Ukweli wa Kustaajabisha Kuhusu Nyota za Angani

Ukweli wa Kustaajabisha Kuhusu Nyota za Angani

Status
Not open for further replies.
Nimewahi kusikia Kuna galaxy nyingi sana,na kila galaxy ina mamilion ya nyota, na kila nyota ina sayari zake kama ilivyo kwa jua letu. naomba ufafanuzi juu ya hili@Monstgala
Tuzinduke thanks, swali lako linafanana kwa namna moja na maswali ya wachangiaji wengine na nilijaribu kufafanua katika post kadhaa zenye kuelezea galaxies kama unaweza kuzipitia kwenye post #72 , #243 , #249 , #252 , #262 , #268
 
Last edited by a moderator:
Bingwa zaidi yangu ni wewe.

Ambaye hata baada ya kuonyeshwa hata wewe umekariri, unakazania kuendelea kukariri kwamba mimi ndiye bingwa wa kukariri.

kadri siku zinavyokwenda unaelimika na kupunguza kariri zako za maneno ya kiingereza na kilatini HAPA JF.
nishani wastahili mkuu, uwezo wako wa kukariri ni SUPER...
 
Mungu ni mkubwa..!!!
nimeonelea nipost mada hii kwa kiswahili ili wote wanaojua lugha hii wafaidike lakini katika kuchangia tutumie lugha yoyote inayotumika hapa jukwaani . Nilipata challenge katika ule uzi wa ufos kwamba je nikiandika kiswahili nitakufa? Nikajibu ”sitakufa” na hii ni jitihada za kuonesha hivyo. 🙂

tukirudi kwenye mada, watu wanapofikiri kuhusu ulimwengu basi wanafikiria nyota. Nyota ndizo zinazofanya sehemu kubwa ya yabisi, kiminika na hewa (matter) inayoonekana na ingawa nyota zote mbali na jua ziko katika umbali usiofikirika kutoka tulipo, bado tunaweza kuziona nyota maelfu kwa maelfu kwa macho yetu wenyewe. Kuna maajabu mengi ya ukweli kuhusu nyota lakini nitaongelea machache yanayovutia na wengine wanaweza kuongezea ili tijifunze au kueleweshana pamoja.

1.idadi ya nyota katika ulimwengu unaoonekana

katika usiku wenye giza tororo katika maeneo ya vijijini au mbali na mji unaweza kujionea nyota zisizo na idadi lakini katika mazingira ya kawaida hapo unakuwa unaangalia nyota kama 2500 na si zaidi ya hapo. Hizo ni moja ya billioni 1/100,000,000 ya jumla ya nyota zilizo katika galaxi tuishiyo (milkyway).

Milky way ni moja ya galaxi kubwa sana katika universe na sisi tumebahatika kuwa ndani ya galaxi hii. Labda kidogo tuangalie kwa kifupi ukweli wa galaxi hii. Diameter (kipenyo) ya milky way kutoka upande mmoja mpaka mwingine ni umbali wa miaka laki moja (100,000) ya mwendo wa mwanga. Mwendo wa mwanga kwa mwaka ni jinsi mwanga unavyosafifi kwa mwaka mzima kutoka point moja mpaka nyingine. Mwanga husafiri kwa mwendo wa kasi kuliko mwendo wa kitu kingine chochote tunachokijua. Kwa mfano katika sekunde moja mwanga unasafiri umbali wa kuzunguka dunia mara saba. Hivyo mwaka mmoja wa kusafiri kwa mwanga (a light year) ni umbali wa kustaajabisha. Inaweza kuchukua miaka elfu kumi na nane kwa chombo chenye kasi zaidi cha anga kusafiri mwaka mmoja wa mwanga. Sasa hapa ku-cover distance ya kipenyo cha milkyway tunazungumzia umbali wa miaka 100,000 ya kusafiri kwa mwanga.

