Ukweli wa magari kuhusiana na kasumba kwamba kuna gari mbovu au ina makosa

Uzi umenoga sana, Naomba wenye uzoefu wa magari fulani fulani wataje weakness/madhaifu yake kwa matumizi ya hapa Bongo. Najua wengi tumeangukia kwenye hilo kundi la kununua magari bila kufanya Utafiti wa kina.
Mfano:
  1. nissan dualis/Murano nyingi zinalalamikiwa kuwa na matatizo ya umeme,
  2. Crown watu wana lalamika udhaifu wa shockups
  3. Rav4 zenye 2az-fe engine kuchoma sana oil....
  4. ...
  5. ...
 
Kwa dualis hebu pitia hii link hapa ya jamaa twitter kuna mengi utayaelewa na binafsi based on experience niko upande wake

Uzi umenoga sana, Naomba wenye uzoefu wa magari fulani fulani wataje weakness/madhaifu yake kwa matumizi ya hapa Bongo. Najua wengi tumeangukia kwenye hilo kundi la kununua magari bila kufanya Utafiti wa kina.
Mfano:
  1. nissan dualis/Murano nyingi zinalalamikiwa kuwa na matatizo ya umeme,
  2. Crown watu wana lalamika udhaifu wa shockups
  3. Rav4 zenye 2az-fe engine kuchoma sana oil....
  4. ...
  5. ...
3. Utembee na chupa ya oil..
Taa ikiwaka ongeza..!
Ni changamoto ambayo ni rahisi kuishi nayo..!
 
[emoji3][emoji3][emoji3] hii ni kwa gari gani kaka kati ya hizo alizoomba mdau ushauri
 
Za siku wakubwa. Leo naomba niwaletee uzi ambao asili yake ni kutoka kwenye group letu la whatsapp la ISAL Motors juu ya malalamiko kwamba kuna gari fulani ni bora kuliko ingine kwamaana ya kudumu na kutokusumbua. Naomba niwaambie kitu kimoja trust me hakuna gari mbaya bali huwa tunajiuliza tunanunua magari kwa sababu zipi waafrika na wazungu tofauti yetu ndo iko hapa.

Wengi wananunua gari sababu eti ina mwonekano mzuri yaani unamkuta mtu anakwambia yani mi gari fulani naipenda tu yani hata nikiwa vipi ntakuja tu kuinunua. Mwingine labda sababu kuna wenzake wengi wanazo mfano vijana wa mjini kuna kipindi huwaambii kitu kuhusiana na Alteza wakazinunua kama njugu baadae upepo ukabadilika ukaamia kwenye crown lakin nakumbuka wakati tunakua kulikua kuna kipindi cha chaser sijui baloon ikaja mark two yan kuna mtu ananunua gari sababu tu its on trending. Alaf kuna mtu ananunua gari fulani sababu tu ataonekana mtu wa hadhi fulani wazungu wanaita for prestige kama sikosei yani ile sifa tu kwamba fulani anamiliki gar fulani kali sana.

Trust me yani kama unanunua gari kwa sababu yoyote kati ya hizo nikizozitaja hapo juu andika wewe utakua ni mtu wa kulia kila siku unless uko na pesa ndefu ambayo si ya mawazo. Yes kuna mwanangu (sitomtaja jina) aliwahi pata ajali pale maeneo ya dar free market ni ajali ambayo wengi watakuwa wanaikumbuka. Yeye alikua na subaru WRX alimgonga mwamba alikuwa na crown kama sikosei. Siwezi elezea hii ajali lakini ile subaru ya jamaa yangu ilipasuka rejeta kioo kilikua na ufa pia alivunja taa na rim ilipinda ya tairi ya mbele moja. Huwez amini jamaa aliagiza WRX mpya afu fresh kabisa coz ni chizi subaru. Mtu kama huyo mwanangu naomba ni mu exclude maana huwez mkuta akikaa akilalamika kwamba labda prado zinachomokaga tyre au zina ubovu fulani ambao hautibiki.

