Ukweli usemwe: Aliyeharibu nchi hii ni Mwalimu Nyerere kwa kushindwa kuwapa Watanzania Elimu

You have nailed it,Hongera.Kweli nikikumbuka tuliosoma Shule za Serikali enzi za Nyerere Elimu Bure ilikuwa Bure kweli,kusafiri baada ya kufungwa shule unapewa warrant na masurufu( mkate ma orange squash etc) Ili kujikimu njiani,ukirudi toka likizo unakuwa refunded Nauli,Shule vitabu tele na Hata maabara zilikuwa na reagents siyo sayansi ya sikuhizi Shule nyingi ni mwendo wa kukariri tu.Hiyo Aridhi angeenda mwendo wa tamaa wa majirani zetu Kenya wa Familia Moja ya Kenyatta kumiliki 1/3 ya Aridhi ya nchi cjui wengine tungejenga wapi pa kujenga vibanda vyetu
Nyerere aliacha viwanda Kila Mkoa lakini vyote vimekuwa privatized bila tija yoyote,hapo napo pa kumlaumu Nyerere?
Nyerere tumpongeze alifanya kazi yake,na alipoachia inapaswa tuendelee kuchukua hatua na siyo kujiliza kama mfano wa watoto wa kiume wenye deko wanaomlaumu baba yao eti hakuwaachia nyumba za urithi,wakati wapo wengi ambao wamepewa elimu na kujijengea Maisha Yao bila kulilia urithi.
 
Nyerere hakupumzika kwa kupenda bali alifosiwa kupumzika,
 
Utakuta hata ukipewa uongoze mtaa , huwezi! Kuongoza Nchi mnadhani jambo Dogo.

Familia zenu mnashindwa kuziongoza.

Bure kabisa.
 
Utakuta hata ukipewa uongoze mtaa , huwezi! Kuongoza Nchi mnadhani jambo Dogo.

Familia zenu mnashindwa kuziongoza.

Bure kabisa.
Angola mbona wameweza? Walikuwa kwenye vita tangu 1975 mpaka 1991 lakini wanatuzidi uchumi kwa mbali.
 
Ndugu yangu Elimu ndio msingi muhimu wa kujenga taifa.

Katika kauli mbiu yake kuhusu maadui watatu wa taifa ilikuwaje akashindwa kuweka mikakati ya maana katika kufuta ujinga?

Hapa tunaongea reality. Nyerere ali fail kuwapatia watanzania elimu.
TATIZO KUBWA LA NCHI HII SIYO ELIMU.

Ni CENTRALIZATION ya KEKI ya Taifa na hivyo imezaa UCHAWA na UNAFIKI.

Watu wanajitoa akili kwa makusudi tu ili kutafuta UGALI.

Pili, kama maamuzi ya kisiasa ndio unayodhani ni sababu, issue ni kwamba ili kuleta mabadiliko kwa ob psychology unatakiwa ni aidha uunganishe watu kwa kutumia COMMON IDEOLOGY. Aidha DINI au KABILA.

Kenya UKABILA ndio nguvu ya kisiasa. Hata urais unategemea ziadi makabila makubwa mawili yaliyounganisha nguvu.

TZ, CUF sasa ni ACT inatumia sana nguvu ya dini kupata wafuasi.

CCM ya Magufuli ilitumia sana ukabila kuvuna kura za MWANZA na Shinyanga na hivyo hivyio Lowassa wa CHADEMA alitumia ukanda kuvuna kura za Arusha NA kILIMANJARO.

Kiuhalisia ingekuwa kila mtu anakula kwa jasho na watu hawapati vyeo kwa uchawa, AKILI ZA WATU WANGETUMIA VIZURI TU.

Hii iko proved.

KABUDI wa TUME ya WARIOBA ni tofauti na kabudi wa MAGUFULI. Same to KITILA MKUMBO, RIOBA (TBC) NK
 
Hilo sio kosa la Nyerere, ni kazi yenu kuitoa CCM sio mtu aliyeondoka 35yrs ago na kufariki over 20yrs ago. Hizo ni cheap excuses
Nimekuuliza njia unanijibu sio kosa la Nyerere . Unajitoa ufahamu ?
 
Kwahiyo unakiri hamna akili za kutatua changamoto zenu zaidi ya kutegemea akili za Nyerere tu? Sasa naelewa kwanini bandari inauzwa.
Hivi umeelewa swali kweli nililo kuuliza au unajitoa ufahamu ?
 

Hakuna tambo yeyote nimekuonesha ndugu, mimi nilikuwa nakuweka sawa uliposema eti mikataba mibovu ni kwaajili ya lugha, hivyo nilikuwa nakujulisha tu yakuwa, hapo Tanzania, kuna shule za serikali (Ilboru na nyingine za vipaji maalumu) na shule za dini na wana aina tofauti ya waalimu na secondari za kawaida.

Seminary za katoliki nyingi walimu ni mapadre na masister ambao hakuna asiye na degree ama zaidi. Kwahivyo, swala sio lugha.
 
Mimi naona kosa kubwa alilolifanya Nyerere ni utaifishaji wa mali za watu binafsi na kuzifanya za umma kisha kushindwa kuziendesha na hatimaye kufa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…