Lowenstern
Member
- Dec 27, 2008
- 34
- 8
sasDs
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
There are two sides to every story. Time will tell.Nimesoma kitabu cha Mkapa, nimeona habari kama hizi kaziruka kabisa hajazitaja vilivyo.
Nikaona huyu Mzee katupunja sana habari hizi.
Itabidi wanahistoria wachimbe chini zaidi.
Why only two?There are two sides to every story. Time will tell.
Everything has two sides, a positive and a negative.Why only two?
To stretch your analogy, there is zero.This is neither positive nor negatives.Everything has two sides, a positive and a negative.
It ain't zero if it's something. Zero is nothing.To stretch your analogy, there is zero.This is neither positive nor negatives
Take the two zeroes out of $100, remain with $1, and see if zero is nothing.It ain't zero if it's something. Zero is nothing.
Take out zero from 0.5 and say what value zero has.Take the two zeroes out of $100, remain with $1, and see if zero is nothing.
For your proposition to hold value, it has to maintain consistency.Take out zero from 0.5 and say what value zero has.
Ushahidi tosha kuwa haupo tayari au hautaki kujifunza usiyoyafahamu.Halafu kuna kanisa linatoa mawazo kuwa afanywe mtakatifu.Kiukweli Nyerere hana sifa za kufanywa mwenye heri na mtakatifu labda mtakatifu wa siasa hapo sawa. 1.Kitendo cha ku saini hati ya kunyongwa mtu hata kama alikosa sifa ya utakatifu inapotea 2.Nyerere alikuwa mchoyo selfish 3.Alijiaminisha kuwa yeye ana akili kuliko watu wengine
Asante1. Inauma na inasikitisha sana unapofunguliwa macho na kuona ukweli halisi, hasa baada ya kuishi gizani kwa miaka zaidi ya 30 au 40!
2. tumeyasikia mengi mno kuhusu Kambona na yalikuwa ni ya upande mmoja na watu waliimba (au waliimbishwa) nyimbo na kukaririshwa ngonjera. Sasa upande wa pili umetoa masimulizi yake kidogo na watu wameanza kupata mwanga kidogo kuhusu yale yaliyojiri. Kina Marko, Luka, na Mathayo hawahusiki na Kambona bana...
I mean wakuu heshima mbele, hamna cha kuongeza nia ninasema kuwa huu ni mwanzo tu wa ukweli kuanza kutoka hadharani, Mwalimu was the greatest, lakini pia alikuwa na mapungufu, ambayo eventually yamekuwa our worst national nightmare!
Uliambiwa na nani mkuu na kwa sababu zipi?Nyerere ndio alikuwa mbaya fullstop!!!!!
Mie nakumbuka duka la kaya, mabasi ya Kamata yanayoitaji mwamvuli ukiwa ndani kwa kuvuja kwake, uda/daladala kwa foleni, mchele wa mdundiko, jiko kununa kitu cha kawaida, midabwada, ndala za matairi, majungu ya mikingamo na list inaendelea mpaka roho yangu inakereka nataka ku-pyuku!!.
Mie toka utoto niliambiwa Nyerere mbaya na nina amini hivyo, ingawa yes kuna mazuri kiduchu alofanya.........................
Mkuu kama naomba tuwekee kipeperushi na sisi hiki kizazi tuone na kujifunza historia yetu vyemaWimbo huu tuliuimba sana tukiwa shule ya msingi, na baadaye hata JKT tukiwa kwenye zile zilizoitwa "ruti machi":
"Kambona aliagiza
Chipaka na Kamaliza,
Pindueni mkiweza,
Nitawapeni mapesa,
Nikitoka safarini Uingereza!"