Nishawahi sikia sana watu wakilalamikia nissan x trail na kuna mzee anayo namba b mpaka leo anapeta nayo na hana presha nkimuuliza ananiambia ina shida za kawaida tu kama changamoto nyingine kwenye magari mengine ambazo zinatatulika. Kiufupi wabongo alieturoga ni mtu mmoja maana huwa hatuna sana udadisi wa mambo. Hizi nissan tunazozilalamikia kila siku kwamba gari mbovu sijui nini ndo gari zilizojazana Nairobi na wanaishi nazo vema kama tunavoishi na toyota hapa Tz sasa ushawahi jiuliza shida iko wapi? Nadhani kuna picha mpaka hapo umeipata akilini mwako wakati nakuleta kwenye mada halisi.

Yani bila kupepesa macho niseme tu wabongo huwa hatujui ni nini tunataka kwa wakati gani na kwa matumizi gani. Yani ukishajua haya. Yote basi hutokaa ukalalamika kuhusiana na gari yoyote utakayoimiliki katika maisha yako. Mimi naamini hakuna gari mbovu au yenye shida fulani kwani zimepita na kukaguliwa vitu vingi sana mpaka kufikia wewe unaendesha hiyo gari. Kuna uzi fulani niliusoma twitter jamaa alisema point kubwa sana ingawa sitoielezea kwa mtiririko aliouongea ila ntaielezea kwa namna nilivoelewa kwamba unamiliki ngamia umeishi nae sana ila baadae ukaja kumiliki farasi lakini matunzo yake unayompa ni kama yale ya ngamia mfano ngamia anatoboa wiki hanywi maji wala chakula alaf umekuja kumiliki farasi unaenda nae kama ulivokua unaishi na ngamia trust me broh utasema hawa wanyama ni legelege sana wala si wastahimilivu. Point yangu hapo igeuze kwenye gari mfano unamiliki starlet zile za zamani alaf ukaja kumiliki crown alaf utunzaji wake unaendelea na mazoea ya starlet trust me utaishia kusema hizi gari ni mbovu zina shida fulani fulani na fulani kumbe ni ww tu.

Kuna hii kasumba imekuja kwamba hizi Nissan dualis huwa zinaungua sana sasa ndugu yangu uliponunua corola yako limited ukaenda kwa fundi mtaani akakuwekea mziki taa kali sijui ukaweka na makolokolo kibao alaf maisha yalaemsa ukaona dualis watu wengi wanazo au ukapenda ilivo basi ukajaaliwa ukainunua then ukarudi kwa yule fundi wako ukamwambia "Nifanyie kama ulivofanya kwenye corola kipindi naiununua maana nilifaidi sana mziki na taa nlikua naona vema" alafu ikaja kuungua hiyo dualis kweli utalalamika kwamba gari ni mbovu zinaungua? come on ndugu zangu hakuna kitu ka hiko.

Hivi ni wangapi ambao gari aliyoinunua aliifanyia tafiti au aliisoma kabla ya kuimiliki au hata baada ya kuinunua alitumia muda kusoma kile kipeperushi cha maelezo na maelekezo ya gari? Kiufupi kama huijui gari yako na unaishi nayo basi shukuru Mungu kwa kukulinda kipindi chote ulichokuwa nayo. Si kwamba nawananga wakuu wangu bali ni katika kupeana elimu tu ili mwisho wa siku wote tuwe safe alaf baada ya hapo ndo tuseme ni mipango ya Mungu lakini si sasa kipindi tunafanya uzembe.

