaa ushimen leo nimekuamini kilasiku nasomaga koment zako za pumba kumbe umejaa historia nzuri hata kuliko hata mleta uzi huu hongera sana nilipoona umekoment nilijua unatoa pumba sijaamini nimesoma mpaka mwisho very interested napenda sana historia za watu mashuhuri
 
Yupo mtwara kijiji cha msijute karb na Kiwanis cha dangote
Me pia nilijua ivo au labda yule ni mdogo wake na kambona anayezumgumziwa hapa .
Yule wa pale msijute nasikiaga alikuwa balozi wa Tz ila nchi siikumbuki .
 
d

daaaa ushimen leo nimekuamini kilasiku nasomaga koment zako za pumba kumbe umejaa historia nzuri hata kuliko hata mleta uzi huu hongera sana nilipoona umekoment nilijua unatoa pumba sijaamini nimesoma mpaka mwisho very interested napenda sana historia za watu mashuhuri
Asante mkuu TANSIS ujue leo nimeamka vizuri bila mning'inio hata kidogo, that's why nimekua Tamam....[emoji4] [emoji4]
 
Siasa ni mbaya sana.Nyerere alikuwa best man harusi ya Kambona.Kikweli Kambona alikuwa sahihi kabisa kuwa huwezi jenga ujamaa ndani ya umasikini.
Hata huko zaire, miaka ya 60 rais kassa vubu alikua baba wa ubatizo wa mtoto wa kanali mobutu wakati huo mobutu akiwa chief of staff
Na mobutu akamuita mtoto huyo joseph kasavubu kama heshima kwa rais huyo
Lakini mobutu alikuja kupindua serikali na kumuweka house arrest rais kasavubu vijijini huko kwenye shamba lake mpaka huyo mzee akaja kufia huko
Na mobutu akabadili jina la mwanae kuwa JEAN PAUL NIWA
 
Historia inaonyesha aligombana na Nyerere, navyanzo mbalimbali vya habari hadi sasa vinashindwa kueleza ukweli juu ya hasa kile kilichosababisha kuzuka kwa tofauti kati ya Mwalimu Nyerere na Kambona.

Kila mtu amekuwa akijaribu kueleza ugomvi wa wawili hawa kadiri ajuavyo.

Kuna madai kwamba viongozi hawa wawili ambao kwa sasa wote ni marehemu, walianza kutofautiana baada ya maasi ya wanajeshi.

Inadaiwa kuwa Nyerere alitaka kuanzisha mfumo wa chama kimoja nchini ili kuimarisha usalama na Kambona alipinga hoja hiyo kwa maelezo kwamba mfumo huo ungezorotesha uhuru na maendeleo ya demokrasia. Hoja hiyo ikafikishwa bungeni kwa maamuzi na kwa bahati mbaya kwa Kambona akashindwa lakini akagoma kusaini muswada huo.

Katika safari ya China ya Mwalimu ya mwaka 1965, alipendezwa na mfumo wa kikomonisti wa Mao, na akataka kuanzisha mfumo kama huo kwa jina la ‘Ujamaa’ hapa nchini.

Dhana ya msingi ya mfumo wa Ujamaa ilikuwa ni kuwahamishia watu katika vijiji vya ujamaa na kutaifisha viwanda na vitegauchumi vilivyokuwa vikimilikiwa na watu binafsi ili kuwa chini ya wananchi, hatua iliyopingwa vikali na Kambona kwa maelezo kwamba ungeongeza umaskini na udhibiti wa serikali kwa watu.

Inadaiwa kuwa kulikuwa na msuguano mkali, kiasi kwamba ilimlazimu Kambona alijiuzulu nyadhifa zake ndani ya serikali na chama na hatimaye yeye na familia yake wakakimbilia Nairobi, Kenya na kisha Uingereza ambako walipatiwa hifadhi ya kisiasa.

Mara baada ya kukimbia nchi, mali za Kambona zilichukuliwa na serikali, huku ndugu zake wawili, wakiwekwa kizuizini bila ya kufikishwa mahakamani na kufungwa kwa zaidi ya miaka kumi.

Inaaminika kuwa wazo la Kambona lilikubaliwa na baadhi ya viongozi wa chama na serikali.

Hii inatokana na kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake, Bibi Titi Mohammed, Michael Kamaliza ambaye alikuwa mwanaharakati wa chama cha wafanyakazi, mwanachama wa TANU na waziri, pamoja na Gray Mattaka, Eliya Chipaka na Prisca Chiombola kwa tuhuma za uhaini.

