Ukweli tunaotakiwa kuujua: Rais atakayekuwa hana wabunge wa kutosha Bungeni hataweza kuleta au kufanya mabadiliko yoyote na Urais wake hautadumu

Dr. Akili naona umefikiria sana na kuuliza maswali unajieleza na kujijibu tena kwa nadharia ya kiuchumi..nasema nadharia ya kiuchumi sababu uchumi huongelea positivity tu negative factors hubaki constant yaani kama hazipo. Sitafanya citation ya vifungu vya katiba kutokana na siasa lakini nakuhakikishia kwa katiba yetu hata Rungwe akishinda Urais wa Nchi ndani ya miezi mitatu tu yaani kabla ya siku mia moja atabadilisha mfumo kuwa wa kwake yeye..utasema watu atawapata wapi..jibu ni kwamba Watanzania njaa kali wanafiki mno..atawapata ambao watatamani kubaki kufaidi tunda la kutawala.

Rungwe natolea mfano tu atabadili uongozi wa tume ya uchaguzi na kuwaweka watu wake ambao kama sasa tu watamtangaza tena kuwa Rais "matumizi sahihi ya DOLA" atabadili wasaidizi wa uchaguzi kwa kuamrisha kuteua watu nje ya wakurugenzi katika manispaa wamsaidie kufanya fojari zake. Hapa sasa ndugu yangu ndio CHAUMA kitapata viti zaidi ya theluthi na wewe Dr. Akili ukiwemo si ajabu..si unataka kula na kura pia japo sasa wajinasibu kuwa Mwana CCM nguli "Unafiki na madaraka". Kwa katiba hii ambayo hata Muasisi wa Uhuru wa Nchi hii alituonya inampa madaraka Rais kuwa Mungu Mtu. Anateuwa bila kushauriwa na hata akishauriwa anahiyari kukubali ama kukataa.

Kwa leo naishia hapo Dr. Akili. Ila kwa ufupisho tu akichaguliwa wa vyama Mbadala basi Rais atatafuta safu yake, ataibadili, atavunja Bunge ataitisha uchaguzi atashinda viti vingi tu kiuhalali ama la..kama tulivyopitishwa bila kupigwa awamu hii..then anatawala kwa ubweche na hatabadili KATIBA kamwee. 😎😎
 
Acha kujitoa ufahamu, hii awamu ina madudu zaidi ya escrow ndo maana CAC independent aliporwa cheo chake, uoga na unafiki unakusumbua kijana

Watu kama nyie tumeishi nao, tumesoma nao tangu primary, vigeugeu, mnapenda kujioendekeza kwa mwenye nacho, wanafiki, wambea......hamfai kabisa kwa maendeleo

Sent from my TECNO KD6 using JamiiForums mobile app
 
Mbona rahisi. Bambikia kesi wote, funga kwa uhujumu uchumi..fanya uchaguzi kwa kuweka wabunge wa chama chako. Unaendelea kutawala.
 
Kwa Katiba hii Rais hana mpaka!
 
..mimi nadhani hilo likitokea WANANCHI tutafaidika zaidi.

..kwasababu kila upande, kwa maana Raisi, na Wabunge, watataka kutufurahisha sisi wananchi.

..pia Bunge litatekeleza barabara wajibu wake wa kuisimamia na kuishauri serikali.

..Bunge halitakuwa wakala wa serikali au Raisi.

..Pia Raisi atakuwa muangalifu kutokutumia madaraka yake vibaya.

..Zaidi Raisi atafanya jitihada za ziada kuwatumikia, na kuwafurahisha wananchi, kwasababu hao ndio ngao yake iwapo bunge litakwenda kinyume naye.
 
Ameishasema eti atawabana wabunge walete maendeleo jimboni!!!?
 
Mbunge na kuleta maendeleo sawa sawa..atawabana ndio unataka awaache.. 😀 😀 ..nimejibu kikada hapo. Ila kwa ukweli wananchi wangejua maendeleo yanaanzia katika kaya wala wasingehangaika na wabunge. Wao wanapitisha tu bajeti lakini anayeiandaa bajeti ni yeyehadi mkurugenzi na baraza lake. Mbunge kama mjumbe wa full Council anachangia tubajeti hiyo. Kule bungeni wanapopiga kelele kwangu hakuna maji barabara kama hakuweka kwenye bajeti ya serikali na ikapitishwa hapo ni ngonjera tu baasi.
 

Kwa taarifa yako kwa katiba hii, bunge na mahakama ni uchafu kama uchafu mwingine. Kitu cha kwanza ukiwa rais bila wabunge wengi hazindui bunge, bali unafanya kazi kama miezi sita, huku ukichota pesa hazina kuhonga wabunge walio wengi waje waunge juhudi. Yoyote atakayegoma unaagiza apigwe risasi au kutekwa. Ndani ya miezi miwili kwa mwendo wa kuunga juhudi, wabunge wote watahamia kwako kisha unaitisha uchaguzi kiini macho, wale wote uwatakao wanapita bila kupingwa. Hizo ndio nguvu alizonazo rais kwenye katiba hii ya kihuni.
 

