Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona?

Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona?

Ujamaa umeyagharimu mataifa mengi sana duniani, ujamaa ni mfumo wa hovyo sana.
Mzee Kichuguu asante for brief,

Unajua huwa sometimes na regret kumezeshwa zile nyimbo za nursery ...Kambona ha ha! wivu ulimshinda shauri ya mapesaaa! But kambona in some extent naona alikua sahihi kupinga mpango wa azimio la Arusha.Hata Nyerere mwenyewe nadhani alikuja kugundua kosa.

ONA LEO MAMBO YA UJAMAA YALIVYO KIMYA KIMYA
 
Ujamaa ni mojawapo ya scam kubwa kuwahi kutokea duniani.
Mkuu Nyani,

Heshima mbele, I like kila ulichosema so far kwenye hii topic, now ngoja tujairbu kuchambua kidogo:-

1. After the mutiny, differences between Kambona and Nyerere began to appear. Nyerere wanted to introduce a one party system into Tanzania to strengthen state security. Kambona argued against the move claiming that it would inhibit peoples freedom and progress towards democracy. However, Kambona was defeated in parliament. He refused to sign the bill.

I mean right here, ndipo mambo yetu yalipoanza kwenda mrama as a nation, na ndio ninayoyasema kila siku, kumbuka kuwa to this point tulikuwa on the right track, kuaniza uchumi, uongozi, mpaka siasa, now look at the turn of events ambazo eventually, ndio zilizotufikisha tulipo!

2. In 1967 after a trip to China in 1965, Nyerere impressed with Maos style of communism, wanted to adopt the same system under the guise of Ujamaa. The main doctrine behind Ujamaa was the relocation of peasants into village communes and the nationalization of all industries and property. Kambona did not agree with the policies, arguing that they would rather increase poverty and state control over the people. He resigned from the Government and the party and later with his family fled to neighbouring Kenya and then UK were he was granted political asylum.

Tizama kiongozi aliyekuwa na uwezo wa kuona mbali, exactly his argument then ndio hasa yalipolalia matatizo yetu, kumbe walikuwepo wenye akili ya kuona mbele, I mean this is very interesting story, pumba na mchele uko clear upande gani?

3. Immediately thereafter, Kambonas properties were confiscated. His two brothers Mattiya and Ottini Kambona were detained without trial and put in prison for over ten years. Other family members were harassed and detained. Some were falsely accused of plotting to overthrow the Tanzanian Government and were tried and imprisoned by the Government.

Wooow! Yaaani kweli haya mambo yalifanyika bongo under Mwalimu?

4. Most famous of these were Bibi Titi who fought alongside Nyerere in the independence movement and was head of the womans wing and also Michael Kamaliza, the former trade unionist and TANU member and government Minister. Other family members included Gray Mattaka, John and Elia Chipaka and Prisca Chiombola. Kambona was also accused of being the ring leader of the plotters while in London and was tried in absentia. The accused finally appealed to the East African High Court and were acquitted. Though they were later rounded up by the Tanzanian government and thrown into jail again.

5. Kambona was also accused of stealing millions of public funds,

6. Kambona challenged the Tanzanian government to request the Kenyan authorities to substantiate the allegations which they never did.

7. In London Kambona led a tough life in exile under considerable financial constraints. However in 1982, his two brothers Mattiya and Otini Kambona were eventually released from detention after the intervention of New Zealand Prime Minister Robert Muldoon.


8. On returning to Tanzania Kambona found that the progress towards democracy was disappointingly slow.


9. His eldest son Mosi Kambona was murdered in London in unexplained circumstances.

Sasa wakuu wangu bado kuna maswali kwamba kwa nini as a nation tupo hapa tulipo? Maana kwanga naona majibu yako clear hapa, kama kuna story ya upande wa pili tungekuwa tumeshaisikia, na pia tuliambiwa Kambona amekimbia Azimio La Arusha, lakini hapa ukweli unajionyesha wazi, au labda tusubiri na upande wa pili ulete yao pia, otherwise I am convinced kuwa huu ndio ukweli wenyewe wa kwa nini taifa letu limekwama!

Ahsante Mtoa Mada, yaanai you made my day!
 
Unajua legacy moja ya Nyerere ambayo inaendelea kutugharimu na ambayo inajionyesha hata katika mada hii ni ukweli kwamba Nyerere alifanya watu wasifikiri kwa kuamini kwamba Mwalimu anafikiri kwa niaba yetu sote.

So, it was not expected during Nyerere era and in CCM in general (even today) to think independently. Why you, wakati Nyerere and CCM were there to think for you. Wewe ni kusubiri tu watakachosema Nyerere na chama halafu wewe unafuata kama askari. Hii inaendelelea hadi leo japokuwa imeanza kubadilika. Ndio maana watu karibu 2000 wanaenda kwenye uchaguzi kwenda kuidhinisha chaguo la mwenyekiti. Ndio maana hadi leo tunaendelea kuwa na nchi ya chama kimoja inayofanya uchaguzi wa mfumo wa vyama vingi. Kwa sababu katika kupiga kura inabidi tumsikilize kwanza kiongozi anasema nini, akisema nataka mafiga matatu, tunaitikia hewala, yeye ndiye mwenye monopoly ya fikra, ndiye anayejua nani anafaa kuwa kiongozi, sisi wananchi ni kufuata tu yale anayosema, hatuwezi kufikiri.

Ndio maana basi inakuwa vigumu kuona mazuri ya Kambona simply because tulikwishaambiwa siku nyingi sana kwamba Kambona alikuwa mbaya na msaliti kwa nchi yake, sio mzalendo. Wewe ni nani leo hata ubadilishe hiyo, wewe unaweza kufikiri kuliko Nyerere na CCM? Thubutu! This is the dirtiest legacy that Nyerere left with us and it gonna cost us dearly for a very long time!
Prof. Karibu tena Jamvini kwa mijadala ya nguvu.
 
