Ukweli usemwe; huu udongo wa Wasira na Warioba sio wa Dunia hii!!

Dr wa Manesi

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2024
Posts
6,479
Reaction score
4,974
Namuangalia warioba, katika umri wa miaka zaidi ya 80, anaweza kuongea anachoongea kwa mpangolio bila kupoteza kumbukumbu ni jambo la ajabu sana. Nina 40+ tayari nauhisi kabisa mchoko wa akili......nikifika 60 sijui kama nitamkumbuka hata jina.

Nikija kwa Wasira, huyu mzee ndo ananichanganya kabisaaa. Kwanza hata mvi Hana mpaka Sasa akiwa na miaka zaidi ya 80. Mimi, na miaka yangu 40 zimejaa tele. Pili uwezo wake wa kumbukumbu ni WA ajabu kabisa.......kuikabili midahalo katika umri kama ule Huku akiwakalisha vijana wanaokuja kwa mihemko wakifikiri wanajua zaidi yake ni maajabu kabisa. Nilitaraji, katika umri ule, asiwe na uwezo wowote wa kueleza Wala kujieleza.

Wanakula nini' hawa wazee au ni majaaliwa tu?!!
 
Wahenga wenzangu hao
Enzi zetu kichwa kikiuma unaenda dukani (sio pharmacy) unanunua Aspro na kichwa kinapoa
Siku hizi kichwa kikiuma mpaka operation

Dawa zilikuwa nne tu enzi hizo
Siku hizi kila kona pharmacy
Tumeishi bila madawa ya kurutubisha ardhi bali nature inajitengeneza

Nywele tunapaka Kanta ingawa hili jina ndio lilitumika na kampuni moja ya India kuanzia miaka ya 40
Na miaka ya 70 bado ilikuwepo 😂😂😜
 
Jitahidi sana kuacha kula chips-mayai; Soda; ukiugua magonjwa madogo-madogo usikimbilie Hospitali haraka-haraka. Subiri kwanza na Uupe mwili nafasi ya kupambana wenyewe. Your Body is what u eat.
 
Jitahidi sana kuacha kula chips-mayai; Soda; ukiugua magonjwa madogo-madogo usikimbilie Hospitali haraka-haraka. Subiri kwanza na Uupe mwili nafasi ya kupambana wenyewe. Your Body is what u eat.
Ila kuacha Chips zege na mishkaki kadhaa nayo inahitaji moyo,halafu unakuta kuna muuzaji pembeni anauza soda baridii...
 
Wahenga wenzangu hao
Enzi zetu kichwa kikiuma unaenda dukani (sio pharmacy) unanunua Aspro na kichwa kinapoa
Siku hizi kichwa kikiuma mpaka operation
Siku hizi watu wamenyweshwa kasumba -hata std. 7 anaona amesoma na akiambiwa Aspro, Panadol, Paracetamol zote ni sawa na Turmeric wanakuona ww ni mshenzi eti hujastaarabika.
Dawa zilikuwa nne tu enzi hizo
Aspro; Chloroquine; Tetracycline /Oxytetracline (a.k.a Rangi mbili) na JV au Iodine Dawa ya kusafishia vidonda na Penicillin. Siku hizi wafanya biashara na Makampuni wanacheza na majina tu lakini active ingredients ni zile zile
Siku kila kona pharmacy
Sisi huku vijijini Pharmacies zetu zipo huko porini. Tumbo likileta za kuleta unachimba mizizi unachemsha unakunywa kikombe na mchezo umeisha.
Tumeishi bila madawa ya kurutubisha ardhi bali nature inajitengeneza
Kweli kabisa mkuu. Tuslifundishawa enzi hizo kilimo cha mzunguko (Crop rotation) na umuhimu wake lakini cku hizi tunasikia Kilimo cha matumizi ya mbegu zilizoboreshwa (GMO) n.k. Halafu watafiti wetu wasomi hawafanyi Research kuona uhusiano uliopo wa magonjwa yaliyoshamiri siku hizi esp. Kansa, Figo, Ini, na magonjwa yasiyoambukiza na Ulaji wa vyakula vitokanavyo na mazao ya mbegu hizo.
Nywele tunapaka Kanta ingawa hili jina ndio lilitumika na kampuni moja ya India kuanzia miaka ya 40
Na miaka ya 70 bado ilikuwepo 😂😂😜
Hahahaa. Siku hizi ni mwendo wa super Black na majina mengi na rangi unayoipenda e.g. Gold, Silver n.k.
 
Hasa toka umri wa miaka ishirini unaendeshwa kwenye defender ya TANU,unakula,kulala,kunya,matibabu popote duniani bure,
Kipindi hiko hapakuwepo na defender ila zilikuwa ni mandolin 4WD. Sasa huyo ndo angepata stress kubwa zaidi kwani hayo marupurupu hana tena na umri ndo umesogea mno, wengi wa mabest na macomrades wake wameshatangulia n.k. Lakini kwake ameridhika na hali yake na kuiona hiko ndo alichojaliwa vingine sio riziki yake. Any way; mm sio msemaji wake acha huenda kuna siku atasema siri ya Afya yake.
wengine hata kunya choo cha public tunalipia.Kwa kifupi hawana stress.
Mkuu; Stress ni mzigo na Dawa ya mzigo ni kuutua. Sio kuutoa mzigo kichwani halafu kuuweka mabegani. Hiyo haitasaidia-mzigo uko pale pale.
Kile kinachokuletea Stress achana nacho. Ona kama sio riziki yako na upite hv.
 
Miaka hiyo ukiona mtu hana mvi ujue kuna kitu anapaka, huelewi wapi?
 
Siri ni maisha mazuri,uhakika wa matibabu na malupulupu ya kodi za wananchi.Kila Mtanzania angepata matibabu na makazi ya uhakika kama wanavyopata,wengi wangeishi na kuwa na Afya kama Warioba na Wasira.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…