JE NI KWELI KWAMBA KUNA GARI ZINA SHIDA?
Kiufupi mimi huwa siamini katika hili bali nachoamini ni kwamba kila gari imetengenezwa kwa mazingira fulani ambayo ukiyatumia abadani hutokuja kuwa mlalamishi . Kiufupi ni kwamba pindi unapotaka kununua gari kikubwa angalia vitu viwili kwanza angalia mfuko wako utaweza kuhudumia gari hiyo? Mfano mzuri ni hizi gari ambazo ni tofauti na toyota mfano Mazda, Isuzu, Honda, Nissan, BMW, FORD nk kwa hapa Bongo huwa vifaa vyake bei ziko juu sasa jiulize nitakapomiliki gari hii ntaweza kuhudumia kwenye upande wa service? Matokeo yake ndo pale unapoimiliki alaf kwenye service unanunua vifaa ambavyo havina ubora kisa tu ni bei rahisi kwakweli kama ni shock up mjomba basi kila baada ya miezi mitano utakuwa unafunga mpya then mwisho wa siku utalalamika bwana hizi gari ugonjwa wake ni shockup maana kila siku nanunua mpya je ni original? Kuna mwingine atakwambia gari fulani ugonjwa wake ni engine zake zinakufa sana je mnatumia Recommended engine fluid au ndo unaenda dukan unaagiza tu. Nadhani point yangu imeeleweka hapo kikubwa kabla ya kununua jiulize utaweza kuimudu? Trust me guys kama gari ukifunga parts genuine au service ukafanya vile inavotakiwa basi watu wakipiga story za vijiweni we utakua unacheka tu na kutabasamu.

Pili angalia pindi unapotaka kununua gari angalia matumizi yako ni yepi je hilo gari litaweza kuhimili mikiki mikiki ya ruti zako? Mfano mtu anamiliki crown afu ruti zake kuiona lami ni kipengele yani yeye ni kupiga shimo mwanzo mwenga broh unachokitafuta utakipata. Kuna gari zimetengenezwa kwaajili ya mikiki mikiki ya off roads na kuna gari zimetengenezwa ni very luxurious yani. Mfano mzuri wengi huwa wanapenda kununua magari kwa wahindi sababu muhindi gari anaendeshea mjini tu yan gari inaweza ikakaa wiki nzima isigonge shimo yani ni palepale city center na ukimkuta mhindi ana gari ya offroad basi anapigaga shimo kwelikweli na wenzetu ni vile tu wengi wana uwezo unakuta ana gari mbili moja ya mjini ingine ni ya safari za kashkash sasa kama umejiona wewe ni mtu wa mazingira ya lami inataftwa kwa tochi au kila siku ni lazma njia yako upige shimo basi fanya maamuzi sahihi kabla hujaanza kulalamika. Na nafurahi kuona sikuhizi wauzaji au waagizaji wa magari huwa wana andaa threads mbalimbali za kuelezea magari na kutoa ushauri wa matumizi yake ni vile tu wabongo wengi sisi ni wavivu kusoma.

Mwisho naomba nielezee kuhusiana na hii kasumba ya spea. Watu wengi huwa wanalalamika Sana kuhusiana na kupatikana kwa spea original za magari. Wakuu dunia sasa ni kijiji hakuna spea ambayo haipatikan ni swala la pesa yako tu but zinapatikana vema kabisa. Binafsi mtu akinitafta na kuulizia spea hata kama inaonekana mpya kabisaa mimi namwambia ni mtumba na kama ni mpya namwambia ni mpya chaguo liwe lakwake but kununua spea mtumba ni safe zaidi kuliko og ambayo huna uhakika nayo kwamba ni kweli og. Now days watu wanakuletea mzigo wenyewe kabisa na wanakwambia ni mpya yenyewe baada ya simu kadhaa unalia. Uzuri wa spea mtumba huwa ni Original ambayo inakuwa imetoka kwenyw gari kama yakwako kwamaana imetengenezwa kiwandani so its pure og ni vile tu inakuwa imetumika kwa muda fulani nisingependa kuelezea sana nisije badilisha mada kuwa bango la biashara lakini naamini wakuu wangu mmepata darasa fulani na madini kadhaa kama kuna kasoro unaweza ongezea kwani namimi naendelea kujifunza na hakuna kitu napenda kama kujifunza. Kwa leo naomba tuishie hapo mpaka wakati mwingine.

