Mimi nina maswali machache yanayopinga hoja hii na naomba mkuu impongo unijibu maswali yangu.
Mkuu impongo hoja zake amezijenga hasa kutoka katika vitabu vya kiimani na kutoka pia katika facts za kisayansi.
Mkuu impongo kabla ya yote unaamini makazi ya mungu ni kwenye jua.
Kwanza sayansi inasemaje kuhusu jua?
Sayansi inatuambia jua ni nyota na lina kipenyo cha 1.39 million kilometers.
73% ya jua ni hydrogen.
25% ni helium na sehemu iliyobaki ni elements kama oxygen,iron carbon na neon.
Biblia inasemaje kutoka mwanzo?
Biblia hapo mwanzo mungu aliumba mbingu na dunia.
Kwa hiyo kumbe mungu aliumba mbingu ambayo ni universe ambamo ndani yake kuna jua sasa je mkuu
(1)@impongo wakati mungu akiumba mbingu ina maana jua halikuwako kwa hiyo mungu alikuwa anaishi wapi?
Quran inasemaje kuhusu mwanzo wa ulimwengu?
Aya ya 11 ya Surat Fuswilat inasema kuwa uumbaji wa mbingu umetokana na gesi kwa kusema: “Kisha akaielekea mbingu na hali i moshi, ndipo alipoiambia (mbingu) na ardhi: Njooni mkipenda au msipende, vyote viwili vikasema: Tumekuja hali ya kuwa wenye kutii.”
Kumbe biblia na qurani vinaonyesha kabisa kuwa mungu aliumba mbingu na ardhi kwa hio kumbe wakati huo alikuwa na makazi yake ambapo mimi na wewe hatupafahamu
Sayansi inasema jua ni miongoni mwa nyota na nyota zipo ndani ya galaxies na galxies zipo ndani ya mbingu.
Kwa hiyo mbingu ni kuuuubwa saaaana kwa maana NASA wanasema katika galaxy yetu sisi tunapoishi kuna nyota bilioni 100 likiwemo jua.
Swali la pili mkuu(2)
impongo Je kwa nini useme jua ndiko kuliko makazi ya mungu wakati kuna billions za nyota?
Sayansi inasema nyota ina mwisho wa kuishi
Inasemekana mwisho wa maisha ya jua ni jinsi miaka inavyokwenda.
Siku zinavyokwenda sayansi inasema jua ndio linavyokuwa kali na kuwa angavu zaidi.
Sayansi inatuambia kuwa jua litazidi kuwa kali zaidi hadi kufikia wakati bahari na vyanzo vya maji kuchemka na pia barafu za kwenye milima kama mt kilimanjaro kuyeyuka.
Je qurani inasemaje kuhusu mwisho?
Katika siku ambayo Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) atawafufua viumbe vyake vyote, jua litashushwa karibu sana na watu ambapo kutaachwa tofauti ya maili moja baina ya jua na watu ardhini. Watu watatopea katika jasho kulingana na amali zao, wengine mpaka kwenye vifundo vya vya miguu, wengine mpaka kwenye magoti yao, wengine mpaka kwenye viuno vyao na wengine watakuwa na hatamu ya jasho na, wakati yalivokuwa yanasemwa haya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliweka mkono mbele ya mdomo wake.
Biblia inasema kuhusu mwisho?
Katika amosi 8.9
Tena itakuwa siku hiyo, asema Bwana MUNGU, nitalifanya jua litue wakati wa adhuhuri, nami nitaitia nchi giza wakati wa nuru ya mchana.
Maneno hayo yote toka katika vitabu vitakatifu hivyo inaonyesha kwamba kumbe mwisho utakuwako.
Swali la tatu.
Je
impongo kweli makazi ya mungu yana mwisho?
Ina maana baada ya maisha ya jua mungu atahama?
Ahsante sana.