Ukweli uliofichwa: Divai aliyotengeneza Yesu haikuwa ya kulevya

Ukweli uliofichwa: Divai aliyotengeneza Yesu haikuwa ya kulevya

Katika kitabu cha Yohana 2:1-25 kuna habari ya muujiza alioufanya Yesu wa kubadili maji kuwa divai - wakati wa arusi ya Kana. Hiyo divai aliyotengeneza Yesu, ilikuwa non-alcoholic; haikulewesha. Huu ni ukweli ambao shetani hapendi uujue ili uangamie kwa dhambi ya ulevi. Twende pamoja sasa nikufichulie ukweli wenyewe.

Watu wamekuwa wakitumia Andiko hilo kuhalalisha unywaji wa pombe. Hebu leo tujifunze sababu zinazoonyesha wazi kuwa divai aliyotengeneza Yesu haikuwa pombe(kileo).

Kulingana na muktadha, neno “divai” katika Biblia linamaanisha ama:
1. Juisi ya zabibu isiyo na kilevi(non-alcoholic) au
2. Pombe

Mstari wenye maana ya kwanza ya divai upo katika Isaya 65:8. Huo mstari unazungumzia juisi mpya ya zabibu, isiyo na alcohol.

“BWANA asema hivi, Kama vile divai mpya ipatikanavyo katika kichala, na mtu mmoja husema, usikiharibu kwa maana mna baraka ndani yake...”


Katika Mithali 20:1 tunasoma maana ya pili ya divai:
"Divai huleta dhihaka na kileo huleta ugomvi; Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima.”

Katika andiko hilo "divai' inamaanisha mvinyo au pombe(alcohol).

Yesu alitengeneza aina ya kwanza ya divai isiyolewesha. Kwanini? Kwa sababu kama angetengeneza pombe, asingesema:
“Wala msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi.”(Waefeso 5:18)

Yesu asiye na dhambi, asingeweza kutengeneza kinywaji kitakachowafanya watu waanguke dhambini. Divai aliyotengeneza Yesu ilikuwa mpya, tamu, na yenye baraka—sio ya kulevya.

Kama ile divai ingekuwa pombe, Yesu asingesema:
"Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wezi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi."(1Kor 6:9-10)

So dear brother/sister, don’t be fooled—Jesus never endorsed drinking alcohol.
Divai? Maana ya divai ni kitu gani?
Hadi leo Wayahudi wanakunywa divai wakati wa Pasaka katika utaratibu ule ule alioufanya Yesu. Hiyo divai haina kilevi?
 
Ile ilikuwa ni juisi ya mzabibu, wine inatokea baada ya kukaa muda mrefu. Ile ilitengenezwa na kunywewa palepale.
Shida ya kukariri mambo, unazungumza kama vile ulikuwepo....
Divai au mvinyo ni "UTAMADUNI" wa myahudi.... (Elewa maana ya UTAMADUNI). Hadi Leo hii Wayahudi wanapoimaliza sabato huandaa mlo maalum na "MVINYO/DIVAI"
 
Safi sana ndugu yangu Otorong'ong'o ,
Umeibua point inayowachanganya watu wengi.

Iko hivi: Biblia ya Kiswahili imetafsiriwa kutoka kwenye lugha za asili.

Kwa Kiswahili, neno “divai,” kwa walio wengi linamaanisha kileo. Lakini katika Biblia ya Kiebrania, neno lililotumika ni "yayin." Neno hilo linamaanisha aina tofauti za juisi ya zabibu—iwe mbichi, iliyochemshwa, au iliyochachuka. Zote zinatumia jina moja tu(yayin). Muktadha wa matumizi ya jina hilo ndio unaotofautisha aina ya juisi, sio jina lenyewe. Ndio sababu katika Yohana 2:10 yametumika maneno "divai njema" kuitofautisha divai ya Yesu na aina nyingine za divai yenye kilevi.