Unajua legacy moja ya Nyerere ambayo inaendelea kutugharimu na ambayo inajionyesha hata katika mada hii ni ukweli kwamba Nyerere alifanya watu wasifikiri kwa kuamini kwamba Mwalimu anafikiri kwa niaba yetu sote.

So, it was not expected during Nyerere era and in CCM in general (even today) to think independently. Why you, wakati Nyerere and CCM were there to think for you. Wewe ni kusubiri tu watakachosema Nyerere na chama halafu wewe unafuata kama askari. Hii inaendelelea hadi leo japokuwa imeanza kubadilika. Ndio maana watu karibu 2000 wanaenda kwenye uchaguzi kwenda kuidhinisha chaguo la mwenyekiti. Ndio maana hadi leo tunaendelea kuwa na nchi ya chama kimoja inayofanya uchaguzi wa mfumo wa vyama vingi. Kwa sababu katika kupiga kura inabidi tumsikilize kwanza kiongozi anasema nini, akisema nataka mafiga matatu, tunaitikia hewala, yeye ndiye mwenye monopoly ya fikra, ndiye anayejua nani anafaa kuwa kiongozi, sisi wananchi ni kufuata tu yale anayosema, hatuwezi kufikiri.

Ndio maana basi inakuwa vigumu kuona mazuri ya Kambona simply because tulikwishaambiwa siku nyingi sana kwamba Kambona alikuwa mbaya na msaliti kwa nchi yake, sio mzalendo. Wewe ni nani leo hata ubadilishe hiyo, wewe unaweza kufikiri kuliko Nyerere na CCM? Thubutu! This is the dirtiest legacy that Nyerere left with us and it gonna cost us dearly for a very long time!
Le Profeseri hii hoja hukupata like hata moja.
Anyways unaweza sema Tena hivi kwasasa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee Jasusi,

Ninakuaminia kwenye hizi kind of ishus, ninaamini kabisa kuwa unayosema ndio ukweli wenyewe kuhsu Kambona, ingawa mpaka leo sielewi kwa nini Mwalimu, alimruhusu huyu Mnyasa kubanda chati, over wabongo, bado sijaelewa!

Maana ukilifuatialia kwa makini ishu lake, utaona jamaa hakuwa na uchungu kabisaa na bongo, halafu vipi kuhusu mtoto wake mmoja anayesadikiwa kuwa ni shoga, aliyepigwa risasi huko majuu, kuna ka-"tetesi" kuwa someone kutoka kunyumba alihusika ili kumkomoa Kambona ni kweli?
Watu wa mpakani mwa nchi husingiziwa Sana kuwa sio Watanzania....inauma Sana hizi mentality

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Prof. Karibu tena Jamvini kwa mijadala ya nguvu.
Ameshaonja utamu wa CCM usidhani atajadili ishu against CCM. Anajipanga kwa 2025 ubunge wa mezani waliopewa itakuwa ngumu sana lazima ajipange na asiwaseme masponsa wake CCM.
 
Paskali/Hamidu
Nakuomba uangalie haya maelezo hapa chini ili upate picha kamili
ya Chuo Cha Kivukoni na uwezo wake wa kuandika historia ya nchi
hii:

LW013K1LkQSY-ksQJMIfrLluBCK19y57yhYU-j_BY8cl-cwkVVtJ0aGvjZjYwlKPlwcWsMzMYgiGqjCjm8fQL_F3DbDFXcb0H88lMHZMEvypsbsmC_dZg48dxd2lCWkmhzzBziAJ4dt1eD8ykoC2Z905bagButKmxHxS1d-VfYiPinqFPrVM3nZ7OOFfbW7nqQ-eG6CSK7qoYlc7WcYHDQW35kOANKQk0jmvX8Kn-FsPioIpZqTiCckBELGHw9gszEZo7DnSZpBt5vNTrYMheFZgtY0eowMYpOA7XiyUxUJyDW4X0kzp-QUP7z27tE_iLPAB-3nyjIt3HsuHcDyk0CCO_70lE5ayaUYWyv8ddi2NLA_ff33LEWcGI2Qhl3-iQgT8iimVy5VKsMmYcij0lk--el0WI48G8CrJeS45zE34C6VvC-fTJ1ibu_Bj_s4IOFuEkiBatncaeGMCvAVFDiXKngmnrna-4V2V1v7Z5rEKtqYOR54LhMwSqII-_VZUpZA2nxOJvm-CMORXaaPoGr0PdGZg-cO5qbTNxMXAqigwQaNbXVSqpC4f9M7CP1t-6XAI=w407-h615-no

Kwa mara ya kwanza Tanzania ilishuhudia kuandikwa kwa historia ya mmoja wa viongozi wakuu wake kupitia kitabu “Simba wa Vita Katika Historia ya Tanzania Rashidi Mfaume Kawawa” kilichoandikwa na Dk. John M. J. Magotti. Sidhani kama katika historia ya Tanzania kuna kumbukumbu ya kuandikwa kwa kitabu kinachohusu maisha ya kingozi yoyote achilia mbali kufanyika kwa sherehe ya kukizindua kitabu hicho Ikulu ikiongozwa na rais mwenyewe. Kwa hakika sherehe ilifana sana na tukakisubiri kwa hamu kitabu madukani ili tupate kunufaika na kumbukumbu za Mzee Kawawa.

