Ukweli wa uwepo wa Mungu na Makazi yake upo hapa

Ni hivi.

Mimi kutojua jibu la nini kilikinga dunia na miale, hakumaanishi jibu ni mungu.

Mimi kutojua jibu la square root ya mbili, hakumaanishi square root ni kumi.

Ukisema square root ya mbilo ni kumi, inabidi unioneshe ni vipi umepata kumi.

Unaweza kuonesha ni kipi kinakufanya ufikiri Mungu ndiye aliyeikinga dunia na miale na si kitu kingine?

Halafu mbona hujaninibu swali langu?

Kama Mungu anapenda sana kuikinga dunia na majanga, kwa nini kaumba ulimwengu ambao mabaya yanaweza kutokea wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezi kutokea bila kupungukiwa lolote?

Hujajibu swali hili.
Mkuu, wewe hujui dunia yetu inalindwa nini lakini hauamini uwepo wa Mungu na Mimi nimekuhakikishia kuwa Mungu yupo ndie anayeilinda Dunia na majanga na nime kuhakikishia kuwa Mungu ni roho haonekani kwa macho na wewe huna jicho la tatu nakuomba uwe na imani uwe na jicho la tatu utaamini na utajua kweli iliyofichika kwako usiye amini!

Kwanini hakuumba ulimwengu ambao uko shwari bila purukushani na majanga yasiwepo!
Mungu alimuumba mwanadamu ili mwanadamu amtukuze alimpa akili ya kujitambua akaumba vyote vilivyomo ktk inchi na ulimwengu akaumba vilivyo vyema na viovu vyote ni vyake jukum ni lako kutambua nini ukifanye una akili timamu ndio sababu unaziona tabu,vita,shida,majanga, kama binadamu tukijitambua na kuishi kwa kumpendeza Mungu haya yote hayawezi kuwepo.

Kama wewe hauamini uwepo wa Mungu na haujui nini kinailinda dunia na majanga makubwa basi niamini Mimi Mungu ndie anayetulinda.

HAUAMINI CHOCHOTE BASI AMINI ON NACHO KUELEZA kumbuka hata ulipo anza shule ulifunzwa 1+1 ndio ukaelewa.
Anza upya haujakosea Mungu ni mwenye huruma atakufundisha utaelewa.
 
Hayo maswali ni mazito sana lakini jamaa kayajibu kisiasa siasa tu kwa mifano mifano mingi hadi kapoteza mantiki yote ya swali...!!

Yaani mtu unamuuliza swali nae anakujibu kwa kuuliza swali tena sio swali maswali... anajua sana kudiverge mjadala kwenye comfort zone yake.
Mkuu tatizo la Kiranga sijui ni nini!
Haamini uwepo wa Mungu lakini hajui nini kinailinda Dunia na majanga makubwa,.
Nimemuuliza ktk science anayoiamini bado amekosa majibu ni dhahiri jibu analo anaamini Mungu labda ni challenge au ni mtu mbishi au anataka kujifunza zaidi.

Mfano mdogo; Sayari na nyota na vyote vilivyomo ktk ulimwengu vimekuwapo na mwanzo ni Mlipuko (Big Bang) ya mkusanyiko uliounda Maumbo mbali mbali Joto lililo kuwapo ni kali sana ambapo aridhi hii ya dunia yetu ilichukua miaka billion kupoa na maisha yakaanza!
Nini kimepandikiza uhai?
Uhai umetoka wp?
Hajui lakini haamini uwepo wa Mungu.
Anadai kuna kitu kingine kinatulinda ila hakijui+
Kiranga ni pasua kichwa
 
Hajui kini haamini uwepo wa Mungu.
Anadai kuna kitu kingine kinatulinda ila hakijui+
Kiranga ni pasua kichwa
Unajua huyu jamaa hapo mwanzo nilivyoanza kumuona akibishana na watu humu kuhusu mada hii ya uwepo wa MUNGU na yeye kuonekana akipinga uwepo wake nilidhani labda jamaa ni fame chaser tu sababu ni nadra sana kukutana na watu wa dizaini yake, lakini kadri siku zinavyokwenda nikaja kugundua kuwa jamaa ni true atheist japo huo uatheist wake yeye mwenyewe una mpwaya kwa maana bado hajawa na argument za kutosha kuback his disbeliefs in God.