Katika maandiko ya mwanzo, watu waliweka juisi ya zabibu kwenye viriba na kuichemsha ili isiweze kuchacha—bado waliiita "yayin"(divai). Pia, katika baadhi ya maandiko, divai mpya (new wine) ilikuwa tu juisi ya zabibu iliyotolewa kutoka shambani. Hivyo basi, sio kila palipoandikwa “divai” panamaanisha kinywaji chenye kilevi kama unavyoelewa wewe.

Labda mfano unaokaribiana na maelezo hayo ni neno "maziwa." Maziwa yanaweza kuwa ya moto, ya baridi, yaliyochacha, ya mgando au fresh. Jina ni lile lile, lakini hali ya maziwa inategemea muktadha.

Narudia tena, Yesu hawezi kutengeneza kinywaji chenye kuwafanya watu walewe halafu aseme kwamba walevi hawataurithi ufalme wa Mungu.
1 Kor 6:9-11
"Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi."

Mpaka hapo hakuna point inayohalalisha unywaji wa pombe. Okay?
Hivi maandiko ya "Wakorinto".... "Waefeso".... "Mithali".... Ni maneno ya Yesu??? Naona umekariri "Yesu" anasema.... "Yesu" anasema....
 
Bado Sana Kuelewa Maandiko.


Nipe Tofauti ya Divai Aliyokunywa Nuhu mara baada ya Kuokol3wa gharikani na Aliyotengeneza Masihi Yesu.

Pili Kumbukq Maandiko yote uliyoyaweka Yamezungumzia Ulevi na si Unywaji wa Divai.

Na Andiko La Harusi Mjini Kana Halitumiki Kuhalalisha Ulevi, Bali Utukufu wa Muujiza Wa Bwana Wetu Yesu Masiha.
Ndiyo maana wakina kiranga hizi mambo hawazishadadii
 
Katika kitabu cha Yohana 2:1-25 kuna habari ya muujiza alioufanya Yesu wa kubadili maji kuwa divai - wakati wa arusi ya Kana. Hiyo divai aliyotengeneza Yesu, ilikuwa non-alcoholic; haikulewesha. Huu ni ukweli ambao shetani hapendi uujue ili uangamie kwa dhambi ya ulevi. Twende pamoja sasa nikufichulie ukweli wenyewe.

Watu wamekuwa wakitumia Andiko hilo kuhalalisha unywaji wa pombe. Hebu leo tujifunze sababu zinazoonyesha wazi kuwa divai aliyotengeneza Yesu haikuwa pombe(kileo).

Kulingana na muktadha, neno “divai” katika Biblia linamaanisha ama:
1. Juisi ya zabibu isiyo na kilevi(non-alcoholic) au
2. Pombe

Mstari wenye maana ya kwanza ya divai upo katika Isaya 65:8. Huo mstari unazungumzia juisi mpya ya zabibu, isiyo na alcohol.

“BWANA asema hivi, Kama vile divai mpya ipatikanavyo katika kichala, na mtu mmoja husema, usikiharibu kwa maana mna baraka ndani yake...”


Katika Mithali 20:1 tunasoma maana ya pili ya divai:
"Divai huleta dhihaka na kileo huleta ugomvi; Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima.”

Katika andiko hilo "divai' inamaanisha mvinyo au pombe(alcohol).

Yesu alitengeneza aina ya kwanza ya divai isiyolewesha. Kwanini? Kwa sababu kama angetengeneza pombe, asingesema:
“Wala msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi.”(Waefeso 5:18)

Yesu asiye na dhambi, asingeweza kutengeneza kinywaji kitakachowafanya watu waanguke dhambini. Divai aliyotengeneza Yesu ilikuwa mpya, tamu, na yenye baraka—sio ya kulevya.

Kama ile divai ingekuwa pombe, Yesu asingesema:
"Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wezi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi."(1Kor 6:9-10)

So dear brother/sister, don’t be fooled—Jesus never endorsed drinking alcohol.
Mimi nilkuwapo mkuu, tulilewa sana na ndiyo maana yule mkuu wa meza alimkaripia yule bwana harusi kwa kuiweka mwisho hiyo divai nzuri! Halafu hivyo vifungu unavyonukuu siyo maneno ya Yesu hayo bali ni ya Mtume Paulo wakati anawaandikia nyaraka hao Waefeso na Wakorintho.
 