Msomaji anaweza kukisoma kitabu chote chenye kurasa 127 kwa muda wa saa moja akawa kakimaliza chote na atakapokiweka chini akawa hakubakia na chochote cha maana katika fikra yake. Kwa nini iwe msomaji asibaki na kumbukumbu yoyote ya kiongozi mkubwa kama Mzee Kawawa mtu aliyeshuhudia kwa macho yake mwenyewe harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika na si hivyo tu yeye mwenyewe ni mmoja wa wale waliopigania uhuru wa Tanganyika na kushika nyadhifa kubwa za uongozi chini ya Mwalimu Julius Nyerere. Kwa kawaida vitabu vya maisha ya viongozi hasa wapigania uhuru huwa vina mambo mengi sana ambayo kwa muda mrefu huwa siri, hayafahamiki hadi hapo kitabu kitakapoandikwa ama kwa mkono wake kiongozi mwenyewe au kuandikwa na muandishi. Mifano ipo mingi. Kitabu kama “Mahatma Gandhi” klichoandikwa na Robert Payne au “Long Walk to Freedom” alichoandika Nelson Mandela mwenyewe au “Seeds of Freedom” alichoandika Bildad Kaggia hakika unapomaliza kusoma vitabu hivi lazima urudi nyuma kufungua kurasa hapa na pale kuzisoma upya zile sehemu zinasosisimua.

Huwezi kupata haya katika kitabu cha Mzee Kawawa. Huwezi kuyapata haya kwa kuwa mwandishi hakuandika kitu. Hakuandika kitu si kama Mzee Kawawa hana historia ya kusisimua na kuwa hana mengi ambayo wengi hawayajui katika maisha yake, nadhani mwandishi hakuwezakuja na jipya labda kwa sababu hakufanya utafiti wa kutosha kuweza kuandika kitabu kinachomuhusu simba wa vita aneunguruma. Kuna msemo wa Kiswahili usemao “Aungurumapo simba mcheza ni nani?” Kwa hakika simba wa vita hakuunguruma kabisa katika kitabu hiki. Sijui lawama zielekezwe wapi.

Mimi simjui Mzee Rashidi Kawawa kwa kiwango cha kusema naweza kunyanyua kalamu na kufanya pitio la kitabu kilichoandikwa kuhusu yeye. Nathubutu kuandika kuhusu kitabu chake kutokana na kumjua kwangu mimi nikiwa kama mwandishi na mtafiti ambae katika kutafiti kwangu nimekutana na jina la Mzee Kawawa hapa na pale katika nyaraka zilizo katika hifadhi ya ukoo wa akina Sykes. Nitatumia uzoefu wangu huu kueleza yale niliyoyaona katika nyaraka hizi na ninayojua kuhusu Mzee Kawawa na kufanya tathmini kwa yale niliyoyasoma katika kitabu cha Magotti.

Miaka kama ishirini iliyopita nikiwa kijana mdogo nilipata hamu ya kuandika historia ya kudai uhuru wa Tanganyika. Sikuona mtu wa kumuendea isipokuwa Ally Sykes. Nilipomueleza kuwa nia yangu ni kuandika kitabu kuhusu marehemu kaka yake Abdulwahid Sykes (1924- 1968) Ally Sykes alinambia kuwa atanipa nyaraka zake zote nizipitie kisha ndiyo nakaenae chini kwa mahojiano ya ana kwa ana. Katika nyaraka alizonikabidhi ndani yake nilikuta barua ya mkono aliyoandika Rashid Kawawa mwaka 1952 kutoka Bukoba akimletea Ally Sykes aliekuwa Dar es Salaam. Barua hii ya Mzee Kawawa kwa Ally Sykes ilikuwa ikimfahamisha Ally Sykes hali ya siasa Kanda ya Ziwa. Hii barua hadi leo ipo katika nyaraka za akina Sykes. Nilipokaa na Ally Sykes kutaka maelezo ya barua ile aliyoandikiwa na Kawawa, Ally Sykes alinipa kisa hiki:

Mwaka 1951 nilichaguliwa kuwa katibu mkuu wa Tanganyika African Government Servants Association (TAGSA). Chama hiki kiliundwa mwaka wa 1927 kwa lengo la kuendeleza maelewano mazuri baina ya serikali ya Malkia na sisi watumishi Waafrika. Rashid Kawawa alikuwa mwana kamati. Mimi nilichaguliwa pamoja na Thomas Marealle kama rais wa TAGSA. Katiba ya TAGSA iliamuru uchaguzi wa kila mwaka, na mimin nilirudishwa madarakani kama katibu mara nne hadi Oktoba, 1954 nilipojiuzulu baada ya kuhamishwa kwenda Korogwe kamaadhabu kwa kuwa miongoni mwa wale wanachama 17 waliounda TANU. Watu kadhaa walishika urais. Stephen Mhando na Dr Wilbard Mwanjisi wote hao waliwahi kuchaguliwa kuwa marais wa TAGSA. Miongoni mwa wanachama watendaji wa TAGSA walikuwa Dr Michael Lugazia na Rashid Kawawa ambao alichaguliwa kuwa katibu baada ya mimi kujiuzulu. Kupitia TAGSA, Kawawa alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Tanganyika Federation of Labour (TFL).

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa ulipokuja kuzuru Tanganyika Agosti, 1951 kwa mara ya tatu, vyama vyote viwili, TAA na TAGSA, viliwakilisha malalamiko kwa ujumbe huo. TAGSA iliwakilisha malalamiko yake kuhusu ubaguzi katika utumishi serikalini kwa mujibu wa kupanga mishahara kufuatana na rangi ya ngozi. Mshahara wa Mwafrika ulikuwa wa chini zaidi kuliko ule aliokuwa akipokea Mzungu au Muasia kwa kazi hiyo hiyo. Kwa mfano Mwandishi wa hati mkato Mzungu alikuwa akipata mshahara mkubwa kuliko Mwafrika aliyekuwa na shahada au digrii kutoka chuo Kikuu cha Makerere. TAGSA vilevile tulilalamika kuhusu kuajiri makarani wa kutoka India na hali walikuwepo Waafrika kutoka Afrika ya Mashariki na Nyasaland ambao wangeweza kujaza nafasi hizo kwa urahisi.