Ndicho tulichofundishwa kuhusu Kambona. Naye pia alisababisha ionekane kuwa huo ndio uliokuwa ukweli (au labda ni kweli ndo ukweli wenyewe huo), kwani kipindi fulani (sikumbuki mwaka gani), ndege ilidondosha vipeperushi vyenye ujumbe kutoka kwa Kambona vikihimiza wananchi waigomee serikali ya Nyerere. Ilikuwa sikukuu sikumbuki sabasaba au nyingine, lakini baba yangu aliokota kimoja na hadi leo kipo nyumbani nimekihifadhi. Ukisoma kipeperushi hicho, kinaashiria alishawahi kudondosha vingine pia siku za nyuma, kwani ndani yake anadai kuwa Nyerere ni mwoga tu anayekimbia kivuli, kwani yeye (Kambona) angetaka kupindua nchi angelipua tu uwanja ambako Nyerere na kabineti yake walikuwa wanatazama ngoma za kienyeji kwenye sherehe ya uhuru siku alipodondosha vipeperushi vingine mbele yake kwa ndege bila kuguswa na mtu! Ati anadai Nyerere alikuwa anashangaa tu wakati watu wanagombea kuokota vipeperushi vya Kambona mbele yake! Kwenye hicho kipeperushi nilichotunza kuna picha ya Nyerere ameshika kichwa, chini yake kuna maneno "Jamani naomba msaada, mambo yamenizidi kimo". Mwisho wa kipeperushi kuna picha ya Kambona na maandishi "Ushindi kwa wananchi" na saini yake Oscar S. Kambona.
Hizo ndizo kumbukumbu nilizonazo kuhusu huyu aliyejiita wakati huo (alipokuwa mkimbizi), "mkombozi" Oscar Kambona.
AsanteNaona mjadala unapamba moto lakini tunasahau kwamba zama za Nyerere kila kitu kilikuwa kinafanyika kwa malengo maalum. Lengo la Nyerere zama hizo ilikuwa ni kuhakikisha kwamba jamii inamkubali yeye na kila kitu anachokianzisha. Mifano michache ya kuonyesha jinsi watanzania tulivyokuwa tunaaminishwa na kupewa vitu vya upande mmoja tu ni kama hii:
Moja, mitaala ya shule za msingi na sekondari ya masomo ya historia na siasa viliandaliwa kwa kuangalia serikali na chama (TANU & ASP na CCM) wanataka nini. Tulikaririshwa imani za chama (TANU na CCM) na vikao vya chama. Tulifundishwa katiba ya CCM, wakati katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ni muhimu sana mtu aijue hatukufundishwa. Kwa hiyo hata vitabu vya siasa na historia ya TANU viliandikwa kwa mtazamo huo huo wa kumuonyesha Nyerere kama hero na ndiyo maana wengine waliochangia, michango yao haionekani kama ni mikubwa sana kuliko mchango wa Nyerere. Kwa hiyo ninachokifikiria mimi ni kwamba tukitumia vitabu vya historia vilivyoandaliwa na makada wa TANU na CCM zama hizo, hatuwezi kuwa na balanced history ambayo haimpendelei wala kumuonea mhusika. Hapa naomba niunganishe mfano wa Afrika ya Kusini, ukisoma historia ya vitabu vilivyoandikwa na makaburu wakati wa utawala wao, vitakuwa vinatukuza makaburu na kuonyesha kwamba makaburu ndiyo wenye haki ya kuishi Afrika ya Kusini na kutawala. Lakini leo hii kuna vitabu ambavyo viko wazi zaidi na mtu akisoma vinatoa balanced information ambayo haipendelei upande wowote.
