Ukweli wa uwepo wa Mungu na Makazi yake upo hapa

Nitamchukiaje Mungu ambaye hayupo na wala hujaweza kuthibitisha kwamba yupo?

Mimi nachukia uongo.

Nachukia kufanywa mjinga.

Mtu akiniambia "Kuna pembetatu duara ya ajabu, ukiikubali utapata uzima wa milele, ikubali" nitaona hizo ni porojo na kuzikataa.

Nikizikataa habari hizo za uongo wa kitu ambacho hakipo utasemaje kwamba nimeichukia hiyo pembetatu duara ambayo hata haipo?

Kabla ya kusema naichukia pembetatu duara, unaweza kuthibitisha kwamba ipo?

Kabla ya kusema namchukia Mungu, unaweza kuthibitisha kwamba yupo?

Na kama huwezi, nitamchukiaje Mungu ambaye huna hata uwezo wa kuthibitisha kwamba yupo?
Inakupasa kuamini kwanza ndio ujue yupo

Jenga imani kwa Mungu hapo utaweza kuwa thabiti na utamjua.

Kichwa chako kipo vizuri kama mtz sina imani na uraia wako !
 
Lakini ni mambo mengi Kama binadamu unaejitambua yatakupa changamoto huna budi kumwamini

Hakuna mwanadamu mwenye majibu fasaha kuhusu Mungu kila la kheri.

Ninachokuomba mwamini Mungu maana hakuna gharama yoyote.
 
Kwa nini niamini Mungu yupo?
 
Kuamini Mungu yupo wakati hayupo kuna gharama sana, unaelewa hili?

Unaelewa hii ni moja ya sababu inanifanya nishikie bango hili suala?

Unaelewa kwamba imani ya Mungu inarudisha nyuma sana nchi masikini kiuchumi?
 
Ulichokifanya sio utafiti ni assumpition baada ya kusoma poorly sources
 
hivi kwani kabla ya ulimwengu kufanyika (big bang) kulikuwepo na nini?
 
URL]
 
Kwa nini niamini Mungu yupo?
Pole na majukumu! Ukiamiani Uwepo wa Mungu ndio utaweza kujifunza mengi na kujua uwepo wa Mungu muumba wa vyote. Ukitaka kujifunza kuhusu viumbe hai lazima ujifunze biological bila kujifunza hutojua utakaa ki ubishani bila majibu.
 
YEHOVA hachunguzwi huwa sitaki hata nipajue anapoishi
Ni vile umekuzwa ktk imani ya uoga sioni hofu kumjua baba yangu Muumba wa vyote na tumepewa akili tuzitumie tumjue yeye kuwa ndiye aliye umba vyote
 
hivi kwani kabla ya ulimwengu kufanyika (big bang) kulikuwepo na nini?
Hewa mgandamizo ya aina mbalimbali na vipande vipande vya aina mbalimbali mlipuko ulipelekea kuundwa kwa sayari na nyota na vyote vilivyopo kwa ujumla wake ktk ulimwengu
 
Ulichokifanya sio utafiti ni assumpition baada ya kusoma poorly sources
Mkuu
Sijawahi kukata tamaa kwa walio shindwa Mawazo yako ni ya kushindwa huamini huwezi kufanya ni mazingira yaliyo kukuza sio kosa lako
 
Pole na majukumu! Ukiamiani Uwepo wa Mungu ndio utaweza kujifunza mengi na kujua uwepo wa Mungu muumba wa vyote. Ukitaka kujifunza kuhusu viumbe hai lazima ujifunze biological bila kujifunza hutojua utakaa ki ubishani bila majibu.
Hujajibu swali uliloulizwa, umefanya circular argument.

Nakuuliza "Kwa nini nilime mtama?" Unanijibu Ukilima mtama ndio utaweza kujifunza mengi kujua kulima mtama".

Hujajibu kwa nini nilime mtama.

Hujajibu kwa nini niamini uwepo wa Mungu.
 
Umefanya nafasi yako. Mungu ni omnipresent-yupo kila mahali. Tatizo unamlinganisha na viumbe. Yeye ni Muumbaji. Yeye tunamwita Niko na yuko kila mahali. Siku moja atatenga wema na uovu...chagua wema ukaishi
 
Hujajibu swali uliloulizwa, umefanya circular argument.

Nakuuliza "Kwa nini nilime mtama?" Unanijibu Ukilima mtama ndio utaweza kujifunza mengi kujua kulima mtama".

Hujajibu kwa nini nilime mtama.

Hujajibu kwa nini niamini uwepo wa Mungu.
Lazima uamini Mungu kwa kuwa kila unachokiona kimekuwapo kwa uweza wa Mungu pia huwezi angalia nyumba kwa inje ukajua mpangilio uliopo ndani lazima uingia ndani ujiifunze kama upo inje utaishia kulalama hujui. mjue Mungu ujifunze utamjua vema
 
Bado unazunguka swali. Hujalijibu.

Nakuuliza kwa nini niamini Mungu yupo, unaniambia lazima niamini.

Sitaki kulazimishwa, nataka kujibiwa mpaka nielewe na kukubali kwa hiyari yangu.

Kwa nini unasema ninachokiona kimekuwepo kwa uwezo wa Mungu?

Ninachokiona leo ni kimbunga kinachoitwa Matthew, kimeua watu masikini 900 huko Haiti.

Kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aumbe ulimwengu ambao unawezekana kuwa na kimbunga kama hiki wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao hauwezekani kuwa na kimbunga kama hiki bila ya kupungukiwa na chochote?
 
Back
Top Bottom