Na maswali kama hayo uliyomuuliza hata akikujibu majibu yake mengi yamekaa kisiasa zaidi na ni mzuri sana wakuamisha mantiki ya kitu ulichomuuliza akitumia maswali yake mengi kwenye kutackle swali na kujikuta huko kwenye comfort zone yake.

Ukimuuliza miujiza inayotokea katika dunia hii chanzo chake ni nini!!? anakwambia unajua kama ni Mungu na sio kitu kingine!!?
.
Alafu pia anaamimi kwamba dini ya Freemasonry ipo lakin haina uhusiano wowote na shetani...!! Sasa wana uhusiano na nani wakati dunia inafahamu wanachama wake ni devil worshippers!!?

Jamaa mbishi sana mpaka kero japo yuko sawa upstair.
 
Kukubali mawazo ya mtu mwingine kuna ubaya gani? Hususan kama yanaonesha contradiction katika dhana nzima ya huyo mungu wenu kuwepo?

Unaweza kuthibitisha mungu yupo?
Unajua katika science tunaambiwa kwamba kila jambo lina sababu ya kuwepo kwake na linaweza kuzuiliwa litokee au lisitokee yaani kifupi kila jambo linawezakana na hakuna kinachoshindikana chini ya jua.

Sasa kuna vitu vingi tu mbona ambavyo vimekuwa vikiumiza vichwa vya hao wanasayansi katika kuviweka namna wanavyotaka wao na wakashindwa.

Kwa mfano devil triangle ni eneo ambalo mpaka leo hii hakuna wanasayansi wenye ufahamu wa kutosha kuhusu eneo lile.... najua utakuwa unajua ni ajali ngapi za vyombo vya anga na maji tangu vita ya kwanza ya dunia zimewahi kutokea baada ya vyombo hivyo kupita usawa wa eneo lile.... Ndio maana hadi leo pataitwa devil triangle kwa sababu hata wanasayansi wenyewe wameshindwa kupaelewa ni nini hasa kinachosababisha ajali hizo na kwani eno lile liwe tofauti na maeneo mengine yote ya bahari katika dunia hii.!!?

Sasa uwepo wa mysterious feature kama hiyo katika uso wa dunia na nyinginezo huoni kwamba ni miujiza ambayo chanzo chake ni Mungu!!?

NASEMA MUNGU YUPO NA HATA WEWE KIRANGA ANAKUPENDA.
 
Mkuu, wewe hujui dunia yetu inalindwa nini lakini hauamini uwepo wa Mungu na Mimi nimekuhakikishia kuwa Mungu yupo ndie anayeilinda Dunia na majanga na nime kuhakikishia kuwa Mungu ni roho haonekani kwa macho na wewe huna jicho la tatu nakuomba uwe na imani uwe na jicho la tatu utaamini na utajua kweli iliyofichika kwako usiye amini!

Hujathibitisha, umehubiri tu.Tofautisha kuthibitisha na kuhubiri.

Kwanini hakuumba ulimwengu ambao uko shwari bila purukushani na majanga yasiwepo!
Mungu alimuumba mwanadamu ili mwanadamu amtukuze

Kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote ahitaji kutukuzwa na watu?

Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao atatukuzwa na watu bila ulimwengu huo kuwa na uovu?

Kwa nini mtu mwenye hela ziszo kikomo ahitaji senti moja ya sisimizi?

alimpa akili ya kujitambua

Kwa nini hakuwapa binadamu wote akili ya kutambua kwamba Mungu yupo bila uwezekano wa swali lolote kuhusu hilo?

akaumba vyote vilivyomo ktk inchi na ulimwengu akaumba vilivyo vyema na viovu vyote ni vyake

Kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aumbe viovu wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao hauna viovu?

Hili ndilo swali.

Ukisema aliumba viovu, unarudis swali. Hujibu swali. Kwamba kaumba viovu ishasemwa kwenye swali. A given. Hilo si swali. Swali ni, kwa nini kaumba viovu wakati ana na alikuwa na uwezo wote wa kuumba ulimwengu ambao viovu haviwezekani bila kupungukiwa kitu?