Mbili, tuliaminishwa kwamba CCM ni baba na mama (japo Nyerere alikanusha wakati akistaafu siasa), maana bila ya kuwa mwanachama wa CCM huwezi kupata baadhi ya mambo muhimu. Mfano, kuingia Mlimani/Muhimbili ilikuwa ni lazima upate recommendation ya Mwenyekiti wa Tawi lako la CCM. Kibaya zaidi, mwenyekiti mwenyewe ni darasa la saba, hapo utake usitake lazima ukawapigie magoti. Sijui impact ya kukosa recommendation, na sometimes watu walikuwa wanaulizwa hata kadi za CCM na UVCCM. Tukiwa JKT wale tuliokuwa hatuna kadi za CCM tulilazimishwa kukata kadi za CCM. Si ajabu hata kuomba kazi ilikuwa lazima uwe na kadi ya CCM na ndiyo maana kulikuwa na matawi ya CCM kwenye mashirika ya umma. Kwa hiyo lengo la hayo yote lilikuwa ni kui-praise CCM na Nyerere. Unaposema zidumu fikra sahihi za Mwenyekiti wa CCM (Nyerere) ulikuwa na maana gani? Ina maana yeye huwa hakosei hata kidogo, je, alikuwa ni Mungu mtu? Baada ya Nyerere kung'atuka CCM sikusikia tena hiyo kauli, hapo kuna walakini, ina maana wenyeviti wengine waliofuatia hawakuwa na fikra sahihi!!!??? Baada ya kukubali hiyo kauli ya fikra sahihi za mwenyekiti wa CCM unategemea kuna mtu angejitokeza kupinga pendekezo la mwenyekiti (Nyerere) kwenye kikao??? Nyerere ana mazuri lakini pia tukubali kwamba alijikweza sana na kuwafanya wenzake wengi wasionekane kama wana hoja au mchango mkubwa kwenye chama na nchi na ndiyo akina Kambona wako gizani na siyo nuruni.
Nina uhakika kwamba kuna watu wanajua mengi kuhusu Kambona lakini kwa sababu za kwao binafsi hawawezi kuyasema wanayoyajua. Na ndiyo maana kwenye vitabu hatuoni huo upande wa pili wa Kambona. Kama kuna mwana CCM ambaye si mnafiki nadhani anaweza kuja kutuambia kwamba hapa kuna ukweli au hakuna ukweli, lakini vitabu vya historia vilivyoandikwa zama za Nyerere haviwezi kutupatia huo ukweli, bali vitatupatia upande wa Nyerere na tena mazuri yake tu, lakini siyo mabaya yake na matumizi mabaya ya dola ya vyombo vya habari.
Nimefuitafuta sana hii historia. Nafurahi leo nimeipataMengi yamesemwa kuhusu Mzee wetu huyu na sisi tuliokuwa shuleni wakati ule tulilishwa kile ambacho naamini ni sumu. Wakubwa tuelimisheni ukweli kuhusu Mzee huyu.
View attachment 1371792
Oscar Kambona
Hii ameandika Simon Martha Mkina
Natumaini waandishi wa historia ya tanzania watampa nafasi yake kwa mchango mkubwa aliyoutoa.
RIP Mzee Kambona
Oscar Salathiel Kambona, alitaka kumpindua Nyerere kwa kushirikiana na wapiganaji wa Umkhonto.
=======
kichakaa man, ameandika;
Marehemu Oscar Kambona alizaliwa mwaka 1925 katika kijiji cha Kwambe kilichopo mwambao mwa ziwa Nyasa, karibu na Mbamba-bay, wilaya ya Mbinga, Mkoa wa Ruvuma. Alikuwa mtoto wa marehemu Rev. David Kambona na Bibi Miriam Kambona.
Rev. Kambona alikuwa ni miongoni mwa waafrika wa kwanza kupata upadre katika kanisa la Anglikana la Tanganyika. Wakati Oscar Kambona akiwa mdogo, baba yake alikuwa akimweleza kuhusu ndoto zake juu ya uhuru wa nchi yake, hivyo Oscar alikuwa akiwa na hamu sana ya kuitumikia nchi yake.
Oscar alipata elimu ya msingi nyumbani kwao, chini ya mwembe (ambao bado upo), katika kijiji chao kwa kuwatumia wazazi wake wote wawili na mjomba wake, ambao wote walikuwa walimu. Baada ya hapo alipelekwa shule ya kati ya Mt. Barnabas, Liuli, na baadaye shule ya Sekondari ya Alliance, ambako alilipiwa ada na Askofu mzungu wa Anglikana kwa vile baba yake hakuweza kumudu kulipa ada ya paundi 30 kwa mwaka.
