Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona?

Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona?

Dada Neema Kambona,kama unapita humu hebu urudi Tanzania uombe kurudishiwa Mali za mzee,wewe ndie mrithi pekee uliye baki kwasasa.Rais Magufuli labda anaweza kukuelewa.
 
Asante mkuu @TANSIS ujue leo nimeamka vizuri bila mning'inio hata kidogo, that's why nimekua Tamam....
emoji4.png
emoji4.png
mmmm mning'inio tena?? utaharibu sasa ila ukovizuri sana
 
Ahsante sana mkuu umeeleza kwa mtiririko mzuri sana sana kiasi hata mbulula Kama DAB ataelewa bila tatizo lolote,hakika Kuna mengi sana chini ya kapeti yamefichwa kwa ajili ya chuki binafsi za watawala,pole sana Oscar Kambona nakumbuka aina fulani ya uchanaji wake wa nywele mpaka ikafikia watu wanasema nichane Kambona
images.jpeg

Naomba kuwasilisha
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Marehemu Oscar Kambona alizaliwa mwaka 1925 katika kijiji cha Kwambe kilichopo mwambao mwa ziwa Nyasa, karibu na Mbamba-bay, wilaya ya Mbinga, Mkoa wa Ruvuma. Alikuwa mtoto wa marehemu Rev. David Kambona na Bibi Miriam Kambona.

Naomba kuwasilisha...
Kwa kifupi ni mnyasa
 
BBC ilianza Matangazo yake kwa lugha ya Kiswahili mwaka 1957. Tarehe 27 Juni 1957 sauti ya Kiswahili ilisikika mara ya kwanza;

msemaji alikuwa Oscar Kambona aliyekuwa wakati ule mwanafunzi wa chuo kikuu huko London na baadaye waziri wa mambo ya nje wa kwanza baada ya uhuru wa Tanzania.

Naombeni kuulize huyu mzee yupo wapi kwa sasa?.

Umeuliza swali zuri, lakini yawezekana majibu yakawatofauti na matarajio yako.

Mfano:
kAMA UNA FAHAMU TAREHE AMBAYO MATANGAZO YA KISWAHIL BBC YALIANZA NA MTANGAZAJI ALIKUWA NANI, KWA NINI HUJUI YUKO WAPI HUYO MTANGAZAJI? ULIKO PATA HIZO TAARIFA, UNAWEZA PIA PATA ALIKO KWA SASA.
 
Historia inaonyesha aligombana na Nyerere, navyanzo mbalimbali vya habari hadi sasa vinashindwa kueleza ukweli juu ya hasa kile kilichosababisha kuzuka kwa tofauti kati ya Mwalimu Nyerere na Kambona.

Kila mtu amekuwa akijaribu kueleza ugomvi wa wawili hawa kadiri ajuavyo.

Kuna madai kwamba viongozi hawa wawili ambao kwa sasa wote ni marehemu, walianza kutofautiana baada ya maasi ya wanajeshi.

Inadaiwa kuwa Nyerere alitaka kuanzisha mfumo wa chama kimoja nchini ili kuimarisha usalama na Kambona alipinga hoja hiyo kwa maelezo kwamba mfumo huo ungezorotesha uhuru na maendeleo ya demokrasia. Hoja hiyo ikafikishwa bungeni kwa maamuzi na kwa bahati mbaya kwa Kambona akashindwa lakini akagoma kusaini muswada huo.

Katika safari ya China ya Mwalimu ya mwaka 1965, alipendezwa na mfumo wa kikomonisti wa Mao, na akataka kuanzisha mfumo kama huo kwa jina la ‘Ujamaa’ hapa nchini.

Dhana ya msingi ya mfumo wa Ujamaa ilikuwa ni kuwahamishia watu katika vijiji vya ujamaa na kutaifisha viwanda na vitegauchumi vilivyokuwa vikimilikiwa na watu binafsi ili kuwa chini ya wananchi, hatua iliyopingwa vikali na Kambona kwa maelezo kwamba ungeongeza umaskini na udhibiti wa serikali kwa watu.

Inadaiwa kuwa kulikuwa na msuguano mkali, kiasi kwamba ilimlazimu Kambona alijiuzulu nyadhifa zake ndani ya serikali na chama na hatimaye yeye na familia yake wakakimbilia Nairobi, Kenya na kisha Uingereza ambako walipatiwa hifadhi ya kisiasa.

