Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona?

Mkumbo hata wewe asaiv mawazo yako yapo kifungoni, najua hata sasa una mapenzi na rais magufuli na ana madhaifu makubwa Mara mia afadhali madhaifu ya nyerere uliyosema hapa, lkn sababu ya keki ya taifa unayopata kwa sasa sidhani kama utaona dhaifu hata moja la magufuli, nimefanya hivi ili kukumbusha kuwa koti la kawawa ndo umelivaa wewe muda huu.
 
wewe lazima ni jasusi mstaafu umeyajuaje haya!
 
Battle ya Kambona na Mwalimu Nyerere ni ya kiitikadi na maono kuhusu uelekeo wa Taifa kuliko ubinafsi unaozungumzwa bila kujali uhalisia wa mambo.

Yale anayoshutumiwa nayo Kambona, alijisafisha nayo kabla hata ya matope kumtapakaa baada ya kurushiwa na wafuasi wa Mwalimu.

Ni ukweli ulio wazi kuwa Kambona hakuupenda Ujamaa ilhal Mwalimu aliuchukia Ubepari. Vyovyote iwavyo leo tu mashahid kuwa Kambona alikuwa na maono sahihi zaidi katika kuendesha nchi kupitia soko huria kuliko kucentralize kila nyenzo ya kiuchumi kama alivyoamini Mwalimu Nyerere.

Hatutaki kuukubali ukweli lakini sera za ujamaa na arrogance ya Mwalimu n chanzo kikuu cha Umaskini wa Tanzania tulio nayo. Alihubir nadharia na kufanya yalioshindwa.

Naiita vita ile ya Mwalimu vs Kambona kama "Wretched Battle of the Country".

Usahihi wa Kambona upo kweny anguko la Ujamaa. Usahihi wa Kambona upo kweny ufukara tulio nao leo hii. Aliiona leo yetu licha ya kuwa aliishi jana yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
 
 
keki ya taifa ni shidaa😄😄😄
 
Kama walitofautiana mitazamo/itikadi basi ni dhahiri kwamba lazima mmoja angeendelea mmoja angebaki.
 
Ni sawa Kawawa alikuwa sahihi hatuna shida na hilo!

Lakini huyu Kambona alishiriki kutunga Sera na Misingi ya Azimio la Arusha,wazi wazi ndani ya jopo la Mwalimu Nyerere! wakakubaliana kwa Umoja jinsi ya kulitekeleza! kwa nini baadaye aligeuka na kulikana? ili kutekeleza kile alicho shiriki kukianzisha?

ni wazi alikuwa ni tatizo la ki-Juda mbele ya macho ya wenye akili hata km huyo angekuwa Rais wetu na kuleta huo Ubepari, angeongoza vibaya, na tungekuwa pabaya zaidi kuliko Ubepari wa mpito tulio nao leo!

Sisi Tanzania siyo maskini hata kidogo sema wewe Mungu amekupiga Kofi tu, Maghorofa haya yoote? Afya bure, Nyumba Bure NH, Nyumba za Biafra kila Mkoa, Barabara lami mpaka chooni, Elimu yetu Bure kwa miaka 50 tu ya Uhuru tuko hapa pazauri,

Taifa la watu tulioathiriwa na Utumwa, Ukoloni, Vita za mara kwa mara za Majirani zetu, lkn bado tuko ngangari, unakufuru bure mwishowe Mungu atuadhibu kwa domo lako! kukosa shkrani! tembea USA uone lundo la Maskini, Lesotho, Senegal ni utachoka wewe! haya maneno ume-copy ya watu vitabuni! sema ya kwako ya dhati moyoni.
 
Dah! eeeh! weee jamaa hatari sana, kwa hiyo umerudi nyumaaa! mpaka siku tarehe mwaka? JF si machejo, hadanganywi mtu humu! umesahau kuwa miaka ya zamani kabla ya uhuru siyo kama ya siku hizi!
 
