Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona?

Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona?

Kama hujanielewa fanyaga hivi!!!.... Chukua herufi mbili za mwanzo ya neno la kwanza yaani ''SA'' na ''WA'' Utapata nini?? ndo jibu lake!
Bado hujatuweka wazi sawia, ila km haupo huru kuzungumzia suala ili bhac weka pemben
 
Bado hujatuweka wazi sawia, ila km haupo huru kuzungumzia suala ili bhac weka pemben
Ndo matokeo ya division zero mnasumbua uraiani huku! ....najua Hukulifikia ??...lkn km ungeenda ungeipata hiyo!
 
Ukweli ni kwamba Kambona was so smart and intelligent & exposure more than Mwalimu. Mwalimu akafanya fitna na kuonekana Kambona ni chawa wa wazungu kitu ambacho si kweli - tulilishwa matango pori mengi sana enzi za primary kwenye somo la siasa.
 
Katika mahojiano na gazeti la new africa huko nyuma Nyerere aliulizwa ikiwa kuvunjika kwa urafiki wake na Kambona ni moja ya mambo yanayomkosesha raha ktk utawala wake,Nyerere alisema hapana na alimshangaa Kambona kama katibu wa TANU alihusika katika maandalizi yote ya azimio la arusha hata kabla halijatangazwa na mwishoni akabadilika kulikana. Kilichomsikitisha Nyerere ni kuwapigia magoti waingereza waliokuwa wakoloni wetu waje wamwokoe wakati wa maasi ya jeshi,wakati tulijidai tunaweza kujitawala.

Toafauti kati ya hawa ni attitude towards money/richness and how to get it.

Nyerere alifuata msimamo wa biblia na wa kikomunisti,kuwa ni ngumu kwa tajiri kuingia ktk ufalme wa Mungu,huwezi kuwa tajiri pasipo kutumia nguvu ya watu wengine hivyo kwa kuwa tajiri umenyonya wengine(marxism),pia maneno ya mtakatifu mmoja kuwa unapompa maskini shati humsaidii bali unampa haki yake! Kambona nafikiri hakuona vibaya mtu kutumia akili na nguvu zake kuchuma mali.

Je historia ya sasa tz tunaweza kuwahukumu vipi hawa waasisi wa taifa letu?mawazo ya yupi yameonyesha ku hold?

Baada ya kuvunjwa azimio la arusha tumejionea na tunaendelea kuona na kujadili viongozi wetu wanavyofuja mali na kuliibia taifa, rushwa, nepotism, etc.

Nakubaliana na mawazo hapo juu kuwa implementation ya azimio ilienda haraka sana kabla hatujawa na skilled personnel ya ku takeover na kuendesha taasisi mbali mbali.

For me Nyerere was right and had the right intention to selfishlessly serve the poor people of tz and lived to his words until his death.
duuh
 
Ndo matokeo ya division zero mnasumbua uraiani huku! ....najua Hukulifikia ??...lkn km ungeenda ungeipata hiyo!
Unajikuta mtu wa coding, sasa unachokieleza km unakifaham vilivyo yanini kutoweka wazi?

NB; mafumbo ya bible yamewafanya wafuasi wa kristo mpaka Leo kubaki makundi makundi - Kila kundi likijiona liko sahihi kuliko
 
Hapana Mkuu mie niko wazi sema hivi....siyo wote mnaoweza kuijua akili kubwa! ndo maana drsani kuna wa kwanza wa pili.3 ,4, 5. 6, 7...... ivoivooooo mpaka mfunga mkia!

sijwahi ona mfunga mkia akilalalamika !!! kubali tu hujui baaas
 
Anyway, wewe akili kubwa na bila shaka ulikuwa wa kwanza Toka umeanza kusoma had kumaliza, ila km huwez dadavua/elezea jambo/kitu ukaeleweka ktk jamii yako ama watu unao waeleza bado unabaki kuwa TRAB AND TRAT
 
Nashukuru, nakupongeza, umekiri kwa kinywa chako kuwa ''akili zangu ni kubwa'' safi sana uendelee ivo! ivio! napendaga saaana sifa za kweli......ila bado kidooogo hujanielewa! siyo tatizo lako!

umenielewa sehemu moja tu, ni sawa!........je! mko watu wangapi ktk jamii yangu hamjanielewa?? ili nijifanyie tathmini tunduizi?........ waweza taja idadi please?..... au subiri...........

jamanie eeehee!! wana nzengo JF njooni huku muwonee !! ambao hamjanielewaga akili kubwa mie niko kazini! niwape masahihisho!...jikusanyeni nirudie...... wakifika watano! nitag! niko hapo nje!
 
B
Ukweli ni kwamba Kambona was so smart and intelligent & exposure more than Mwalimu. Mwalimu akafanya fitna na kuonekana Kambona ni chawa wa wazungu kitu ambacho si kweli - tulilishwa matango pori mengi sana enzi za primary kwenye somo la siasa.
Bypass believe that the
 
Kambona nalia gizaa......Pindueni mkiwezaaaa nitawapeniii mapesaa nikirudii uwingereza..... Wale wakongwe wenzangu tukumbushane aka kanyimbo
 
Kambona nalia gizaa......Pindueni mkiwezaaaa nitawapeniii mapesaa nikirudii uwingereza..... Wale wakongwe wenzangu tukumbushane aka kanyimbo
Nahitaji huu wimbo sanaaa.....

sana tunawahesabu haoooooo
waliokufa kwa tabu..................

mtunzi lazima alikuwa kijana machachari wa tanu
 
Kambona asiongeondoka yangemkuta ya Denan Kimathi, Mwalimu on his prime hakupenda kabisa mtu wa kumchallenge. angalia kina Mtei
 
Kuna Mtanganyika huwa nakaanae naye huwa haishi kuongea mazuri ya huyu OSCAR KAMBONA katika historia ya Nchi hii kwa hakika anathibitisha kuwa KAMBONA alikua ndiye mzalendo wa kweli katika Taifa hili Mungu ampumzishe Mahali salama huko aliko.
 
