Ukweli uliofichwa: Divai aliyotengeneza Yesu haikuwa ya kulevya

Ukweli uliofichwa: Divai aliyotengeneza Yesu haikuwa ya kulevya

Yesu asingeweza kutengeneza divai ya kuwafanya watu wapige yowe, wagombane na kupata majeraha.

Mithali 23:29-35
"Ni nani wapigao yowe? Ni nani wenye huzuni? Ni nani wenye ugomvi?
Ni nani walalamikao? Ni nani wenye majeraha bila sababu? Ni nani wenye macho mekundu? Ni wale ambao hawabanduki penye divai, wale wakaao chonjo kuonja divai iliyokolezwa. Usiitamani divai hata kwa wekundu wake, hata kama inametameta katika bilauri, na kushuka taratibu unapoinywa. Mwishowe huuma kama nyoka; huchoma kama nyoka mwenye sumu. Macho yako yataona mauzauza, moyo wakoutatoa mambo yaliyopotoka. Utakuwa kama mtu alalaye katikati ya bahari, kama mtu alalaye juu ya mlingoti wa meli. Utasema, “Walinichapa, lakini sikuumia; walinipiga, lakini sina habari..."


Yesu asingetengeneza divai ya kuwafanya watu wapatwe na madhara hayo.
Kasome tafsiri asili ya kigiriki ambayo ndiyo origin ya Agano jipya utajua hiyo Divai iliyobora ni ipi. Kigiriki ni Oivoc au Oinos maana yake alkoholic, na maandiko ya kigiriki yanatamka wazi kuwa waliishiwa oivoc au oinos na si ole oivoc ambayo ndio juice. Juice sio divai au wine. Juice ni juice tuu.
Kwa wanaoishi Dodoma wanaelewa zaidi maana hizo process zinafanyika sana sana huku. Wine iliyobora ni ile iliyokaa muda mrefu, kuna wine zimevundikwa kwa takribani miaka 50 mpaka 100,uliza kiwa kilichokuwa kinaitwa Dodoma wine ndio utajua.
Wine iliyokaa muda mrefu ni bora na ghari sana sana.
Hivyo usipotoshe maandiko kwa sababu ya interest zako binafsi na ubinafsi uliokithiri kwako.
Mimi sinywi kileo cha aina yeyote na si sapoti mtu yeyote anywe kwa sababu ya mmomonyoko wa kimaadili ya watu kunywa ili walewe(satanic verse).
Lakini siwezi kupingana na maandiko eti kisa watu wanalewa!!?
Basi viungo vya uzazi vipigwe marufuku kwa kuwa watu wazini ovyo ovyo. Yeyote mwenye kiungo cha uzazi ni dhambi akikate akitupe..
Visu vinatumika kuulia watu vipigwe marufuku, sumu zipigwe marufuku, magari yanaua watu yapigwe marufuku... Vitu ndivyo vinavyotenda dhambi??? Au mtumiaji ndiye anaweza kutumia kutendea dhambi???
 
Katika kitabu cha Yohana 2:1-25 kuna habari ya muujiza alioufanya Yesu wa kubadili maji kuwa divai - wakati wa arusi ya Kana. Hiyo divai aliyotengeneza Yesu, ilikuwa non-alcoholic; haikulewesha. Huu ni ukweli ambao shetani hapendi uujue ili uangamie kwa dhambi ya ulevi. Twende pamoja sasa nikufichulie ukweli wenyewe.

Watu wamekuwa wakitumia Andiko hilo kuhalalisha unywaji wa pombe. Hebu leo tujifunze sababu zinazoonyesha wazi kuwa divai aliyotengeneza Yesu haikuwa pombe(kileo).

Kulingana na muktadha, neno “divai” katika Biblia linamaanisha ama:
1. Juisi ya zabibu isiyo na kilevi(non-alcoholic) au
2. Pombe

Mstari wenye maana ya kwanza ya divai upo katika Isaya 65:8. Huo mstari unazungumzia juisi mpya ya zabibu, isiyo na alcohol.

“BWANA asema hivi, Kama vile divai mpya ipatikanavyo katika kichala, na mtu mmoja husema, usikiharibu kwa maana mna baraka ndani yake...”


Katika Mithali 20:1 tunasoma maana ya pili ya divai:
"Divai huleta dhihaka na kileo huleta ugomvi; Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima.”

Katika andiko hilo "divai' inamaanisha mvinyo au pombe(alcohol).

