Ukweli uliofichwa: Divai aliyotengeneza Yesu haikuwa ya kulevya

Ukweli uliofichwa: Divai aliyotengeneza Yesu haikuwa ya kulevya

Nimeishakuambia Yesu hawezi kutengeneza tungi halafu aseme wapiga tungi hawataurithi ufalme wa Mungu(1 Wakorintho 6:9-10)

Au ulipiga tungi nini, kabla ya kusoma huu uzi? Maana wanaopiga tungi macho yao yanaona mauzauza, kama Maandiko yanenavyo katika Mithali 23:33
View attachment 3311218
Naona mauzauza tu Yesu hakufungua Bar pale Kana aligawa Pombe bure hakuchukua hata 100 ya mtu
 
Sira 31 : 31

Usimkaripie jirani yako kwenye pombe,
wala usimdharau anapofurahia karamu.
Usimwambie neno la kumwonya,
wala usimsumbue kwa kumtaka alipe deni.
 
Sira 31 : 28

Pombe ni kama uhai kwa mtu ukinywa kwa kiasi. Maisha yafaa nini bila pombe? Imeumbwa iwafurahishe watu.
 
Katika kitabu cha Yohana 2:1-25 kuna habari ya muujiza alioufanya Yesu wa kubadili maji kuwa divai - wakati wa arusi ya Kana. Hiyo divai aliyotengeneza Yesu, ilikuwa non-alcoholic; haikulewesha. Huu ni ukweli ambao shetani hapendi uujue ili uangamie kwa dhambi ya ulevi. Twende pamoja sasa nikufichulie ukweli wenyewe.

Watu wamekuwa wakitumia Andiko hilo kuhalalisha unywaji wa pombe. Hebu leo tujifunze sababu zinazoonyesha wazi kuwa divai aliyotengeneza Yesu haikuwa pombe(kileo).

Kulingana na muktadha, neno “divai” katika Biblia linamaanisha ama:
1. Juisi ya zabibu isiyo na kilevi(non-alcoholic) au
2. Pombe

Mstari wenye maana ya kwanza ya divai upo katika Isaya 65:8. Huo mstari unazungumzia juisi mpya ya zabibu, isiyo na alcohol.

“BWANA asema hivi, Kama vile divai mpya ipatikanavyo katika kichala, na mtu mmoja husema, usikiharibu kwa maana mna baraka ndani yake...”


Katika Mithali 20:1 tunasoma maana ya pili ya divai:
"Divai huleta dhihaka na kileo huleta ugomvi; Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima.”

Katika andiko hilo "divai' inamaanisha mvinyo au pombe(alcohol).

Yesu alitengeneza aina ya kwanza ya divai isiyolewesha. Kwanini? Kwa sababu kama angetengeneza pombe, asingesema:
“Wala msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi.”(Waefeso 5:18)

Yesu asiye na dhambi, asingeweza kutengeneza kinywaji kitakachowafanya watu waanguke dhambini. Divai aliyotengeneza Yesu ilikuwa mpya, tamu, na yenye baraka—sio ya kulevya.

Kama ile divai ingekuwa pombe, Yesu asingesema:
"Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wezi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi."(1Kor 6:9-10)

So dear brother/sister, don’t be fooled—Jesus never endorsed drinking alcohol.
DR Mambo Jambo pitia hapa...

Kumbe ipo tofauti ya Divai na mvinyo ?
 
Sira 31 : 28

Kunywa pombe wakati wake na kwa kiasi,
kwaleta shangwe moyoni na furaha rohoni.
Kitabu cha Sira hakikubaliki. Hakina uvuvio wa Roho Mtakatifu(not divinely inspired). Wanaokitumia ni wale tu walioko msibani sasa - ameondoka Mkuu wao😢
 
Moja ya vitabu 72 vya Biblia Takatifu, Hekima ya Yoshua bin sira
Madhehebu ya Kiprotestanti, yanatambua vitabu 66 tu, ndivyo vilivyoandikwa kwa uongozi wa Roho Mtakatifu. Vitabu 66 ndivyo vinavyokubalika kama Maandiko Matakatifu ya kweli(Biblia). Hicho cha Sira ni cha wapiga tungi tu.
 