Nahitaji huu wimbo sanaaa.....

sana tunawahesabu haoooooo
waliokufa kwa tabu..................

mtunzi lazima alikuwa kijana machachari wa tanu
Kwanza tunawahesabu waliokufa kwa tabu,bila hata matibabu wengi hawana hesabu waliokufa kwa tabu dunianiiii,
Kambona aliagiza Chipaka na kamalizaa,pindueni mkiweza nitawapeni mafedhaa nikirudi safarini uingerezaaa

Nakumbuka hapo tu....sijui ni nani alikatunga haka kasongi
 
Ndugu zangu nani ningependa kuchangia kidogo kuhusu Oscar Kambona.

Leo nimefanya kipindi kizima cha TV kuhusu maisha ya Oscar Kambona toka alipojiunga na TANU pale TANU HQ, New Street mwaka wa 1954 hadi alipokosana na Mwalimu Nyerere mwaka wa 1967 na kuondoka kwake kwenda uhamishoni Uingereza.

Nimeeleza yaliyotokea katika maasi ya Tanganyika Rifles (TR) tarehe 20 Janaury 1964 na jinsi Kambona akiwa Waziri wa Ulinzi alivyokabiliana na uasi ule na mwishowe kuweza kuwatuliza askari na wakarudi Colito Barracks.

Msaada ukatafutwa kwa Waingereza na Royal Marines ambao manowari yao haikuwa mbali na pwani ya Tanganyika wakaja na kuwanyang'anya silaha waasi.

Kwa siku tatu zile za maasi kiongozi aliyeonekana na kusikika katika radio akiwatuliza na kuwafariji wananchi alikuwa Oscar Kambona.

Mawaziri wote walijificha.

Baada ya waasi kunyang'anywa silaha ndipo Mwalimu Nyerere akajitokeza hadharani na kuzungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa kwa kipindi chote cha maasi alikuwa Dar es Salaam.

Nyota ya Kambona iling'ara kwa yale aliyofanya katika kukabiliana na maasi lakini haiba ya Mwalimu Nyerere ilikuwa imepungua kwani kulikuwa na minong'ono mitaani kuwa Kambona angelitaka angeliweza kuchukua serikali.

Katika hili wanahistoria kila mmoja katika miaka iliyopita amekuwa na lake la kusema.

Baada ya maasi Kambona akawa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje nafasi aliyoishika hadi mwaka wa 1967 alipokinzana na Mwalimu Nyerere kuhusu Azimio la Arusha.

Katika mabadiliko ya Baraza la Mawaziri mwaka huo Kambona akateuliwa kuwa Waziri wa Serikali za Mitaa.

Inasemekana Kambona wala hakupata kuingia katika ofisi hii yake mpya na akajiuzulu kutoka serikalini.

Turudi nyuma kidogo.

Mwaka wa 1963 Mwalimu Nyerere alilivunja Baraza la Wazee wa TANU lililokuwa na wajumbe 126 wote Waislam.

Baraza hili halihitaji maelezo mengi kwani ndilo lililomtia nguvu kubwa Nyerere kukubalika Dar es Salaam.

Sababu zilizotolewa za kuvunjwa kwa Baraza la Wazee wa TANU ni kuwa lilikuwa linachanganya dini na siasa.

Kuanzia hapo Mwalimu Nyerere akawa mbali na wazee hawa na hawa wazee wakajiweka mbali na TANU hakuwarudi tena pale Lumumba ambako wengi walifanya kama baraza yao ya kukutana nyakati za jioni kwa mazungumzo.

Wakati Nyerere kajikata na wazee hawa Kambona alibakia na uhusiano mzuri na wazee wengi wa TANU mmojawapo akiwa Mshume Kiyate.

Mshume Kiyate kwa upande wake hakuweka kinyongo dhidi ya Nyerere kwa kulivunja baraza lao.

Ushahidi wa roho yake nyeupe ni pale baada ya maasi Mshume Kiyate alikwenda kumpa pole Nyerere na kumvisha kitambi kama ishara ya mapenzi yake kwake.

Huenda si wengi wanalijua hili.

Kambona alikuwa mtu karimu sana na wazee wengi walinufaika na mkono wake wa kutoa.

Kambona hakuchusha machoni pa wazee hawa na pengine kwa wananchi wengi wa kawaida. .

Swali la kujiuliza ni kuwa, je, Mwalimu alikuwa anafahamu kuwa alikuwa anaanza kupoteza mapenzi kutoka kwa baadhi ya watu waliompenda sana kuanzia mara ya kwanza alipoka Dar es Salaam mwaka wa 1952 na ugomvi wake na Kambona kule kuvunja Baraza la Wazee kulikuwa kunajenga taswira mpya katika historia ya chama cha TANU?

Nakuwekea hapo chini kipande kifupi cha video katika yale niliyozungumza katika kipindi hiki cha Oscar Kambona:

View: https://youtu.be/VXjj3-_Yyw8
 
Back
Top Bottom