Mara baada ya kukimbia nchi, mali za Kambona zilichukuliwa na serikali, huku ndugu zake wawili, wakiwekwa kizuizini bila ya kufikishwa mahakamani na kufungwa kwa zaidi ya miaka kumi.

Inaaminika kuwa wazo la Kambona lilikubaliwa na baadhi ya viongozi wa chama na serikali.

Hii inatokana na kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake, Bibi Titi Mohammed, Michael Kamaliza ambaye alikuwa mwanaharakati wa chama cha wafanyakazi, mwanachama wa TANU na waziri, pamoja na Gray Mattaka, Eliya Chipaka na Prisca Chiombola kwa tuhuma za uhaini.

Viongozi hao walihukumiwa pamoja na Kambona licha ya kuwa alikimbilia London lakini walikata rufaa katika Mahakama Kuu ya Afrika Mashariki na wakaachiwa huru.

Hata pamoja na kuachiwa huru,walikamatwa na serikali na kufungwa tena.

Tuhuma kubwa ya Kambona ni kwamba aliiba pesa nyingi za umma, na kukamatwa nazo alipopekuliwa katika uwanja wa Embakasi, mjini Nairobi jambo ambalo alilipinga kwa miaka mingi na kuliweka wazi katika taarifa yake kwa waandishi wa habari Septemba 6, 1967 huko London. Kambona alikwenda mbali zaidi akaitaka serikali ya Tanzania kuiomba Kenya kutoa ukweli juu ya jambo hilo, jambo ambalo halikufanyika hadi kifo chake.

Inaaminika kuwa maisha ya Kambona jijini London yalikuwa ya shida na dhiki. Mwaka 1982, baadhi ya ndugu wa Kambona waliachiwa toka kizuizini baada ya juhudi za Waziri Mkuu wa New Zealand, Robert Muldoon.

Mwaka 1990, Kambona akiwa na matumaini makubwa ya mabadiliko ya kisiasa katika Tanzania, aliunda chama kiitwacho Tanzania Democratic Alliance, akiwa bado uhamishoni.

Mwaka 1992, wakati mfumo wa vyama vingi ulipoanzishwa Tanzania, Kambona aliomba kurudi nchini.

Hata hivyo, serikali ya Tanzania ilimkatalia katakata. Kuona hivyo, Kambona aliiomba serikali ya Uingereza kumpa pasi ya kusafiria kurudi Tanzania, lakini pia akakumbana na tishio la kukamatwa na kuwekwa ndani pindi angelitua.

Septemba 5, 1992, bila woga wa kukamatwa, Kambona alitua katika ardhi ya Tanzania na hakushikwa, badala yake alipewa miezi mitatu awe amekamilisha utata wa uraia wake.

Nia yake ya kushiriki kwa nguvu katika harakati za siasa ilitiwa doa na kudorora kwa afya yake akisumbuliwa na shinikizo la damu.

Afya yake ilizidi kuwa mbaya, na hivyo akalazimika kurudishwa tena London Uingereza kwa matibabu.

Hata hivyo, Juni,1997, Kambona alifariki akipishana kwa siku chache tu na mdogo wake Otini Kambona ambaye pia alikuwa nchini humo kwa matibabu ya moyo.

Katika namna ambayo yaweza kuelezwa kuwa ni tendo pekee la kumuenzi mwanasiasa huyo mashuhuri, serikali ilikubali kusafirisha mwili wake na wa Otini na pia shughuli zote za mazishi.

Kambona ameacha mke na watoto wawili, akiwemo Neema Kambona ambaye hivi karibuni alijiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) tawi la London. Mtoto wa kwanza, Mosi Kambona aliuawa miaka si mingi sana iliyopita mjini London katika mazingira ya kutatanisha.

Kambona ameondoka, lakini pamoja na kuwepo kwa dosari hiyo ya kusigana katika siasa, alifanya makubwa mengi. Ni kiongozi pekee ambaye askari wa jeshi walipoasi na kuwalazimu Mwalimu Nyerere na Rashid Kawawa kukimbia, angeweza kutwaa madaraka ya nchi baada ya kufanya mazungumzo yaliyowalainisha wanajeshi hao.