Hii pia ina maana unapochukua telescope ukafanikiwa kuziona nyota zilizoko upande mwengine wa mwisho wa galaxi, basi unaziona jinsi zilivyokuwa miaka 100,000 iliyopita, kwa sababu mwanga uliotoka kwenye nyota hizo miaka laki moja iliyopita ndio kwanza unatufikia. Hii ni sawa pia kwamba kama kuna kiumbe katika upande mwingine wa galaxi na anaiangalia dunia kwa telescope basi ataiona dunia kama ilivyokuwa miaka 100,000 iliyopita.

milky_way.jpg


katika picha hiyo ya milkyway galaxi unaweza kudhani mojawapo ya vidoti hivyo ni jua letu. Ukweli ni kwamba kama ukiikuza picha hiyo ifikie ukubwa wa saizi ya dunia, bado ungehitaji microscope ili kuweza kuona kidoti cha mwanga wa jua letu. Hii ni kutokana na kwamba kama milkyway galaxi ingepunguzwa iwe kama size ya dunia, basi jua lingekuwa 1/50 ya millimita (kipenyo). Hii ni sawa na kidoti tusichoweza kukiona kwa macho.

Milkyway ni bonge la dude na lina idadi ya nyota kati ya bilioni 100 hadi 400 lakini kumbuka hii ni galaxi moja tu.

kwani kuna galaxi ngapi?

mwaka 1995, wanasayansi walichagua kajisehemu kadogo sana katika anga ambako kwa macho ya kawaida kalikuwa kanaonekana hakana nyota yoyote wala mwanga wowote. Pia kwa telescope ya kawaida kaeneo haka bado kalionesha hakana kitu chochote yani ni giza tu. Eneo hili dogo ambalo lilionekana tupu ni kama vile eneo linaloweza kuzibwa na mpira wa tenis ukiwa juu yako kwa mita mia.
Kw amuda wa siku kumi wanasayansi wakitumia hubble telescope, walichunguza eneo hili ambalo lilidhaniwa halina kitu na picha nii chini ndicho walichovumbua:

hudf_hst_big-600x749.jpg



ajabu!

Kila kinachoonekana katika picha hiyo si nyota tena, hata kidoti kidogo kabisa cha mwanga ni galaxi nzima. Katika picha hii tu kuna zaidi ya galaxi 10,000 na kila moja ikiwa na zaidi ya nyota billioni 100. Lakini kumbuka hiki ni kisehemu kidogo sana cha anga tunayoiona kama vile saizi ya kichwa cha pini.

Hivyo picha hii ilisaidia makadirio ya ulimwengu uonekanao (observable universe) kwamba una zaidi ya galaxi bilioni 100, ambayo inafanya jumla ya nyota katika ulimwengu tunaoweza kuuona kuwa kwenye kati ya 100 sextillion stars.
Ili kuweka kiasi hiki katika njia inaweza kufikirika kirahisi, chuo kikuu cha hawaii kilitumia muda wa kutosha katika kukokotoa kadirio la kila punje ya mchanga duniani ambampo walipata jibu kuwa dunia ina quintillion 7.5 za mchanga.
Hivyo basi, kwa kila punje moja ya mchanga duniani kuna nyota 10,000 katika universe.

2. Nyota hazijakaribiana

ukiweka kando mfumo wa nyota pacha, nyota nyingi ziko pekee zikiwa hazina chochote pembeni kwa umbali mkubwa sana katika kila uelekeo, yani ziko pweke sana. Jua letu ni mojawapo, nyota iliyo karibu kabisa na sisi ni proxima centauri, umbali wa miaka minne na nusu ya kusafiri kwa mwanga au miaka elfu sabini ukisafiri na chombo chenye mwendo mkali cha nasa.

Tukiweka mfano rahisi kama jua ni mpira wa tennis uko katikati ya jiji la dar es salaam basi proxima centauri ni mpira mwingine wa tenis ukiwa katikati ya jiji la maputo maputo umbali wa karibia kilomita 1600.