Hujajibu swali hili.

jukum ni lako kutambua nini ukifanye una akili timamu ndio sababu unaziona tabu,vita,shida,majanga, kama binadamu tukijitambua na kuishi kwa kumpendeza Mungu haya yote hayawezi kuwepo.

Hujajibu swali. Unalikwepa tu. Kwa nini Mungu kaumba ulimwengu ambao maovu yanawezekana wakati alikuwa na kila uwezo, upendo na ujuzi wa kuumba ulimwengu ambao maovu hayawezekani bila ya kupungukiwa chochote?

Kama wewe hauamini uwepo wa Mungu na haujui nini kinailinda dunia na majanga makubwa basi niamini Mimi Mungu ndie anayetulinda.

Unahubiri. Sitaki mahubiri. Nataka uthibitisho. Thibitisha. Usihubiri.

HAUAMINI CHOCHOTE BASI AMINI ON NACHO KUELEZA kumbuka hata ulipo anza shule ulifunzwa 1+1 ndio ukaelewa.
Anza upya haujakosea Mungu ni mwenye huruma atakufundisha utaelewa.

Kwa nini unafikiri wewe ndiye wa kunifundisha mimi na si mimi wa kukufundisha wewe ikiwa huyo Mungu wako unayemuamini wewe, wewe mwenyewe humuelewi na wala huwezi kumuelezea?
 
Unajua katika science tunaambiwa kwamba kila jambo lina sababu ya kuwepo kwake na linaweza kuzuiliwa litokee au lisitokee yaani kifupi kila jambo linawezakana na hakuna kinachoshindikana chini ya jua.

Sasa kuna vitu vingi tu mbona ambavyo vimekuwa vikiumiza vichwa vya hao wanasayansi katika kuviweka namna wanavyotaka wao na wakashindwa.

Kwa mfano devil triangle ni eneo ambalo mpaka leo hii hakuna wanasayansi wenye ufahamu wa kutosha kuhusu eneo lile.... najua utakuwa unajua ni ajali ngapi za vyombo vya anga na maji tangu vita ya kwanza ya dunia zimewahi kutokea baada ya vyombo hivyo kupita usawa wa eneo lile.... Ndio maana hadi leo pataitwa devil triangle kwa sababu hata wanasayansi wenyewe wameshindwa kupaelewa ni nini hasa kinachosababisha ajali hizo na kwani eno lile liwe tofauti na maeneo mengine yote ya bahari katika dunia hii.!!?

Sasa uwepo wa mysterious feature kama hiyo katika uso wa dunia na nyinginezo huoni kwamba ni miujiza ambayo chanzo chake ni Mungu!!?

NASEMA MUNGU YUPO NA HATA WEWE KIRANGA ANAKUPENDA.
Hapa ulichosema ni kama mtu anayesema.

Hatujui square root ya mbili ni nini.

Lakini square root ya mbili lazima itakuwa kumi.

Mimi nitakuuliza swali dogo tu.

Unaweza kuthibitisha kwamba square root ya mbili ni kumi?

Unaweza kuthibitisha kwamba kupotea kwa meli hiyo devils triangle kunatokana na Mungu?

Na kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote apoteze meli? Hana kitu kingine muhimu zaidi cha kufanya?
 
Hujathibitisha, umehubiri tu.Tofautisha kuthibitisha na kuhubiri.

Kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote ahitaji kutukuzwa na watu?

Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao atatukuzwa na watu bila ulimwengu huo kuwa na uovu?

Kwa nini mtu mwenye hela ziszo kikomo ahitaji senti moja ya sisimizi?

Kwa nini hakuwapa binadamu wote akili ya kutambua kwamba Mungu yupo bila uwezekano wa swali lolote kuhusu hilo?

Kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aumbe viovu wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao hauna viovu?

Hili ndilo swali.