Imeandikwa na Mgaya

Tunauza Spea za gari aina zote aina zote Taa, Mabampa, Milango, Show, Mountings, Engine, Gearbox, Radiator, shockups Nk. Tunapatikana ilala machinga complex tunaangaliana na msikiti wa songea Tucheki 0693163110 au 0655513132

View attachment 2519092
Mkuu unaijua vizuri Passo.. heheheee... nyiee acheni tuu. Tena upate ya pistoni 3.

Unaijua vizuri engine ya 1zz. Kanunue Allion, utakuja kutusimulia

Hizo ni kwa uchache tuu
 
Boss una passo ya piston tatu af unapiga ruti za dar mwanza mara musoma mtwara unategemea nini? Tumia hiyo gari kwa trip za town tu safari fupi fupi kama utaona shida. Allion ina shida gani?

Tatzo mkuu sidhani kama umenielewa. Hakuna gari isiyo na weakness hata moja ila matumizi yako ndo yanaenda kufumua mshono wa yale matatizo ila kama ukitumia kwa mazingira na matumizi yaliyo ndani ya uwezo wa gari huwez skia hizo shida
 
Magari,kama zilivyo bidhaa nyingine,yapo yenye ubora,yapo yasiyo na ubora.
Halikadhalika bado kuna mambo nje ya gari yenyewe,yanayosabisha kuonekana mbovu,au kuharibika haraka..Ikiwemo watumiaji,mazingira na ufundi.
 
Boss una passo ya piston tatu af unapiga ruti za dar mwanza mara musoma mtwara unategemea nini? Tumia hiyo gari kwa trip za town tu safari fupi fupi kama utaona shida. Allion ina shida gani?

Tatzo mkuu sidhani kama umenielewa. Hakuna gari isiyo na weakness hata moja ila matumizi yako ndo yanaenda kufumua mshono wa yale matatizo ila kama ukitumia kwa mazingira na matumizi yaliyo ndani ya uwezo wa gari huwez skia hizo shida
Msingi wako nimeuelewa vizuri sana, na point yako ya wabongo kutozingatia manuals ni ya msingi sana.

You still have to understand kua zipo gari sumbufu, delicate. Huo usemi wa mtaani kua gari flani zinasumbua, sio wa uongo.

Nimekupa mfano engine ya 1zz ni kubwa lakini kama ni mtu wa magari then utakua unaijua kua ni kichefuchefu

Swift

Steering rack za umeme ni ugonjwa hata iwe kwenye vanguard.

Point yako ni ya msingi ila elewa pia gari vimeo zipo
 
Mkuu unaijua vizuri Passo.. heheheee... nyiee acheni tuu. Tena upate ya pistoni 3.

Unaijua vizuri engine ya 1zz. Kanunue Allion, utakuja kutusimulia

Hizo ni kwa uchache tuu
Msingi wako nimeuelewa vizuri sana, na point yako ya wabongo kutozingatia manuals ni ya msingi sana.

You still have to understand kua zipo gari sumbufu, delicate. Huo usemi wa mtaani kua gari flani zinasumbua, sio wa uongo.

Nimekupa mfano engine ya 1zz ni kubwa lakini kama ni mtu wa magari then utakua unaijua kua ni kichefuchefu

Swift

Steering rack za umeme ni ugonjwa hata iwe kwenye vanguard.

Point yako ni ya msingi ila elewa pia gari vimeo zipo
Hapo umenena..
Hiyo 1ZZ changamoto ile mbaya..!
 
Msingi wako nimeuelewa vizuri sana, na point yako ya wabongo kutozingatia manuals ni ya msingi sana.

You still have to understand kua zipo gari sumbufu, delicate. Huo usemi wa mtaani kua gari flani zinasumbua, sio wa uongo.

Nimekupa mfano engine ya 1zz ni kubwa lakini kama ni mtu wa magari then utakua unaijua kua ni kichefuchefu

Swift

Steering rack za umeme ni ugonjwa hata iwe kwenye vanguard.

Point yako ni ya msingi ila elewa pia gari vimeo zipo
Boss hyo gari kuwa kimeo ni kwa mazingira yako na matumizi yako tu

Nimesema hapo juu Dualis hapa bongo zinaungua nyingine watu wanalalamika matatzo kibao lakini kwa ulaya ndo gari pendwa kilichobadilika ni jina tu.

Na katika hizo gari sumbufu unazosema kuna watu wanazo miaka hazijaleta shida au wao wanakuwa ni special order?
 
Umeshinda
Maana hutaki kuelewa
 
Umeshinda
Maana hutaki kuelewa
Nisipoelewa mimi haimaanishi wengine hawajaelewa ila cha msingi kila mtu kaona na atachagua wapi pa kuelewa mkuu ila i have got a point nawew una point thats fair. Kwenye pumba zangu watu wataacha kwenye point watachukua the same na kwako pia
 
Za siku wakubwa. Leo naomba niwaletee uzi ambao asili yake ni kutoka kwenye group letu la whatsapp la ISAL Motors juu ya malalamiko kwamba kuna gari fulani ni bora kuliko ingine kwamaana ya kudumu na kutokusumbua. Naomba niwaambie kitu kimoja trust me hakuna gari mbaya bali huwa tunajiuliza tunanunua magari kwa sababu zipi waafrika na wazungu tofauti yetu ndo iko hapa.

Wengi wananunua gari sababu eti ina mwonekano mzuri yaani unamkuta mtu anakwambia yani mi gari fulani naipenda tu yani hata nikiwa vipi ntakuja tu kuinunua. Mwingine labda sababu kuna wenzake wengi wanazo mfano vijana wa mjini kuna kipindi huwaambii kitu kuhusiana na Alteza wakazinunua kama njugu baadae upepo ukabadilika ukaamia kwenye crown lakin nakumbuka wakati tunakua kulikua kuna kipindi cha chaser sijui baloon ikaja mark two yan kuna mtu ananunua gari sababu tu its on trending. Alaf kuna mtu ananunua gari fulani sababu tu ataonekana mtu wa hadhi fulani wazungu wanaita for prestige kama sikosei yani ile sifa tu kwamba fulani anamiliki gar fulani kali sana.

Trust me yani kama unanunua gari kwa sababu yoyote kati ya hizo nikizozitaja hapo juu andika wewe utakua ni mtu wa kulia kila siku unless uko na pesa ndefu ambayo si ya mawazo. Yes kuna mwanangu (sitomtaja jina) aliwahi pata ajali pale maeneo ya dar free market ni ajali ambayo wengi watakuwa wanaikumbuka. Yeye alikua na subaru WRX alimgonga mwamba alikuwa na crown kama sikosei. Siwezi elezea hii ajali lakini ile subaru ya jamaa yangu ilipasuka rejeta kioo kilikua na ufa pia alivunja taa na rim ilipinda ya tairi ya mbele moja. Huwez amini jamaa aliagiza WRX mpya afu fresh kabisa coz ni chizi subaru. Mtu kama huyo mwanangu naomba ni mu exclude maana huwez mkuta akikaa akilalamika kwamba labda prado zinachomokaga tyre au zina ubovu fulani ambao hautibiki.

Nishawahi sikia sana watu wakilalamikia nissan x trail na kuna mzee anayo namba b mpaka leo anapeta nayo na hana presha nkimuuliza ananiambia ina shida za kawaida tu kama changamoto nyingine kwenye magari mengine ambazo zinatatulika. Kiufupi wabongo alieturoga ni mtu mmoja maana huwa hatuna sana udadisi wa mambo. Hizi nissan tunazozilalamikia kila siku kwamba gari mbovu sijui nini ndo gari zilizojazana Nairobi na wanaishi nazo vema kama tunavoishi na toyota hapa Tz sasa ushawahi jiuliza shida iko wapi? Nadhani kuna picha mpaka hapo umeipata akilini mwako wakati nakuleta kwenye mada halisi.

Yani bila kupepesa macho niseme tu wabongo huwa hatujui ni nini tunataka kwa wakati gani na kwa matumizi gani. Yani ukishajua haya. Yote basi hutokaa ukalalamika kuhusiana na gari yoyote utakayoimiliki katika maisha yako. Mimi naamini hakuna gari mbovu au yenye shida fulani kwani zimepita na kukaguliwa vitu vingi sana mpaka kufikia wewe unaendesha hiyo gari. Kuna uzi fulani niliusoma twitter jamaa alisema point kubwa sana ingawa sitoielezea kwa mtiririko aliouongea ila ntaielezea kwa namna nilivoelewa kwamba unamiliki ngamia umeishi nae sana ila baadae ukaja kumiliki farasi lakini matunzo yake unayompa ni kama yale ya ngamia mfano ngamia anatoboa wiki hanywi maji wala chakula alaf umekuja kumiliki farasi unaenda nae kama ulivokua unaishi na ngamia trust me broh utasema hawa wanyama ni legelege sana wala si wastahimilivu. Point yangu hapo igeuze kwenye gari mfano unamiliki starlet zile za zamani alaf ukaja kumiliki crown alaf utunzaji wake unaendelea na mazoea ya starlet trust me utaishia kusema hizi gari ni mbovu zina shida fulani fulani na fulani kumbe ni ww tu.

Kuna hii kasumba imekuja kwamba hizi Nissan dualis huwa zinaungua sana sasa ndugu yangu uliponunua corola yako limited ukaenda kwa fundi mtaani akakuwekea mziki taa kali sijui ukaweka na makolokolo kibao alaf maisha yalaemsa ukaona dualis watu wengi wanazo au ukapenda ilivo basi ukajaaliwa ukainunua then ukarudi kwa yule fundi wako ukamwambia "Nifanyie kama ulivofanya kwenye corola kipindi naiununua maana nilifaidi sana mziki na taa nlikua naona vema" alafu ikaja kuungua hiyo dualis kweli utalalamika kwamba gari ni mbovu zinaungua? come on ndugu zangu hakuna kitu ka hiko.

Hivi ni wangapi ambao gari aliyoinunua aliifanyia tafiti au aliisoma kabla ya kuimiliki au hata baada ya kuinunua alitumia muda kusoma kile kipeperushi cha maelezo na maelekezo ya gari? Kiufupi kama huijui gari yako na unaishi nayo basi shukuru Mungu kwa kukulinda kipindi chote ulichokuwa nayo. Si kwamba nawananga wakuu wangu bali ni katika kupeana elimu tu ili mwisho wa siku wote tuwe safe alaf baada ya hapo ndo tuseme ni mipango ya Mungu lakini si sasa kipindi tunafanya uzembe.

JE NI KWELI KWAMBA KUNA GARI ZINA SHIDA?
Kiufupi mimi huwa siamini katika hili bali nachoamini ni kwamba kila gari imetengenezwa kwa mazingira fulani ambayo ukiyatumia abadani hutokuja kuwa mlalamishi . Kiufupi ni kwamba pindi unapotaka kununua gari kikubwa angalia vitu viwili kwanza angalia mfuko wako utaweza kuhudumia gari hiyo? Mfano mzuri ni hizi gari ambazo ni tofauti na toyota mfano Mazda, Isuzu, Honda, Nissan, BMW, FORD nk kwa hapa Bongo huwa vifaa vyake bei ziko juu sasa jiulize nitakapomiliki gari hii ntaweza kuhudumia kwenye upande wa service? Matokeo yake ndo pale unapoimiliki alaf kwenye service unanunua vifaa ambavyo havina ubora kisa tu ni bei rahisi kwakweli kama ni shock up mjomba basi kila baada ya miezi mitano utakuwa unafunga mpya then mwisho wa siku utalalamika bwana hizi gari ugonjwa wake ni shockup maana kila siku nanunua mpya je ni original? Kuna mwingine atakwambia gari fulani ugonjwa wake ni engine zake zinakufa sana je mnatumia Recommended engine fluid au ndo unaenda dukan unaagiza tu. Nadhani point yangu imeeleweka hapo kikubwa kabla ya kununua jiulize utaweza kuimudu? Trust me guys kama gari ukifunga parts genuine au service ukafanya vile inavotakiwa basi watu wakipiga story za vijiweni we utakua unacheka tu na kutabasamu.

Pili angalia pindi unapotaka kununua gari angalia matumizi yako ni yepi je hilo gari litaweza kuhimili mikiki mikiki ya ruti zako? Mfano mtu anamiliki crown afu ruti zake kuiona lami ni kipengele yani yeye ni kupiga shimo mwanzo mwenga broh unachokitafuta utakipata. Kuna gari zimetengenezwa kwaajili ya mikiki mikiki ya off roads na kuna gari zimetengenezwa ni very luxurious yani. Mfano mzuri wengi huwa wanapenda kununua magari kwa wahindi sababu muhindi gari anaendeshea mjini tu yan gari inaweza ikakaa wiki nzima isigonge shimo yani ni palepale city center na ukimkuta mhindi ana gari ya offroad basi anapigaga shimo kwelikweli na wenzetu ni vile tu wengi wana uwezo unakuta ana gari mbili moja ya mjini ingine ni ya safari za kashkash sasa kama umejiona wewe ni mtu wa mazingira ya lami inataftwa kwa tochi au kila siku ni lazma njia yako upige shimo basi fanya maamuzi sahihi kabla hujaanza kulalamika. Na nafurahi kuona sikuhizi wauzaji au waagizaji wa magari huwa wana andaa threads mbalimbali za kuelezea magari na kutoa ushauri wa matumizi yake ni vile tu wabongo wengi sisi ni wavivu kusoma.

Mwisho naomba nielezee kuhusiana na hii kasumba ya spea. Watu wengi huwa wanalalamika Sana kuhusiana na kupatikana kwa spea original za magari. Wakuu dunia sasa ni kijiji hakuna spea ambayo haipatikan ni swala la pesa yako tu but zinapatikana vema kabisa. Binafsi mtu akinitafta na kuulizia spea hata kama inaonekana mpya kabisaa mimi namwambia ni mtumba na kama ni mpya namwambia ni mpya chaguo liwe lakwake but kununua spea mtumba ni safe zaidi kuliko og ambayo huna uhakika nayo kwamba ni kweli og. Now days watu wanakuletea mzigo wenyewe kabisa na wanakwambia ni mpya yenyewe baada ya simu kadhaa unalia. Uzuri wa spea mtumba huwa ni Original ambayo inakuwa imetoka kwenyw gari kama yakwako kwamaana imetengenezwa kiwandani so its pure og ni vile tu inakuwa imetumika kwa muda fulani nisingependa kuelezea sana nisije badilisha mada kuwa bango la biashara lakini naamini wakuu wangu mmepata darasa fulani na madini kadhaa kama kuna kasoro unaweza ongezea kwani namimi naendelea kujifunza na hakuna kitu napenda kama kujifunza. Kwa leo naomba tuishie hapo mpaka wakati mwingine.

Imeandikwa na Mgaya

Tunauza Spea za gari aina zote aina zote Taa, Mabampa, Milango, Show, Mountings, Engine, Gearbox, Radiator, shockups Nk. Tunapatikana ilala machinga complex tunaangaliana na msikiti wa songea Tucheki 0693163110 au 0655513132

View attachment 2519092
Gari nyingi tu zinatoka kiwandani na shida ndio maana kunakuwa na recalls.

Wanaozidisi Murano siyo kwa ubaya, transmission nyingi za CVT za nissan ni kichefuchefu. JATCO Mungu anawaona.