3. Baadhi ya nyota ni kubwa kuliko maelezo

nyota kubwa sana zinaitwa red hypergiants hizi ni kubwa kweli kweli. Mojawapo ya haya majidude makubwa kabisa linaitwa vy canis majoris. Kama ukizidisha saizi ya jua letu mara 1, 420 ndio unaweza kupata size ya vy canis majoris.

Tukirudisha mfano wa mpira wa tenis inakuwa kama jua ni size ya mpira wa tenis basi vy canis majoris, ni sawa na jengo la ghorofa 16, hapa sijui lipi litafit kama mfano kwa jiji letu la dar, ppf tower? Kama nyota hii ndo ingekuwa jua letu basi kwa maana ya kuwa katikakati ya solar system basi sayari zote zingemezwa.

Nyota nyingine kubwa katika level ya hypergiant ambayo saizi yake inakaribia vy canis majoris ni betelgeuse. Hii inaonekana angani kwa macho kusipokuwa na mbalamwezi.

4. Baadhi ya nyota ni ndogo haswa lakini nzito kupindukia.

pale nyota kubwa inapokufa kwa kulipuka (supernova), mvuto wa ndani(gravitational collapse) unajitokeza na kusababisha nyota changa (netron star). Matter ambayo sijui kwa kiswahili inaitwa nini imeundwa kwa atoms na atoms zimeundwa kwa nafasi tupu kwa kiasi kikubwa. Kitu pekee kinachoipa atom uzito wake ni kiini kidogo (nucleus) katikati yake. Kupata picha ya hii fikiriria atom ni duara kubwa la kilomita moja, kwa size hiyo atom itakuwa size ya mbegu kunde ikielea katikati. Uzito wa atom yote unakuwa sawa na uzito wa mbegu ya kunde.

Sasa kinachotokea katika mvuto wa kuvunjika kwa nyota inayokufa ili kuwa nyota changa ni kwamba atoms zinakandamizwa pamoja kwa nguvu sana kiasi kwamba kila nafasi tupu kwenye atom inaachia na vile viini au kwa mfano tuliotumia, zile mbegu za kunde katikati ya miduara ya atoms zinagandamana pamoja. Sasa fikiria nafasi tupu zote katika duara la kilomita moja.moja zimeachia na zile mbegu sasa zimeshonana kwenye eneo dogo kabisa. Kwa hiyo badala ya kuwa na eneo la kilomita moja lenye uzito wa mbegu moja ya kunde sasa eneo hili lina uzito wa karibia mbegu za kunde 1,000,000,000,000,000,000.

Hivyo ndivyo inavyokuwa nyota changa inapozaliwa kunakuwa hakuna nafasi tupu, ni neutrons ambazo zimegandana na uwiano wa uzito wake kwa kulinganisha ukubwa ni trillioni mara trillioni ya uzito wa nyota ya kawaida. Matokeo yake unakuta nyota changa yenye ukubwa wa kilomita 25 tu ina uzito wa mara tatu ya jua au sawa na uzito wa dunia millioni moja.

mambo mengine ya kustaajabisha kabisa!

katika nyota changa (netron star) kijiko kimoja cha chai kina uzito sawa na mapiramidi mia tisa ya giza kule misri. Mkandamizo wa nyota changa ni sawa na kuweka meli moja kubwa ya mizigo juu ya punje moja ya mchanga. Nyota hizi hujizungusha kwa kasi sana (spinning) kufikia mara 642 kwa sekunde moja hii ikiwa na maana kidoti katika eneo la kati la nyota hii kinazungunguka kwa kasi ya umbali wa zaidi ya mzunguko mzima wa dunia kwa sekunde. Nyota hizi ni zenye joto kali sana 10,000,000,000,000 kelvin, kama mara 1000 zaidi ya katikati ya jua.