Vyama vyetu hivi viwili TAA na TAGSA viliwakilisha malalamiko haya tukifahamu fika kwamba Uingereza ilikuwa ikiitawala Tanganyikachini ya vifungu nambari 76 na 77 vya Umoja wa Mataifa ambavyo viliwekwa ili kuendeleza maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ya nchi zilizokuwa chini ya udhamini. Kama mdhamini Uingereza ilitakiwa kuhimiza na kuheshimu haki za binadamu na uhuru wa kwa wote bila kubagua kwa misingi yajinsia, lugha au dini. Lakini Uingereza ilikuwa ikipuuza vifungu hivi bila aibu. TAGSA tuliwakilisha malalamiko haya ili Umoja wa Mataifa ujue matatizo halisi ya ukoloni nchini Tanganyika.

Mimi nikiwa katibu wa TAGSA nilifuatilia serikalini masuala yaliyoainishwa ndani ya malalamiko yetu. Suala lililokuwa likituhangaisha sanawakati ule ilikuwa uajiri wa Wahindi kutoka India, jambo ambalo niliieleza serikali halikuwa na faida, maadam kulikuwako na Waafrika ndani ya nchi ambao wangeweza kujaza nafasi zile. Jambo hili lilikuwa likisababisha manugíuniko makubwa miongoni mwa Waafrika. Hakuna majibu maridhawa yaliyopatikana kutoka kwa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa. Barua tulizoandika serikalini juu ya masuala hayo zilipuzwa na Chief Secretary, Bruce Hutt. Katika kufuatilia malalamiko haya, Niliandika barua moja kali sana na kwa mara ya kwanza bila kutafuna maneno niliuliza uhalali wa Waingereza kututawala Waafrika wa Tanganyika. Nillimwambia Katibu Mkuu kuwa kwa kuwa serikali imeshindwa kupata ufumbuzi kwa matatizo ya Waafrika, Uingereza lazima ijitoe Tanganyikana Umoja wa Mataifa utawale Tanganyika. Barua hiyo ilimkasirisha Katibu Mkuu na siku chache baadaye nilipokea barua kutoka serikalini iliyokuwa imejaa vitisho, dharau, stihizai na makemeo. Nikajibiwa kuwa hakuwa na suala la Umoja wa Mataifa kutekeleza utawala wa moja kwa moja Tanganyika.

Dkt Mwanjisi alikuwa amegusa suala nyeti sanakwa kuzungumzia matatizo ya ubaguzi wa rangi uliokuwa ukitukabili Waafrika wa . Kawawa, kama mjumbe wa kamati, akaniandikia barua akanitahadharisha nisichapishe ile hotuba ya Dkt Mwanjisi katika jarida la TAGSA bila idhini ya kamati ya utendaji. Kufuatia majibishano haya kati ya TAGSA na serikali, Dkt Mwanjisi kama alivyofanyiwa Dk Kyaruzi kabla yake, akahamishwa kutoka hospitali ya Sewa Haji mjini Dar es Salaamhadi Kingolwira Prison Hospitalkaribu na Morogoro. Kawawa na yeye akapewa uhamisho kwenda Bukoba na mimi nikapewa uhamisho kwenda Mtwara. Dk Mwanjisi na Kawawa walikubali uhamisho wao na wakaondoka Dar es Salaam. Mimi nilikataa uhamisho na nikabakia Dar es Salaam kupinga uhamisho wangu.

Alipokuwa Bukoba ndipo Kawawa akamwandikia Ally Sykes barua ile ya mwaka 1952 akimweleza hali ya siasa kamaalivyoikuta Kanda ya Ziwa. Huyu ndiye Kawawa niliyemjua mimi kupitia nyaraka na mahojiano na Ally Sykes. Kwa kweli inasikitisha kuwa Dk Magotti hakupata fursa ya kuziangalia nyaraka hizi muhimu sana katika siyo historia ya Kawawa bali katika historia ya kuundwa kwa TANU na kudai uhuru wa Tanganyika. Endapo angepata nafasi ya kuziona hizi nyaraka zingempelekea katika kuwajua wazalendo wengine waliotajwa mle ndani kama Dk. Kyaruzi, Dk. Wilbard Mwanjisi ambao Kawawa alikuwanao katika harakati za TAGSA. Katika majina hayo angeweza kudodosa mengi kutoka kwa Mzee Kawawa na hivyo kuandika yale ambayo hayafahamiki kwa wengi. Hii imgekifanya kitabu kiwe cha maana.

Mathalan Kawawa angeeleza mtafaruku kati ya Mwalimu Nyerere na Dk. Mwanjisi nini chanzo chake na nini ikajakuwa matokeo yake. Halikadhalika angempa fursa Mzee Kawawa kumuhadithia mchango wa Dk. Michael Lugazia katika kuasisi kwa TANU hasa kipindi kile cha 1953 wakati TAA ilipokuwa inatayarisha rasimu ya katiba ya TANU. Kwa ufupi ni kuwa Dk Lugazi alikuwa akijaribu kuamsha ari ya TAA Bukoba ari iliyokufa kutokana na kufungwa kwa kiongozi wa TAA Bukoba Ali Migeyo. Kisa cha Ali Migeyo ni moja ya visa vinavyosikitisha sana katika historia ya Tanganyika kwani aliwekwa kizuizini na Mwalimu Nyerere kama alivyofungwa na Waingereza. Haiwezekani kuwa Kawawa asiwe na habari na kile kilichopelekea mpigania uhuru hodari kama Ali Migeyo aishie jela tena wakati nchi ikiwa huru. Migeyo alifungwa na wakoloni kwa kuwahamasisha Watanganyika kudai uhuru labda Mzee Kawawa angeulizwa angeeleza ni nini kilitokea wakaamua kumfunga Migeyo kama walivyomfunga Waingereza.