Yesu alitengeneza aina ya kwanza ya divai isiyolewesha. Kwanini? Kwa sababu kama angetengeneza pombe, asingesema:
“Wala msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi.”(Waefeso 5:18)

Yesu asiye na dhambi, asingeweza kutengeneza kinywaji kitakachowafanya watu waanguke dhambini. Divai aliyotengeneza Yesu ilikuwa mpya, tamu, na yenye baraka—sio ya kulevya.

Kama ile divai ingekuwa pombe, Yesu asingesema:
"Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wezi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi."(1Kor 6:9-10)

So dear brother/sister, don’t be fooled—Jesus never endorsed drinking alcohol.
Kwanza umepotoshwa ...kama unasema yesu ni mungu jua tu kuwa mungu si chini ya dhambi yoyote hivyo yesu kufanya pombe siyo shida kwa sababu yeye ndiye aliye umba pombe ...ni kipi kikuu... kufanya pombe au kuumba pombe ....mungu ndiye mwenye kuharamisha kitu chochote au kuharalisha kitu chochote . SASA JIBU NI KWAMBA.....👉 YESU ALIFANYA POMBE SIYO JUISI USHAHIDI NI YULE MGENI ALIVYO SEMA ....KUWA WATU WAKICHA KULEWA NDIYO ULETWA,ILIYO DHAIFU ILA WEWE UMELETA NJEMA HATA SASA....PIA USHAHIDI NI MANENO YA YESU ALIYO SEMA KUWA ...👉 YOHANA ALIKUJA ALI WALA ANYWI MKASEMA ANA PEPO MIMI NIMEKUJA NAKULA NA NAKUNYWA MKASEMA MLEVI NA MLAFI RAFIKI YAO WATOZA USHURU.
 
Watu wanashindwa kutofautisha kati ya divai na mvinyo. Divai ikihifadhiwa kwa muda mrefu ndo inakuwa mvinyo.
Wine ni nini
1000106414.jpg
 
Kitabu cha Sira hakikubaliki. Hakina uvuvio wa Roho Mtakatifu(not divinely inspired). Wanaokitumia ni wale tu walioko msibani sasa - ameondoka Mkuu wao😢
Anayekubali vitabu ni nani?
Anayetoa uvuvio ni nani?
 
Mathayo 11v18-19 Maana Yohama alikuja hali wala hanywi wakasema ana pepo
Mwana wa Adamu alikuja akila na kunywa wakasema mlafi huyu na mlevi .........

Luka 7v34 Mwana wa Adamu amekuja,anakula na kunywa nanyi mwasema ,Tazama mlafi huyu na mnywaji wa divai ,rafiki wao watoza ushuru na wenye dhambi ......

Sikia hii
Mathayo 15v16-17 Yesu akasema hata sasa ninyi nanyi mngali hamna akili ?Hamjafahamu bado ya kuwa kila kiingiacho kuinyani hupita tumboni kikatupwa chooni?

Marko 7v14-15 Akawait makutano tena, akawaambia, Nisikieni nyote na kufahamu .Hakuna kitu kilicho nje ya mtu kikimwingia chaweza kumtia unajisi(kumfanya kuwa na dhambi ),bali vile vimtokavyo .......

Siyo kwamba natetea pombe,ila kunywa pombe siyo dhambi
na usimtetee Yesu ,
Yesu alitamka tu na maji yakaw pombe

Hivi vifungu vya Biblia Walokole Huwa Wanavikwepa hawafundishani..! Bali Wanatafuta vipande vichache vichache Kwenye Biblia vya Kuja kubishania..!

Biblia kimsingi haijawahi kufundisha kuwa Divai ni dhambi Bali inasisitiza utumiaji Wa KIASI. Zab 104 : 13-15, Muhubiri : 9: 7. Timotheo Wa Kwanza 3 : 8.

Tito 2 : 3 vivyo hivyo na Wazee Wa Kike wawe na mwenendo Wa Utakatifu , wasiwe wasingiziaji, wasiwe Wenye kutumia mvinyo NYINGI,Bali wafundishao mema...!

Tunaweza kuona hadi bibi zetu Wa kike wanasisitizwa wasitumie mvinyo NYINGI..! Walokole msipotoshe maandiko , ombeni ufafanuzi.
 
Kama inakutibu, si pombe tena, ni dawa! Pia sikujua kuwa watu wanakwenda vilabuni kunywa pombe ili kutibiwa. Najua tu vituo vya afya. Mengine ni mtazamo wako na nitauheshimu hata nisipokubaliana nao. Nitaendelea kuamini wasemacho madaktari bingwa.

