Ukweli Usemwe: Uongozi wa Rais Samia ni Changamoto

Ukweli Usemwe: Uongozi wa Rais Samia ni Changamoto

Samia alifeli kwa kumteua Makamba na Mwigulu, sasa hivi naye amegundua madaraka ni matamu kaanza kuteleza tena kwenye ishu ya katiba.

Ccm hawana nia njema kabisa na mwananchi wa kawaida.

Ishu sio katiba ishu ni usimamizi, katiba ya sasa ikitumika ipasavyo bado ni katiba Bora,

Katiba mpya kama haitotumika vizuri still itakuwa ni worse
 
Kwani mbowe aliswekwa gerezani na magufuli? Kama katiba mpya itashusha bei ya mafuta basi sawa
Katiba ni sheria kuu/muongozo mkuu/mlinzi wa sheria nyingine/hubeba miongozo yote ihusuyo nchi.

Hivyo basi,tutakapopata katiba mpya yenye maono ya mipango ya sasa na ya mbele tutaweza kudhibiti watu,vitu,hali na mali ili nchi iongozeke kistaarabu bila kusahau haki,wajibu, na demokrasia.
 
Ishu sio katiba ishu ni usimamizi, katiba ya sasa ikitumika ipasavyo bado ni katiba Bora,

Katiba mpya kama haitotumika vizuri still itakuwa ni worse
Katiba hii angalau Nyerere aliitumia kwa udhibiti wa hali halisi na nafsi yake ili kuleta tija taifani.

Usitegemee waliopo wataweza kuitumia bila kujiuliza "kwani mtamfanya nini" akikosea makusudi au kuteleza!
 
Unaposimama katika nafasi ya mwananchi wa kawaida ndio utaelewa ninachomaanisha.

Ni majuzi tu nilisafiri kwenda mozambique.

Ile nchi haijatulia na haijawahi kutulia lakini nimeshangaa kukuta bei ya mafuta ya kula ikiwa ni nafuu mno.

Bei ya mafuta ya Kula ya Tanzania ni zaidi ya mara mbili ya ile ya Msumbiji.

Dizeli, Petrol na Mbolea Msumbiji ni nafuu sana ukilinganisha na Tanzania, wanatuzidi wapi?

Nikirudi kwa mama, Mwaka mmoja wa kuwa madarakani kila kitu kimebadilika gharama za Maisha zimepanda mno, uonevu kwa wakulima wa Korosho umerudi upya.

Bei ya magari, TV, Computer n.k Zimekuwa juu Kabisa.

Kama hali itaendelea hivi uchaguzi unaofuata......
Hapa Tanzania hatuna serikali makini, wao wako bize tu kutengeneza plans za kubomoa wapinzani wanaotaka kuleta maeneleo hapa nchini.
 
Katiba hii angalau Nyerere aliitumia kwa udhibiti wa hali halisi na nafsi yake ili kuleta tija taifani.Usitegemee waliopo wataweza kuitumia bila kujiuliza "kwani mtamfanya nini" akikosea makusudi au kuteleza!

Hata katiba mpya ikija still hakuna kitu mtafanya, watanzania sio watu wa hulk za aina hiyo, watapiga kelele watu wachache Tu

So hata katiba mpya ikija I'm telling you no changes yoyote, unless mnataka Tu kupunguza mamlaka ya rais but still atakuwa ni rais na ni amiri jeshi mkuu
 
Hata katiba mpya ikija still hakuna kitu mtafanya, watanzania sio watu wa hulk za aina hiyo, watapiga kelele watu wachache Tu

So hata katiba mpya ikija I'm telling you no changes yoyote, unless mnataka Tu kupunguza mamlaka ya rais but still atakuwa ni rais na ni amiri jeshi mkuu
Huo sasa ni ubashiri ulioegemea hali ya hasi tu.

Kwani haujakaa ukajichekechea mambo na kubashiri hali chanya yaweza kutokea?

Unasemaje kuhusu hiyo katiba mpya ambayo itaeleza consequences za kiongozi ambaye ataamua kujiamulia yake iwe ni wakati wa uongozi wake au baada ya uongozi wake?
 
Huo sasa ni ubashiri ulioegemea hali ya hasi tu.Kwani haujakaa ukajichekechea mambo na kubashiri hali chanya yaweza kutokea?Unasemaje kuhusu hiyo katiba mpya ambayo itaeleza consequences za kiongozi ambaye ataamua kujiamulia yake iwe ni wakati wa uongozi wake au baada ya uongozi wake?

Hata ya sasa inatoa mwongozo kama huo but mbona hawafati?

So hata mpya itakuwa the same
 
Hivi kama tunalipa nauli kwa mtandao, na tuna lipa tanesco kwa mtandao, na tunalipia viwanja kwa mtandao , tunafanya selection ya vyuo na application kwa mtandO hivi HATUWEZI KUFANYA UCHAGUZI KWA MTANDO.?
Inawezekana.Ila kuna genge hilohilo likikusikia watajitahidi kila namna wakuumize,kukukatisha tamaa,kukupa kilema,kukuua au wakupige exile,detention na kukunyang'anya hata huo uhuru mdogo wa kujieleza.The new Mexico in Africa!
 
Ni rahisi kwa kiasi gani, Ni vyema ukaweka takwimu za bei msumbiju vs Tanzania, Msumbiji kiasi gani na Tanzania kiasi gani?...

Hakuna siku Tanzania kuliwahi kuwa na unafuu wa maisha kwa maana ya hizo inflation, kila miaka huwa zinapanda tu..

Shida yetu kuu ni controlling kila mahala kuanzia kwenye Birth rate, death rate, population growth, mpangilio mbovu wa makazi, plan mbovu za makazi, miundombinu mibovu, na shida nyingine nyiiiingi ambazo zinahitaji nguvu kubwa kuanzia ngazi ya familia na muda wa kufanya..
Hahaaa! Umepigwa upofu na mataputapu gani?

Tumia vitu vyenye TBS unayosingizia ni huo ulevi.

Kwani msumbiji pupulation na death rate hakuna?

Au ili iitwe population ni lazima ilingane na TZ?
 
Haiwabani vilivyo na kuwaelekeza bila kuwapa chaguzi la nini la kufanya na wakati gani.

Inawapa "uhuru" mpana hadi wanajisahau na kuiona Tanzania ni kama familia yao au ashakum si matusi,hawara yao.
Hata ya sasa inatoa mwongozo kama huo but mbona hawafati?

So hata mpya itakuwa the same
 
Hivi uchaguzi wa tz unaujua wewe au huujui? Kura yako haisadii chochote katika maamuzi. Umchague usimchague lazima awe rais. Kila Mara chadema wanawwambia muandamane kura zikibiwa Ila huwa mnawaona vichaa. Sasa onjeni joto la jiwe
Tukupe kura,alafu bado tukulindie hizo Kura!?

Kama Chadema wanaibiwa hadi Kura,Sasa siku wakipata Nchi,si wataibiwa na Nchi yenyewe!?

Kila chama kilinde Kura zake, Wananchi tuna mambo mengi ya kufanya!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom