Ukweli wa uwepo wa Mungu na Makazi yake upo hapa

Ukweli wa uwepo wa Mungu na Makazi yake upo hapa

Mungu anakaa kwenye jua! Mwanafalsa wa kale (ancient philosophy) sikumbuki jina alisema ukweli upo kwenye moto, lakini alishindwa kujieleza. Yote hayo ni maoni kwani jibu la uwepo wa Mungu kila mtu na maoni yake. Mimi nafikiria hivi, nimetoka kwa wazazi wangu, nao walitoka kwa wazazi wao, ukiendelea huna mwisho, basi kuna chanzo chake, ni kipi? Basi kila kitu kina mwanzo wake na kuna mwanzo wa vyote, ndio Mungu. Anakaa wapi? Hakuna jibu. Basi shughulika Na vinavyoonekana, vingine unapoteza mda. Hakuna utafiti mbele na Muumba
Dunia ina mengi Mungu ametupa akili tuzitumie
 
Hakuna cha wazungu na hatupaswi kujishusha huu ni utafiti lengo nikuelezea bayana kwa lugha yetu adhimu ya kiswahili ili walau kila mtu ajifunze tatizo wengi mmeshikwa akili hamfikirriii inje ya box
Sawa wewe uliye mjanja endelea kupoteza muda kufanya utafiti ambao utaambulia sifuri ya mafanikio
 
Huyu mleta mada anajiona ana upeo mkubwa kufikia kumchunguza Mungu alipo..ujinga ulioje huu
 
Ni kweli ktk universe Kuna ma bilioni ya galaxy na katika kila galaxy kuna billion ya nyota (jua) na ktk nyota (jua) kuna Sayari na ktk sayari kuna miezi ([emoji287] moon) .
Kuhusu supernova nyota hufa baada ya mda wake kuisha na nyota ikifa sayari zake na miezi hufa, lakini maelezo yangu yanahusu uwepo wa MAKAZI YA MUNGU KTK MOJA WAPO YA NYOTA (JUA) hili linatanabahishwa ki Bible na scientific Rejea
Bible, Kutoka 19,20 Mungu ameshuka ktk moto.
Science, Katika nyota (Majua) ndio penye uthibitisho hapawezi kukaribiwa na chochote kwa sababu ya moto mkali wa myeyungano waki nuclear

Rejea 1Timotheo 6:16 Mungu huishi pasipo karibiwa ktk Nuru ya mbali.

Mkuu kama haujanielewa niulize tu
Mkuu visivyokaribiwa angani ni billions hasa nyota zenye joto kali.
Sasa kwa nini usadiki ni jua ndiko makazi ya mungu?
Je makazi ya mungu yana mwisho?kwa maana tafiti zinainesha jua ni nyota na nyota ina life span yake ndio maana hulipuka wakati fulani.
Sasa mkuu kama jua likiisha kwisha ina maana maskani ya mungu pameharibika.
Kwa hiyo mungu atahama?
Ahsante
 
Sayansi hiyo hiyo inasema, capacity ya Jua ku-bear life katika Dunia yetu hii ni miaka 11bn, na sasa we are almost halfway...so after that, Mungu atahamia kweye nyota nyingine au ataenda wapi ?
 
Sayansi hiyo hiyo inasema, capacity ya Jua ku-bear life katika Dunia yetu hii ni miaka 11bn, na sasa we are almost halfway...so after that, Mungu atahamia kweye nyota nyingine au ataenda wapi ?
Ngoja tumsubiri atatujibu nini...
Kwa maana nasa na bajeti yao na vyombo walivyonavyo pia kuna watu wana akili sana kule wanafanya kazi usiku na mchana na wanapiga picha kwa kutumia telescopes za teknolojia za juu sijawahi kusikia hata wakisadiki mungu aliko zaidi ya kusema jua lina life span.
Ila huyu ndugu yetu ni mawazo yake binafsi yamemtuma hajawahi hata kwenda mwezini.
 
Mimi nina maswali machache yanayopinga hoja hii na naomba mkuu impongo unijibu maswali yangu.
Mkuu impongo hoja zake amezijenga hasa kutoka katika vitabu vya kiimani na kutoka pia katika facts za kisayansi.

Mkuu impongo kabla ya yote unaamini makazi ya mungu ni kwenye jua.
Kwanza sayansi inasemaje kuhusu jua?
Sayansi inatuambia jua ni nyota na lina kipenyo cha 1.39 million kilometers.
73% ya jua ni hydrogen.
25% ni helium na sehemu iliyobaki ni elements kama oxygen,iron carbon na neon.
Biblia inasemaje kutoka mwanzo?
Biblia hapo mwanzo mungu aliumba mbingu na dunia.
Kwa hiyo kumbe mungu aliumba mbingu ambayo ni universe ambamo ndani yake kuna jua sasa je mkuu
(1)@impongo wakati mungu akiumba mbingu ina maana jua halikuwako kwa hiyo mungu alikuwa anaishi wapi?

Quran inasemaje kuhusu mwanzo wa ulimwengu?
Aya ya 11 ya Surat Fuswilat inasema kuwa uumbaji wa mbingu umetokana na gesi kwa kusema:
“Kisha akaielekea mbingu na hali i moshi, ndipo alipoiambia (mbingu) na ardhi: Njooni mkipenda au msipende, vyote viwili vikasema: Tumekuja hali ya kuwa wenye kutii.
Kumbe biblia na qurani vinaonyesha kabisa kuwa mungu aliumba mbingu na ardhi kwa hio kumbe wakati huo alikuwa na makazi yake ambapo mimi na wewe hatupafahamu

Sayansi inasema jua ni miongoni mwa nyota na nyota zipo ndani ya galaxies na galxies zipo ndani ya mbingu.
Kwa hiyo mbingu ni kuuuubwa saaaana kwa maana NASA wanasema katika galaxy yetu sisi tunapoishi kuna nyota bilioni 100 likiwemo jua.
Swali la pili mkuu(2) impongo Je kwa nini useme jua ndiko kuliko makazi ya mungu wakati kuna billions za nyota?

Sayansi inasema nyota ina mwisho wa kuishi
Inasemekana mwisho wa maisha ya jua ni jinsi miaka inavyokwenda.
Siku zinavyokwenda sayansi inasema jua ndio linavyokuwa kali na kuwa angavu zaidi.
Sayansi inatuambia kuwa jua litazidi kuwa kali zaidi hadi kufikia wakati bahari na vyanzo vya maji kuchemka na pia barafu za kwenye milima kama mt kilimanjaro kuyeyuka.

Je qurani inasemaje kuhusu mwisho?
Katika siku ambayo Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) atawafufua viumbe vyake vyote, jua litashushwa karibu sana na watu ambapo kutaachwa tofauti ya maili moja baina ya jua na watu ardhini. Watu watatopea katika jasho kulingana na amali zao, wengine mpaka kwenye vifundo vya vya miguu, wengine mpaka kwenye magoti yao, wengine mpaka kwenye viuno vyao na wengine watakuwa na hatamu ya jasho na, wakati yalivokuwa yanasemwa haya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliweka mkono mbele ya mdomo wake.

Biblia inasema kuhusu mwisho?
Katika amosi 8.9
Tena itakuwa siku hiyo, asema Bwana MUNGU, nitalifanya jua litue wakati wa adhuhuri, nami nitaitia nchi giza wakati wa nuru ya mchana.

Maneno hayo yote toka katika vitabu vitakatifu hivyo inaonyesha kwamba kumbe mwisho utakuwako.

Swali la tatu.
Je impongo kweli makazi ya mungu yana mwisho?
Ina maana baada ya maisha ya jua mungu atahama?
Ahsante sana.

Sawa wewe uliye mjanja endelea kupoteza muda kufanya utafiti ambao utaambulia sifuri ya mafanikio
Mkuu chenye faida hapa Duniani ni kimoja tu kuijua kweli inatuweka huru lakini mengine yote ni ubatili mtupu yanapita
 
Huyu mleta mada anajiona ana upeo mkubwa kufikia kumchunguza Mungu alipo..ujinga ulioje huu
Mkuu,,, Mungu amenipa akili niitumie kuijua kweli ili nichague wapi niende wapi
 
Mkuu visivyokaribiwa angani ni billions hasa nyota zenye joto kali.
Sasa kwa nini usadiki ni jua ndiko makazi ya mungu?
Je makazi ya mungu yana mwisho?kwa maana tafiti zinainesha jua ni nyota na nyota ina life span yake ndio maana hulipuka wakati fulani.
Sasa mkuu kama jua likiisha kwisha ina maana maskani ya mungu pameharibika.
Kwa hiyo mungu atahama?
Ahsante
Mkuu nyota yetu ya Jua ni ndogo lakini kuna mizinga ya nyota ni mikubwa ambayo hayana hesabu inayoelezeka kibinadam

15 ambako yeye kwa majira yake atakudhihirisha, yeye aliyehimidiwa, Mwenye uweza peke yake, Mfalme wa wafalme, Bwana wa mabwana;
1 Timotheo 6 :15

16 ambaye yeye peke yake hapatikani na mauti, amekaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hakuna mwanadamu aliyemwona, wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye hata milele. Amina.
1 Timotheo 6 :16
 
Ngoja tumsubiri atatujibu nini...
Kwa maana nasa na bajeti yao na vyombo walivyonavyo pia kuna watu wana akili sana kule wanafanya kazi usiku na mchana na wanapiga picha kwa kutumia telescopes za teknolojia za juu sijawahi kusikia hata wakisadiki mungu aliko zaidi ya kusema jua lina life span.
Ila huyu ndugu yetu ni mawazo yake binafsi yamemtuma hajawahi hata kwenda mwezini.
Mkuu nimeona nikujibu kutumia Bible naamini ndio kitabu kitakatifu unachotumia

15 ambako yeye kwa majira yake atakudhihirisha, yeye aliyehimidiwa, Mwenye uweza peke yake, Mfalme wa wafalme, Bwana wa mabwana;
1 Timotheo 6 :15

16 ambaye yeye peke yake hapatikani na mauti, amekaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hakuna mwanadamu aliyemwona, wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye hata milele. Amina.
1 Timotheo 6 :16
 
mchichapori.

Mkuu pole na majukum ya kila siku.

1.Nyota zinazongaa ni Ma-Jua kama ilivyo nyota ya Jua letu tofauti ni ukubwa wa kila nyota

2.Kuhusu Jua (nyota) letu ikifa Mungu ataenda wapi kwanza mimi sikuthibitisha ni Nyota ipi alipo Mungu ndiyo maana nimesema mojawapo ya nyota (Jua) ndiko kuna makazi ya Mungu.

Kwa mfano fikiri miaka 11.5 billion ijayo inaonekana milk away Galax yetu itaungana na Galaxy ya Andromeda huenda zitatengeneza mvutano na inawezekana Andromeda na milk away ma billion ya Majua (nyota) ikawa kitu kimoja kinachotoa mnururisho wa moja kwa moja kama nyota moja je unafikiri ikiwa hivi si milele haitaweza kuzimika kwa maana hata dark energy itakuwa haina nguvu ya kuzuia galaxy nyingine kuvutwa na kumezwa.

3.Huenda makazi ya Mungu ni nyota kubwa zilizoshikana mabillion ya Galaxy zisizokwisha Milele.

4.Jua letu litakwisha (supernova) lakini ukweli wa Mungu kuishi ktk nuru isiyoweza kukaribiwa ni dhahiri isiyopingika

God is not a three dimensional being so it is impossible to describe God in a three dimensional world
Makazi yake anayajua mwenyewe
 
Back
Top Bottom