Kuna gari ili iwe durable utahitaji kuimaintain kama ndege.(Preventive Maintenance za kutosha).

Asilimia kubwa ya BMW from 90s, unakuta Cooling system pekee ina seals 20+ au 30+ na maplastic kibao, ukutaka kuendesha mpaka likuzimie ndio ukumbuke kurekebisha with time utalia milio yote.

Hapo engine inataka 95 octane petrol. Halafu mtu anakoishi mafuta ni ya vidumu. Atatoboa kweli?.
 
Maboko ni mengi.. Hayawezi kutosha hapa..
2AZ FE.. hii engine common sana hapa.. Hata uitunze vipi itakula oil..!

Hata ukichunguza ukajua namna ya kuishi nayo.. Haiondoi concept ya gari ina matatizo..!

Tofautisha brand new na new model..
2010 inaweza kuwa new model..!
Series ya AZ zote zinabugia Oil.
 
Kuna engine zinagonga 200k bila shida yoyote.
Kwa ulaya watu hawatumii gari mpaka kufikia 200k so mtu unapotaka kununua gari unatakiwa kujua aina hizi za gari so that uweze kuish nayo muda mrefu. Ulaya mtu anatumia gar km 20000 au 30000 gari inakua imekwisha choka kwake so hayo matatizo ya kula oil au ku breez au nini hawez kuyaona sabab hafikii huko na hata mazingira yao yanafanya haya matatizo tunayoyaongelea yasionekane. Solution ni kujua aina ya gari unayoenda kununua itaweza kuhimili? Fikiria mkuu tuseme hizi aina za engine zenye matatizo znapofika km fulani zipo lakin hushangai watu bado wanaendelea kununua?
Kuna mdau hapo juu nimempa ushauri kama unajua gari fulani hazitaki kitu fulani either mazingira au labda zikifika umbali fulani zinasumbua kwanini tunanunua tena kwa wingi ili kesho uanze kulalamika? Kuna watu hapo juu wamenibishia tu wengine ili waonekane wanabisha, wengine wana hoja lakin nimeongea gari zote hakuna gari isiyo na weakness ilimradi tu imeumwa na wanadamu basi lazma iwepo weakness yani lazima ila matumizi yetu ndo yanafanya hzo weakness zionekane kwa sana mfano engine zenye shida ya kula oil namna ya kuepuka ni kuhakikisha oil level yako ipo sawa muda wote which means service ufanye mara kwa mara gari inakuwa inachekiwa kitu ambacho ni very rare kwa bongo sasa kama ni hivo huna huo uwezo kwanini ununue? Lakini watu hawajui wanaendelea kuzinunua kama njugu
 
Gari nyingi tu zinatoka kiwandani na shida ndio maana kunakuwa na recalls.

Wanaozidisi Murano siyo kwa ubaya, transmission nyingi za CVT za nissan ni kichefuchefu. JATCO Mungu anawaona.

Kuna gari ili iwe durable utahitaji kuimaintain kama ndege.(Preventive Maintenance za kutosha).

Asilimia kubwa ya BMW from 90s, unakuta Cooling system pekee ina seals 20+ au 30+ na maplastic kibao, ukutaka kuendesha mpaka likuzimie ndio ukumbuke kurekebisha with time utalia milio yote.

Hapo engine inataka 95 octane petrol. Halafu mtu anakoishi mafuta ni ya vidumu. Atatoboa kweli?.
Angalau umepata point yangu mkuu hapo kwenye maintanance ya kutosha which means kama gari haina hiyo maintanance ya kutosha basi kila siku litazuka hilo tatizo ila kuna watu wanaweza kuzi maintain na wanaishi nazo mfano nimetoa hapa wa dualis ambayo inalalamikiwa lakini ulaya ndo gari pendwa. Sasa ili kuepuka yote hayo kwanini ununue while u cant maintain it?
 
Back
Top Bottom