Nikushauri tu kuwa ni uungwana na busara kuheshimu maoni ya wengine badala ya kuwaita waongo maana sote tuna uelewa na mitazamo tofauti.
A little bit exaggeration of my view point. Pole, never meant to hurt your feelings.
 

Biblia katika agano jipya iliandikwa kwa lugha hii. Hiyo ni Yohana 2:1-12
---

📖 ΙΩΑΝΝΗΣ 2:1–12 (Greek Text)

1 Καὶ τῇ ἡμέρᾳ τῇ τρίτῃ γάμος ἐγένετο ἐν Κανᾷ τῆς Γαλιλαίας, καὶ ἦν ἡ μήτηρ τοῦ Ἰησοῦ ἐκεῖ·
2 ἐκλήθη δὲ καὶ ὁ Ἰησοῦς καὶ οἱ μαθηταὶ αὐτοῦ εἰς τὸν γάμον.
3 Καὶ ὑστερήσαντος οἴνου λέγει ἡ μήτηρ τοῦ Ἰησοῦ πρὸς αὐτόν, Οἶνον οὐκ ἔχουσιν.
4 Καὶ λέγει αὐτῇ ὁ Ἰησοῦς, Τί ἐμοὶ καὶ σοί, γύναι; οὔπω ἥκει ἡ ὥρα μου.
5 Λέγει ἡ μήτηρ αὐτοῦ τοῖς διακόνοις, Ὅ τι ἂν λέγῃ ὑμῖν ποιήσατε.
6 Ἦσαν δὲ ἐκεῖ λίθιναι ὑδρίαι ἓξ κεῖμεναι κατὰ τὸν καθαρισμὸν τῶν Ἰουδαίων, χωροῦσαι ἀνὰ μετρητὰς δύο ἢ τρεῖς.
7 Λέγει αὐτοῖς ὁ Ἰησοῦς, Γεμίσατε τὰς ὑδρίας ὕδατος. Καὶ ἐγέμισαν αὐτὰς ἕως ἄνω.
8 Καὶ λέγει αὐτοῖς, Ἀντλήσατε νῦν καὶ φέρετε τῷ ἀρχιτρικλίνῳ. Οἱ δὲ ἤνεγκαν.
9 Ὡς δὲ ἐγεύσατο ὁ ἀρχιτρίκλινος τὸ ὕδωρ οἶνον γεγενημένον, καὶ οὐκ ᾔδει πόθεν ἐστίν, οἱ δὲ διάκονοι ᾔδεισαν οἱ ἠντληκότες τὸ ὕδωρ, φωνεῖ τὸν νυμφίον ὁ ἀρχιτρίκλινος
10 καὶ λέγει αὐτῷ, Πᾶς ἄνθρωπος πρῶτον τὸν καλὸν οἶνον τίθησιν, καὶ ὅταν μεθυσθῶσιν, τὸν ἐλάσσω· σὺ τετήρηκας τὸν καλὸν οἶνον ἕως ἄρτι.
11 Ταύτην ἐποίησεν ἀρχὴν τῶν σημείων ὁ Ἰησοῦς ἐν Κανᾷ τῆς Γαλιλαίας, καὶ ἐφανέρωσεν τὴν δόξαν αὐτοῦ· καὶ ἐπίστευσαν εἰς αὐτὸν οἱ μαθηταὶ αὐτοῦ.
 
1 Tim 5 : 23

Tokea sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yakupatayo mara kwa mara
Mvinyo ulitumika kama dawa kwa Timotheo, na si kunywa tu. Kama valium ambavyo hutumika kama nusu kaputi kwenye upasuaji. Si kama dawa za kulevya.
 
DR Mambo Jambo pitia hapa...

Kumbe ipo tofauti ya Divai na mvinyo ?
SIku zote Huwa nasema Dini ni Manipulative Tools Mojawapo kwenye Matrix Tuliyopo..

Utetezi mwingi unafanywa kwenye Mambo ambayo Yako wazi na Hayahitaji hata Elimu kubwa Kuyajua..

Yaani Ni kwamba watu wanaamini Ukitumia Manipulative ways kwa Kugeuza maneno basi utaweza Kuwateka Watu.
La hasha Watu husoma na kufahamu ukweli..
Ila Si kwamba Huwezi kuteka Watu unaweza Kuteka Wale wasio kuwa na Elimu pia...