Oscar alikuwa akisimulia jinsi alivyoweza kumshawishi Askofu huyo amlipie ada kwa kusema sala ya Baba yetu kwa kizungu. Oscar alichaguliwa kwenda ‘Tabora Boy’s Senior Government School’, ambako alionana na Julius Nyerere kwa mara ya kwanza; wakati huo Nyerere alikuwa anafundisha katika shule ya kikatoliki.
Baada ya kumaliza masomo ya sekondari alienda katika shule yake iliyopita ya Alliance kama mwalimu na baadae alichaguliwa kuwa ‘Schoolmaster’. Ilikuwa katika mkutano wa kitaifa wa walimu, mnamo mwaka 1954, ambapo Kambona na Nyerere walikutana tena.
Kambona alikuwa tayari kukitumikia chama cha TANU ambacho kilikuwa kimeanzishwa muda si mrefu, lakini Nyerere akasema wasingeweza kumwajiri kwa vile chama kilikuwa hakina fedha.
Kambona akasema chama hakikuwa na fedha kwa vile hakikuwa na ‘organising secretary, na ndipo alipoamua kufanya kazi hiyo ili kujenga chama, bila ya malipo’. Aliishi kwa kutegemea akiba aliyojitunzia kwa kufanya kazi miezi 6.
Katika kipindi hiki Kambona alisafiri sehemu mbalimbali za nchi na kuonana na machifu na wazee wa vijiji ili kusajili wanachama. Katika miezi 6 alifanikiwa kusajili wanachama 10,000, na hadi kufikia mwaka mmoja alikuwa amepata wanachama hai 100,000. Kambona alitumia michango aliyopata kufungua akaunti ya kwanza ya TANU.
alienda Butiama kumshawishi Nyerere achukuwe uongozi wa chama moja kwa moja. Baada ya miaka mitatu Kambona aliamua kwenda kusomea sheria katika Chuo cha Middle Temple, nchini Uingereza mwaka 1957 kwa ufadhili wa Gavana.
Akiwa London Kambona alikuwa kiongozi wa chama cha wanafunzi wa Tanganyika na Mwenyekiti wa tawi la TANU la London. Ni wakati huo ambapo Kambona alipata fursa ya kukutana kwa mara ya kwanza na watu mashuhuri kama George Padmore, mwanaharakati wa umoja wa Afrika, ambaye alimshawishi ahudhurie mkutano wa mwaka 1958 wa waafrika wote(All Africa’s Peoples Conference), uliofanyika nchini Ghana muda mfupi baada ya kupata Uhuru.
Akiwa Ghana Kambona alipata nafasi ya kukutana na mwanaharakati mwingine maarufu wa siasa za Afrikla, Kwame Nkurumah. Akiwa uingereza Kambona alikuwa mwaafrika wa kwanza kutangaza taarifa ya habari kwa Kiswahili katika idhaa ya kiswahili ya BBC.
Aliporudi nchini Tanganyika, mwaka 1959, TANU ilikuwa imeshaweka bayana madai yake ya kupewa serikali ya madaraka, vinginevyo TANU ilikuwa tayari kuanzisha mapambano kama ilivyokuwa kwa Mau Mau ya Kenya. Wakiwa London wakisubiri kupewa madaraka ya ndani, Nyerere na Kambona walijadili hatua mbalimbali ambazo zingechukuliwa ili kuepuka kutoweka kwa amani.
Wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Londoni 1991, Kambona alikumbuka matukio kama hivi, ‘’Bwana Nyerere alikuwa akiishi nami katika chumba kidogo nilichopewa chuoni.
Tulijadiliana ni namna gani angeweza kurudi nyumani na kuonana na wafuasi wake bila kupewa serikali ya madaraka. Baadae nilifanikiwa kumshauri kuwa wakati atapozungumza na vyombo vya habari katika the East African Arch aseme kuwa walowezi wa kizungu ambao wapo Tanganyika wana hekima zaidi katika kanda ya Afrika Mashariki.
