Ndugu yangu mungu haishi kwenye jua na kufika kwa mungu ni vigumu sana,mungu anasema kwenye Quran tukufu ameipamba anga la mwanzo la dunia kwa nyota,jua na mwezi pamoja na vitu vingine vinavyofanana na hivyo.Kwahiyo maana yake umbali wa dunia,vitu vinavyofanana maumbile na dunia pamoja na umbali wa nyota ya mwisho bado kwa mungu ni mbigu ya kwanza katika mbingu saba alizoumba.
Quran inaelezea vizuri sana mpangilio wa mbingu saba alizoumba mwenyezi mungu,nyota kutoka ya kwanza mpaka ya mwisho zimetofautiana kwa umbali mkubwa sana.Kama kuifikia nyota ya mwisho kwa umbali ni vigumu na kwakua nyota,dunia na vitu au sayari zinazofanana na dunia zipo katika mbingu ya kwanza na kwakua binadamu kwasasa hasa uwezo wa kuifikia nyota ya mwisho ambayo ipo kwenye mbingu ya kwanza.Basi mwanadamu hana uwezo wa kujua alipo mungu na mungu haishi kwenye jua.NB;matabaka saba ya mbingu tunayofundishwa kwenye jiograph shuleni ni matabaka yaliyopangiliwa na binadamu na yote yapo kwenye mbingu ya kwanza.Sahau kabisa kuhusu mbingu ya pili mpaka ya saba na mungu hajaribiwi,kwa vile wote tutakufa basi tutaujua ukweli baada ya kufa