Ukisema aliumba viovu, unarudis swali. Hujibu swali. Kwamba kaumba viovu ishasemwa kwenye swali. A given. Hilo si swali. Swali ni, kwa nini kaumba viovu wakati ana na alikuwa na uwezo wote wa kuumba ulimwengu ambao viovu haviwezekani bila kupungukiwa kitu?

Hujajibu swali hili.

Hujajibu swali. Unalikwepa tu. Kwa nini Mungu kaumba ulimwengu ambao maovu yanawezekana wakati alikuwa na kila uwezo, upendo na ujuzi wa kuumba ulimwengu ambao maovu hayawezekani bila ya kupungukiwa chochote?

Unahubiri. Sitaki mahubiri. Nataka uthibitisho. Thibitisha. Usihubiri.

Kwa nini unafikiri wewe ndiye wa kunifundisha mimi na si mimi wa kukufundisha wewe ikiwa huyo Mungu wako unayemuamini wewe, wewe mwenyewe humuelewi na wala huwezi kumuelezea?
Katika maisha yangu sijawahi kukosa hitimisho ktk mijadala na mambo mengi ninayo jifunza wewe unakuwa mtu unaye nifanya nisifike hitimisho hata kama kila kitu kipo wazi unakielewa.

Sijui kwa makusudi au ni ubishani lakini rejea katika sayansi ktk uwepo wa ulimwengu uhai umeanza kwa nguvu za asili (super natural) na kusitawi kwa kila aina ya kiumbe na mimea mpaka hivi sasa uhai unaendelea.
Mlipuko ambao ulisababisha kuwepo kwa sayari na nyota vyote vilivyomo kuipamba mbingu (ulimwengu) vimekuwapo kwa makusudi aliye sababisha mlipuko huo ndiye anajua alicho kidhamiria kukifanya.

Pia ilikuwa ni joto Kali lililopelekea billion ya miaka kwa dunia yetu kupoa na joto hilo lilichoma uhalisia wote wa kuwapo na mbegu ya chochote kuchipuka na Jua lilikuwa halina kizuizi cha miali ya sumu ilikuwa ikifika ktk dunia moja kwa moja ili miali isifike lazima kuwepo na oxygen na Maji itokee evaporation hewa ipande ifike ktk uksnda wa kati igande izuie miali ya sumu kufika duniani.

Mungu ndiye aliye Fanya haya yote!
Mungu ndiye chanzo cha uumbaji na kila ukionacho hata usicho ukiona.
Yeye ni Alpha na Omega Mwanzo na mwisho.

Mimi huo ni ushahidi wangu kwa Mungu ninaye mwamini lakini wewe usiye amini hauna ushahidi.

Niambie ni jina gani labda unapendekeza tumuite huyu muumbaji wa haya labda shida ni jina linakukanganya?
 
Hapa ulichosema ni kama mtu anayesema.

Hatujui square root ya mbili ni nini.

Lakini square root ya mbili lazima itakuwa kumi.

Mimi nitakuuliza swali dogo tu.

Unaweza kuthibitisha kwamba square root ya mbili ni kumi?

Unaweza kuthibitisha kwamba kupotea kwa meli hiyo devils triangle kunatokana na Mungu?

Na kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote apoteze meli? Hana kitu kingine muhimu zaidi cha kufanya?
Mkuu maswali yako yanalenga nini haswa mbona wewe ni mgumu wa kumwelewa mtu?
Wewe Unaamini ulimwengu ulikuwepo tu? Au Unaamini nini haswa?
Unacho kiamini huwezi kukithibitisha?
Isije kuwa tunajadiliana na mwanasiasa tunapoteza muda mwingi!
Tuthibitishie unacho kiamini?
 
Unajua katika science tunaambiwa kwamba kila jambo lina sababu ya kuwepo kwake na linaweza kuzuiliwa litokee au lisitokee yaani kifupi kila jambo linawezakana na hakuna kinachoshindikana chini ya jua.

Sasa kuna vitu vingi tu mbona ambavyo vimekuwa vikiumiza vichwa vya hao wanasayansi katika kuviweka namna wanavyotaka wao na wakashindwa.