Bila tamaa Kambona, alikwenda Kigamboni kuwachukua Mwalimu Nyerere na Kawawa waliokuwa mafichoni, na kubaki mwaminifu kwa nafasi yake ya uwaziri aliyokuwa nayo.

Kambona kasahaulika pamoja na uaminifu huo na mema yote kiasi kwamba hakuna hata sehemu ya kumbukumbu inayomwelezea kwa mazuri yake. Ameingizwa katika kapu la waliosahaulika.
Kuna thread katika jukwaa la historia imeelezea hili suala kwa mapana..
Pamoja na madhaifu ya Oscar lakini anastahili heshima yake na haswaa kutokana na hoja zake za mwanzo zilizomtofautisha na Nyerere , zilikuja kuwa kweli baada ya kushindwa kwa ujamaa na impact za ujamaa tulizonazo hata leo
 
Kwa wanaofahamu yaliyofichika Kambona alisaidia kutuliza vuguvugu la mapinduzi mwaka 1967 japo mchango wake ulionekana hauna maana baada ya kupishana mawazo na mwenye mji Mungu ailaze mahala pema roho yake
 
Kuna thread katika jukwaa la historia imeelezea hili suala kwa mapana..
Pamoja na madhaifu ya Oscar lakini anastahili heshima yake na haswaa kutokana na hoja zake za mwanzo zilizomtofautisha na Nyerere , zilikuja kuwa kweli baada ya kushindwa kwa ujamaa na impact za ujamaa tulizonazo hata leo
Ebu ipandishe tuisome mkuu....
 
BBC ilianza Matangazo yake kwa lugha ya Kiswahili mwaka 1957. Tarehe 27 Juni 1957 sauti ya Kiswahili ilisikika mara ya kwanza;

msemaji alikuwa Oscar Kambona aliyekuwa wakati ule mwanafunzi wa chuo kikuu huko London na baadaye waziri wa mambo ya nje wa kwanza baada ya uhuru wa Tanzania.

Naombeni kuulize huyu mzee yupo wapi kwa sasa?.
Alikwisha fariki na kaburi lake lipo Kinondoni karibu na kaburi la Kanumba, pia picha take inatumiwa kwenye Avatar ya mmoja wa wana JF.
 
Nadhani kama mawazo na mtazamo wa Kambona vingefuatwa labda nchi yetu isingekuwa na umaskini huu! Sema ndio hivyo tena Mwalimu Nyerere alikuwa mbishi na kaubabe fulan hivi! R. I. P Kambona wewe ni shujaa usiye imbwa!
 
Historia inaonyesha aligombana na Nyerere, navyanzo mbalimbali vya habari hadi sasa vinashindwa kueleza ukweli juu ya hasa kile kilichosababisha kuzuka kwa tofauti kati ya Mwalimu Nyerere na Kambona.

Kila mtu amekuwa akijaribu kueleza ugomvi wa wawili hawa kadiri ajuavyo.

Kuna madai kwamba viongozi hawa wawili ambao kwa sasa wote ni marehemu, walianza kutofautiana baada ya maasi ya wanajeshi.

Inadaiwa kuwa Nyerere alitaka kuanzisha mfumo wa chama kimoja nchini ili kuimarisha usalama na Kambona alipinga hoja hiyo kwa maelezo kwamba mfumo huo ungezorotesha uhuru na maendeleo ya demokrasia. Hoja hiyo ikafikishwa bungeni kwa maamuzi na kwa bahati mbaya kwa Kambona akashindwa lakini akagoma kusaini muswada huo.

Katika safari ya China ya Mwalimu ya mwaka 1965, alipendezwa na mfumo wa kikomonisti wa Mao, na akataka kuanzisha mfumo kama huo kwa jina la ‘Ujamaa’ hapa nchini.

Dhana ya msingi ya mfumo wa Ujamaa ilikuwa ni kuwahamishia watu katika vijiji vya ujamaa na kutaifisha viwanda na vitegauchumi vilivyokuwa vikimilikiwa na watu binafsi ili kuwa chini ya wananchi, hatua iliyopingwa vikali na Kambona kwa maelezo kwamba ungeongeza umaskini na udhibiti wa serikali kwa watu.