Alichofanya Setfree ni Kutumia Maneno ya Kiswahili kujaribu kuwaaminisha Watu kwa Kuwamanipulate yaani Kugeuza Akili zao ili waamini Kile anachotaka kuwaaminisha..

Sasa twende kwenye Mada..

Je Divai na Mvinyo Ni Tofauti? (Nadhani ndo Mjadala Upo Hapa)

Kama utakuwa Uliwahi Kusoma Kiswahili Au Aina za Maneno Utakuwa Unafahamu Aina Za Maneno zilizokuwa Zinaitwa Visawe..(au kwa Kingereza Synonyms)..

VIsawe ni aina ya Maneno yenye Maana Sawa yanayotumika kuelezea maana Moja japo yanaweza kutumika katika muktadha tofauti wa maelezo aidha kwenye maandishi au kwenye maongezi..

kwa Mfano:- Haraka na Upesi, Furaha na Shangwe, Hasira na Ghadhabu, Giza na Kiza, Maandiko na Maandishi, Kazi na Shughuli, Hofu na Uoga, n.k

Sasa Mvinyo ni Kisawe cha Divai

Maana Yake Sehemu zote walizotumia Neno Divai Pia Wanaweza Kutumia Neno Mvinyo na Sehemu zote walizotumia Neno Mvinyo wanaweza Kutumia Neno Divai..(Nitaonyesha)..

Tuanze na Aya aliyotoa

"Yohana 2:3

"Hata divai ilipowatindikia, mamaye Yesu akamwambia, Hawana divai. "

"And when they wanted wine, the mother of Jesus saith unto him, They have no wine."

Aya aliyotoa Divai Inakuwa Mentioned Kwenye Biblia Kama Wine..

Sasa twende Kigiriki Kabla Hatujatoa Conclusion..

Yohana 2:3 (Ἰωάννης 2:3)

Καὶ ὑστερήσαντος οἴνου λέγει ἡ μήτηρ τοῦ Ἰησοῦ πρὸς αὐτόν, Οἶνον οὐκ ἔχουσιν.

Na Kwa matamshi..

Kai hysterēsantos oinou legei hē mētēr tou Iēsou pros auton, Oinon ouk echousin.


Sasa ushauri wangu Aende akatafute Maana Ya neno Oinon au οἶνος (oinos) la Kigiriki Maana Yake ni nini?

Namsaidia Neno οἶνος (oinos), Lililotumiwa na mwandishi wa Yohana kwenye maandishi ya Asili ya Kigiriki auu Kiyunani linamaanisha Fermented Wine (Na hili Pia anahitaji Kuelezwa maana Yake?)
Screenshot_20250422_054325_Chrome.jpg



Je Mvinyo na yenyewe ina jina Tofauti Na Hilo la Wine au οἶνος (oinos) kwa Ligha ya Kigiriki Au Ni majina Sawa kwa Kingereza ba Kigiriki ila Tifauti kwenye Kiswahili??

Tuanze na Timotheo Tutamalizia Wengine..

1 Timotheo 5:23
"Tokea sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yakupatayo mara kwa mara."

"Drink no longer water, but use a little wine for thy stomach's sake and thine often infirmities."


Twende kwenye Lugha Asilia sasa Ya Kigiriki..

1 Timothy 5:23

Μηκέτι ὑδροπότει, ἀλλὰ οἴνῳ ὀλίγῳ χρῶ διὰ τὸν στόμαχόν σου καὶ τὰς πυκνὰς σου ἀσθενείας.


Inavyotamkwa!

"Mēketi hydropotei, alla oinō oligō chrō dia ton stomachon sou kai tas pyknas sou astheneias."

"Drink no longer water, but use a little wine for thy stomach's sake and thine often infirmities."


Umeona Neno Oino pale Juu likiw Linamaanisha Mvinyo na Tumeona Kwenye Yohana wameandika Divai ila Kwenye Kingereza Its Still wine na Kigiriki it still Oinos..

So Watanzania Tulichezewa na Maneno??

So kwa Mimi nimemaliza Maana Naweza Kuandika Mpaka Kesho naomba Kusema hivi..

Nahisi hapo umepata Jibu kuwa Swala sio Mvinyo wala Divai kwa sababu ni kitu kimoja labda Tungeanza Kudiscuss Ile Mvinyo au Ile Divai Ilikuwa na Pombe (Alcohol) hapo itakuwa Good Motive..
 