Mwenye kuongeza, maswali, kupungunguza kuhusu nyota haya karibuni…
 
Mkuu Monstgala/Mgalanjuka, nashukuru kwa hii elimu adimu sana, naomba unijibu maswali kazaa
(a)kwanini galaxy yetu imepewa jina la MILK WAY GALAXY? au ile iliyo karbu nasi kwanini imeitwa ANDROMEDA? Swali langu hapa linasimamia upande wa kutaka kujua kuna uhusiano gani kati ya jina la galaxy yetu na galaxy yenyewe? Kwa mfano mimi naitwa NICOLAX nilipewa ilo jina kutokana na kuzaliwa siku na mwezi mmoja na astronomer nicolas corpenicus
So inakuaje hii dude na jina lake

.made in mby city.
 
Mkuu Monstgala/Mgalanjuka, nashukuru kwa hii elimu adimu sana, naomba unijibu maswali kazaa
(a)kwanini galaxy yetu imepewa jina la MILK WAY GALAXY? au ile iliyo karbu nasi kwanini imeitwa ANDROMEDA? Swali langu hapa linasimamia upande wa kutaka kujua kuna uhusiano gani kati ya jina la galaxy yetu na galaxy yenyewe? Kwa mfano mimi naitwa NICOLAX nilipewa ilo jina kutokana na kuzaliwa siku na mwezi mmoja na astronomer nicolas corpenicus
So inakuaje hii dude na jina lake

.made in mby city.

Mkuu , kama yalivyo mambo mengi sana katika sayansi yenye majina ambayo asili yake ni Wayunani basi Milky Way ni mojawapo. Hawa watu (Greek) wao walianza utafiti wa anga zamani sana hivyo mpaka sayansi inaaza kupata miziz mambo mengi ambayo ni phenomenon zenye ushawishi wao walikuwa tayari wameshaanza kuchunguza, kuvumbua na kutoa majina. Hivyo Milky way inatokana na tafsiri ya jina hilo ambalo awali lilikuwa kwa kiyunani lactea circle ama mzunguko wa maziwa. Lakini si kwamba jamii nyingine za kale hazikuwa na majina kwa jinsi ya wao walivyokuwa wanaliona anga, la hasha! Jamii nyingi zilikuwa tayari na majina fulani kuhusu mkusanyiko wa nyota ambazo ziko ndani ya galaxi hii kwa jinsi ya tafsiri ambazo wao waliona zinafaa.

Tha same goes to Andromeda, ambalo ni jina la miungu ya kizamani ya wayunani (wagiriki). Kwa hiyo kwenye upande wa anga ambao watu hawa walidhani miungu inaishi huko basi pia maumbo yaliyoko angani pamoja na nyota kwa namna nyingi vilipewa majina ya miungu au vitu walivyokuwa wakiabudu.

Majina hutolewa na wavumbuzi au pia jumuia ya wanasayansi wanaweza kuamua kutokana na mambo fulani. Mfano sasa kuna nyota nyingi ambazo hazikuwa na majina na unaweza kufanya mpango (inaweza kuwa kununua) nyota ile ikaitwa jina lako.
 
(a)Bwana Monstgala/Mgalanjuka kuna washkaji wamenikamata na kaswali kakiaina nilipo waambia kua duni inazunguka jua, nyota zote pamoja na jua letu vinazunguka dude baya liitwalo black-hole, na galaxy pia nazo zinazunguka basi wakaniuliza so galaxy inazunguka nini???
(b)mkuu umeongelea habari ya kuipa nyota jina langu kwa mpango maalumu(ikiwezekana kulipia) sasa hapa atalipwa nani kwa kuipa nyota jina langu?

.made in mby city.
 