Kwa mfano devil triangle ni eneo ambalo mpaka leo hii hakuna wanasayansi wenye ufahamu wa kutosha kuhusu eneo lile.... najua utakuwa unajua ni ajali ngapi za vyombo vya anga na maji tangu vita ya kwanza ya dunia zimewahi kutokea baada ya vyombo hivyo kupita usawa wa eneo lile.... Ndio maana hadi leo pataitwa devil triangle kwa sababu hata wanasayansi wenyewe wameshindwa kupaelewa ni nini hasa kinachosababisha ajali hizo na kwani eno lile liwe tofauti na maeneo mengine yote ya bahari katika dunia hii.!!?

Sasa uwepo wa mysterious feature kama hiyo katika uso wa dunia na nyinginezo huoni kwamba ni miujiza ambayo chanzo chake ni Mungu!!?

NASEMA MUNGU YUPO NA HATA WEWE KIRANGA ANAKUPENDA.
Mku pia Mungu ni mwenye upendo Kiranga hana dhambi maana alitendalo halijui
 
Mkuu maswali yako yanalenga nini haswa mbona wewe ni mgumu wa kumwelewa mtu?
Wewe Unaamini ulimwengu ulikuwepo tu? Au Unaamini nini haswa?
Unacho kiamini huwezi kukithibitisha?
Isije kuwa tunajadiliana na mwanasiasa tunapoteza muda mwingi!
Tuthibitishie unacho kiamini?
Kwa nini ninachoamini mimi kiwe muhimu wakati thread ni ukweli kuhusu uwepo wa Mungu?

Nikikwambia mimi naamini Papa Francis ni Mmakonde Maraba, tena ni Baba yake mkubwa rais Mkapa, na alimpigia kampeni sana katika kanisa katoliki mpaka Mkapa akawa rais, hilo litasaidia nini katika kujua kwamba Mungu yupo au hayupo?

Sitaki kuamini, nataka kujua.

Naamini huyo Mungu mnayemsema hayupo, angekuwepo ulimwengu usingekuwa hivi ulivyo.

Naamini jua litachomoza kesho asubuhi, japo lilipatwa leo.
 
Unajua huyu jamaa hapo mwanzo nilivyoanza kumuona akibishana na watu humu kuhusu mada hii ya uwepo wa MUNGU na yeye kuonekana akipinga uwepo wake nilidhani labda jamaa ni fame chaser tu sababu ni nadra sana kukutana na watu wa dizaini yake, lakini kadri siku zinavyokwenda nikaja kugundua kuwa jamaa ni true atheist japo huo uatheist wake yeye mwenyewe una mpwaya kwa maana bado hajawa na argument za kutosha kuback his disbeliefs in God.

Na maswali kama hayo uliyomuuliza hata akikujibu majibu yake mengi yamekaa kisiasa zaidi na ni mzuri sana wakuamisha mantiki ya kitu ulichomuuliza akitumia maswali yake mengi kwenye kutackle swali na kujikuta huko kwenye comfort zone yake.

Ukimuuliza miujiza inayotokea katika dunia hii chanzo chake ni nini!!? anakwambia unajua kama ni Mungu na sio kitu kingine!!?
.
Alafu pia anaamimi kwamba dini ya Freemasonry ipo lakin haina uhusiano wowote na shetani...!! Sasa wana uhusiano na nani wakati dunia inafahamu wanachama wake ni devil worshippers!!?

Jamaa mbishi sana mpaka kero japo yuko sawa upstair.
Mkuu kweli ni nadra watu wa namna hii ila anajikanganya sana anaposema kwanini kisiwe kitu kingine kilichofanya haya sasa Mimi nimemuomba abuni jina lingine tuite huyo muumbaji maana Mimi ninaloliona ni Mungu labda yeye anadhani akiita jina lingine atapata maana ingine na atajifurahisha nafsi
Hili jamaa lina challenge's Walimu wana kazi kumfunza Kiranga inahitaji dakika 360 kwa kipindi
 
Kwa nini ninachoamini mimi kiwe muhimu wakati thread ni ukweli kuhusu uwepo wa Mungu?