Inadaiwa kuwa kulikuwa na msuguano mkali, kiasi kwamba ilimlazimu Kambona alijiuzulu nyadhifa zake ndani ya serikali na chama na hatimaye yeye na familia yake wakakimbilia Nairobi, Kenya na kisha Uingereza ambako walipatiwa hifadhi ya kisiasa.

Mara baada ya kukimbia nchi, mali za Kambona zilichukuliwa na serikali, huku ndugu zake wawili, wakiwekwa kizuizini bila ya kufikishwa mahakamani na kufungwa kwa zaidi ya miaka kumi.

Inaaminika kuwa wazo la Kambona lilikubaliwa na baadhi ya viongozi wa chama na serikali.

Hii inatokana na kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake, Bibi Titi Mohammed, Michael Kamaliza ambaye alikuwa mwanaharakati wa chama cha wafanyakazi, mwanachama wa TANU na waziri, pamoja na Gray Mattaka, Eliya Chipaka na Prisca Chiombola kwa tuhuma za uhaini.

Viongozi hao walihukumiwa pamoja na Kambona licha ya kuwa alikimbilia London lakini walikata rufaa katika Mahakama Kuu ya Afrika Mashariki na wakaachiwa huru.

Hata pamoja na kuachiwa huru,walikamatwa na serikali na kufungwa tena.

Tuhuma kubwa ya Kambona ni kwamba aliiba pesa nyingi za umma, na kukamatwa nazo alipopekuliwa katika uwanja wa Embakasi, mjini Nairobi jambo ambalo alilipinga kwa miaka mingi na kuliweka wazi katika taarifa yake kwa waandishi wa habari Septemba 6, 1967 huko London. Kambona alikwenda mbali zaidi akaitaka serikali ya Tanzania kuiomba Kenya kutoa ukweli juu ya jambo hilo, jambo ambalo halikufanyika hadi kifo chake.

Inaaminika kuwa maisha ya Kambona jijini London yalikuwa ya shida na dhiki. Mwaka 1982, baadhi ya ndugu wa Kambona waliachiwa toka kizuizini baada ya juhudi za Waziri Mkuu wa New Zealand, Robert Muldoon.

Mwaka 1990, Kambona akiwa na matumaini makubwa ya mabadiliko ya kisiasa katika Tanzania, aliunda chama kiitwacho Tanzania Democratic Alliance, akiwa bado uhamishoni.

Mwaka 1992, wakati mfumo wa vyama vingi ulipoanzishwa Tanzania, Kambona aliomba kurudi nchini.

Hata hivyo, serikali ya Tanzania ilimkatalia katakata. Kuona hivyo, Kambona aliiomba serikali ya Uingereza kumpa pasi ya kusafiria kurudi Tanzania, lakini pia akakumbana na tishio la kukamatwa na kuwekwa ndani pindi angelitua.

Septemba 5, 1992, bila woga wa kukamatwa, Kambona alitua katika ardhi ya Tanzania na hakushikwa, badala yake alipewa miezi mitatu awe amekamilisha utata wa uraia wake.

Nia yake ya kushiriki kwa nguvu katika harakati za siasa ilitiwa doa na kudorora kwa afya yake akisumbuliwa na shinikizo la damu.

Afya yake ilizidi kuwa mbaya, na hivyo akalazimika kurudishwa tena London Uingereza kwa matibabu.

Hata hivyo, Juni,1997, Kambona alifariki akipishana kwa siku chache tu na mdogo wake Otini Kambona ambaye pia alikuwa nchini humo kwa matibabu ya moyo.

Katika namna ambayo yaweza kuelezwa kuwa ni tendo pekee la kumuenzi mwanasiasa huyo mashuhuri, serikali ilikubali kusafirisha mwili wake na wa Otini na pia shughuli zote za mazishi.

Kambona ameacha mke na watoto wawili, akiwemo Neema Kambona ambaye hivi karibuni alijiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) tawi la London. Mtoto wa kwanza, Mosi Kambona aliuawa miaka si mingi sana iliyopita mjini London katika mazingira ya kutatanisha.

Kambona ameondoka, lakini pamoja na kuwepo kwa dosari hiyo ya kusigana katika siasa, alifanya makubwa mengi. Ni kiongozi pekee ambaye askari wa jeshi walipoasi na kuwalazimu Mwalimu Nyerere na Rashid Kawawa kukimbia, angeweza kutwaa madaraka ya nchi baada ya kufanya mazungumzo yaliyowalainisha wanajeshi hao.