(a)Bwana Monstgala/Mgalanjuka kuna washkaji wamenikamata na kaswali kakiaina nilipo waambia kua duni inazunguka jua, nyota zote pamoja na jua letu vinazunguka dude baya liitwalo black-hole, na galaxy pia nazo zinazunguka basi wakaniuliza so galaxy inazunguka nini???
(b)mkuu umeongelea habari ya kuipa nyota jina langu kwa mpango maalumu(ikiwezekana kulipia) sasa hapa atalipwa nani kwa kuipa nyota jina langu?

.made in mby city.

Nicolax , galaxies ziko kwenye mwendo pia kwa sababu ulimwengu unaexpand lakini si lazima kila kitu kizunguke kingine. Galaxies zote ziko kwenye makundi makubwa na madogo yanayoitwa Galaxy clusters, galaxy zinajikusanya hivi kutokana na gravity au inaweza kuwa dark energy(no confirmation yet on some behavior of such enormous things). Makundi makubwa sana ya galaxies yanaitwa superclusters haya ndio mojawapo ya madude makubwa kuliko chochote katika ulimwengu na yako mengi kona zote za ulimwengu kila moja laweza kuwa na billions of galaxies. Kuna post fulani hapo kabla hujazipitia vizuri hebu chungulia post no 243
 
Nicolax , Galaxies zote ziko kwenye makundi makubwa na madogo yanayoitwa Galaxy clusters, galaxy zinajikusanya hivi kutokana na gravity au inaweza kuwa dark energy(no confirmation yet on some behavior of such enormous things). Makundi makubwa sana ya galaxies yanaitwa superclusters haya ndio mojawapo ya madude makubwa kuliko chochote katika ulimwengu na yako mengi kona zote za ulimwengu kila moja laweza kuwa na billions of galaxies. Kuna post fulani hapo kabla hujazipitia vizuri

Acording to second newton law, kitu chochote ili kiweze ku move lazima kuwe na external force iliyokua applied on the body, sasa ni kitu gani kilicho zipa force na kusababisha movement za nyota,sayari,vimwondo,galaxy n.k.?

.made in mby city.
 
Acording to second newton law, kitu chochote ili kiweze ku move lazima kuwe na external force iliyokua applied on the body, sasa ni kitu gani kilicho zipa force na kusababisha movement za nyota,sayari,vimwondo,galaxy n.k.?

.made in mby city.

Wanasayansi wamethibitisha kwamba licha ya kwamba galaxies, nyota zilizomo, sayari, vimwondo, mavumbi na hata blackholes viko kwenye mwendo, lakini pia mwendo huo unaongezeka kasi.

1. Kuwa kwenye mwendo kunadhaniwa kusababishwa na Big-Bang, mwendo huu ni moja ya sababu za Big-bang theory.

2. Mwendo kuongezeka kasi zaidi na zaidi hii haina explanation iliyokuwa confirmed, lakini suggestion zinalenga Dark energy kuwa nyuma ya acceleration hii.

Hii concept ni muhimu sana maana inachangia/ilichangia kussuport Big-Bang theory kwa maana ya kwamba ule mlipuko lazima usababishe expansion. Katika moja ya matokeo ya hii kitu ina maana itafika kipindi baada ya muda mrefu sana galaxies zote na zitakuwa zimesafiri mbali sana na kutawanyika kiasi ambacho hatutaweza kuona galaxy nyingine karibu.


Baada ya muda mrefu Astrophysicists wanabashiri kutakuwa Heat death ya Universe. Hapa ni pale energy itakapokuwa imesambaa na kubalance katika ulimwengu wote hivyo hakuna area itakayokuwa ina nishati iliyojikusanya na kusababisha activity fulani. Hii ni kutokana na the laws of thermodynamics.
 