Kitabu kimegusia kazi alofanya Kawawa kama mtumishi wa serikali ya kikoloni katika kambi za raia wa Kenyawalioshukukiwa kuwa ni Mau Mau. Katika hawa wafungwa walikuwawepo wananchama wa TANU ingawa hawa walikuwa Wakenya. Maarufu katika hawa alikuwa Dome Okochi Budohi (ambae kadi yake ya TANU ilikuwa na 6) na Patrick Aoko. Budohi alicheza senema pamoja na Kawawa iliyoitwa “Wageni Wema.” Kawawa na Budohi walikuwa wakifahamiana vizuri sana kwa sababu wote walikuwa wasanii. Budohi alikuwa mmojawapo katika bendi ya vijana wa mjini iliyojulikana kama Skylarks. Bendi hii baadaye ilibadilisha jina na kuitwa Blackbirds. Matangazo ya radio yalipoanza Tanganyika, Blackbirds midundo ya Blackbirds ilikuwa haikosekani kusikika radioni katika Sauti ya Dar es Salaam. Kawawa kama walivyo vijama wote wa Dar es Salaam wa wakati ule alikuwa mmmoja wa wapenzi wa bendi hii na alikuwa hakosekani Ukumbi wa Arnatouglo bendi hii ikitumbuiza katika ile miaka ya 1950. Ilikuwa katika ule upigaji muziki wa Budohi ndipo alipoungana na Kawawa katika kutengenezwa kwa senama hiyo ya “Wageni Wema” ambayo mwandishi kaitaja lakini aliishia hapo tu.

Budohi na Aoko ni kati ya wafungwa wa Mau Mau waliokuwa Handeni ambako Kawawa alikuwa na jukumu la kuwaangalia. Budohi ndiyo alikuwa mtu wa kati baina ya TAA na KAU na kuanzia hali ya hatari ilipotangazwa Kenya mwaka 1952 Budohi na Aoko wakawa katika jicho kali la makachero. Makachero hawa Waafrika wanafahamika na wengine walikuja kufanya kazi hiyohiyo katika Tanganyikahuru. Hiki ndicho kipindi ambacho Kaimu Rais wa TAA na Katibu wa TAA Abdulwahid Sykes alipokutana na Kenyatta Nairobi. Wakati Wakenya hawa wanafungwa Tanganyika, viongozi wa KAU akina Bildad Kaggia, Jomo Kenyatta, Kun’gu Karumba, Achieng Oneko, Paul Ngei na Fred Kubai walikuwa wamekamatwa Kenya. Kawawa ni mmoja kati ya viongozi hawa na ingependeza sana kama kupitia kwake tungeelezwa jinsi KAU na TAA ilivyokuwa ikishirikiana kwani haiwezekani kuwa Budohi na Kawawa uswahiba wao ukaishia kwenye kucheza senema tu.

Wanaharakati wote walishtushwa na kutiwa mbaroni kwa Budohi na Aoko. Haiwezekani kuwa iwe Mzee Kawawa kasahau matukio haya muhimu. Budohi na Aoko walikuwa wamefungwa minyororo walipokuwa katika selo pale Kituo cha Kati cha Polisi kwa sasa jumba hiloliko kituo cha mabasi kinachojulikana kama“station.” Waliwekwa pale kwa miezi sita muda wote wakiwa na minyororo miguuni. Waliwekwa pale kwa miezi sita wakihojiwa kabla hawajapelekwa Handeni walipomkuta Kawawa. Hivi ndivyo vitu ambavyo kwa hakika vingeongeza ladha ya kitabu cha Mzee Kawawa endapo mwandishi angechukua muda kutafiti na kuzungumza na watu waliokuwa katika harakati wakati ule ambao bado wa hai kama Ally Sykes na mdogo wake Balozi Abbas Sykes na wengine wengi ambao walikuwepo wakati ule kama Mzee Chipaka.

Katika migomo ya wakati wa kudai uhuru hakuna mgomo uliofanikiwa na kuvuta hisia za wananchi kama mgomo wa reli wa mwaka 1960 uliodumu kwa siku 62. Ukiachia kutajwa tu kama sehemu ya historia undani wake na jinsi mipango yake ilivyokwenda na nafasi ya viongozi wa Tanganyika Railway African Union (TRAU) walivyopata misaada kutoka nchi za Mashariki hivi havijawekwa wazi. Si treni, meli wala mabasi ya railway yaliyotembea kwa mieizi mitatu. Mipango ya mgomo huu ilifanyika Tabora ambako ndiko palikuwa na karakana kuu ya reli na hapo ndipo palipokuwa makao makuu ya viongozi wa TRAU, Salum Abdallah mwenyekiti na Kassanga Tumbo katibu. Kawawa ana mengi katika kadhia hii kwa kuwa yeye wakati ule ndiye alikuwa Katibu Mkuu wa TFL. Inasemekana mgomo huu miezi michache kabla Tanganyika haijapata uhuru ndiyo ilikuwa kama zinduo kwa Mwalimu Nyerere kutambua kuwa hakuwa peke yake na sauti kwa wananchi. Walikuwapo viongozi wengine pembeni yake ambao nao wakipiga wananchi wanacheza. Ilimdhihirikia kuwa huko mbeleni wanakokwenda ipo siku atapambana na viongozi hawa. Hivyo ndivyo ilivyotokea.

