Ukweli usio mchungu: Serikali ya awamu ya tano imejitahidi kupambana na ufisadi na ubadhilifu

Ukweli usio mchungu: Serikali ya awamu ya tano imejitahidi kupambana na ufisadi na ubadhilifu

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,170
Reaction score
6,757
Moja kwa moja kwenye mada husika wadau wa Jf.

Huko nyuma ilikiwa ni aibu maana watu walikuwa hawafanyi ufisadi bali ni kujichotea na kujijazia. Fikiria skendo la Escrow watu walichota bil of Tsh kama wanachukua sh mia mbil ya kula karanga.

Alichofichua leo waziri mkuu ni ushahidi tosha kuwa kuna madiliko makubwa, tulizoea kusikia watu wakichota bil 60+,bil 150+ na ilikuwa kama watu wanajichotea karanga kwenye mfuko wa bibi.Vipi kama ingekuwa kama enzi za Kagoda,Epa na Meremeta. Ilikuwa ni aibu sana. Najua kila mtu anakubali kuna mabadiliko makubwa.

Leo hii wanaopiga Mil 900 wanadakwa na kushughulikiwa! Maana yake ni kuwa hata upigaji wa dili kubwa zilizosababisha tukashindwa kujenga hospita za wilaya,vituo vya afya na zahanati umebanwa.

Najua kuna wabongo wenye roho za korosho dhidi ya Ccm na serikali yake watasema hamna mabadiliko.

Nyankurungu@ Buzirayombo on the way to Chato on vacation.
 
Vyanzo vya ufisadi huwa ni miradi mikubwa, iwe ya ujenzi, manunuzi au mikataba ya aina yoyote.
Leo ukiulizwa ndege imenunuliwa kwa sh ngapi hujui, mradi wa Stiglers unajengwa kwa fedha zipi hujui, SGR inajengwa kwa fedha zipi hujui. Mikataba ya madini iliyofanyiwa marekebisho bado yana utata mtupu.

Ufisadi huwa unafichuliwa na Vyombo huru vya habari, Wapinzani walio huru kufanya shughuli zao za kisiasa pamoja na Wanaharakati ambao haki zao zinaheshimiwa na kulindwa. Katika utawala huu hakuna chombo hata kimoja kati ya hivi ambavyo vipo huru kusema. Huwezi sema hakuna ufisadi eti kisa rais wako anasema anapambana na Majizi.

Mfano kwenye suala la e- passports, John Heche alizungumza kuwa kuna ufisadi ulifanyika katika uingiaji wa Zabuni lakini kilichofuata ni yeye kutishiwa maisha badala ya kuambiwa atoe ushahidi na uchunguzi ufanyike.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali Ndugu Abbas ambaye pasina shaka alionekana kutimiza wajibu wake kwa maadili makubwa aliondolewa kwa sababu za kutengeneza. Unatoa wapi huo udhubutu wa kusema serikali ni safi hii.

Kama umeanzisha mada kwa lengo la kuingiza siku basi najutia muda wangu niliotumia kukujibu, ila kama ulianzisha kulingana na uelewa na upeo wako basi tumia majibu yangu kutafakari maoni yako.
 
Kuna upambanaji wa ufisadi au kupambana na matumizi ya neno fisadi? Huwezi kupambana na ufisadi huku ukiwa adui wa uhuru wa vyombo vya habari.
Nilijua tu mtajitokeza kupinga haya mafanikio. Unataka uhuru gani wa habari ambao unaakisi mapambano ya ufisadi?
 
Kuna upambanaji wa ufisadi au kupambana na matumizi ya neno fisadi? Huwezi kupambana na ufisadi huku ukiwa adui wa uhuru wa vyombo vya habari.
Upo sahihi Mkuu, umejiondoa katika shirikisho la serikali zilizo na uwazi duniani, umemuondoa CAG muadilifu, unabinya uhuru wa vyombo vya habari, unawanyima wapinzani majukwaa ya kusemea, mikataba haiko wazi halafu tukuamini wewe si fisadi sababu unasema tu unapambana na Ufisadi??
 
Laiti hao yooote yanayofanywa na viongozi wa awamu hii kupambana na ufisadi wangalikua hawatokanu na serikali ya awamu iliopita kweli ningesema kuna mapambano.

Laiti ile miaka mitano ilipita ya awamu hii ingelikua imetoa taswira ya matokeo chana ya upambanaji na ufisadi ningesadiki kweli kuna mapambano ya ufisadi

Mimi ninachodhani mapambano yaliopo ya ufisadi ni kuutoa ufisadi uliokuwepo na kutengeneza ufisadi want Sina mpya ambao hatuwezi kuujua au kuisikia kwa sababu ambazo hao wanaopambana wameziweka.

Kwa kua maisha yapo na muda upo, na tecnologia ipo tuwe wavumilivu tuu wakati tutakapokuja kuambiwa ufisadi ulifanyika wakati wa awamu hii ikiwa madarakani.
 
5 tena!!!
tapatalk_1607940808235.jpeg
 

 
Walivyoshika panga tu wakachungulia kila sehemu wakagundua pako empty wenzao wameshakula nyama, maziwa na asali yote! Yale ya ardhini kizungumkuti, ya mtwara imeshawekwa rehani, wakaona isiwe tabu watakula wapi sasa? Wakaamua kuanzisha “mawayt elefanti” ili wapatamo pakupigia.... stuka ewe mdanganyika!
 
Una miezi miwili toka umejisajili Jamii Forum, naamini ukiendelea kukaa humu utajifunza namna ya kubishana kwa hoja bila ya kushambulia watu. Karibu sana na endelea kujifunza.
Wewe ni nani? Mpaka ulete maswali ya kipuuzi kama haya?
 

Nyankurungu2020
Ha ha ha haaa..
Ebu njoo huku ubishane na wakuu wako wa huko Lumumba
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Kwa hili hata mimi nimeona. Tatizo nawaza labda wameamua tu kutokana na kukosa vile vyanzo bwereree vya fedha kutoka kwa mabeberu
 
Back
Top Bottom