Ukweli wa uwepo wa Mungu na Makazi yake upo hapa


To God be the encomium.

Hilo swali ulilomuuliza kwenye paragraph ya kwanza lina uzito sana na halihitaji jibu jepesi jepesi tu, linahitaji jibu lenye ushawishi wa hali ya juu ambalo nadhani litakuwa ni kitu kipya kabisa kwa wengine hapa.

Ila kama kawaida yake ameskip swali hilo na kukupeleka kwenye comfort zone yake na kukuchanganyia na maahrage na bamia ndani ya bakuli moja yaani kauliza maswali mengine kabisa ambae yeye kwake ndio mtindo uliochagua kujibu kila anapouliza swali.

Angalia hapa alichokujibu... sasa hapo kuna uhusiano kweli na swali hilo ulilomuuliza!?


Kiranga uache kujibu swali kwa kuuliza maswali badala yake ujibu kwanza swali uliloulizwa kwanza ndio wewe uulize swali lako..!! kwa style hiyo unanifanya nione kumbe bado huo uatheist wako haujakomaa na hauna strong back up zaidi ya blaah... blaah hizo chache ulizonazo!!

Unakumbuka kuna siku niliwahi kukuuliza hizo deliverence zinavyofanywa na watu kama kina TB Joshua wanatumia magic power ambayo chanzo chake ni nini!!? ukanijibu hivi "unajuaje kama kuna chanzo chake ni Mungu na sio kitu kingine?".... na mimi nikakwambia uniambie hicho chanzo kingine ni kipi!! haukujibu swali hili.

Na leo Impongo kakuuliza swali lile ulilokimbia siku ile..!!

Asee i'm in doubt with your atheism.
 

Unakubali kwamba ukisema kitu A kinasababishwa na kitu B una wajibu wa kuthibitisha kwamba kitu A kinasababishwa na kitu B?
 
Kwa maana fupi tu ya haya maelezo yako yoote uliyoandika unachosema ni kwamba, hayo yote ambayo hadi hivi sasa tunayoyaona ni miujiza kuna siku yatapatiwa uthibitisho na yatakuwa na enough scientific explanations na baada ya hapo itakuwa sio miujiza tena si ndio hivyo!!?

Hapo ni sawa na kusema Tanzania ni nchi ya dunia ya tatu na haina uwezo hata chembe wa kuitawala dunia, na kwa sababu swala hilo la tanzania kuitawala dunia bado ni imagnation tu basi isipo siku litawezekana hivyo ni swala la muda tu na hapo hapo haujui mtaanzaje.

Kwa hiyo kila kitu kinasababu yake ya kwanini kimekuwepo na vile ambavyo bado havijawa na sababu hadi leo hii, kuna siku sababu zao zinapatikana tu-kiranga logic
 

Hata kitu sayansi ikishindwa kukipatia jibu milele, kushindwa huko kukipatia jibu kunathibitishaje kwamba jibu ni Mungu?

Kushindwa kujua njia ya moja kwa moja kutoka Dar es Salaam kwenda Mtwara kunathibitishaje kwamba njia hiyo inapitia juu ya Mlima Kilimanjaro?

Ukiniambia kwamba njia ya moja kwa moja kutoka Dar es salaam kwenda Mtwara inapitia juu ya mlima Kilimanjaro, inabidi unioneshe njia hiyo inapitia vipi juu ya mlima Kilimanjaro.

Hutakiwi kusema tu kwamba, kwa sababu mimi sijui njia ya moja kwa moja ya kutoka Dar es salaam kwenda Mtwara, basi njia hiyo lazima inapitia juu ya mlima Kilimanjaro, kwa sababu mlima Kilimanjaro ni mlima mfupi kuliko yote Afrika.
 
Kwa staili hii ya mjadala ya kutaka majibu yatoke upende mmoja tu na mwingine ukiukiza nao unaishia kutoa maswali lukuki ni ngumu kufikia muafaka...
 
Lakini si hautakuwepo kuthibitisha ulicho Kuwa ukiamini?
 
Kwa staili hii ya mjadala ya kutaka majibu yatoke upende mmoja tu na mwingine ukiukiza nao unaishia kutoa maswali lukuki ni ngumu kufikia muafaka...
Ninaamini tutafika mwisho na Kiranga ataludi kundini
 
Jambo lipi ambalo unaweza kusema A inasababishwa na B bila ya kuwa na wajibu wa kuthibitisha kwamba A inasababishwa na B ?
Unahitaji nini ili uwe na uhakika kuwa ili mimba ipatikane ni lazima Mme akutane kimwili na Mke ndio mimba itungwe INA maana kama kitendo kilifanyika siri utakataa kwa kuwa hujaona
 
tujadili kwa kutoa mawazo yetu pia naomba tuangalie maandiko yanasemaje kuhusu hilo.je kama uwepo wa M/mungu umebuniwa tu tuseme hao watu wa zamani walikuwa na akili kuliko sisi?.
quran surat al rahmani:arhamani mwingi wa rehma amefundisha quran amemuumba mwanadamu akamfundisha kubaini jua na mwezi huenda kwa hisabu....swali kama quran inasema jua na mwezi huenda kwa hisabu mtume(s.w.s)alifahamu vipi kama vinaenda kwa hisabu?
 
Ili uthibitishe kitu ni lazima ufanye utafiti au uone lakini vingine havionekani kilahisi na itakupasa kubobea katika utafiti ili ujue sasa wewe kwa kuwa haujabobea na Mimi nimebobea nimekuletea majibu ya msingi nielewe nia mini Mimi na umwani Mungu muumba wa vyote ukiwemo wewe.

Kama unataka kumjua Mungu itakupasa ubobee kama Mimi kumjua itakuchukua mda lakini lazima hisia zote uelekeze kwake usimtafte kwaajiri ya umaarufu wako hutomwona
 
Mkuu huyu Kiranga mbishi sana kuwa Mungu hayupo!
Lakini nimemuuliza katika sayansi ulimwengu umetokana na mlipuko miaka billion 12 iliyopita chembechembe zikakusanyika zikatengeneza mamiloni ya sayari na nyota na vyote vilivyomo ktk tanga
Lakini ilichukua billions of year dunia yetu kupoa na uhai kuanza na dunia ilikuwa joto Kali ambapo hakukuwa na mbegu yoyote ilikuwa hai kuweza kuanza uhai joto lilikuwa Kali na jua lilitema sum ktk uso wa dunia hakuna chochote kingewexa kustawi nani aliweka hewa ya ukanda kuchuja sumu ya miale ya jua nani alileta oxygen ili uhai uanze hajui ukimwambia ni Mungu haamini !Kiranga ni pasua kichwa Ngoja niingie kibaruani kwanza maana wewe ni pasua kichwa
 
Ana uwezo wa kuumba jiwe likawa zito kiasi kwamba hataweza kamwe kulibeba?

Jibu ndiyo au hapana.
Nilicheka kuona na wewe umetumia hako hoja.

Tushajadili suala hili nikakwambia kuwa kushindwa sio uwezo. Kumbuka tunajadili uwezo,sasa unapokuja na suala la kuumba jiwe na kushindwa kulibeba ndiyo inaleta maana gani?
 
Unaniuliza habari za Big Bang nilikwambia lini kwamba nazikubali?

Kwa nini unauliza "nani aliweka hewa" na si "nini kiliweka hewa"? Unauliza swali ambalo lina bias kwenda kwenye jibu unalolitaka wewe?

Nikikwambia kwamba sijui jibu la swali lako, kutokujua kwangu kunathibitishaje jibu ni Mungu?

Ukiniuliza square root ya mbili ni nini, nikakwambia sijui, kutokujua kwangu kunathibitishaje kwamba square root ya mbili ni kumi?

Utasemaje square root ya mbili ni kumi bila kutuonesha umepataje kumi?

Unaweza kuthibitisha hiyo hewa ililetwa na Mungu? Unaweza kuthibitisha haikuweza kutokea kwa njia nyingine yoyote?
 
Nilicheka kuona na wewe umetumia hako hoja.

Tushajadili suala hili nikakwambia kuwa kushindwa sio uwezo. Kumbuka tunajadili uwezo,sasa unapokuja na suala la kuumba jiwe na kushindwa kulibeba ndiyo inaleta maana gani?
Hujajibu swali.

Hujaelewa swali.

Swali halijauliza kushindwa. Limeuliza kuweza kuumba.

Jibu ndiyo au siyo.
 
Wewe herufi za Kiswahili tu zinakushinda.

Halafu unajitapa umebobea.

Umebobea nini? Ungumbaru?
 
"Katika utafiti wangu nimejifunza kwa kuwa Jua ndilo lina Uhai kwa Viumbe basi kuna uwezekana mkubwa wa 94.6% Muumba anaishi katika Jua" kwahiyo muumba anaishi kwenye jua pamoja na viumbe gani??
Hivyo viumbe vinauwezo sawa na muumba??
Jua kiumbe, mwezi kiumbe, sayar ni viumbe na mwisho wao vyote vitazima ila kudhihirisha ukiumbe wao...!
##kuleta amri kumi kupitia radi mwanga sio sababu yakusema anaishi kwenye jua/radi kwasababu rad/mwanga pia husafiri kwenye hewa... Je, tunaweza kusema muumba yupo kwenye jua na hewa??
 
Kama umeshindwa kuwa na jibu ina maana hujui lakini anae fahamu amekueleza ametafiti kubaliana nae
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…