Alikubali kusema hivyo endapo na yeye Kambona angekubali kukatisha masomo yake ya sheria huko London na kurudi Tanganyika ili ampe nguvu na kumuunga mkono katika kikao cha kamati kuu ya TANU wakati akitetea tamko lake la wenye hekima zaidi.
Katika uchaguzi wa kwanza TANU ilishinda viti vyote isipokuwa kimoja. TANU iliunda serikali ya mambo ya ndani chini ya Nyerere ambaye alikuwa Waziri kiongozi wa kwanza.
Na katika harakati hizo za matayarisho ya serikali ya ndani, Kambona alimwoa Flora Moriyo wakati wakiwa kwenye msafara wa harakati za kukamilisha matayarisho ya uhuru na serikali ya Uingereza. Harusi ilifungwa katika kanisa la Mt. Paul, London, na Nyerere ndiye alikuwa msimamizi. Kambona aliteuliwa kuwa waziri wa Elimu.
Baadaye alishika nyadhifa za waziri wa Mambo ya Ndani, Mambo ya nchi za nje na Ulinzi na Tawala za Mikoa. Pia alikuwa mwenyekiti wa kwanza wa Kamati ya Ukombozi ya Umoja wa Nchi Huru za Afrika na mwenyekiti wa utayarishaji wa AOU charter.
Mwaka 1964, Kambona alifanya kazi kubwa katika kuunganisha Zanzibar na Tanganyika, akiwa pamoja na Raisi Nyerere, Raisi Karume na Waziri Kiongizi Hanga. Hii ilikuwa ni baada ya mapinduzi ya Zanzibar.
Wakati wa wanajeshi wa kikosi cha Calito walipoasi mwaka 1964 Kambona alikuwa msuluhishi mkuu kati ya serikali na wanajeshi hao. Nyerere na Kawawa walienda mafichoni Kigamboni. Baada ya siku tatu za majadiliano Kambona aliafiki kuongeza kasi ya kuwawezesha waafrika kushika hatamu jeshini.
Katika mahojiano na gazeti la Daily Telegraph la London Kambona alisema, ‘baada ya kuwatuliza wanajeshi nilikwenda kuwatafuta viongozi wengine na kuwarudisha mjini kwa kutumia Land Rover yangu’. Hatimaye maasi hayo yalidhibitiwa kabisa na majeshi ya Uingereza na Nyerere alimsifu Kambona bushara na uaminifu wake.
Tofauti kati ya Nyerere na Kambona zilianza kujitokeza baada ya maasi ya wanajeshi. Nyerere alitaka kuanzisha mfumo wa chama kimoja nchini ili kuimarisha usalama. Kambona alipinga hoja hiyo kwa maelezo kwamba mfumo huo ungezorotesha uhuru wa watu na maendeleo ya demokrasia.
Hata hivyo, Kambona alishindwa bungeni; alikataa kusaini muswada (bill). Mwaka 1967, baada ya safari ya China ya mwaka 1965, Nyerere akiwa amependezwa na mfumo wa kikomonist wa Mao, alitaka kuanzisha mfumo kama huo kwa jina la ujamaa.
Dhana ya msingi ya mfumo wa ujamaa ilikuwa ni kuwahamishia watu katika vijiji vya ujamaa na kutaifisha viwanda ana mali. Kambona hakukubaliana na utaratibu huo kwa maelezo kwamba ungeongeza umaskini na udhibiti wa serikali kwa watu.
Alijiuzulu kutoka katika serikali na Chama na hatimaye yeye na familia yake walikimbilia Kenya na kisha Uingereza ambako walipatiwa uhifadhi wa kisiasa. Mara baada ya kuondoka mali za Kambona zilichukuliwa.
Ndugu zake wawili, waliwekwa kizuizini bila ya kufikishwa mahakamani na kufungwa kwa zaidi ya miaka kumi. Wanafamilia wengine walinyanyaswa na kuwekwa kizuizini. Wengine kati yao walibambikiziwa kesi za uhaini, wakafikishwa mahakamani na kisha kufungwa na serikali.
Kati yao walikuwa Bibi Titi ambaye alipigania uhuru pamoja ana Nyerere na alikuwa kiongozi wa jumuia ya kina mama. Alikuwepo pia Michael Kamaliza ambaye alikuwa mwanaharakati wa chama cha wafanyakazi, mwanachama wa TANU na waziri.
Wengine ni pamoja na Gray Mattaka, John ana Eliya Chipaka na Prisca Chiombola. Kambona alituhumiwa kuwa kiongozi wa wahaini wakati akiwa London na alihukumiwa bila kuwapo. Watuhumiwa hatimaye walikata rufaa katika mahakama kuu ya Afrika Mashariki na wakaachiwa huru.
Hata hivyo, baadae walikamatwa na serikali na kufungwa tena. Kambona alituhumiwa kuwa aliiba pesa nyingi sana zikiwa ni mali ya umma, kitu ambacho Kambona alikataa katika taarifa yake na waandishi wa habari Septemba 6 huko London 1967.
Tuhuma hizo zilisema kuwa ‘’ Kambona amekutwa na pesa nyingi sana kama karanga alipopekuliwa katika Uwanja wa ndege Embakasi Nairobi’’ Hata hivyo Kambona katika taarifa yake kwa waandishi wa habari alikanusha kuhusika na tuhuma hizi na badala yake akaipa serikali ya Tanzania kuiomba serikali ya Kenya kutoa ukweli juu ya jambo hilo- jambo halikufanyika.
Akiwa Londoni Kambona aliishi maisha ya shida na dhiki. Katika mwaka 1982 ndugu zake Kambona na Otini Kambona walifunguliwa kutoka kizuizini baada ya juhudi za waziri mkuu wa New Zealand Robert Muldoon. Katika mwaka 1990 Kambona akiwa na matumaini makubwa ya mabadiliko ya kisiasa katika Tanzania hususani mabadiliko ya demokrasia, aliunda chama kiitwacho Tanzania Democratic Alliance.
Wakati vyama vingi vilipoanzishwa Tanzania 1992 Kambona aliomba kurudi Tanzania. Serikali ya Tanzania ilimkatalia katakata na kudai kuwa Kambona hakuwa Mtanzania. Kambona badala yake aliomba Serikali ya Uingereza kumpa pasi ya kusafiria kurudi Tanzania. Hata hivyo Serikali ya Tanzania ilitamka kwamba pamoja na kupata pasi hiyo itamweka ndani pindi atakapoingia Tanzania.
Pamoja na msimamo huo wa Serikali, Kambona alitua kwenye ardhi ya Tanzania tarehe 5 september 1992. Hakuna mamlaka iliyomkamata bwana Kambona bali alipewa miezi mitatu awe amekamilisha utata wa uraia wake. Baada ya kurudi, Tanzania aliona kuwa harakati za kuelekea kwenye demokrasia ya kweli zilikuwa zikienda kwa mwendo wa kinyonga.
Hata hivyo Kambona hakuweza kujihusisha kwa kiasi kikubwa na siasa kutokana na matatizo ya kiafya hususani shinikizo la damu. Hatimaye Oscar Kambona alifariki akiwa katika matibabu mjini London mwezi Juni 1997.
Mdogo wake Otini Kambona naye alifariki katika kipindi hichohicho kutokana na magonjwa ya moyo. Wote wawili walizikwa Tanzania, na serikali ya Tanzania iligharimia gharama zote za usafirishaji miili ya marehemu ndugu hawa.
Oscar Kambona ameacha mke na watoto wawili. Mtoto wao wa kwanza Mosi Kambona aliuawa mjini London katika mazingira ya kutatanisha. Roho ya Oscar Kambona na ndugu na jamaa wote waliotangulia MWENYEZI MUNGU aziweke pema peponi, Amin.
Kumsoma bonyeza hapa