Boss elewa point yangu. Gari unapoagiz inakua na km ngapi? Achana na china japan mzee ulaya gari zinakuja na km chache sababu mtu anaweza akatumia miaka kadhaa na asifikishe hizo km na hata hizo warrantee zinatoka sabab wanajua kwa matumizi yao huwez fika huko unless its transport car ambayo si tunazozizungumzia humu. Sasa fikiria kwa condition hiyo na mazingira hayo unafkiri first user ataona hayo madhaifu tunayoyaongelea bongo? Sisi tunaoenda km laki moja laki mbili ndo tutaona trust me sababu ya miundombinu yao watu wanatumia sana public transport hasa kwa safari za mbali hebu fikiria natoka dar naenda mwanza mfano kwa ndege ni masaa mawili matatu au kwa treni ni masaa may be matano kuna haja gani ya kuendesha masaa kumi na kutumia gharama wakati naweza tumia public transport?
Af mjomba wewe unavochukulia gari kuchoka kibongo bongo sio kama nchi za wenzetu kuna gari ngapi tunaletewa bongo zinahesabika zimechoka au zimezidi muda wanaotaka lakini zikija bongo ni mpya? Km 30,000 kwa umasikini wetu ni mpya ila wenzetu wanaonunua zero km hiyo gari kwao ishatumika na ishachoka. Huwa siongei kwa kukurupuka mzee naongea kwa ushahidi unless umekuja hapa ili kupinga kila nachoongea then nikuache na hiyo ego yako....
Bro iko hivi
Nimekaa Germany,France na Netherland
Kule gari zinatembea sio mchezo,kukuta gari ina km laki 2 ni kawaida sana endapo haimsumbui mtumiaji!
Ni kweli warranty nyingi ni 100,000km or 3 years whichever comes first!
Gari nyingi za zamani ukikuta mitandaoni ina km chake inawezekana gari ilikuwa sumbufu from the beginning
Mfano BMW ya 2007 ina 30,000km afu bei chee
Ifanyie tafiti,omba inspection report,maintenance records na accident history kabla hujanunua
Uchache wa ‘km’ hau justify uimara na bei ya gari[emoji845]
Tena gari zilizotembea km nyingi ni imara sana
Tembelea mitandaoni
Hizi hybrid car nyingi utakuta zinauzwa na ni 100,000km + na bado bei zimesimama
Jaribu kuangalia pia mfano
Mazda cx-5 nyingi zinaanzia kilometer laki moja mpk laki 2 lakini zinauzwa na zinatoka vizuri
Hii inamaanisha hizi hazikuleta usumbufu kwa previous owner ndo maana zikagonga 200,000km+
Kuna factors nyingi nje ya km chache[emoji28]