Bila tamaa Kambona, alikwenda Kigamboni kuwachukua Mwalimu Nyerere na Kawawa waliokuwa mafichoni, na kubaki mwaminifu kwa nafasi yake ya uwaziri aliyokuwa nayo.

Kambona kasahaulika pamoja na uaminifu huo na mema yote kiasi kwamba hakuna hata sehemu ya kumbukumbu inayomwelezea kwa mazuri yake. Ameingizwa katika kapu la waliosahaulika.
Ubarikiwe mkuu
 
d

daaaa ushimen leo nimekuamini kilasiku nasomaga koment zako za pumba kumbe umejaa historia nzuri hata kuliko hata mleta uzi huu hongera sana nilipoona umekoment nilijua unatoa pumba sijaamini nimesoma mpaka mwisho very interested napenda sana historia za watu mashuhuri
Ndg usione watu wanatoa koment za pumba humu ukawadharau

Kuna watu ni so smart humu wanajitoa akili tu
 
Vitu vingi kwenye historia ya TZ vimetiwa kapuni kutokana na maslahi binafsi ndo maana hata la kambona sishangai
 
Historia inaonyesha aligombana na Nyerere, navyanzo mbalimbali vya habari hadi sasa vinashindwa kueleza ukweli juu ya hasa kile kilichosababisha kuzuka kwa tofauti kati ya Mwalimu Nyerere na Kambona.

Kila mtu amekuwa akijaribu kueleza ugomvi wa wawili hawa kadiri ajuavyo.

Kuna madai kwamba viongozi hawa wawili ambao kwa sasa wote ni marehemu, walianza kutofautiana baada ya maasi ya wanajeshi.

Inadaiwa kuwa Nyerere alitaka kuanzisha mfumo wa chama kimoja nchini ili kuimarisha usalama na Kambona alipinga hoja hiyo kwa maelezo kwamba mfumo huo ungezorotesha uhuru na maendeleo ya demokrasia. Hoja hiyo ikafikishwa bungeni kwa maamuzi na kwa bahati mbaya kwa Kambona akashindwa lakini akagoma kusaini muswada huo.

Katika safari ya China ya Mwalimu ya mwaka 1965, alipendezwa na mfumo wa kikomonisti wa Mao, na akataka kuanzisha mfumo kama huo kwa jina la ‘Ujamaa’ hapa nchini.

Dhana ya msingi ya mfumo wa Ujamaa ilikuwa ni kuwahamishia watu katika vijiji vya ujamaa na kutaifisha viwanda na vitegauchumi vilivyokuwa vikimilikiwa na watu binafsi ili kuwa chini ya wananchi, hatua iliyopingwa vikali na Kambona kwa maelezo kwamba ungeongeza umaskini na udhibiti wa serikali kwa watu.

Inadaiwa kuwa kulikuwa na msuguano mkali, kiasi kwamba ilimlazimu Kambona alijiuzulu nyadhifa zake ndani ya serikali na chama na hatimaye yeye na familia yake wakakimbilia Nairobi, Kenya na kisha Uingereza ambako walipatiwa hifadhi ya kisiasa.

Mara baada ya kukimbia nchi, mali za Kambona zilichukuliwa na serikali, huku ndugu zake wawili, wakiwekwa kizuizini bila ya kufikishwa mahakamani na kufungwa kwa zaidi ya miaka kumi.

Inaaminika kuwa wazo la Kambona lilikubaliwa na baadhi ya viongozi wa chama na serikali.

Hii inatokana na kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake, Bibi Titi Mohammed, Michael Kamaliza ambaye alikuwa mwanaharakati wa chama cha wafanyakazi, mwanachama wa TANU na waziri, pamoja na Gray Mattaka, Eliya Chipaka na Prisca Chiombola kwa tuhuma za uhaini.

Viongozi hao walihukumiwa pamoja na Kambona licha ya kuwa alikimbilia London lakini walikata rufaa katika Mahakama Kuu ya Afrika Mashariki na wakaachiwa huru.

Hata pamoja na kuachiwa huru,walikamatwa na serikali na kufungwa tena.