Kambona Anatakiwa kusafishwa jina , kulikuwa na dhana mbili Moja kutofautiana kiitikadi na mwalimu , lakini kubwa ni ile kuonewa Wivu na wenzake kwani wakati wa Maasi ya 1964 yeye ndiye alikuwa nyota wa mchezo na laiti angetaka angeweza kutwaaa madaraka , lakini haikua kwenye akili yake , alipambana sana kusaidia Mwalimu awe salama , pamoja na Kawawa ...baada ya pale wenzake walianza kumuona tishio haswa KAWAWA wakaanza kupeleka maneno ya uchonganishi kwa NYERERE.....
Andrew Nyerere yuko hapa atuambie maana hizi zilikuwa family friends
 
Imagine walituma watu wakamuuwa Mwanaye just to frustrate him
 
Alikuwa anamuamini Saana ...
 
Inasisimua

Sent from my TECNO WX3 using JamiiForums mobile app
 
We jamaa sio mtu mzuri yaani unawakumbushia wenzako mambo ya nyuma
 
Nyerere alikuwa anakopi vitu tokea USSR ama uchina analeta hapa nyumbani.hata alama ya nyundo ,jembe aama mundo pia mwenge amekopi tokea USSR.aliyekaa Russia ataleta shuhuda nzuri nadhani. Namie Nina uhakika mana nimeishi huko miaka miwili so Nina uhakika nachoongea
 
Kuna muda unaweza kushiriki katka maamuzi fulan ila utakapokaa na kutafakari kwa kina unaweza ona kabisa kuwa ulikosea. Kubadili mwelekeo juu ya kutafuta usahihi wa kile ulichokiazimia kimakosa awali ndo ukomavu wa fikra. Kushiriki katka kuandaa azimio la Arusha na kisha kuja kulipinga sioni kama ni shida ikiwa aliliona kwa jicho la tatu kuwa n janga la nchi kwa siku za usoni. Haya maisha yanahitaji mnyumbuliko wa kiwakati, hivyo kuna haja ya kurudufu maamuzi na misimamo yetu kila mara kama inaendana na wakati na mivumo ya pepo za ulimwengu. Hivyo naendelea kusisitiza kuwa Kambona alikuwa Big Brain.

Kuhusu umaskini/na ufukara nmeungumza kwa istilah pana ya kinchi na sio kwa kupoint vitu vichache kama ulivyofanya mwanabodi. Tanzania ina rasilimali nyingi ila bado ni Nchi ya Taifa Fukara. Ni ukweli ulio dhahir kuwa asilimia kubwa ya watu wa nchi hii n mafukara. Serikali ina bajet yenye nakisi kubwa. Nchi ina reserve ndogo ya Dhahabu safi katka mabenk ya kiulimwengu, fedha yetu n yenye thamani ndogo, urari wetu kibiashara n hasi (Export vs Import). Hizi zote n miongon mwa alama za nchi maskini. Hayo maghorofa na miundombinu unayosema ww, yamemuondolea shida na dhiki yule mkulima wabjembe la mkono mwenye kutegemea hisan ya hali ya hewa?

Kawawa na Nyerere wote walikuwa failures katka maamuzi mengi yaliyohusu mustakabali wa nchi. Jaribu kutafuta ngano za Sir George Kahama kuhusu usuhuba wake yeye na Mwalimu Nyerere husuan yey Kahama akiwa anasoma England, anasema kabisa kuwa Nyerere alikuwa ana damu ya kichifu hivyo hakuwa na uvumilivu wa kupingwa juu ya kile alichokiamin licha ya kutajwa kuwa na uwezo mkubwa wa kusikiliza hoja. Wengi wa wafuasi wake walikuwa n wale wa "Zidumu Fikra za Mwenyekit".

Kitendo cha Mkapa kutogusia battle ya Nyerere vs Kambona kweny kitabu chake inaweza kutupa tafsir ya ukweli unaofichwa ambao kama angeamua kuuweka wazi basi huenda baadhi ya watu wangehis kuwa Mwalimu kafanyiwa dharau na Hayati Ben Mkapa.

Tusome na kudadisi yaliyo nyuma ya pazia yasiosemwa wala kuandikwa kuhusu Mwalimu Nyerere.
 
Hauwezi kuwa na boga ambalo ua lake si la boga! Kambona na Kawawa walikuwa ni ndugu, wajomba. Kutokana na udugu huu serikali ililazimika kumkubali kimyakimya kuwa mtanzania badala ya mmalawi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…