Shukrani sana ndugu Monstgala/Mgalanjuka kwa maelezo yako yaliyo nifanya niitafute hiyo theory ya big-bang ili twende sawa
Ila mkuu kwa mara nyingi sana nimeona unaandika hii kitu inaitwa dark energy ambayo inanikumbusha nyuma kwenye ule uzi wa "ALINS AND UFO JE TUKO PEKE YETU?"
Ulisewa ET class5 wapo more intelligent, more wise, more advanced than the rest classes ambao wanatumia dark energy ambayo ni kama 73% ya energy yote ulimwenguni
Sasa mimi nataka kujua hii kitu ikoje, inafanyaje kazi?, inakuaje? Transformed? Na mambo mengine kama hayo
Natanguliza shukrani kwako mkuu wangu

.made in mby city.
 
Shukrani sana ndugu Monstgala/Mgalanjuka kwa maelezo yako yaliyo nifanya niitafute hiyo theory ya big-bang ili twende sawa
Ila mkuu kwa mara nyingi sana nimeona unaandika hii kitu inaitwa dark energy ambayo inanikumbusha nyuma kwenye ule uzi wa "ALINS AND UFO JE TUKO PEKE YETU?"
Ulisewa ET class5 wapo more intelligent, more wise, more advanced than the rest classes ambao wanatumia dark energy ambayo ni kama 73% ya energy yote ulimwenguni
Sasa mimi nataka kujua hii kitu ikoje, inafanyaje kazi?, inakuaje? Transformed? Na mambo mengine kama hayo
Natanguliza shukrani kwako mkuu wangu

.made in mby city.

Mkuu labda tu tusichanganye topics maana itakuwa mkanganyiko mkubwa. Ila kwa nguvu nyingine zilizo katika universe niliwahi kuandika hivi kwenye bandiko fulani;

Kuna maguvu mengi tunayoyajua na kubwa kama gravity ni Law kwa kuwa tunaijua uzuri na tunaipima bila shida. Lakini hizi nguvu kubwa zaidi ni hypothesis, bado hamna kitu firm kutokana na ukubwa wa issue yenyewe. Natumia lugha nyepesi na kuita nguvu (inaweza ikawa kitu kingine) maana sipati mamneno mazuri ya kuelezea.

Nikiziweka nguvu hizi katika percentages kutokana na recent studies ni kwamba kubwa kabisa ni Dark energy (cosmological constant) hatuijui vizuri ila ipo. Yani uwiano wa elimu au information tusizonazo/tusiyojua kuhusu hii kitu ni mkubwa sana kulinganisha na ule wa yale machache tunayojua. Kwa nini hatuijui? Ni ngumu kupima, kuiona, kuishika, kuinua yani tunaona matokeo yake tu. Kwa nini ipo? kwa sababu tuna ushahidi wa kutosha jinsi universe inavyo-expand na kuna nguvu inayofanya hii process (expansion). Ni kubwa kiasi gani, ni takribani 68% ya kila kitu kilicho ulimwenguni au katika universe.

Nguvu ya pili au kitu cha pili cha ajabu ambacho kipo inaitwa Dark matter. Hii ipo ila haiwezi kuonekana kwa kuwa kila kitu hata mwanga unapenya kati yake yani hai-interact na kitu chochote. Hii ndio inashikilia universe kwa kuwa isingekuwepo basi ile dark energy ingetutawanya ndani ya sub-second. Ulimwengu ukiangaliwa kwa ujumla unaonekana kuwa na umbo kama nyuzi (web) zilizoshikana hii kitu inadhaniwa kuwa behind this phenomena. Hii ni asilimia takribani 27 (27%) ya kila kitu ulimwenguni.

Alafu ndio tuna matter hii tunaijua na sisi, mawe, maji, gas, sayari, nyota na chochote kinachooneka ndio part yake. Hii ni asilimia takribani 5 tu ya kila kitu katika universe.

Kwa hiyo kila kitu kinachoonekana katika universe ni asilimia tano tu ya kile tusichokiona lakini kipo kwa hakika kutokana na yale tunayoona kama matokeo yake.