Viongozi hao walihukumiwa pamoja na Kambona licha ya kuwa alikimbilia London lakini walikata rufaa katika Mahakama Kuu ya Afrika Mashariki na wakaachiwa huru.

Hata pamoja na kuachiwa huru,walikamatwa na serikali na kufungwa tena.

Tuhuma kubwa ya Kambona ni kwamba aliiba pesa nyingi za umma, na kukamatwa nazo alipopekuliwa katika uwanja wa Embakasi, mjini Nairobi jambo ambalo alilipinga kwa miaka mingi na kuliweka wazi katika taarifa yake kwa waandishi wa habari Septemba 6, 1967 huko London. Kambona alikwenda mbali zaidi akaitaka serikali ya Tanzania kuiomba Kenya kutoa ukweli juu ya jambo hilo, jambo ambalo halikufanyika hadi kifo chake.

Inaaminika kuwa maisha ya Kambona jijini London yalikuwa ya shida na dhiki. Mwaka 1982, baadhi ya ndugu wa Kambona waliachiwa toka kizuizini baada ya juhudi za Waziri Mkuu wa New Zealand, Robert Muldoon.

Mwaka 1990, Kambona akiwa na matumaini makubwa ya mabadiliko ya kisiasa katika Tanzania, aliunda chama kiitwacho Tanzania Democratic Alliance, akiwa bado uhamishoni.

Mwaka 1992, wakati mfumo wa vyama vingi ulipoanzishwa Tanzania, Kambona aliomba kurudi nchini.

Hata hivyo, serikali ya Tanzania ilimkatalia katakata. Kuona hivyo, Kambona aliiomba serikali ya Uingereza kumpa pasi ya kusafiria kurudi Tanzania, lakini pia akakumbana na tishio la kukamatwa na kuwekwa ndani pindi angelitua.

Septemba 5, 1992, bila woga wa kukamatwa, Kambona alitua katika ardhi ya Tanzania na hakushikwa, badala yake alipewa miezi mitatu awe amekamilisha utata wa uraia wake.

Nia yake ya kushiriki kwa nguvu katika harakati za siasa ilitiwa doa na kudorora kwa afya yake akisumbuliwa na shinikizo la damu.

Afya yake ilizidi kuwa mbaya, na hivyo akalazimika kurudishwa tena London Uingereza kwa matibabu.

Hata hivyo, Juni,1997, Kambona alifariki akipishana kwa siku chache tu na mdogo wake Otini Kambona ambaye pia alikuwa nchini humo kwa matibabu ya moyo.

Katika namna ambayo yaweza kuelezwa kuwa ni tendo pekee la kumuenzi mwanasiasa huyo mashuhuri, serikali ilikubali kusafirisha mwili wake na wa Otini na pia shughuli zote za mazishi.

Kambona ameacha mke na watoto wawili, akiwemo Neema Kambona ambaye hivi karibuni alijiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) tawi la London. Mtoto wa kwanza, Mosi Kambona aliuawa miaka si mingi sana iliyopita mjini London katika mazingira ya kutatanisha.

Kambona ameondoka, lakini pamoja na kuwepo kwa dosari hiyo ya kusigana katika siasa, alifanya makubwa mengi. Ni kiongozi pekee ambaye askari wa jeshi walipoasi na kuwalazimu Mwalimu Nyerere na Rashid Kawawa kukimbia, angeweza kutwaa madaraka ya nchi baada ya kufanya mazungumzo yaliyowalainisha wanajeshi hao.

Bila tamaa Kambona, alikwenda Kigamboni kuwachukua Mwalimu Nyerere na Kawawa waliokuwa mafichoni, na kubaki mwaminifu kwa nafasi yake ya uwaziri aliyokuwa nayo.

Kambona kasahaulika pamoja na uaminifu huo na mema yote kiasi kwamba hakuna hata sehemu ya kumbukumbu inayomwelezea kwa mazuri yake. Ameingizwa katika kapu la waliosahaulika.
Ahsante sana mkuu umeeleza kwa mtiririko mzuri sana sana kiasi hata mbulula Kama DAB ataelewa bila tatizo lolote,hakika Kuna mengi sana chini ya kapeti yamefichwa kwa ajili ya chuki binafsi za watawala,pole sana Oscar Kambona nakumbuka aina fulani ya uchanaji wake wa nywele mpaka ikafikia watu wanasema nichane Kambona
 
Back
Top Bottom