Tuhuma kubwa ya Kambona ni kwamba aliiba pesa nyingi za umma, na kukamatwa nazo alipopekuliwa katika uwanja wa Embakasi, mjini Nairobi jambo ambalo alilipinga kwa miaka mingi na kuliweka wazi katika taarifa yake kwa waandishi wa habari Septemba 6, 1967 huko London. Kambona alikwenda mbali zaidi akaitaka serikali ya Tanzania kuiomba Kenya kutoa ukweli juu ya jambo hilo, jambo ambalo halikufanyika hadi kifo chake.

Inaaminika kuwa maisha ya Kambona jijini London yalikuwa ya shida na dhiki. Mwaka 1982, baadhi ya ndugu wa Kambona waliachiwa toka kizuizini baada ya juhudi za Waziri Mkuu wa New Zealand, Robert Muldoon.

Mwaka 1990, Kambona akiwa na matumaini makubwa ya mabadiliko ya kisiasa katika Tanzania, aliunda chama kiitwacho Tanzania Democratic Alliance, akiwa bado uhamishoni.

Mwaka 1992, wakati mfumo wa vyama vingi ulipoanzishwa Tanzania, Kambona aliomba kurudi nchini.

Hata hivyo, serikali ya Tanzania ilimkatalia katakata. Kuona hivyo, Kambona aliiomba serikali ya Uingereza kumpa pasi ya kusafiria kurudi Tanzania, lakini pia akakumbana na tishio la kukamatwa na kuwekwa ndani pindi angelitua.

Septemba 5, 1992, bila woga wa kukamatwa, Kambona alitua katika ardhi ya Tanzania na hakushikwa, badala yake alipewa miezi mitatu awe amekamilisha utata wa uraia wake.

Nia yake ya kushiriki kwa nguvu katika harakati za siasa ilitiwa doa na kudorora kwa afya yake akisumbuliwa na shinikizo la damu.

Afya yake ilizidi kuwa mbaya, na hivyo akalazimika kurudishwa tena London Uingereza kwa matibabu.

Hata hivyo, Juni,1997, Kambona alifariki akipishana kwa siku chache tu na mdogo wake Otini Kambona ambaye pia alikuwa nchini humo kwa matibabu ya moyo.

Katika namna ambayo yaweza kuelezwa kuwa ni tendo pekee la kumuenzi mwanasiasa huyo mashuhuri, serikali ilikubali kusafirisha mwili wake na wa Otini na pia shughuli zote za mazishi.

Kambona ameacha mke na watoto wawili, akiwemo Neema Kambona ambaye hivi karibuni alijiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) tawi la London. Mtoto wa kwanza, Mosi Kambona aliuawa miaka si mingi sana iliyopita mjini London katika mazingira ya kutatanisha.

Kambona ameondoka, lakini pamoja na kuwepo kwa dosari hiyo ya kusigana katika siasa, alifanya makubwa mengi. Ni kiongozi pekee ambaye askari wa jeshi walipoasi na kuwalazimu Mwalimu Nyerere na Rashid Kawawa kukimbia, angeweza kutwaa madaraka ya nchi baada ya kufanya mazungumzo yaliyowalainisha wanajeshi hao.

Bila tamaa Kambona, alikwenda Kigamboni kuwachukua Mwalimu Nyerere na Kawawa waliokuwa mafichoni, na kubaki mwaminifu kwa nafasi yake ya uwaziri aliyokuwa nayo.

Kambona kasahaulika pamoja na uaminifu huo na mema yote kiasi kwamba hakuna hata sehemu ya kumbukumbu inayomwelezea kwa mazuri yake. Ameingizwa katika kapu la waliosahaulika.[/QUOTEDu jamani!
 
Nadhani kama mawazo na mtazamo wa Kambona vingefuatwa labda nchi yetu isingekuwa na umaskini huu! Sema ndio hivyo tena Mwalimu Nyerere alikuwa mbishi na kaubabe fulan hivi! R. I. P Kambona wewe ni shujaa usiye imbwa!
Na tungeufuata ushauri wa Kambona khs ubepari pengine leo 80% ya ardhi yetu ingemilikiwa na Viongozi wa CCM kama ilivyo kwa Kenyatta family huko Kenya.

Maskini wa Tz yule choka mbovu kukuta anamiliki heka 5 ni kawaida tu nenda Kenya hapo utakubali mziki arifu.
 
Back
Top Bottom