Dr. Akili naona umefikiria sana na kuuliza maswali unajieleza na kujijibu tena kwa nadharia ya kiuchumi..nasema nadharia ya kiuchumi sababu uchumi huongelea positivity tu negative factors hubaki constant yaani kama hazipo. Sitafanya citation ya vifungu vya katiba kutokana na siasa lakini nakuhakikishia kwa katiba yetu hata Rungwe akishinda Urais wa Nchi ndani ya miezi mitatu tu yaani kabla ya siku mia moja atabadilisha mfumo kuwa wa kwake yeye..utasema watu atawapata wapi..jibu ni kwamba Watanzania njaa kali wanafiki mno..atawapata ambao watatamani kubaki kufaidi tunda la kutawala.Ni sawa kabisa. Rais tuliomchagua akiona kuwa wawakilishi wetu bungeni hawapikiki chungu kimoja, tumempa mamlaka ya kulivunja bunge na kuitisha uchaguzi mkuu wa urais na ubunge. Yaani anarudi kwetu tuamue kama yeye aendelee kuwa rais au hao wawakilishi wetu waendelee kuwa wabunge na tuchague rais wanayeendana nao.
Ndiyo demokrasia yenyewe. Kwa hiyo uchaguzi utakaporudiwa, iwe kwa wabunge wetu kumu impeach rais au kwa rais kuvunja bunge, sisi wenye nchi ndiyo tutaamua nani kati yao hafai kwa kupitia sanduku la kura. Na kwa vyo vyote ccm itatoa tena wabunge zaidi ya theluthi mbili ya wabunge wote bungeni. Huu ndiyo ukweli kwa hali yetu. Hivi vyama vingine bado vichanga sana kuweza kupata wabunge wa kutosha. Hivyo tukichagua rais kutoka vyama hivyo tutakuwa tunapoteza muda na pesa bure kwani uchaguzi mkuu mpya utabidi ufanyike. Tutake tusitake uchaguzi mkuu utabidi urudiwe. Hadi sasa ccm ina wabunge tayari 18 kibindoni, kiasi ambacho ndiyo chadema na ukawa ilipata kwenye uchaguzi mkuu wa 2015. Mwaka huu ukawa haipo, imebaki kugawana hiyo 10% itakayoachwa na ccm kwa vyama vyote vya upinzani. Na kwa ukweli rais hatatoka chadema, ndiyo maana Mbowe akawa mjanja na kujitoa kugombea nafasi hiyo. Akaamua kujaribu karata yake jimbo la Hai ambako ana 30% chance ya kushinda. Huko kwenye urais chance ya kushinda ni 0%. Mwamba analijua hilo.
Rungwe natolea mfano tu atabadili uongozi wa tume ya uchaguzi na kuwaweka watu wake ambao kama sasa tu watamtangaza tena kuwa Rais "matumizi sahihi ya DOLA" atabadili wasaidizi wa uchaguzi kwa kuamrisha kuteua watu nje ya wakurugenzi katika manispaa wamsaidie kufanya fojari zake. Hapa sasa ndugu yangu ndio CHAUMA kitapata viti zaidi ya theluthi na wewe Dr. Akili ukiwemo si ajabu..si unataka kula na kura pia japo sasa wajinasibu kuwa Mwana CCM nguli "Unafiki na madaraka". Kwa katiba hii ambayo hata Muasisi wa Uhuru wa Nchi hii alituonya inampa madaraka Rais kuwa Mungu Mtu. Anateuwa bila kushauriwa na hata akishauriwa anahiyari kukubali ama kukataa.
Kwa leo naishia hapo Dr. Akili. Ila kwa ufupisho tu akichaguliwa wa vyama Mbadala basi Rais atatafuta safu yake, ataibadili, atavunja Bunge ataitisha uchaguzi atashinda viti vingi tu kiuhalali ama la..kama tulivyopitishwa bila kupigwa awamu hii..then anatawala kwa ubweche na hatabadili KATIBA kamwee. 😎😎