impongo
JF-Expert Member
- Feb 18, 2015
- 8,764
- 7,758
- Thread starter
- #541
Mkuu, wewe hujui dunia yetu inalindwa nini lakini hauamini uwepo wa Mungu na Mimi nimekuhakikishia kuwa Mungu yupo ndie anayeilinda Dunia na majanga na nime kuhakikishia kuwa Mungu ni roho haonekani kwa macho na wewe huna jicho la tatu nakuomba uwe na imani uwe na jicho la tatu utaamini na utajua kweli iliyofichika kwako usiye amini!Ni hivi.
Mimi kutojua jibu la nini kilikinga dunia na miale, hakumaanishi jibu ni mungu.
Mimi kutojua jibu la square root ya mbili, hakumaanishi square root ni kumi.
Ukisema square root ya mbilo ni kumi, inabidi unioneshe ni vipi umepata kumi.
Unaweza kuonesha ni kipi kinakufanya ufikiri Mungu ndiye aliyeikinga dunia na miale na si kitu kingine?
Halafu mbona hujaninibu swali langu?
Kama Mungu anapenda sana kuikinga dunia na majanga, kwa nini kaumba ulimwengu ambao mabaya yanaweza kutokea wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezi kutokea bila kupungukiwa lolote?
Hujajibu swali hili.
Kwanini hakuumba ulimwengu ambao uko shwari bila purukushani na majanga yasiwepo!
Mungu alimuumba mwanadamu ili mwanadamu amtukuze alimpa akili ya kujitambua akaumba vyote vilivyomo ktk inchi na ulimwengu akaumba vilivyo vyema na viovu vyote ni vyake jukum ni lako kutambua nini ukifanye una akili timamu ndio sababu unaziona tabu,vita,shida,majanga, kama binadamu tukijitambua na kuishi kwa kumpendeza Mungu haya yote hayawezi kuwepo.
Kama wewe hauamini uwepo wa Mungu na haujui nini kinailinda dunia na majanga makubwa basi niamini Mimi Mungu ndie anayetulinda.
HAUAMINI CHOCHOTE BASI AMINI ON NACHO KUELEZA kumbuka hata ulipo anza shule ulifunzwa 1+1 ndio ukaelewa.
Anza upya haujakosea Mungu ni mwenye huruma atakufundisha utaelewa.