Kutokana na jinsi tusivyojua mengi kuhusu hii area ni vigumu kuelezea kwa hakika umuhimu au usalama wake kwa sisi lakini jinsi tulivyo ni matokeo ya kuwapo kwa hizi kitu ama sivyo universe na mambo yake hakika yasingekuwa hivi.
 
Shukrani sana bwana Monstgala/Mgalanjuka, hakika una maelezo yenye ushawishi
Mkuu wangu kwenye ile picha ya galaxy yetu ya "MZUNGUKO WA MAZIWA" katikati yake nimeona mwanga mkuu, unaong'aa kuliko sehemu yoyote ya hii galaxy yetu
Kwangu inaniletea mkanganyiko kidogo kwa sababu nilitegemea katikati kusiwe na kitu au mwanga kidogo au kuwe kuna giza kutokana na ukweli kwamba pale katikati kuna dude baya sana liitwalo black-hole, sasa hapa nashindwa kujenga picha tena kichwani kuwa hili dude au hii sehemu likimeza nyota na chochote kilicho karibu inakuaje, mara ya kwanza nilijua hili dude au hii sehemu, ikimeza nyota au chochote kilicho karibu basi itakuwa brighter zaidi, ila baadae ukaja na maelezo kua hili dude ni kama sehemu(point) ambayo hata mwanga haupiti, sasa Monstgala/Mgalanjuka ningependa nifahamu huo mwanga mkuu katikati ya galaxy yeu ya "MZUNGUKO WA MAZIWA" imekuajekuaje mpaka iko vile??? japo najua ile ni mfano wa picha nzima ya galaxy yetu

.made in mby city.
 
Shukrani sana bwana Monstgala/Mgalanjuka, hakika una maelezo yenye ushawishi
Mkuu wangu kwenye ile picha ya galaxy yetu ya "MZUNGUKO WA MAZIWA" katikati yake nimeona mwanga mkuu, unaong'aa kuliko sehemu yoyote ya hii galaxy yetu
Kwangu inaniletea mkanganyiko kidogo kwa sababu nilitegemea katikati kusiwe na kitu au mwanga kidogo au kuwe kuna giza kutokana na ukweli kwamba pale katikati kuna dude baya sana liitwalo black-hole, sasa hapa nashindwa kujenga picha tena kichwani kuwa hili dude au hii sehemu likimeza nyota na chochote kilicho karibu inakuaje, mara ya kwanza nilijua hili dude au hii sehemu, ikimeza nyota au chochote kilicho karibu basi itakuwa brighter zaidi, ila baadae ukaja na maelezo kua hili dude ni kama sehemu(point) ambayo hata mwanga haupiti, sasa Monstgala/Mgalanjuka ningependa nifahamu huo mwanga mkuu katikati ya galaxy yeu ya "MZUNGUKO WA MAZIWA" imekuajekuaje mpaka iko vile??? japo najua ile ni mfano wa picha nzima ya galaxy yetu

.made in mby city.
NICOLAX Kinachosababisha mwanga ule katikati ya milkyway galaxy ni nishati inayoponyoka kabla ya kuingia kwenye eneo lile la super massive blackhole ambalo chochote hakiwezi kutoka hata muda ndani yake hauwezi kwenda mbele wala nyuma. Nishati hii kwa kuwa ni mkusanyiko wa kila kitu kinachovutwa na gravitational force ya dude hili, basi inakuwa kwenye mgandamizo mkubwa ajabu na hivyo friction yake ni ya kutisha. Kutokana na friction hii basi mwanga mkali sana unaotokana na radiation unatokea. katika baadhi ya super massive blackholes mwanga huu au radiation hii inafyatuka kwenda matrillioni ya kilomita na inaitwa Quasar. Hii ni moja ya vitu virefu kwelikweli na vyenye mwanga mkali sana katika universe.
 