Kiasi, kiasi, kiasi! Hakuna jambo ukalifanya kwa kuzidisha lisikupeleke ukafanya dhambi. Msimtilie Yesu maneno yenu kwa kusindwa kuielewa biblia. . Kunywa alcohol ufurahie maisha, kuwa tu na KIASI! Mbona hamsemi Paul alipomshauri Timotheo anywe pombe kwa kiasi kwa ajili ya afya yake? Usisahau Biblia na maana zake ni zilezile toka Mwanzo hadi ufunuo, ikikupiga chenga tafuta maana vizuri kwengine. Yesu hakuja kuitengua torati, bali kuikamilisha.
 
Kitabu cha Sira hakikubaliki. Hakina uvuvio wa Roho Mtakatifu(not divinely inspired). Wanaokitumia ni wale tu walioko msibani sasa - ameondoka Mkuu wao😢
Akili yako iko sawa kweli? Biblia ina vitabu 72 vilivyoandikwa, kuchambuliwa kwa umakini na Kanisa, Wewe ni nani uje uchambue hiki kinafaa kile hakifai wakati hata hivyo unavyoona vinafaa pia umepewa na Kanisa?

Unaposema wako msibani unamaana gani? Kwamba Pope amefariki? Wewe hautafariki? Kwamba hiyo ndiyo umeona point ya kukebehi? Kiti cha Petro - Mtume kipo,Kilikuwepo na kitazidi kuwepo! Mpaka Yesu atakaporudi kuchukua Kanisa lake
 
Madhehebu ya Kiprotestanti, yanatambua vitabu 66 tu, ndivyo vilivyoandikwa kwa uongozi wa Roho Mtakatifu. Vitabu 66 ndivyo vinavyokubalika kama Maandiko Matakatifu ya kweli(Biblia). Hicho cha Sira ni cha wapiga tungi tu.
Protestant no mtoto wa Catholic, Hajui wala haelewi hiyo Biblia iliandaliwaje, Halafu mnakuja kuchambua vitabu vyenu 66 mnavyoona vinawafaa 😀😀 haujasoma Sylabus nzima alafu unasema upo konki, Uko serious unataka kwenda mbinguni kweli??
 
Kila kinywaji kina kileo inatofautiana tu kiwango. Vingine vina 0% na vingine vina 1% nk...

Pombe sio dhambi ila ni mzizi wa dhambi. Kwa maana ya kuwa ukidumu kwa muda kwenye huu mzizi basi utachipusha mmea (dhambi)..

Halafu pombe haina shida ila akili ya mtu mshenzi ndo ina shida. Pombe hufanya akili yako iwe wazi mbele ya kadamnasi.

Maisha yafaa nini bila pombe?...
 
Mathayo 11v18-19 Maana Yohama alikuja hali wala hanywi wakasema ana pepo
Mwana wa Adamu alikuja akila na kunywa wakasema mlafi huyu na mlevi .........

Luka 7v34 Mwana wa Adamu amekuja,anakula na kunywa nanyi mwasema ,Tazama mlafi huyu na mnywaji wa divai ,rafiki wao watoza ushuru na wenye dhambi ......

Sikia hii
Mathayo 15v16-17 Yesu akasema hata sasa ninyi nanyi mngali hamna akili ?Hamjafahamu bado ya kuwa kila kiingiacho kuinyani hupita tumboni kikatupwa chooni?

Marko 7v14-15 Akawait makutano tena, akawaambia, Nisikieni nyote na kufahamu .Hakuna kitu kilicho nje ya mtu kikimwingia chaweza kumtia unajisi(kumfanya kuwa na dhambi ),bali vile vimtokavyo .......

Siyo kwamba natetea pombe,ila kunywa pombe siyo dhambi
na usimtetee Yesu ,
Yesu alitamka tu na maji yakaw pombe
Umemaliza yote. Hawa watu sijui wakoje. Na watakuja na excuse kwenye hilo
 
Back
Top Bottom