Inasemekana Mwalimu Nyerere akimtumia Kawawa alianza mipango kabambe ya kujitayarisha hilo lisitokee. Hii ilikuwa nukta muhimu sanakwani haukupita muda baada ya uhuru kupatikana mwaka wa 1961 viongozi hawa wa vyama vya wafanyakazi wakajikuta wamewekwa kizuizini. Wasomaji wangependa kujua Kawawa alijihisi vipi wakati viongozi wenzake wa vyama vya wafanyakazi aliofanya nao kazi wakati wa kudai uhuru wakishirikiana na TANU kama Victor Mkello, Paul Pamba, Abdallah Mwamba, Hassan Khupe, Salum Abdallah na wengine wengi walipokamatwa mwaka wa 1964 na kuwekwa kizuizini kwa amri ya Mwalimu Nyerere. Maelezo ya Mzee Kawawa katika mambo haya yangetia mwanga katika yale mengi yasiyofahamika katika historia ya Tanzania.

Waislam wangependa sana kujua hisia za Kawawa kama muumini alihisi vipi wakati makachero walipomvamia mzalendo aliyepigania uhuru wa Tanganyika Mufti wa TanganyikaSheikh Hassan bin Amir usiku wa manane na kumrudisha Zanzibar na kuwekewa masharti kuwa hana ruhusa kurejea Tanzania Bara. Nilitegemea kusoma sakata zima la kukamatwa kwa Sheikh Hassan bin Amir na kuvunjwa kwa East African Muslim Welfare Society (EAMWS) jumuia ya Waislam iliyokuwa ikipanga kujenga Chuo Kikuu Dar es Salaam.

Nilitegemea halikadhalika kusoma mchango wa Mzee Kawawa katika kuunda Bakwata. Mengi yamesemwa kuhusu hujuma hii kwa Waislam moja wapo ni kuwa EAMWS ilivunjwa kwa shinikizo la Kanisa Katoliki likimtumia Mwalimu Nyerere. Hili si jambo la siri tena tafiti mbalimbali zimefanywa na vitabu kuandikwa na waandishi kutoka nje ya Tanzania kuhusu tatizo hili la kujitokeza udini mapema baada ya uhuru kupatikana. Kwa kuwa Kawawa alikuwa pamoja na Mwalimu Nyerere na alishiriki katika kuunda Bakwata wananchi hasa Waislam wangenufaika kusoma hisia zake wakati maamuzi hayo yanapitishwa na serikali. Kwa hakika kuna maamuzi mengi sanaambayo Kawawa alishiriki yaliwaumiza sanaWaislam katika juhudi zao za kujitafutia elimu. Waislam wangependa sana kujua ni kipi kilikuwa kinamsukuma kufanya vile.

Kwa yeyote atakaepata bahati ya kusoma kitabu cha maisha ya Mzee Kawawa ni wazi hatakuta jipya ambalo hakuwa akilijua kabla. Kwa ajili hii basi mlango bado uko wazi kwa watafiti wengine kuandika kitabu kuhusu Rashidi Mfaume Kawawa kwani maisha ya Mzee Kawawa bado hayajaandikwa. Hata hivyo tumpongeze mwandishi kwa kazi hii kwani ni baada ya yeye kutuandikia kitabu ndipo nasi tumepata nguvu ya kunyanyua kalamu zetu na kusema.

Mohamed Said
3rd January 2010

Ukipenda unaweza ukaingia hapa:Mohamed Said: TUNAMKUMBUKA MZEE RASHID MFAUME KAWAWA ALIYETUTOKA TAREHE 31 DESEMBA 2009
Asante!.
 
Katika hili namuona magufuli,anapenda sifa za kisiasa ambazo zinaitia nchi kwenye hasara kubwa kiuchumi na kuturudisha nyuma kimaendeleo..angalia anavyomess na uchumi na wawekezaji.Halaf anajiona yeye ni nation hero!!Hero my foot!

Definetely, by Mwalimu ambaye he never wanted any to share spotlight with him, katika kipindi chake chote cha utawala hakupenda kuwa na competition, ndio maana alizungukwa na all the mediocres, ambao sasa wanatupeleka pabaya, Mao alizungukwa na kuwakubali strong competitors, nina kitabu kinaitwa " The Privete Life Of Chairman Mao" kilichoandikwa na daktari wake private wa zamani, anaitwa Dr. Li Zhisui, kimechapishwa na Random House naomba mkuu wangu MMJ, kitafute uyaone mwenyewe live jinsi Mao alivyokuwa akipigwa mawe na viongozi wenziwe kila alipojaribu kuleta nonesense ideas, sasa itashangaa kwa nini China inayoyoma tu mbele na sisi kina Mkapa ndio wameishia kuwa mabepari sisi tunaimba nyimbo za kumsifu Mwalimu, na Azimio La Arusha tu!

3. by jamaa aliyekuwa hataki Watanzania waendelee

Mwalimu, alipenda sana ujiko wa siasa, alikuwa willing hata ku-sacrifice taifa letu kwa kujali ujiko wake binafsi, alitupelekea kwenye vita vya Uganda, just kuongezea tu ujiko wake kisiasa, alitaka wabongo tuendelee lakini hakuwa an vision ya how to do it na hakutaka kusikiliza wengine au the brain kama kina Professor Rweyemamu, matokeo yake ni here we are completely lost out!
[/QUOTE]Walimu tabia zao ndiyo hizo mpaka sasa.Kujiona wao ndiyo WANAJUA kila kitu na wengine wote ni wanafunzi wao.
 
Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Firrauni.Kisa kilikuwa kama ifuatavyo Bwana mmoja alikuwa na mkewe ambaye mjamzito wa kuweza kujifungua wakati wowote.Sasa siku moja yule mkewe akasikia harufu ya mishikaki nyumba ya jirani,hivyo akamtuma kijana wake mtogo na pesa ili aende kuomba kununua baadhi ya mishikaki.Kwa bahati mbaya wale wenye mishikaki wakamjibu yule kijana aliyetumwa kuwa mishikaki ilikuwa haiuzwi,ni ya chakula cha nyumbani.

Kijana akapeleka jibu kwa mama yake na haikupita muda yule mama mimba yake ikaharibika.Aliporudi Bwana wake toka kazini akamueleza kisa kizima cha mishikaki mpaka mimba kuharibika.Na kwa akili ya yule Bwana ile mimba iliharibika kwa kukosa mishikaki.Hivyo basi alikwenda kudai fidia kwa wale wenye mishikaki kwakuwa mimba ya mkewe imeharibika.Na wale wenye mishikaki wakakataa kulipa fidia.

Yule Bwana akaamua kwenda kwa Mussa na akamueleza kisa kizima na Mussa akamjibu kuwa mimba haiwezi kuharibika kwa kukosa mishikaki bali ilikuwa ni Kudrah ya Mungu.Hakuridhika na jibu hivyo akaamua kwenda kwa Pharaoh (Firauni),na akamweleza kisa kizima na hukumu ya Firauni ikawa kuwa yule bwana mwenye mishikaki anatakiwa afanye tendo la ndoa na mke ambaye mimba yake imeharibika mpaka atakapopata mimba nyingine na hiyo ndiyo fidia.

Ukweli ni kwamba pamoja na sifa tunazo mpa Nyerere kama Baba wa Taifa lakini bado yako mambo mengi ambayo yamejificha na hii inatokana na wakati ule hakukuwa na uhuru wa vyombo vya habari hivyo kila alichosema nyerere kilikuwa ni ukweli natulikuwa atuwezi kumkanusha.Wako watu kama akina Kambona ambao waliona mbali lakini kwa rigidity yake mwalimu alikana mawazo yao.

sio yote yanayosemwa juu ya Idd Amini ni sahihi,mengine yako EXAGGERATED.Nilipata kuona mkanda mmoja wa video wamwonyesha Amin akila nyama za watu lakini ile ni mikanda ambayo imetengenezwa na watu kwa maslahi yao. Tukumbuke pia ugomvi kati ya Amin na Nyerere ndio umefanya kuenea kwa hiyo kasumba na uongo.Yuko askari mmoja alipata kusema kuwa Tanzania ndio walikwenda vunja daraja la mto Kagera kwa justification ya vita kisa rafiki ya Nyerere ambaye ni Milton Obote arudi tena madarakani.

Ukistaajabu ya Idd Amin Utayaona ya Nyerere.
Hapo kwa Musa na Firauni,mkuu umeua.[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nyerere ndio alikuwa mbaya fullstop!!!!!

Mie nakumbuka duka la kaya, mabasi ya Kamata yanayoitaji mwamvuli ukiwa ndani kwa kuvuja kwake, uda/daladala kwa foleni, mchele wa mdundiko, jiko kununa kitu cha kawaida, midabwada, ndala za matairi, majungu ya mikingamo na list inaendelea mpaka roho yangu inakereka nataka ku-pyuku!!.

Mie toka utoto niliambiwa Nyerere mbaya na nina amini hivyo, ingawa yes kuna mazuri kiduchu alofanya.........................
Si wengi wanayafahamu hayo.
 
Mwandishi wa makala hiyo kuibalance angeweza kabisa kwenda kufanya interview na watu wengine ambao wanahusika katika hii issue. Kuna watu wapo waulizwe, aulizwe Malecela, aulizwe Kawawa, wapo viongozi wanaojua historia yetu kwanini inaogopwa kuulizwa? Kwanini maneno ya Kambona yachukuliwe kama msaafu kamili?

Mtu mwenye uchungu anaweza kutia chumvi hadithi yoyote na hakuna mtu mwenye uchungu kama mtu mwenye kisasi. Binafsi katika suala hili ninasoma nikiwa skeptic kwa sababu ninafahamu saikolojia ya maumivu; watu wengi maumivu yakianza maisha yao husimama. Na miaka kwa wengine haiponyi maumivu hayo.

Kuna mambo kadhaa ambayo ni ya kweli (facts)

a. Kambona alishiriki kikamilifu na kwa kiasi kikubwa katika Uhuru wa Tanganyika. That is a historical fact.

b. Kambona alikuwa na nafasi mbalimbali za uongozi mara baada ya uhuru. That is a fact.

c. Kambona alishiriki kikamilifu katika kuituliza nchi na hususan wanajeshi baada ya maasi ya 1964 (ambayo hayakuwa ya Tanzania peke yake). That is a fact.

d. Kambona baada ya kutangazwa Azimio la Arusha aliondoka Tanzania na kwenda kuishi Uingereza akijipa uhamisho. That is a fact.

e. Wakati vyama vingi vimeanza Kambona alirudi nyumbani na kujaribu kuwasha moto aliodhania kauacha. Haukuwaka. That is a fact.

f. Kambona alifariki akiwa hajapatanishwa kabisa na Mwalimu. That is a fact.

Now,

Kuna hadithi mbili zinazoendelea. Kuna ile ambayo wengi tulijifunza miaka ya sabini na mwanzoni mwa themanini kuhusu Kambona. Na kuna habari ambayo imeanza kusimuliwa sana pembeni na kumpa ushujaa Kambona (mythification of Kambona) na pia kumtengenezea kisa cha ukuu (legend). Kati ya pande hizi mbili (official version) na ile ya maelezo yake yeye mwenyewe kuna ukweli.

