Ukweli usio mchungu: Serikali ya awamu ya tano imejitahidi kupambana na ufisadi na ubadhilifu

Ni kweli ila imeshindwa kutenganisha kati ya ufisadi na biashara, na imesababisha uchumu wa watu kutetereka.
 
Huna hoja za kujadili na watu,umegeuka mganga mpiga ramli.
Mkuu, nilidhani umeanzisha uzi ili watu wajadili kwa mitazao mbalimbali, mingine kukubaliana, mingine kuweka nyongeza na mngine hata kupingana na maudhui ya mada yako. Lakini naona kama vile unapanic na kujibu kimipasho mipasho
 
Asante sana mkuu.
 
Kuna upambanaji wa ufisadi au kupambana na matumizi ya neno fisadi? Huwezi kupambana na ufisadi huku ukiwa adui wa uhuru wa vyombo vya habari.
Ni CDM na ACT tu wanaopinga kwa makusudi juu ya jinsi Serikali inavyopambana na ufisadi - Dkt John Pombe Magufuli kwa kweli ni mwamba
 
Ni CDM na ACT tu wanaopinga kwa makusudi juu ya jinsi Serikali inavyopambana na ufisadi - Dkt John Pombe Magufuli kwa kweli ni mwamba

Hakuna upambanaji wa ufisadi, bali kuna vita dhidi ya matumizi ya neno fisadi.
 
Ni CDM na ACT tu wanaopinga kwa makusudi juu ya jinsi Serikali inavyopambana na ufisadi - Dkt John Pombe Magufuli kwa kweli ni mwamba
Ana umwamba gani yeye mwenyewe mwizi tu yule.
Alishiriki kuuza nyumba za umma kwa mahawala zake kina kabula wale alikuwa akiwafuata mabibo hostel usiku.
Alinunua nyumba za NIC Kwa shilingi laki 6 Kyle dodoma. Yani ghorofa linunuliwe kwa laki 6???
Alipora KOROSHO za WAKULIMA?
Aliita watengeneza ndege na kukaa nao akiagiza ndege atakazo vila kufuata sheria za manunuzi ya umma?
Huyo ndiyo mwamba wa kupambana na ufisadi?
 
Hakuna upambanaji wa ufisadi, bali kuna vita dhidi ya matumizi ya neno fisadi.
Labda ungejenga hoja hii kwa kutoa mifano - nachojua ni kwamba kipindi cha nyuma ukipita na gari zuri watu waliongea "ufisadi", mikataba mingi ilikuwa ten %, watu walihamisha fedha kinyemela nk

Utawala huu umedhibiti hali hii na kufuatilia kwa karibu matumizi ya fedha za umma
 
Wakati huo ufisadi mkubwa unafanyika ni chama gani kilikuwa madarakani na discount ya ndege iko wapi na ni kiasi gani.

Kisha ule uwanja wa ndege wa Chato ulijengwa kwa fedha kiasi gani mbona imekuwa siri na fedha za covid-19 zilizotolewa na wazungu zilitumikaje.

Wakati unaandika usiandike kama vile unaandikia jukwaa la watoto wa chekechea.

Please be advised accordingly.
 

Kinachokufanya uamini ufisadi umeisha ni kwakuwa vyombo vya habari haviko huru kuongea, na wapinzani ni marufuku kukosoa. Unapoondoa mfumo wa Open Government jua unapigwa mchana kweupe.

Wakati mwingine ni vyema ukakaa kimya tu, unafuatilia matumizi ya fedha za umma, huku serikali inafanya kazi barabarani kati ya Dodoma na Da! Jaribu kufuatilia uone pesa ya umma inavyopotea kwa safari zisizo na tija kwa viongozi kutoka Dar kwenda Dodoma na kinyume chake. Ni kweli miradi ilikuwa na 10%, je manunuzi ya hizi ndege unajua bei yake kwa uhalisia? Ujenzi wa bwawa la SG una uhakika na bei yake?
 
Manunuzi na ujenzi wa miundombinu watu wanapiga kama kama ila uwe kipenzi cha godfather
 
Hongera umeongea ukweli ambao mababeli wengi hawapendi kusikia, kwa sasa nchi ina nidhamu kubwa sana.
 
Neno fisadi limezaa mafisadi wanaopigwa nyundo. Hujapata majibu jinsi mafisadi wanavyobanwa?

Ukishafanya mambo kwa kificho huna uadilifu wa kubana mafisadi, sana sana utakachofanya ni uonevu wa kimadaraka.
 
Aliyeshinda tenda ya ujenzi uwanja wa chato alishindanishwa na nani,tenda ilitangazwa lini,uligharimu kiasi gani?
Trilioni za Assad vipi?
Sare za polisi makontena na makontena ya Lugola zipo wapi?
Sanamu la Mwl.Nyerere lilitafuna kiasi gani?
Ununuzi wa ndege kwa cash mchakato wake ulifuata taratibu,upi?
Fedha za TRA Kisutu Branch ziko wapi na kiasi gani kimeshakusanywa hadi jana?

Watanzania siyo wajinga!
 
Nilijua tu mtajitokeza kupinga haya mafanikio. Unataka uhuru gani wa habari ambao unaakisi mapambano ya ufisadi?
Tuwe wakweli nidhamu imeboreka,wakati huo huo ufisadi na rushwa bado vinafanyika na vingine vinaonekana kawaida.Yafaa tujipangie madaraja kwa vipimo tutakavyo kubaliana mafanikio ni yapi na kushindwa ni kupi hii itatusaidia kama taifa.
 
NIDA,kitwanga,Lugola,Bandari,x,y,z,,,,,,
nk!!!!!??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…