Watu hunywa pombe Ili walewe!
Kushiba sana pia ni dhambi kadiri ya maandiko....Je! watu hula ili washibe sana wamkosee Nyumba???

Epuka kujiabisha kwenye Karne hii AI .....Reasoning ndogo kama hii inakushinda
 
Divai? Maana ya divai ni kitu gani?
Hadi leo Wayahudi wanakunywa divai wakati wa Pasaka katika utaratibu ule ule alioufanya Yesu. Hiyo divai haina kilevi?
Nimeeleza aina za divai. Tafadhali soma tena uzi.
 
Mimi nilkuwapo mkuu, tulilewa sana
Ulikuwepo miaka 2000+ iliyopita? Kwanini unafanya mzaha na dhambi ya uongo? Hujui kuwa waongo hawataurithi ufalme wa Mungu?
Halafu hivyo vifungu unavyonukuu siyo maneno ya Yesu hayo bali ni ya Mtume Paulo wakati anawaandikia nyaraka hao Waefeso na Wakorintho.
2 Tim 3:16-17
"Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki."
 
Ile Sherehe ya Kana haikuwa ya Kidini:

Kama huku kwetu ndoa inafungwa Kanisani na baada ya hapo mambo ya mila na desturi yanaendelea:

Yaani ulete soda kwenye sherehe ya harusi halafu mzee wa meza aifurahie:.

Pia soda haina ubora wa nyingine iwe tamu na nyingine iwe dhaifu, soda zote utamu unafanana:

Kawaida katika sherehe kwanza inaletwa pombe iliyo bora kiviwango:

Watu wakisha changamka ndio inaletwa yenye ubora hafifu:
Hiyo ni baada ya pombe bora kumalizika:
 
Uliionja ukagundua haileweshi? Ile ilikuwa ni divai (wine) siyo juice. Kumbuka kuwa kunywa pombe siyo dhambi; na wala kulewa siyo dhambi pia.

Dhambi ni matendo kumi yaliyoandikwa kwenye kitabu cha Kutoka (Exodus) Sura ya 20 Aya ya tatu hadi ya kumi na 17 (Exodus 20:3-17) . Hakuna ilipoandikwa kuwa usile nguruwe au usinywe pombe au hata kusema usilewe

  1. Usiwe na miungu mingine ila mimi. Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
  2. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami nawarehemu maelfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.
  3. Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako, maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.
  4. Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.
  5. Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.
  6. Usiue.
  7. Usizini
  8. Usiibe
  9. Usimshuhudie jirani yako uongo
  10. Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala chochote alicho nacho jirani yako
 
Ulikuwepo miaka 2000+ iliyopita? Kwanini unafanya mzaha na dhambi ya uongo? Hujui kuwa waongo hawataurithi ufalme wa Mungu?

2 Tim 3:16-17
"Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki."
Sasa kama wewe umetudanganya sisi tufanyeje sasa? Walevi mpaka walitaka kumpiga bwana harusi wewe unasema ilikuwa haileweshi?
 
Pombe ya siku ile ilikuwa ya viwango bora sana:
Ila aliyo itengeneza Yesu ilikuwa na ubora zaidi:
Yaani ilikuwa tamu kupita Safari Lager:
Watu walikunywa na kufurahi:
Soda au Juice haijawahi kumfurahisha mtu, labda watoto wadogo:
 
Yani wewe utoje zako kyela uje utufundishe bible🤣🤣?!
 
Kama ile divai ingekuwa pombe, Yesu asingesema:
"Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wezi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi."(1Kor 6:9-10)
Kitabu cha wakorinto aliandika Paulo au yesu..?
 
Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wezi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi."(1Kor 6:9-10)
Amina mtumishi wa Bwana
 
Back
Top Bottom