Yesu asingeweza kutengeneza divai ya kuwafanya watu wapige yowe, wagombane na kupata majeraha.

Mithali 23:29-35
"Ni nani wapigao yowe? Ni nani wenye huzuni? Ni nani wenye ugomvi?
Ni nani walalamikao? Ni nani wenye majeraha bila sababu? Ni nani wenye macho mekundu? Ni wale ambao hawabanduki penye divai, wale wakaao chonjo kuonja divai iliyokolezwa. Usiitamani divai hata kwa wekundu wake, hata kama inametameta katika bilauri, na kushuka taratibu unapoinywa. Mwishowe huuma kama nyoka; huchoma kama nyoka mwenye sumu. Macho yako yataona mauzauza, moyo wako utatoa mambo yaliyopotoka. Utakuwa kama mtu alalaye katikati ya bahari, kama mtu alalaye juu ya mlingoti wa meli. Utasema, “Walinichapa, lakini sikuumia; walinipiga, lakini sina habari..."


Yesu asingetengeneza divai ya kuwafanya watu wapatwe na madhara hayo.
(Ni wale ambao awabanduki kwenye divai ) unajua nini maana ya kuto kubanduka kwenye divai? Maana yake walevi...labda ujui mlevi ni nani ?labda unadhani kulewa ndiyo mlevi ...neno mlevi ni sawa na neno mlafi ......Ulafi kwenye mambo ya chakula ni dhambi na Ulevi kwenye mambo ya pombe ni dhambi .. sasa mlevi na mlafi ni nani ? Mlevi ni mtu ambaye pombe inatawala akili zake na mlafi ni mtu ambaye kula kunatawala akili zake ...hivyo akili inapo tawaliwa na kunywa pombe ndiyo ulevi na akili inapo tawaliwa na kula vyakula huo ni ulafi hivyo watu wasio banduka kwenye pombe ni WALEVI
 
Katika kitabu cha Yohana 2:1-25 kuna habari ya muujiza alioufanya Yesu wa kubadili maji kuwa divai - wakati wa arusi ya Kana. Hiyo divai aliyotengeneza Yesu, ilikuwa non-alcoholic; haikulewesha. Huu ni ukweli ambao shetani hapendi uujue ili uangamie kwa dhambi ya ulevi. Twende pamoja sasa nikufichulie ukweli wenyewe.

Watu wamekuwa wakitumia Andiko hilo kuhalalisha unywaji wa pombe. Hebu leo tujifunze sababu zinazoonyesha wazi kuwa divai aliyotengeneza Yesu haikuwa pombe(kileo).

Kulingana na muktadha, neno “divai” katika Biblia linamaanisha ama:
1. Juisi ya zabibu isiyo na kilevi(non-alcoholic) au
2. Pombe

Mstari wenye maana ya kwanza ya divai upo katika Isaya 65:8. Huo mstari unazungumzia juisi mpya ya zabibu, isiyo na alcohol.

“BWANA asema hivi, Kama vile divai mpya ipatikanavyo katika kichala, na mtu mmoja husema, usikiharibu kwa maana mna baraka ndani yake...”


Katika Mithali 20:1 tunasoma maana ya pili ya divai:
"Divai huleta dhihaka na kileo huleta ugomvi; Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima.”

Katika andiko hilo "divai' inamaanisha mvinyo au pombe(alcohol).

Yesu alitengeneza aina ya kwanza ya divai isiyolewesha. Kwanini? Kwa sababu kama angetengeneza pombe, asingesema:
“Wala msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi.”(Waefeso 5:18)

Yesu asiye na dhambi, asingeweza kutengeneza kinywaji kitakachowafanya watu waanguke dhambini. Divai aliyotengeneza Yesu ilikuwa mpya, tamu, na yenye baraka—sio ya kulevya.

Kama ile divai ingekuwa pombe, Yesu asingesema:
"Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wezi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi."(1Kor 6:9-10)

So dear brother/sister, don’t be fooled—Jesus never endorsed drinking alcohol.
Ila wewe dada unapenda kujitekenya na kujichekesha mwenyewe.
Mimi mkristo pia ila hizo tabia punguza.

Acha kutafakari biblia vile unavyotaka wewe iwe. Divai ilikua na pombe, na hakuna tatizo lolote kwenye hilo.
Vincenzo Jr kweli tusinywe mvinyo kama alivyotuonyesha bwana wetu 😂 😂
 
Back
Top Bottom