Nikikwambia mimi naamini Papa Francis ni Mmakonde Maraba, tena ni Baba yake mkubwa rais Mkapa, na alimpigia kampeni sana katika kanisa katoliki mpaka Mkapa akawa rais, hilo litasaidia nini katika kujua kwamba Mungu yupo au hayupo?
Mungu yupo hili halihitaji ushahidi! Katika moja ya post zako unaandika kwanini kisiwepo kingine kilichosababisha uhai je hicho unachokifikili wewe ndio Mungu mwenyewe muumbaji.

Makusudi mengine ya yeye kutuumba kuweka majanga mbali mbali Vita, njaa,umasikini, magonjwa,kifo,utajiri, yeye mwenyewe anajua kusudio lake.
Nyota na sayari katika anga na vilivyomo anajua yeye kusudio lake
 
Kwa nini ninachoamini mimi kiwe muhimu wakati thread ni ukweli kuhusu uwepo wa Mungu?

Nikikwambia mimi naamini Papa Francis ni Mmakonde Maraba, tena ni Baba yake mkubwa rais Mkapa, na alimpigia kampeni sana katika kanisa katoliki mpaka Mkapa akawa rais, hilo litasaidia nini katika kujua kwamba Mungu yupo au hayupo?

Sitaki kuamini, nataka kujua.

Naamini huyo Mungu mnayemsema hayupo, angekuwepo ulimwengu usingekuwa hivi ulivyo.

Naamini jua litachomoza kesho asubuhi, japo lilipatwa leo.
Unacho amini kinakuwa na umuhimu pale unapolenga mahala husika ila ukajikanganya katika matamushi.
1;anasema ni tobo
2;asema ni tundu
==>Mwalimu mwenye busara atawapa marks sawa maana tofauti ni matamushi ila mlicholenga ni kimoja.
 
Huwezi kuamini kuwa jua litachomoza wakati kila sekunde 1 hujui nini kitakukuta
 
Mungu yupo hili halihitaji ushahidi! Katika moja ya post zako unaandika kwanini kisiwepo kingine kilichosababisha uhai je hicho unachokifikili wewe ndio Mungu mwenyewe muumbaji.

Makusudi mengine ya yeye kutuumba kuweka majanga mbali mbali Vita, njaa,umasikini, magonjwa,kifo,utajiri, yeye mwenyewe anajua kusudio lake.
Nyota na sayari katika anga na vilivyomo anajua yeye kusudio lake
Hujathibitisha Mungu yupo.

Unahubiri tu.

Nimekuuliza kwa nini Mungu kaumba hivi, hakuumba vile, umesema hujui.

Kama hujui hata huyo Mungu wako anafanya vitu vipi, una hakika gani kwamba Imani yako kwamba yupo ni sahihi?

Humuelewi huyo Mungu. Huwezi kumuelezea kwa ufasaha.

Kwa nini unafikiri yupo wakati hata kumuelezea huwezi?
 
Huwezi kuamini kuwa jua litachomoza wakati kila sekunde 1 hujui nini kitakukuta
Unafahamu maana ya kuamini?

Unaweza kutoa definition ya kuamini na kunieleza kwa nini siwezi kuamini kwamba jua litachomoza, wakati nishakuambia naamini jua litachomoza?

Kitakachonikuta mimi kina uhusiano gani na jua kuchomoza?

Nikigongwa na gari na kufariki sekunde moja ijayo, jua likachomoza kesho, kugongwa kwangu na gari kutazuia jua lisichomoze?

Unaelewa kwamba unaandika kizembe?
 
Unacho amini kinakuwa na umuhimu pale unapolenga mahala husika ila ukajikanganya katika matamushi.
1;anasema ni tobo
2;asema ni tundu
==>Mwalimu mwenye busara atawapa marks sawa maana tofauti ni matamushi ila mlicholenga ni kimoja.

1.Hujathibitisha kwamba Mungu yupo.
2. Hujajibu kuondoa contradiction ya kama Mungu mjuzi wa yote, mwenye upendo wote na uwezo wote kaumba ulimwengu huu, kwa nini kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani.

Kwa nini unafikiri mtu yeyote anayetumia akili yake akubali kuamini Mungu huyu yupo?
 
Hapa ulichosema ni kama mtu anayesema.

Hatujui square root ya mbili ni nini.