Nilidhani nina hoja kumbe unaoongea utoto mtupu.
 
Tunazungumzia utawala wa sheria. Bunge ndilo suprem. Ndiyo demokrasia. Rais akienda kinyume cha hapo anakuwa dictator. Hivyo ili Lissu aweze kuendesha nchi wakati ni lazima aiendeshe kidikiteta kwani hatakuwa na support la wabunge walio wengi. Na akifanya u dictator bunge litamu iimpeach mara moja.

Unapaswa pia kujua kuwa katiba yetu hairuhusu rais asiyekuwa na angalao nusu ya wabunge wa majimbo. Katiba yetu imeweka bayana kwa mfano kama Lissu ikatokea (Mungu apishe mbali) akapita kwenye kura za urais na CCM wakapata majority of votes za wabunge kama ilivyo kawaida yao, basi serikali itakayoundwa itakuwa ya mseto; Waziri Mkuu atatoka ccm na nusu ya mawaziri watatoka ccm. Haya ni kwa mjibu wa katiba yetu ya nchi. Na kwamba bunge litakapomu impeach Lissu na uchaguzi kurudiwa yeye Lissu katiba haimuruhusu kuwa mgombea urais tena bali Waziri Mkuu. Hivyo Lissu atakuwa rais wa muda mfupi sana kwa vyo vyote vile kwa mjibu wa katiba yetu.
 
Dr Akili,
Kuna ukweli umeanza kuukubali, twende mdogomdogo, tutafika tu
Nimefurahi sana huu ukweli wake sasa wameza kuukubali sasa MUNGU ni mwema siku zote si umeona mh.magufuli nae ameaza kuukubali ukweli kuwa anaweza ishia miaka mitano.kwaza aliaza alipotembelea GEREZA butimba kwamba na yeye ni mfungwa mtarajiwa.maneno huumba kile kinachokuja mbele yako
 
Pamoja na hofu uliyonayo nakutakia jioni njema utake usitake.
 
Michezo walioicheza ccm miaka yote toka mfumo WA vyama vingi uaze kwenye chaguzi ndio mtayochezewa nanyi
 
Umesahau 1.5tilion mkuu
 
Nauliza hivi ni majimbo mangapi mzee wa ubweche kasimamisha wabunge? Maana nchi tushampa tayari! Jiwe atateuliwa kuwa waziri wa bara bara na madaraja kwenye serikali ya mzee wa ubwabwa ili aongeze madaraja mpunga uje mjini kwa wingi
Tundu atakua wazir wa sheria jasus mstaaf mambo ya nje
 

Ni hivi baada ya Magufuli kukaa madarakani, imefahamika pasi na shaka kuwa katiba yetu ni kama gazeti la udaku, ambalo rais anaweza kutii porojo zilizoko ndani ama la. Hayo maelezo yako yote marefu hayana maana yoyote. Katiba nchi hii itatekelezwa tu iwapo rais anataka na si vinginevyo.

Mfano mrahisi kuwa katiba nchi hii ni kama gazeti la udaku, kuna siku mchana wa saa 7, Magufuli alipokea wanaccm kwenye kamisheni ya jeshi huko Arusha, huku jeshi likiwa limetengwa kabisa kikatiba na mambo ya siasa. Haya yalikuwa yanafanyika mbele ya CDF, tena akiwa na tabasamu zito! Katika mazingira hayo kuna katiba au gazeti la udaku? Hayo maelezo yako yote kwenye huu uzi, nimeyaona ni upuuzi kama upuuzi mwingine.
 
Na hapo ameshateuwa ma DC wake wakurugenzi wake hapo ndipo watakapojua
Mbunge gani anataka bunge livunjwe? Wakishaingia hutawasikia maana wakileta ujinga Rais anavunja bunge tunarudi kwenye uchaguzi wa wabunge na yeye ndiye anasimamia uchaguzi. Thubutuuuuu!
 
Hataweza kufanya hayo maana bunge litakuwa limesha mu impeanch. Na katiba yetu haimuruhusu kuunda serikali yake pekee. Katiba inamtaka Waziri Mkuu atoke kwenye chama chenye wabunge wengi na nusu ya mawaziri watoke kwenye chama chenye wabunge wengi. Na bunge litalapo mu impeanch rais wa aina hiyo haruhusiwi kuwa mgombea urais tena. Huu ndiyo ukweli kwa mjibu wa katiba ndugu yangu, utake usitake.
 
Hivi wewe kwa akili yako unadhani uchaguzi ukirejewa chini ya serikali ya chadema na tume huru ya uchaguzi, ccm itashinda hata majimbo 20? Thubuutu.
 
Hii kazi rahisi sana. Kama mimi ni Rais halafu najiona nina wabunge wachache ninanunua wabunge wa kutosha. Kama Lumumba walitumia 1.5 trillion kununua, mimi nitatumia trillion 3. Tena pale Hazina nitamweka mtoto wa shangazi kuwa Paymaster General.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…