Ukweli wa uwepo wa Mungu na Makazi yake upo hapa

Tofautisha kati ya kuumba na kuunda
Sawa huyo mungu alipata wapi akili ya kuumba huu ulimwengu, na alifikiria atapata faida gani? na kabla hajaumba huu ulimwengu yeye alikua anafanua nini? Na saizi anafanya nini?
 
Unaamini dini yoyote au ni mpagani?
Mimi sina dini na wala sio mpagani ninamashaka sana na hizi dini na ninaona ni kama utumwa
Na ninaamini walioleta hizi dini ndio wapagani na tena wanadhambi kubwa sana
Kwasababu leo hii watu wanauana na kubaguana kwaajili ya hizi dini kabla hizi dini hazijaja watu walikua wanaishi vizuri kwa upendo.
 
Nahoji imani ya mtu ili tuelewane kwa kuongea "lugha" moja.
 
Mjingawewe [emoji35] kweli hata aliyekuchagulia hilo jina hakukosea
 
impongo umemwachia nani aendeshe gurudumu...?
au utafiti wako ndo uliishia hapo..?
 
Hiyo miaka yako 16 bora ungekula Bata tu maana huu unaoita utafiti ni upuuzi mtupu
Mkuu haujanitendea badala ya kunipa moyo unanikatisha tamaa kweli Binadamu ni wa Ajabu
 
Huu siwezi kuurefer Kama utafiti was kisayansi Kama ulivyidai mi naona hapa umefanya falsafa tu ambayo haina logic. By the way naomba ni kuulize kwa kuwa umechanganya dini na sayansi kwa mujibu wako hili ndo swali langu. Kwa mujibu wa biblia dunia ndo ilikuwa ya kwanza kuumbwa kabla ya jua nasi tunaamini mungu Hana mwanzo wala mwisho yaani Alfa na omega hivyo kabla ya jua kuumbwa mungu aliishi wapi?
 
Utafiti wa Sayansi
Kwa upande wangu utafiti wako haukai akilini mwangu...Mungu hakai kwenye nyota yeyote wala sayari na jua letu ni dogo sana kuna mapande ya nyota namaanisha jua ni nyota yani kuna nyota kubwa sana hata jua letu ni dogo sana sizani Mungu akae kwenye nyota ndogo kama hiyo..Mungu yuko popote..Sasa Embu tofautisha hizo nyota mbili hapo Sun na Uy Scuti

Utafiti wa Bibilia
Hapa nakubaliana na wewe.Mungu alipokea sadaka kwa njia ya moto..Aliwajia wanaadamu kwa njia ya moto..Kuna story ya Musa umesahau ungeongezea hapo"Musa aliona kichaka kina waka moto bila ya kuteketea na akaambiwa hapo ni mahali patakatifu vua viatu vyako"
 

pole Mkuu kwa kupoteza muda mwingi kwa kufanya utafiti ambao ingetosha kuwauliza layman wakakupa majibu mazuri zaidi ya hayoo ukaujua ukweli kuhusu Mungu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…