Lakini square root ya mbili lazima itakuwa kumi.

Mimi nitakuuliza swali dogo tu.

Unaweza kuthibitisha kwamba square root ya mbili ni kumi?

Unaweza kuthibitisha kwamba kupotea kwa meli hiyo devils triangle kunatokana na Mungu?

Na kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote apoteze meli? Hana kitu kingine muhimu zaidi cha kufanya?

Sina hakika kama umenielewa vizuri nikichokimaanisha katika maelezo yangu yote yale na hadi kutoa mfano wa hiyo devil triangle.

Nilichozungumzia mimi ni huwepo wa sehemu zenye maajabu ya kipekee ambayo hata wana sayansi wenyewe hawawezi kukupa full scentific details kuhusu tabia za eneo hilo.... na ndio hapo nikataja hiyo devil tringle kama moja wapo wa sehemu hizo..

na moja wapo ya maajabu hayo ya kipekee katika sehemu hiyo ni pamoja na kuwa na gravitational force kubwa kuliko sehemu zingine zote za bahari, na hadi leo hii bado haijafahamika kwa usahihi ni kwanini eneo hilo liwe na utofauti huu ambao kwa namna nyingine umeiweka dunia hatarini hasa kwa vyombo vya usafiri vya..!! wamebaki na speculation tu.

Na tukirudi katika science tunaambiwa kila kitu kinawezekana everything can be profoundly scientifically proved but kwa hili wamechemka hadi kesho!!

Sasa, maajabu hayo yanasababishwa na nini kama sio Mungu mwenyewe??

Hichi ndio nilichomaanisha na hiyo mifano yako ya pembe tatu sijui square root wala hata haisuani na kitu nilichokiongea.

Nadhani kwa kurudia hivi umenielewa.
 
Sayansi kushindwa kujua kitu kinatokana na nini kunathibitishaje kwamba kitu hicho kinatokana na Mungu?

Huelewi maana ya uthibitisho.

Uthibitisho kwamba hiyo triangle yako miujiza inatokana na Mungu utakuja pale utakapoweza kuonesha kwamba miujiza hiyo inatokana na Mungu.

Usitake kusema kwamba sayansi kutojua jibu la kitu, maana yake jibu lake ni Mungu.

Leo jua limepatwa. Kwa maelfu na maelfu ya miaka watu walikuwa hawajui jua kupatwa kunatokeaje.

Watu wakaona huu ni muujiza. Ni kazi ya Mungu. Kama wewe unavyoona huo muujiza wa triangle.

Baadaye watu wakaja kugundua kwamba kupatwa kwa jua kunaweza kuelezewa kwa mizunguko ya mwezi na jua tu. Hata hakuhitaji habari za Mungu.

Sasa kama mtu aliamini kwamba kupatwa kwa jua ni muujiza ambao haueleweki na binadamu kwa sababu ni muujiza wa Mungu, na leo tumeelewa kwamba kupatwa kwa jua kunatokana na mizunguko ya jua na mwezi kuingiliana kutokana na perspective ya dunia, mtu huyu ambaye aliamini kupatwa kwa jua ni muujiza wa Mungu atasemaje? Ataendelea kuamini Mungu?

Kwa nini unaunganisha kitu ambacho sababu yake haijajulikana kuwa kimetokana na Mungu?

Unaweza kuonesha uhusiano uliopo kati ya hiyo triangle na huyo Mungu?

Nimekuuliza, kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote azamishe vyombo na kuua binadamu?

Hujanijibu.

Unachosema hapa ni sawa na mtu ananiuliza, "Unajua square root ya mbili?" Namjibu "Sijui". Ananijibu "Ni kumi"

Nikimuuliza "Unaweza kunionesha njia inayokufanya upate kumi kama square root ya mbili?" Hawezi. Hajui. Kakariri tu square root ya mbili ni kumi.

Nikimbishia anakataa. Anasema kwamba kwa sababu mimi sijui square root ya mbili ni ngapi, jibu ni kumi.

Usiseme tu Mungu ndiyo kasababisha hiyo triangle.

Tuoneshe kasababishaje.
 
Back
Top Bottom