Nasikitika kuwa hakuna mtu aliyepata nafasi ya kumuuliza Mwalimu "what happened to Kambona and why did you exile him". Hata hivyo wapo watu wanalojua jibu hilo ndio maana nimesema "waulizwe". Kwanini hamtaki hilo?
Kesi ya nyani uipeleke kwa ngedere?
 
Katika ku-balance story, msije hangaika kumuuliza Kawawa; huyu hajawahi kuwa na mawazo yake mwenyewe tangu nianze kumsikiliza. Atakachowaeleza ni hayohayo ya Nyerere ambayo tayari mnayajua.
Nimesoma ile article mara kibao, sijaona hata chembe ya chumvi. Alichofanya yule mwandishi ni kusimulia kile ambacho hakijawahi kusimuliwa.

Lazima tukiri kwamba pamoja na mazuri ya mzee wetu Nyerere, ndani ya nguo zake alikuwa ni mtu hatari sana hasa katika kuwafanya wanasiasa wenzake waonekana ovyo mbele ya jamii. communist style. Unakumbuka jinsi Amini alivyochafuliwa: mla watu, alionyeshwa akibeba nyama za watu na huku inzi wakimzonga, lakini wote sasa tunajuwa kwamba pamoja na ubaya wa Amini hakufikia kiwango cha kubeba nyama za watu kwenye mzegazega, huo ulikuwa ni umafia aliofanyiwa.

Pamoja na mapenzi yangu kwa Nyerere, nasikitika kwamba huyu mzee alijaribu kwa mafanikio makubwa kuua kila kipaji cha mtu yeyote mwingine aliyeibuka. As a result, yeye peke yake mpaka leo anaonekana ndiye aliyekuwa hero. Lakini sote tunajua ukweli kwamba isingewezekana yeye tu peke yake alete mazuri. Sasa swali la kujiuliza hao wengine walikuwa akina na nani na kwa nini hatuwajui?
Msome Mohamed Said jukwaa la historia utayajua mengi usiyoyajua.
 
Mimi nilimuamini Iddi Amin, kilichomg'oa Iddi Amin Uganda ni kama kilichomng'oa Jamshid Zanzibar. Ni Islamophobia tu, hakuna zaidi.
Umeanza sasa!!! km ni ivo basi alikuwa dhaifu sana,.... pamoja na kusaidiwa na lile jamaa renye mzuzu!!karafi sijui gadafi
 
1. mzee historia inategemea nani anaisimulia... mzee mambo yote yaliyosemwa hapo yametokana na simulizi. Sasa kabla hatujaanza kuruka ruka kuwa we found "it" ni vizuri kujiuliza.
a. Msimulizi ana lengo lolote jingine la kutusimulia anachotusimulia? b. Msimulizi anahusika vipi katika kisa anachosimulia (is he a hero or the anti hero "villain")?
c. Je, msimulizi ananufaika vipi na masimulizi anayoyasimulia?
d. Katika kisa cha historia je kuna watu wengine wanaoweza kutupa masimulizi yanayolingana na msimulizi huyo na watu hao wako huru kiasi gani?


2. lakini kwa wasomi we need outside source.

3. Je, Kawawa ni reliable source wa matukio ya awali ya historia yetu..?


Mkuu Heshima mbele, basically historia duniani huandikwa na walioko kwenye power, Mwalimu na kina Kawawa, wameandika ya kutosha kuhusiana na ishu ya Kambona, toka tukiwa watoto, sasa hii ni kwa mara ya kwanza tunapata story kutoka the other side, binafsi sihitaji kuambiwa anymore kuhusu Kambona, maana nimeiamba toka primary school jinsi alivyokuwa malaya na kukimbilia Uk, secondary, JKT, vyuoni nimeimba vya kutosha story ya Kambona kutoka kwa side ya Mwalimu,

Nimekutana na viongozi wengi waliosoma na Kambona, kama kina Lusinde, Marehemu Kanyama, Hashim Mbita, Nyirenda, nimeongea na waliofanya kazi naye kwenye siasa, imetosha, yanayosemwa sasa ndio hasa ya upande wake, Mwalimu pia aliwahi kusema baadhi yake, kama vile Kambona kuondoka na masanduku ya pesa nyingi sana alizokamtwa nazo Nairobi, airport, na akasema kuwa askari wa Kenya walipomuuliza what to do na Kambona, Mwalimu akaawambia kuwa wamuachie aende zake, sasa leo tunaambiwa kuwa ulikuwa ni uongo maana na yeye aliwataka serikali watoe ushidhi toka kwa askari wa Kenya, lakini hakuna kitu,

Sasa cha muhimu hapa kwenye ishu kama hizi ni kukubaliana kutokubaliaana, maana ya kumsubiri Kawawa eti aje aweke hii habari sawa hayo mimi simo, the main point yako kama ninakuelewa ni the motive za waanaoandika hizi story, which is great argument ila unachosahau ni kuwa it works both ways, yaani upande wa Kambona na Mwalimu!

Otherwise, I am enjoying this yaani to the bottom of my soul!


History is written by the winners!Historia ya Tanzania iliandikwa na watu wa Nyerere!huwezi kuona kipande chochote kitakachomponda Nyerere katika historia ya TANGANYIKA ingawa Watanzania Leo tunayapambania mawazo ya OSCAR KAMBONA😄😄

Hii nchi ni yetu sote,binadamu tunatofautiana mitazamo,tunapotofautiana tutafute namna nzuri ya kukubaliana kutokukubaliana.
 
Back
Top Bottom