Last edited by a moderator:
NICOLAX Kinachosababisha mwanga ule katikati ya milkyway galaxy ni nishati inayoponyoka kabla ya kuingia kwenye eneo lile la super massive blackhole ambalo chochote hakiwezi kutoka hata muda ndani yake hauwezi kwenda mbele wala nyuma. Nishati hii kwa kuwa ni mkusanyiko wa kila kitu kinachovutwa na gravitational force ya dude hili, basi inakuwa kwenye mgandamizo mkubwa ajabu na hivyo friction yake ni ya kutisha.Quasar. universe.

Welcome back mkuu Monstgala/Mgalanjuka cjakuonapo hapa jukwaani??
Mkuu leo nina maswali mawili kwako
(1)nimeonelea nisilete mkanganyiko katika hii topic basi ingelikua vyema kama ningepeleka swali langu la kwanza katika maada ya "MUDA WA ULIMWENGU"
(2)mkuu ivi sisi binadamu 2naweza ku extract dark energy na kutumia kwa matumizi ya kawaida kama tunavyo tumia energy kutoka katika sources zingine tofauti tofauti katika local planet
 
Last edited by a moderator:
Welcome back mkuu Monstgala/Mgalanjuka cjakuonapo hapa jukwaani??
Mkuu leo nina maswali mawili kwako
(1)nimeonelea nisilete mkanganyiko katika hii topic basi ingelikua vyema kama ningepeleka swali langu la kwanza katika maada ya "MUDA WA ULIMWENGU"
(2)mkuu ivi sisi binadamu 2naweza ku extract dark energy na kutumia kwa matumizi ya kawaida kama tunavyo tumia energy kutoka katika sources zingine tofauti tofauti katika local planet

Mkuu NICOLAX, Dark energy hatuijui ukiachilia mbali wazo la kwamba siku moja tutaweza kuitumia. Hata jina hili Dark energy halina maana ya kwamba nishati hii ni nyeusi bali kwa kuwa hatujui vyema chanzo chake na jinsi ilivyo. Kwenye hili hamna ufafanuzi kwa physics iliyopo, hakuna principle wala sheria za kifizikia zinazoweza kuendana na theory hii lakini kwa hakika nguvu hiyo ipo na effects zake zinaonekana kwa vipimo. Mfano kupanuka kwa universe. Hata phenomenon za ajabu kabisa katika maeneo yaliyoko mbali sana katika ulimwengu zinahusishwa na nguvu hii pale ambapo ufafanuzi wa sayansi na fizikia ya kawaida unagonga mwamba.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu NICOLAX, Dark energy hatuijui ukiachilia mbali wazo la kwamba siku moja tutaweza kuitumia. Hata jina hili Dark energy halina maana ya kwamba nishati hii ni nyeusi bali kwa kuwa hatujui vyema chanzo chake na jinsi ilivyo. Kwenye hili hamna ufafanuzi, hakuna principle wala sheria za kifizikia zinazoweza kuendana na theory hii lakini kwa hakika nguvu hiyo ipo na effects zake zinaonekana kwa vipimo. Mfano kupanuka kwa universe. Hata phenomenon za ajabu kabisa katika maeneo yaliyoko mbali sana katika ulimwengu zinahusishwa na nguvu hii pale ambapo ufafanuzi wa sayansi na fizikia ya kawaida unagonga mwamba.

Ubarikiwe mkuu Monstgala/Mgalanjuka, tukiachana na hii kitu ya dark energy naomba unieleweshe mwanzo wa hii kitu inaitwa ozone layer, hii kitu ilitengenezwaje?? Pia ningependa pia kufaham ina nguvu kiasi gani kiasi cha kutulinda sisi and our local planet?? Ina ukubwa gani nikimaanisha diameter kutoka upande wa ndani mpaka nje

.made in mby city.
 
Last edited by a moderator:
hii ni faida mojawapo ya kuwepo JF! tunashukuru sana mkuu! sasa wakuu ile topiki ua UMFO sikifanikiwa kuisoma, nawezaje kuipata kwa sasa!! thanks
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom