Masuala ya uwepo wa mungu ni ya imani.
Hakuna aliyetaka kujua Mungu abakaa wapi.
Mungu hachunguzwi.Mungu anaaminiwa.
Kwa kifupi ulichokifanya sio utafiti bali ni utunzi wa riwaya.Hujaongeza ufahamu wowote wa mwanadamu.
Nashauri utumiye miaka yako iliyobaki vizuri.
Kama wewe ni mkristo jaribu kusoma biblia.Katika agano la kale tunaambiwa wanadamu walijaribu kujenga mnara wa babeli ili wafike aliko Mungu.Mungu akakasirika akawafanya waongee lugha mbali mbali wakashindwa kuelewana , wakaacha kujenga mnara wa babeli.Wewe kujaribu kutafuta makazi ya Mungu ni kujaribu tena kujenga mnara wa babeli.
Soma pia agano jipya Mathayo 25 kuhusu Mfano wa Yesu juu ya talanta.Bwana alitaka kusafiri akawaitwa watumwa wake watatu.Akampa wa kwanza talanta tano, wa pili talanta 2 na watatu talanta moja.Yule wa kwanza akazalisha zaidi akapata talanta kumi.Yule wa pili akajituma akapata talanta nne.Yule wa tatu alaifukia talanta.Bwana wao alivyorudi alikasirisha sana na yule aliyeifukia talanta na akashindwa kuzalisha.Wewe kujikita katika utafiti hewa wa miaka 16 ni kufikia talanta uliyopewa na Mungu.
Amka ndugu.Achana na hayo mambo.